Leo hapa kwa Morombo Mwalimu Oscar Saba ameanza huduma rasimi katika huduma aliyoiasisi ya Ukombozi Gospel ama Ug Kwa Kifupi.
Na utajionea picha mbali mbali za matukio yaliyojiri mahali hapo.
Ujumbe wa leo ama wa Semina hii unatoka kwenye kitabu chake cha Tajirika kibibilia uitwao, "Mbinu Teule zitakazo wawezesha watu waliokoka kutoka kwenye Umasikini"
Mwalimu alianza kwa kusema kuwa watu wengi waliokoka leo wanaishi maisha ya umasikini ikiwa ni matokeo ya wao kutokutambua kuwa zipo kanuni zinazoweza kuwakwamua kutoka kwenye hali hiyo.
Alianza kwa kuwataka watu waliokoka kuutafuta kwanza Ufalume wa Mbinguni, huku akifafanua lile andiko la Yohana kwa Gao ya kwamba afanikiwe katika mambo yote kama vile roho yake ifanikiwavyo, alisema Bibilia ya kingereza imetumia neno Nafsi, ikiwa na maana ya kwamba ni kama vile nafsi yake ifanikiwavyo.
Alisem pia Mungu anamtaka huyu mtu ama maombi haya ya Yohana yanamtaka Gao afanikiwa kama roho ama nafsi yake ifanikiwavyo ikiwa na maana ya kwamba Mungu anataka tufanikiwe kwanza rohoni, Kisha ndipo tufankiwe mwilini.
Huku akiongeza kwamba shida kubwa ya wapendwa wa leo wanapenda kufanikiwa kwanza mwilini ndipo waje wa fanikiwe rohoni, ila Yohana ana sema ni kama vile roho ifanikiwavo, maana yake roho ya mtu anayehitaji haya maombi ni lazima iwe imefanikia.
Aliwataka wapendwa kuutafuta kwanza Ufalume wa Mbinguni ndiposa wafanikiwe rohoni kisha mwilini watafanikiwa. Kanuni hiyo ya Ufalume wa Mbinguni hakuigusia kiundani leo bali alisema anajenga msingi katika baadhi ya mada kisha kesho ataanza nayo. Kanuni hiyo inapatika kwenye kitabu kile cha, Mathayo 6:33 Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa.
Na kabla ya Kanuni hiyo aligusia mambo makuu mawili ikiwemo la MUDA, alisema maisha ya mafanikio ya mtu aliyeokoka yamefungwa katka muda, ndiposa Yakobo hakufanikiwa nje ya miaka 20, na Wana wa Iziraeli walikaa jangwani,
Tuanze na maandiko ya Yakobo ambayo anayabaisnisha hayo wakati alipokuwa akinena na mjomba wake yaani Labani.
Pia alisema katika swala la Mda ya kwamba wana wa Iziraeli walikaa jangwani mika 40, kwa hiyo wasingaliweza kufanikiwa nje ya huo mua. Kumbukumbu la Torati 8:2 Nawe utaikumbuka njia ile
yote Bwana, Mungu wako aliyokuongoza miaka hii arobaini katika jangwa, ili
akutweze, kukujaribu kuyajua yaliyo moyoni mwako, kwamba utashika amri zake, au
sivyo.
Jambo lingine lilikuwa ni mapito,Alibainisha ya kwamba Mungu kabla ya kutubariki ni lazima atupime kama kweli hizo baraka tutazimudu ama zitatutoa kwa Yeu kama tukizipata, na njia pekee ya kudhibitisha hilo ni mapito kama Shule na majaribu kama Mtihani. Amelifafanua hilo katika andiko hilo la Torati, (8:Nawe utaikumbuka njia ile
yote Bwana, Mungu wako aliyokuongoza miaka hii arobaini katika jangwa, ili
akutweze, kukujaribu kuyajua yaliyo moyoni mwako, kwamba utashika amri zake, au
sivyo.).
Alisema kuwa hilo andiko hapo linasema kwamba Mungu aliwapitisha ili awatweze, kuwapima ma kuwajaribu ili ajuwe kama watashika amri zake au la, kwa hiyo ndivyo ilivyo kwa watu waliokoka ni lazima wapimwe ili Mungu kujiridhishe kama watazishika amri zake mara baada ya kubarikiwa.
Kwa mujibu wa Mwalimu ni kwamba hatupaswi kumuacha Mungu mara baada ya kubarikiwa ikiwa huo ndio msisitizo mkuu katika somo ili huku akiwa na lengo la kuwataka wapendwa kufanikiwa ila mafanikio hayo yawadumishe kwa Yesu, alibainisha ya kwamba kufanikiwa kwa mpumbavu ni kuingamiza nafsi yake.
Ndiposa Mungu huwataka waliokoka kuutafuta Ufalume wa Mbinguni kwanza na haki yake. Alisema neno haki ni la kisheria, kwani hakuna haki bila Sheria, na kwenye Sheria kuna kanuni, Ndiposa yeye Mungu amemtuma kuja kuwapa kanuni, ili kuacha mtido wa kutafuta fedha kwanza badala ya Mungu kwanza.
Ninakuitimishia na mfano alioutoa wa mfalme Sulemani; Aliomba, Moyo wa Akili, Pili Maarifa na Tatu Hekima ila MUNGU alimpa na Utajiri. Kwa nini?
Sababu aliutafura kwanza Ufalume wa Mbinguni na hayo Mengine yote Mungu aliyatenda, Mpendwa ni yangu rai kuunga na Mwalimu kesho kwenye Live Facebook ili kupa mafundisho hayo moja kwa moja na kutembea akauti yetu ya Clip ili kusikiliza mafundisho hayo kwa njia ya sauti.
Kila la heri tukutane tena Keshoa, Na sasa tazama Picha
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni