Jumapili, 4 Juni 2017

AGANO LA CHUMVI,

KINACHOKUFANYA UNIOGOPE NI NINI

Mungu ameweka mfumo maalumu ambao ninauita “System” ya Mungu ya namna atakavyo watunza watumishi wake, na jambo hili ameliweka kwa mfumo wa Agano, na mimi nitakuchambulia kama lilivyowekwa. Ikumbukwe pia miongoni mwa masomo ambayo Mungu amenipa kuyafundisha ni yale ya kiagano ndani ya Bibilia na endelea kunifwatilai kwani yamkini siku moja nikapata kibali cha kukujuza baadhi ya maagano hayo ikiwemo Agano Jipya na nguvu yake kwani limekamilishwa kwa Damu na Mwili wa Krsto na tafsiri ya maneno ya Yesu katika Luka 22 anaposema kikombe hiki ni Agano jipya, Sanjari na kauli ya Kitabu kile cha Waebrania kinaposema ya kwamba Nguvu ya hilo Agano ipo kwenye mauti na sababu ya maagano ya kipepo yanayolenga familia kuwa na nguvu pale muhusika anapokufa.


Pia kwenye Bibilia yapo maagano kama lile la Daudi ambalo ni miongoni mwa maagano yenye nguvu na katika kitabu kile cha Yeremia Mungu ananishangaza anapolifananisha na Agano la Usiku na Mchana ambalo usipopekuwa Bibilia kwa jicho la Tatu huwezi kuliona hilo la Usiku na Mchana.
Pia lipo Agano la Nuhu, Agano lingine ni lile Musa alilofunga na Mungu nami naliita Agano la Mlimani. Kumbuka kuna maagano ya Mungu na yapo pia ya kipepo. Na mtu huweza kuingia agano na jambo hilo liwaka na matokeo kwa kizazi chake. Mfano Agano la Mungu na Ibrahimu linamatokeo pia kwetu.

Kwenye Agano kuna vitu wakadha wakadha ikiwemo Kiapo cha Uaminifu, Mfano Rahabu na wale wapelelezi walimwapia , na Mungu anasema kuwa amemwapia Daudi kwamba hata mwambia Uongo, Ndio maana watu wanapoenda kwa waganga hulazimika kuapa.

Pia Ishara, Agano la Mungu na Nuhu lilikuwa na Ishara ya Upinde wa Mvua, alikadhalika kwa upande wa Shetani, wengine Ishara zao huwa ni ugonjwa fulani ama hali fulani, ndio maama wengine Paka akilia usiku kwa sauti fulni, ama wakimuona mnya fulani na jamii nyingine huwa ni Kakakuona, ama Bundi ama Nyanyi.
Pia kwa wengine huwa ni aina fulani ya vifo. Huwa ni Ishara ya kuhitaji utimizwaji wa Agano hilo. Katika jamii ya kichaga kijana aliyefikia umri wa kufanyiwa mila asipofanyiwa huwa kuna aina fulani ya tatizo humpata na wazee hutambua kuwa ni matokeo ya agano la kipepo kutokutimizwa ila tuliokoka huko hatupo.
Ishara nyingine ni kuota ukiwa unakula Nyama za watu, Unakunywa damu, kuwa na watu walikokufa ama unafanya matambiko au unakula chakula.
Hii ni Ishara kubwa sana ya kwamba babu zako ama wazazi wako waliingia maagano na Mapepo na kama mtaalamu wa kiroho wa mambo haya ninakushauri kuyavunja maana ndoto hizo zitaadhiri hali yako ya kiro na kukupa mapooza ama usipochukua hatua za haraka utajikuta ukiwa mazito kwenda ibadani au kuanza kuwa mvivu kuomba na kusoma Neno na Mungu akikuotesha ndoto basi utaota ukiwa huu mzito kutembea, ama miguu inauma na kwa bahati mbaya wengine huugua kabisa miguu. Ndio maana kesi za magonjwa kama haya mimi huzishuhulikia kiroho zaidi na maandiko yake yapo.

Msomaji wangu hili sio soma la Maagano, ila nimeguswa kukupa utangulizi huo mpana na huwenda nikaandika kitabu kiitwacho NGUVU YA MAAGANO KIROHO, Ila wakati nakuandikia utangulizi huu Mungu amenipa kibali cha kukuandikia makala ya kuwanasua watu wanaoota ndoto wanakula vyakula na wale waliyopo kwenye vifungo vya kipepo vya kimaagano.

Turejee kwenye kiini ama mukutadha wa somo letu ambalo linazungumzia Agano la Chuvi ikiwa ni miongoni mwa maangano yakimungu ndani ya Bibilia.
Kwanza fahamu ya kwamba Agano ni mapatano kati ya pande mbili ama zaidi yenye makubaliano ndani yake, na makubaliano hayo huwa na mashariti ambayo ni lazima yafwatwe na matoke ya kufwatwa na madhara ya kutokufwatwa.
AGANO LA CHUMIVI, Nia Agano ambalo Mungu aliingia na Haruni pamoja na nyumba yake, Lenye matokeo na kwa Wana wa Walawi. Na leo hawa ni watumsihi wanaohudmu madhabauni. Makuhani ama watumishi wenye Wito ule wa huduma tano.
Na kama Mungu alifonga na Haruni na Nyumba yake ni fika kwamba Mustakabali mzima wa maisha ya Mchungaji huwa na matokeo pia kwenye familia yake. Maana yake ni hii Mchungaji, Mwalimu, Mtume, Mwinjilisti ama Nabii akikaa kwenye nafasi yake vyema huweza na familia yake hunufaika ila asipokaa basi na familia yake huteseka.
Na Agano hili ndilo linalotoa muongozo na utaratibu wa kuwatunza watumishi wa Mungu, kabla ya kukupa andiko la udhibitisho pia fahamu ya kwamba Mtumishi wa Mungu huweza kuishi maisha magumu kiuchumi na sababu ikawa ni nje ya hili na yaweze kuwa ni Mapito, Vita ama Uonevu wa Adui. Kwa sababu hizo fwatilia somo langu kwenye “internent” lililopo kwa njia ya Sauti na Video liitwalo; “SABABU 4 ZA MAJIRA MAGUMU KWA WATU WALIOKOKA,” Ingawaje kwenye somo nilitoa 5.
Tuchunguze maandiko. Hesabu 18: 19 Sadaka zote za kuinuliwa za vitu vitakatifu, wana wa Israeli wavisongezavyo kwa Bwana, nimekupa wewe na wanao na binti zako pamoja nawe, ni haki yenu ya milele; ni agano la chumvi la milele mbele za Bwana kwa ajili yako, na kizazi chako pamoja nawe.
20 Kisha Bwana akamwambia Haruni, Wewe hutakuwa na urithi katika nchi yao, wala hutakuwa na fungu lo lote kati yao; mimi ni fungu lako, na urithi wako, katika wana wa Israeli.
21 Na wana wa Lawi, nimewapa zaka yote katika Israeli kuwa urithi wao, badala ya huo utumishi wautumikao, maana, ni huo utumishi wa hema ya kukutania.

Mungu analiita Agano la Chumvi, hapo tunamuona Mungu akiwapa Uridhi wa Sadaka, na kila kinachotolewa madhabauni, pamoja na Mungu kutamka bayana ya kwamba hawatakuwa na uridhi popote pale bali Yeye wenyewe ndiye fungu lao, na urihi wao. Na analiita kuwa ni Agano la milele.

Sasa nisikilize ili nikusaidiye, Wana wa Lawi na Nyumba ya Haruni hakuna jinsi wangefaya biashara ama kuamua kulima Zabibu ama Tini na kufanikiwa. Maana tayari Mungu ameshawawekea mfumo wakuwalisha.
Kusudi la Mungu kufanya hivyo ni ilikuwafanya wawe “concentrated ” ama “busy” na kazi yake.
Leo hii wapo Watumishi wanofanya utumishi huku wakiwa nje ya mfumo wa Mungu aliowaitia, na wanashangaa kila wanachokifanya kinagoma. Ndiposa watumishi walioitwa na kukaidi ama kuchelewa kuitika wanajikuta kila kitu wanachokifanya kinagoma, hii ni dalili ya Mungu kuwajuza ya kwamba lipo Agano nililofanya na Walawi na Haruni na wewe ni sehemu ya Agano hilo kwa hiyo badili Fikra zako na nitazame mimi kwani mimi ni fungu lako na huna uridhi tena katika shuhuli nyingine yoyote ile.
Kuna siku wakati ninaitwa niliota ndoto ya kuwa kuna mtu ambaye sikumuona sura alifungua mlango nakunipa Chumvi kipakiti kimoja cha kama gramu mia, (kama nipo sahihi kwa kipimo hicho), na kunipa nyingine iliyokwepo kwenye katoni kubwa huku nikiitumia ile pakiti moja na kisha kuanza kutumia ile nyingine baada ya muda.

Nilitambua ya kwamba ni MUNGU anajaribu kunigusia kuhusu Agano hili, na anitaka nimtazame Yeye kama fungu langu na uridhi wangu. Watumishi wengi wanakwama hapa, mimi nilijaribu kufungua biashra mara baada ya kufukuzwa kazi huku dhamira yangu ikiwa ni njema tu, ila kila biashara ilidumaa na kisha kufa.

Ni kweli sio jambo dogo kuuelewa mfumo huu ila Mungu akuongoze ili kuuishi vyema maana hakika hutafanikiwa nje ya FIKRA hizi za Mungu za kukutunza. Mungu wakati ananifundish jambo hili alinipa mfano wa ajabu sana. Aliniambia; Eliya alikuwa na Upako wa kufunga mvua kwa muda wa miaka mitatu na nusu, na kuifungulia na maandiko yanasema kwa neno lake, ikiwa na maana alifanya hivyo bila kushauriana na Mungu na Mungu aliona ni vyema.

Ila hakuwa na upako wa kuamua namna atakavyo ishi kiuchumi ama ale nini. Bali kula kwake na kuisihi kwake kulitegemea maelekezo rasmi ya Mungu. Mfano ilimpasa kutulia kwenye kijito cha Kerithi mahali ambapo Mungu alimpangia. Pili kunguru alitumwa kumletea chakula, ingalikuwa ni uamuzi wa Eliya asingali kubali kulishwa na kunguru. Ndivyo ilivyo leo kwani wapo watumsihi wanaotunzwa na watu ambao kibinadamu watumishi ndio waliopaswa kuwatunza.
Tatu, alipaswa kulishwa na mwanamke mjane, ambapo kiuwalisia ilikuwa ni jambo gumu. Sasa jiulize Swali hili; Nini kingalitokea kama Eliya angegoma kuishi kwenye kijito kile cha Kerithi?, ama kulishwa na kunguru na kuhitaji kujilisha mwenyewe? 3, Kama angegomea maelekezo ya Mungu ya kwenda kwa mwanamke mjane wa Serepta?

Huo ndio mfumo ambao Mungu alimuekea Eliya. Na Eliya aliishi vyema katika huo mfumo, na wewe yakupasa utambuwe mfumo ambao Mungu amekuwekea na usiishi kwa mazoea, ingawaje mara nyingi Mungu hapendelezwi na watu wake kufanya biashara ila wapo wachache ambao wamepewa mfumo huo. Ikiwemo Paulo Mtume, kuna wakati alishona mahema ili kujipatia riziki.

Mfumo wa Yesu ulimpa kibali cha kufungua kinywa cha samaki ili kujipatia fedha ya kodi, Mitume wa kanisa la kwanza walilishwa na wapendwa waliouza mashamba yao, viwanja na hata nyumba. Nikusihi sana kumuhji Mungu kuhusu mfumo aliokuweke na mimi sijakuzuia kulima, ama kushona mahema kama Paulo Mtume ama kufanya biashara kwani wapo Watumshi walibaatika kupewa hivyo ingawaje wengine wamepewa Sadaka, ama Zaka kama ilivyokuwa kwa Walawi na wana wa Haruni.

Jambo muhimu hapa ni kumsikiliza Mungu, na Mungu huweza kukupa mfumo kwa muda fulani na kisha kuubadilisha, mfano Mama Mcuungaji ama mama Mwalimu huweza kufanya biashara fulani kwa muda na mara baada ya huduma kukua Mungu akaamua kubadilsha mfumo na kukupa Zaka na vitu visongezewavyo madahabauni. Ikifikia hapo tambua kwani Paulo hakushona mahema nyakati na siku zote, wala Elia hakukaa kwenye kijito siku zote.
Tatizo kubwa ni kwamba kwa wapendwa wa leo kijito kikikauka wanabaki hapo, wanasahau kuwa ni majira ya kulishwa na kunguru ama mwamke Mjane wa Serepta.

Maana yangu ni hii, kama ulikuwa unafanya jambo fulani na limegoma jua kijito kimekauka na msikilize Mungu, kwani wengi hukimbilia maombi ya vita ili kumpinga Shetani. Ni kweli kuna wakati ni Shetani ila pia upo wakati ambo ni Mungu.

Jaribu kujiuliza Swali hili; Nini kingalitokea kama Eliya angefanya maombi ya vita ili kijito kijawe na maji? Hakika angekwama na jina la Mungu lingaliweza kutukanwa.

Nisikize mama Mchungaji na mtoto wa mchungaji, ama mwinjilsiti au Nabii unayenisikiliza. Maisha yakiwa magumu huku mkimtumikia Mungu haimaanishi kuwa Mungu amewaacha bali yakupasa kumsaidi mumeo ama baba yako katika kumuhoji Mungu na yafaa umuombe kwa kina awasaidiye mtambuwe mfumo anaotaka kuuishi. Suluhu sio kujuta kwa baba ama mumeo kuitwa au wewe kuolewa na huyo mwanaume ama kuwa mwana kwenye hiyo familia, bali ni wewe kujua kijito kimekauka na muhoji Mungu; Unataka niende wapi ama nifanye nini?. Msaidiye mumeo kubeba mzigo, kumbuka Agano hili la Chumvi ni kwa ajili ya Haruni na nyumba yake maana yake na wewe ni sehemu ya utambuzi ama Suluhu ya jambo hili.

Ni maliziye na mfano wa mama mchungaji mmoja jana yaani juzi ya leo alionipa kwa kuniambia kuwa amekuwa na wakati mgumu kiuchumi na kiafya na wakati akienda hospitalini alitamka maneno magumu ikiwemo ya yeye kujiuliza alipotoka na huyo mwaoume. Yaani anajuta kuolewa naye. Nilimuelewa kiundani sana na nilifahamu kiini cha jambo hili. Mimi nimeanza kuiombea hiyo familia ya kwamba Mungu awasaidiye wakae kwenye mfumo sahihi.
Kumbua pia kutokutumika ama kuwa Yona ni sehemu ya kukaa nje ya Agano. Nina mengi ya kukujuza ila Muda umenitupa Mkono tuonane kesho kwenye makaa nyingine yenye taswira ya kiagano. Ila niombi langu kwa washirika kuwaombe watumishi wao ili wakae kwenye Agano hili maana wanaweza kuwa na Mtumishi mwenye Upako wa kuuponya UKIMWI ila anaishi nyumba ya mabanzi ama mwenye upako wa kufufua wafu ila watoto hawana ada. Mkumbuke Eliya, Upako wake haukumletea chakula bali mfumo sahihi ndio uliyomtunza.

Kama hujaokoka na unataka kuokoka ama ulirudi nyuma kiroho na unataka kutengeneza na BWANA kwa upya leo, tafadhali fwatisha nami maneno haya kwa Imani, Sema: BWANA YESU, NINAKUPENDA, NINAKIRI NA KUAMINI MOYONI MWANGU KUWA WEWE NI MUNGU, ULIKUFA NA KUFUFUKA KWA AJILI YANGU, INGIA NDANI YANGU KAMA BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YANGU LEO, AMENI.
Hongera kwa kuokoka na tafuta kanisa la watu waliokoka ukasali hapo.

Na Huduma ya UKOMBOZI GOSPLE, Arusha Tanzania, Kwa Maombi, Ushauri, Maswali au Sadaka wasiliana nasi, Barua pepe: ukombozigosple@gmail.com  Simu: +255 759 859 287 pia waweza itumia kwa M-PESA. Zaidi www.ukombozigospel.blogspot.com   #UkomboziGosple  #MwalimuOscarSamba
Pia #Like #Penda Page/Ukurasa wetu au kundi la Fb, ili kupata habari hizi kwa haraka, zaidi. Ug Ukombozi Gosple,                                                                                       PAGE: https://www.facebook.com/Ug-Ukombozi-Gosple                                               
Pia kwenye mtando Mpya wakitanzania wa                                                                                 2 DAY SKY: https://www.2daysky.com/home


 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni