Mwalimu Oscar Samba akifundisha katika semina jana hapa Morombo Arusha Tanzania |
Na Mwandishi
wetu, Ug Ministry.
Ninakukaribisha
katika jina la Yesu Kristo Bwana wetu na Mwokozi wetu katika sehemu hii ya 5 ya
ujumbe wetu kama alivyofundisha Mwalimu jana kwenye semina inayofanyika hapa
mkoani Arusha kwenye viwanja ya Morombo nchini Tanzania.
Kama ilivyo
ada alianza kwa kutoa msisitizo kwa watu kuutafuta kwanza ufalume wa mbinguni
na haki yake na kisha hayo mengine ikiwemo ya uchumi ama utumishi
watazidishiwa.
Mwalimu wetu
alitoa utangulizi uliyolenga kuwakumbusha wanafunzi wake mahali aliponzia tangu
siku ya kwanza na kusema ya kwamba alitamani kugusia somo la Agano la Chumvi
ili kuwasaidia watumishi wa Mungu maana ni Agano la kitumishi ila kwa jana
hakupata kibali ila siku ya mwisho ya semina huenda akakipata na ikumbukwe kuwa
hasemi jambo kwa akili zake bali hunena lile ambalo Roho anataka alinene kwa
wakati gani na sehemu gani.
Jana
alizungumzi mbinu moja teule nayo ni MALANGO au LANGO, aliwataka watu kuvuta
taswira ya mlango au geti ambalo lina kuwa na dhima ama jukumu la kumruhusu mtu
kuingia au kutoka na pia ukifungwa humzuilia kuingia au kutokuingia.
Alikadhalika kwenye ulimwengu wa roho ndivyo ilivyo ili Baraka za kiuchumi
zimfikiliye mtu ni lazima zipitiye katika mlango wa rohoni. Alisema zaidi
kuhusu swala hili waweza kutafuta kitabu chake cha MALANGO KWENYE ULIMWENGU WA
ROHO, punde kitokapo.
Alibainisha
kwamba yapo malango ya aina mbili, ya kwanza ni yale ya dhambi na ya pili ni ya
Baraka ambayo ndiyo aliyoyazungumzia kimapana zaidi jana. Ya dhambi alitoa
mfano kwa Kaini pale Mungu alipomwambia kuwa dhambi inakuotea mlangoni ya
kupasa uishinde, na maandiko kwenye kitabu kile cha Waefeso 4:27 wala msimpe
Ibilisi nafasi.
Maana yake
kubwa hapo nikutokumpa Shetani mlango maana kabla Yuda hajamsaliti Yesu
maandiko yanasema ya kwamba alitafuta nafasi, yaani alitafuta mlango, kwa hiyo
kwa Yesu kuna mlango uliokuwa wazi uliyompa nafasi Yuda ya kufanya jambo lile
ama Shetani kupitia Yuda. Alibainisha ya kwamba Yuda mwenyewe alikuwa ni
nafasi, maana likuwa ni mtumishi ama mtu wa karibu kwa Yesu. Ndio maana kwenye
ndoa mwanandoa mwenzako anapokutamkia neno baya kama la kutokufanikiwa huwa na
nguvu maana yeye ni mlango na ametumika kama lango la dhambi au uaribifu, ndio
maana pia ni hatari sana kama mtumishi atakuwa na watumishi wasaidizi na mmoja
wapo akawa kinyume naye, maana yake anafanyika lango kwenye ulimwengu wa roho lilola
uaribifu, kama Yuda.
Tuingiye
sasa katika lango la Baraka ambalo ndilo kiini cha somo letu siku ya leo, Ili
Mungu kukubariki ni lazima lango lako liwe wazi na kama limefungwa lifunguwe
kwa maombi.
Tuyaone
malango kibibilia kabla ya kukujuza mifano ya hayo malango; Isaya
60: 11 Malango yako
nayo yatakuwa wazi daima; Hayatafungwa mchana
wala usiku; Ili watu wapate kukuletea utajiri wa mataifa, Na wafalme wao
wakiongozwa pamoja nao.
Maana yake
utajiri unapaswa kupitia kwenye hayo malango, Fungua nami kitabu kile cha Mwanzo
22: 17 katika kubariki
nitakubariki, na katika kuzidisha nitauzidisha uzao wako kama nyota za
mbinguni, na kama mchanga ulioko pwani; na uzao wako utamiliki mlango wa adui
zao;
Umeona hilo
jambo hapo, anasema kuwa uzao wako utamiliki malango ya adui zako, kwa hiyo ili
kuwa tajiri mtu uliyeokoka yakupasa kumiliki malango ya adui zako.
Andiko
jingine ni lile la Rebeka mkewe na Isaka wakati anaagwa, (Send-off, kwa lugha
ya leo), wazazi wake na jamaa yake walimtamkia baraka tele ikiwemo ya kumiliki
malango ya adui zake. Ndiposa Mwalimu akasema ni jambo la muhimu sana kumtamkia
baraka binti yako ama mwanao wakati wakumuaga maana ukimuaga na manung’uniko
yataambata naye na wasipojua kuyatangua rohoni huweza kuwasumbua daima. Na
jambo hilo ni la kweli maana kama kwa Rebeka maneno ya mwisho ya wazazi na
nduguze yalikuwa na nguvu hiyo ni fika kwamba hata mabaya huwa hivyo.
Tutazame
maneno hayo na ninataka upate uwakika ya kwamba malango yapo kiroho kweli, Mwanzo
24: 60 Wakambarikia
Rebeka, wakamwambia, Ndugu yetu, uwe wewe mama wa kumi elfu, mara elfu nyingi,
na wazao wako waurithi mlango wa hao wawachukiao.
Kwenye Isaya
tumeona malango kuwa wazi, kwa Ibrahimu kumiliki ya adui, na kwa Rebeka tunaona
ya kuridhi malango ya adui.
Huu ulikuwa
ni unabii wa kuja kuimili Kanani na
utajiri wake, kwa hiyo ni fika ya kwamba umekubaliana na Mwalimu ya kwamba
ni kweli malango yapo.
Tuyadodose
hayo Malango sasa, Lango la kwanza ni Urithi, tumeona watoto wengi wa
viongozi nao wakiwa viongozi, wa wafanya biashara nao wakiwa wafanya bisahara,
kwa bahati mbaya kwa lango baya wale wa kahaba nao wapo wanaokuwa makahaba.
Ukiona hivyo
jua ni swala la urithi, Isaka na
hatimaye Yakoo walirithi Baraka, yule mwana mpotevu alirithi Baraka kutoka kwa
wazi wake. Hata kama wazi wako wasipokupa mali ama hawapo, lango hili
hukurithisah kitu kilichopo ndani yao.
Lango
jingine ni NDOA, maisha ya mtu kabla
hajaoa na baada ya kuoa kwake huwa tofauti, kwani lango hili hupitisha Baraka kama
litakaa salama, ndio maana hata afya yake, uchumi wake na maisha kwa ujumla
hunawiri. Ila kama ndoa hiyo ikiingiliwa na migogoro shetani huligeuza lango
hili na kupitishia hapo balaa na mikosi ndio maana wanandoa wakigombana kila
kitu kinagoma ikiwemo uchumi, ukiona hivyo jua fika ni kwamba Shetani
ameligeuza nakulitumia kama lango la dhambi laana au uaribifu kama
nilivyokujuza aina hiyo lango hapo awali.
Katika lango
la Baraka ukisoma maandiko ya Isaka wakati anaona, tunamuona Ibrahimu akimbariki
Isaka na kumrithisha mali yake baada ya Isaka kuoa, maana yake lango hili ndilo
lilopitisha Baraka zake. Ndio maana kabla ama wakati wakuoa Shetani huleta vita
kwa watu, hapa Shetani hana shida na Ndoa yako bali ana shida na Lango hili
maana anajua litapitisha nini. Ndio maana akishindwa kuwazuia kuoana
atahakiksha anapenyeza migogoro kwenye hiyo ndoa ili alitumie lango hili kama
la uaribifu.
Lango lingine
ni WAZAZI, wanayo nguvu kubwa sana
katika kuyabariki maisha yako, wapo watu wanaoishi maisha magumu kwa sababu ya
kutokupata Baraka za wazazi. Tazama maisha ya Yakobo, na Esau, yalikuja kuwa
tofauti na nduguye kwa sababu ya kuzipata Baraka za wazazi. Na wewe hakikisha
unawaendea wazazi na ukiweza andaa sadaka ama zawadi kisha piga wagoti mbele
yao waombe msamaha kwa lolote ulilowai kuwakosea yamkini ukiwa mdogo kisha
waombe wakuwekee mikono ya Baraka.
Jingine ni ARIDHI,Lango hili ni la ajabu sana na
ni wachache wanajua kulitumia, sehemu unayofanyia biashara ina nguvu kubwa sana
ama kazini kwako. Na hata nyumbani, hiyo aridhi ikifungwa ni dhairi kwamba hata
uchumi wako utafungwa. Ndio maana wachawi wakija hunena maneno kwenye hiyo aridhi
ama wanaoenda kwa waganga huelekezwa kuchota udongo hapo ama kuchimbia hapo
vitu. Lango hili likiwa limefungwa lifunguwe kwa maombi ya rehema kisha tangua
maneno na ufute na kuangamiza kila kilicho cha kipepo hapo.
Musa aliitajika
kuisogelea aridhi ambayo Mungu anaiita ni Takatifu, Mungu angeweza kuzungumza
naye akiwa mbali maana kama aliweza kuisikia sauti ya vua viatu ni fika
angeweza kusikia maelekezo ya Wito wake, ila Mungu alimtaka aisogelee ile
Aridhi ambayo kiroho ilikuwa ni Lango, maana tayari ni Takatifu na lango hilo
ndilo lilokuwa na nguvu ya kupitisha kile ambacho Mungu alikusudia ndani yake
kipite.
Na wewe
hunabudi kuhakiksiha aridhi unayofanyia biashara ama kuishi inakuwa takatifu
ili Mungu awezekupitisa Baraka ama riziki zako kwa siku ya leo kesho na
kadhalika.
Lago jingine
la mwisho kama alivyofundisha Mwalimu jana ni MBINGU AMA ANGA , Mwalimu Samba alisemakuwa kama Anga lako
limefunwa ni hakika hutaweza kupokea Baraka zako. Kwani Danieli wakati anatia
nia ya maombi, alishapewa majibu yake, anaingia kwenye maombi tayari akiwa na
majibu yake, ila hayakumfikia kwa sababu mkuu wa uajemi alikuwa amekaa kwenye
lango hili na malaika mwenye majibu alishindwa kupenya ama kupita hapo mlangoni
kwa sababu ya mlango kufungwa. Ila Danieli alifanya maombi ya sku 21, yaliyolenga
kufungua Anga lake.
Alitoa mfano
wake ya kwamba kuna siku alikuwa anapita mahali pa gumu sana kimaisha na aliona
njozi akiwa ndani kwake kwamba kuna ndege anapasua dari “silingbodi,” na alikuwa
na kitu cheupe mdomoni: Alifahamu fika ya kwamba ile ametumia nguvu kupenya
kuna shida kwenye Anga lake. “Na wewe
ukina hivyo yakupasa ulifnguwe.” Mwalimu alifafanua.
Alisoma
maandiko kwenye kitabu cha Zaburi yaliyosadifu dhairi shairi ujumbe huo,
Zaburi 78: 23 Lakini
aliyaamuru mawingu juu; Akaifungua milango ya mbinguni;
24 Akawanyeshea mana ili wale; Akawapa nafaka ya mbinguni.
25 Mwanadamu akala chakula cha mashujaa; Aliwapelekea chakula cha kuwashibisha.
24 Akawanyeshea mana ili wale; Akawapa nafaka ya mbinguni.
25 Mwanadamu akala chakula cha mashujaa; Aliwapelekea chakula cha kuwashibisha.
Tunaonah apo
ili Mungu kuwapa chakula wana wa Iziraeli walikuwa jangwani ilimbidi ayaamuru
Mawingi, ikiwa na maana yalikuwa na nguvu fulani, kisha akaifungua milango ya
Mbinguni, maana yake Angani ama Mbinguni ipo milango, na ikifungwa hutaweza kupitishiwa
Baraka au riziki kwenye biashara yako kama atakavyo Mungu.
Baada ya
Mungu kuifungua, mstari unaofwata tunaona matokeo yake ikiwa ni watu hawa
kupata chakula, kwa hiyo milango hiyo ilipitisha MANA, Soma tena hiyo mistari…
Natumai umenata taswira halisi hapo.
Kwa hiyo kuna
wakati tunamlaumu Mungu kwa kutokutubariki kumbe tatizo sio kwake kwani alisha achilia
baraka kama ilivyokuwa amekwisha kuachilia majibu kwa Danieli ila wakuu wa anga
wakipepo wamekaa kwenye hilo lango na Baraka haziwezi kupenya. Kwa hiyo ni
wangu wito kukutaka kuwa mwepesi wa maombi ya vita ili kufungua anga lako
ikiwezekana ombea malango yako ya Baraka kila siku. Lango jingine ambalo jana
hakulitaja Mwalimu ni lile la juzi ambalo ni Agano, alisema jana kwamba Agano
huweza kufanyika lango la Baraka ama dhambi au uaribifu na huwa hivyo kama ni
la kipepo ila la kimungu kama lile la Ibrahimu ni lango la Baraka kwetu.
Usikose kutazama
video yake kwenye YouTube Channel yetu ya Ukombozi Gospel, pia jana Mwalimu alibainisha
pasipo kificho ya kwamba ni vyema kuokoka, na fahamu somo hili ama mbinu hizi
teule za kutoka kwenye umasikini haiziwezi kuwa halisi kwako kikamilifu kama
huja okoka, kwa hiyo yakupasa kuokoka ili ukifa pia leo uweze kwenda Mbinguni.
Kama
hujaokoka na unataka kuokoka ama ulirudi nyuma kiroho na unataka kutengeneza na
BWANA kwa upya leo, tafadhali fwatisha nami maneno haya kwa Imani, Sema: BWANA
YESU, NINAKUPENDA, NINAKIRI NA KUAMINI MOYONI MWANGU KUWA WEWE NI MUNGU,
ULIKUFA NA KUFUFUKA KWA AJILI YANGU, INGIA NDANI YANGU KAMA BWANA NA MWOKOZI WA
MAISHA YANGU LEO, AMENI.
Hongera kwa
kuokoka na tafuta kanisa la watu waliokoka ukasali hapo.
Na Huduma ya
UKOMBOZI GOSPLE, Arusha Tanzania, Kwa Maombi, Ushauri, Maswali au Sadaka
wasiliana nasi, Barua pepe: ukombozigosple@gmail.com
Simu: +255 759 859 287 pia waweza itumia kwa M-PESA. Zaidi www.ukombozigospel.blogspot.com #UkomboziGosple #MwalimuOscarSamba
Pia #Like
#Penda Page/Ukurasa wetu au kundi la Fb, ili kupata
habari hizi kwa haraka, zaidi. Ug Ukombozi Gosple,
PAGE: https://www.facebook.com/ugukombozigospel/
Pia kwenye mtando
Mpya wakitanzania wa
2 DAY SKY:
https://www.2daysky.com/home
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni