Na Mwalimu Oscar Samba #Ug Ministry |
Siku moja
wanafunzi wa Yesu walikuwa wakisafiri majini ama ziwani na walilenga kufika
nga’ambo ya ziwa ili kufanya jambo fulani, lakini walipokuwa katika safari yao,
Punde si Punde bahari ili kumbwa na Mawimbi makubwa yaliyoambatana na Upepo
mkali.
Hali hiyo
iliwapa hofu kubwa mno, Lakini katika mazingira yote hayo hawakukubali kukwama
safarini bali walimwamsha Yesu aliyekuwa akipiga usingizi, Hii ina maana kubwa
sana na hapo mbeleni nitaifafanua.
Tuyadodose
maandiko ili kujionea jambo hili kiunaga ubaga, Soma Marko 4:35-41. Marko 4:35 Siku ile kulikuwa jioni,
akawaambia, “Na tuvuke mpaka ng’ambo.” 37Ikatokea dhoruba kuu ya upepo,
mawimbi ya kakipiga chombo hata kikaanza kujaa maji. 38 Naye mwenyewe alikuwapo
katika Shetri, amelala juu ya mto; wakamwamsha, wakamwambia, Mwalimu sii kitu
kwako kuwa tunaangamia?” 39 Akaamka, akaukeme upepo, akaiambia bahari, “Nyamaza
utuliye!” Upepo ukakoma, kukawa shwari kuu.
Hapo ninapata
funzo kubwa naamini nawe unapata jambo la kushangaza sana; ya kwamba mtu huyu
tuliye naye sio wakufananishwa kwani anaweza kutuliza mambo yaliyoonekana kuwa
ni magumu maishani mwetu na wewe sasa jenga imani hiyo na usisite kumuamsha ili
atulize yanayokusonga. Ili na kwako kuwe, “SHWARI
KUU”
Maandiko
hayo yanatuonyeshe dhairi shairi kwamba YESU alikuwa na malaka juu ya mawimbi,
na upepo, na ukitazama kiumakini utagundua kuwa mamlaka hii tulishapewa tangu
enzi za umbaji wa ulimwengu Mungu alipowaambia Adamu na Hawa kuwa amewapa uwezo
wa kutawala ndege wa angani, (Mamlaka dhidi ya Anga), Samaki wa Baharaini, (Ni
Mamlaka juu ya bahari), Na Wanyama wote wa Nchi kavu, (Ikiwa ni mamlaka juu ya
Aridhi) pamoja na hayo mamlaka hiyo inaambatana na vitu vilivyopo sehemu
husika.
Kwa hiyo
adui mkubwa aliyewafanya wasiweze kuitumia hiyo mamlaka ni kwanza ni Uelewa
wao, hawakulijua hili, maana walikuwa na Yesu, ni kweli ila hawakujua kama
anauwezo wa kutuliza hadi mawimbi na upepo, ndio maaana baada ya mujiza huo
wanashangaa,
“.. Wakaambiana, ‘Ni nani
huyu, hata upepo na bahari humtii? ” Mariko 4:41.
Fikiri kwa kina kwamba wapo na Yesu miaka ya kutosha ila bado hawakufahamu mamlaka/uwezo
aliyo nao, kuhusu tatizo walilokuwa nalo.
Na wewe
yamkini umeokoka ila hujafahamu uwezo wa Yesu kuhusu dhoruba zinazokukumba,
usimwamshe Yesu katika mtazamo wa wale wanafunzi walio mwamsha ili wateseke
wote na Yesu katika kupamba na ile hali kwani hawakutarajia YESU kutenda lile,
ndio maana walimwambia hivi,
“..Sii,
kitu kwako kuwa tunaangamia,” Mariko 4:38. Katika Luka walitumia maneno; Bwana mkubwa
huku wakiita zaidi ya mara moja. Usipotazama andiko hilo kwa jicho la uchunguzi
hutaiona hii fikra ya wanafunzi, ila iinajidhirisha pale wanaposhangaa uweza
wake mara baada ya mujiza kutendeka hali inayobainisha bayana ya kwamba kumuasha
kwao hakukuwa na taraja ya mujiza ule bali kulikwa na mtazamo wa “tupambane
sote.”
Nataka
kukujengea Imanii ili utambue ya kwamba hilo unalolipitia Yesu analiweza kwa
shabaha ya kukataka kuacha kuwatazama wanadamu ambao hawatakusaidia badala yake
wengine wataishia kukusema ama kukusengenya hali itakayokukwamisha kiroho kwani
maneno hayo yanatakumiza bure badala yake unapaswa kumtaza YESU huku ukitambua
ya kwamba ndani yake ipo Mamlaka na itumiye kama alivyokupa ili utulize hayo
mawimbi na upepo kwani Yesu aliukemea na wewe kemia hiyo misukosuko kwenye ndoa
yako, uchumi familia au huduma sasa.
Jambo la
pili lilikuwa ni WOGA, ukiogopa ni dhairi kwamba Imani yako itayumba hali
itakayokufanya kushindwa kuitambua ama kuitumia mamlaka uliyopewa na Yesu
Kristo juu ya hayo matatizo.
Tuone
mafundisho haya ya Uoga kwenye ujumbe huu kama nilivyokudokezea kwenye kitabu changu
cha Namna ya Kuishi Wakati wa Majaribu
au Mapito katika Ukurasa ule wa 31 na kuendelea.
“….Natumai sasa utakubaliana
nami vyema pale Yesu alipokuwa na wanafunzi wake katika boti na mawimbi ya kaja
wakaogopa Yesu aliwauliza “Imani yenu iko wapi” Luka 8:25. Akiwa
anamaanisha kuwa wameogopa na hofu ilimdhirishia Yesu kuwa tatizo ni Imani,
katika swala hili;Tutazame tena Mathayo 8:26 Akawaambia “mbona mmekuwa waoga,
enyi wa Imani haba” Waoga alafu wa Imani Haba , haba maana yake
chache,Kwenye luka anataka kujua walipo iweka imani yao, hapa anawaambia
kuwa Imani mliyo nayo ni chache, Joshu anawaambia “wala msiwaogope”
Twende
kwenye Marko tuone Mfano ama stori hiyo hiyo ya dhoruba ziwani. Marko 4:40
Akawambia , “mbona mmekuwa waoga? Hamna imani bado ?”. Hapa
Yesu anauliza Uwoga pili hamna Imani bado jumlisha na hoja ya luka na Mathayo
changanya na hiyo ya Marko (“Imani yenu iko wapi” + “mbona
mmekuwa waoga, enyi wa Imani haba” na “mbona mmekuwa waoga?
+Hamna imani bado ?”)
Kuna kitu nilikuaidia kukudokezea hapa mbeleni nacho ni hiki, Yesu
alipokuwa amelala sio kwamba hakujua kitakachotokea, La! Asha!! Alijua fika,
ila alikuwa akihitaji kuona au kupima ama kufahamu kiwango cha wanafunzi wake
kumjua, pili Uwezo wao wakukabilina na matatizo na tatu kiwango cha Imani yao.
Ndiposa alipoamka aling’aka hali iliyoonyesha kuwa amekasirshwa na matokeo ya
mtihani uliowakumba.
Nakudhibitisha hilo tazama kwa kina maneno yake katika vitabu vyote vitatu,
1. Imani yenu iko wapi 2.
enyi wa Imani haba 3. Hamna imani bado ?”).
Kwa anayetazama mambo kwa jicho la tatu kama mimi, kuna kitu anajifunza
hapo, na miongoni mwacho ni hiki cha kiwango cha Imani na Sehemu ilipowekwa,
hali inayomaanisha kuwa ukimya wa Yesu ulikiwa ukiashiria usimamamizi wa Mtihani.
Walioenda shule walao hadi chekechea wanafahamu kuwa sura ya Mwalimu
wakati anafundisha ni tofauti na ile wakati akiwa anasimamia mtihani, na ujio
wa sura ya wakati wa kutoa matokeo unategemea na ujibuji au ufaulu wako wa
mtihani. Ukifeli utaona mikunjo ya ndita na hamaki ila ukifaulu utaona furaha
na tabasamu mwanana, linaloambata na jicho angavu .
Na yamkini umekuwa katika wakati kama huo, wa Yesu kulala kwenye
Shetri, Madamu umembeba mzima mzima kama alivyo, yakupasa sasa kuhakikisha
unamuasha kwani kwa kuukemea upepo na mawimbi kwa jina lake na sio kwa kupiga
yowe za kuogopa kuzama huku ukimwambia kuwa mbona unateseka na mapito na Yeye
yupo kimiya, akiamka katika hali hiyo atanga’aka juu yako na kukuuliza
ulipoiweka imani yako ila ukiukemea upepo na mawimbi ataamka na kukupiga tafu
huku akikupongeza na hakika hatakuita wa IMANIA HABA, MUOGA ama HUNA IMANI bali
atakupongeza kwa kukupa “BIG FIVE” ikiwa ni
ishara ya kufaulu mtihani kwani ukimya wake ulikuwa ni sura ya kusimamia
mtihani.
Natumai umependezwa na ujume huu uliokujia wakati muafaka na tayari
moyoni mwako umeshaazimia kuchukua hatua ambazo miongoni mwazo ni maombi ya kufunga
na kuomba yatakayokuwa na taswira ya maombi ya vita na yenye mamlaka ilengayo kuukemea upepo na dhoruba. Tumia
pia maandiko ya mamlaka ikiwemo lile la Petro alivyokabidhiwa mamlaka pale
kwenye Mathayo 16:19, Mathayo 10:1, Luka 10:19 pia Marko 16:16-18, huku ukijua kuwa Yesu
amekabidhiwa vyote na kama ndivyo ukiviitaji atakupa tena na zaidi; Mathayo
28:18. Usiyasahau na yale ya umbaji kwenye mwanzo.
Niombe kwa Mungu ili nifundishe mapema somo langu liitwalo, “NAMNA YA
KUTUMIA MALAKA KIBIBILIA.” Sio kwamba Mungu wa leo hatendi Ishara na miujiza
kama enzi za uandishi wa Bibilia, anatenda tena yamkini na kuzidi sema shida
ingalipo kwetu sisi ambao hatujui namna ya kuzitumia hizi malaka maana hata
wakina Petro walikuwa nazo ila hawakujua nammna ya kuzituamia na baadaye Petro
na Yohana walipojua ndipo yule kiwete waliyekwepo kwenye mlango mzuri wa kanisa
ama hekalu alipopona. Tuonane kesho Swaiba.
Usikose
makala ya Kesho itwayo NYUMA YA MLIMA.
Kama
hujaokoka na unataka kuokoa tafadhali fwatisha nami maneno haya kwa Imani,
Sema: BWANA YESU, NINAKUPENDA, NINAKIRI NA KAUMINI KUWA WEWE NI MUNGU, ULIKUFA
NA KUFUFUKA KWA AJILI YANGU, INGIA NDANI YANGU KAMA BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA
YANGU LEO, AMENI.
Hongera kwa
kuokoka na tafuta kanisa la watu waliokoka ukasali hapo.
Na Huduma ya
UKOMBOZI GOSPLE, Arusha Tanzania, Kwa Maombi, Ushauri, Maswali au Sadaka
wasiliana nasi, Barua pepe: ukombozigosple@gmail.com
Simu: +255 759 859 287 pia waweza itumia kwa M-PESA. Zaidi www.ukombozigosple.blogspot.com #UkomboziGosple #MwalimuOscarSamba
Pia #Like
#Penda Page/Ukurasa wetu au kundila Fb, ili kuupta habari hizi kwa haraka,
zaidi. Ug Ukombozi Gosple,
PAGE: https://www.facebook.com/Ug-Ukombozi-Gosple
Endelea kusoma makala nyingine.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni