Mwalimu Oscar Samba akifundisha |
NA Mwandishi Wetu, Ug Ministry. |
Leo ni siku ya tatu ya ujumbe wetu huu Mubashara kama ulivyofundishwa na Mwalimu wetu kwenye Semina ya Mkutano wa Neno la Mungu inayoendelea ikiwa ni siku 8, hapa Mkoani Arusha nchini Tanzania kwenye viwanja vya Morombo.
Jana Mwalimu
alianza kwa msisitizo kwenye andiko ambalo Mungu ametupa kutembea nalo kwenye
semina hii nzima la kuutafuta kwanza Ufalume wa Mbinguni na Haki yake na kisha
hayo mengine yote tutazidishiwa. Ni Mathayo 6:33.
Alisema kuwa
inampasa kila mwana wa Nuru kuutafuta kwanza Ufalume wa Mbinguni na haki yake
kisha Mungu atamzidishia akirudia mfano wa Mfalume Sulemani wa kumtafuta kwanza
Mungu kwa kumuomba Moyo wa Hekima, Akili, Maarifa na kisha Mungu kumpatia hivyo
vyote huku akimpa na Fedha. Kwa sababu alitafuta kanuni au mbinu teule ilizomuwezesha
kutoka kwenye umasikini.
Mbinu
aliyoanza nazo jana mara baada ya utangulizi huo ilikuwa ni Mbinu ya 3, “FANI”
au UJUZI, Alibainisha, “Fani au Ujuzi ni kitu muhimu sana ambacho humsaidia mtu
kupata fedha ama kujikwamua kutoka kwenye umasikini”
Alielezea
kiini cha pwenti hiyo; “Msingi mkubwa wa pwenti hii ni siku moja nilikuwa innatoka
kanisani, jirani ama karibia na kufika nyumbani, nilimuona fundi umeme akiwa amevaa
varoli lake, ndipo Roho Mtakatifu akaniambia, ‘Mwanangu huyu mtu anaishi mjini
kwa fani yake ya ufundi umeme’, nilitulia kimya ili kujua nini Roho ananiambia,
alisema; ‘Tatizo watoto wangu hawalitambui hili. Wakisha okoka wanataka kuishi
kwa imani, bila kujua imani bila matendo imekufa’. Mara baada ya ujumbe huo
sikupoteza muda bali nilichukua kalamu na dafutari kisha kuanza kuandika ujumbe
ule na kuweka kwenye kitabu changu”
Aliwataka
watu waliokoka kuhakikisha ya kwamba wanakuwa wepesi wakuwa na fani au ujuzi
ili uwawezeshe kujikwamua kimaisha.
Alisema
ujuzi waweza kuwa ni udakitar, udereva, ama ufundi wowote ule. Ilikuwa ni rai
yake kuwataka vijana kutokupoteza muda na wazazi wao pia bali wawasomeshe
watoto kama Mithali inavyowataka kumshika sana elimu. Alitoa pia mfano wa Paulo
mtume aliyekuwa mtumishi wa Mungu wa madhabauni ila alikuwa na fani ya kushona
mahema, iliyomsaidia. Na katika hili aliwataka hata wale wenye wito wa
kumtumikia Mungu kuhakikisha wanakuwa na ujuzi kwani utawasaidia. Alitanabaisha
kwamba unaweza kuitwa 2010 ila Mungu akataka utumike 2030, na kuhoji hapo
katikati utakuwa ukila nini?.
Onyo lake lilielekea
kwa wale wanaosikia kuitwa nakutaka kuacha Shule, huku akiwaambia ni kosa bali
watafute hekima ya Mungu katika hilo.
Mbinu
nyingine ya 4, ni KIPAWA/KARAMA au KIPAJI, Mwalimi alisisitiza sana ya kwamba
mafanikio ya mtu yamefungwa kwenye kipawa ama kipaji au karama ambayo Mungu
amempatia. Alisoma maandiko yafwatayo.
Mithali 17: Kipawa
ni kama kito cha thamani machoni pake yeye aliye nacho; Kila kigeukapo
hufanikiwa.
Pia aliambatanisha
na hili hapa; Mithali 18: Zawadi ya mtu humpatia nafasi; Humleta
mbele ya watu wakuu.
Alisema ya
kwamba kipaji au kipawa humuwezesha mtu kukaa na watu wakuu, kama Yusufu
alivyokaa na Farao Mfalume wa Misiry, humpatia nafasi ikiwa na maana ya cheo,
alikadhalika humpatia mafanikiao katika maisha yake.
Alitoa
ufafanuzi ya kwamba neno zawadi ni sawa na kipaji ama kipawa ambapo Bibilia ya
kingereza ya KJV imetumia neno moja katika kipawa na zwadi ambalo ni “Gift”,
Yaani zawadi.
Alitoa mfano
wa Mwimbaji wa nyimbo za Injili Rose Muhando, na Bonyi Mwaitege, Pia Mwalimu
Mwakasege, wanatambulika kwa mujibu wa karama ama vipaji vyao. Na wanaishi
kwavyo. Pia alisema wanaishi mjini kwa hivyo vipawa.
Alitoa mfano
wa mgunduzi wa mtandao wa Facebook, anaishi na amefanikiwa kwa mujibu wa
ubunifu wake, waliobuni vyombo vya muziki wananufaishwa kwa ubunif huo. Ndiposa
aliwataka watu kutumia vipawa vyao vyema ili kujikwamua kimaisha.
Alisoma habari
za Yusufu aliyekuwa gerezani ila alitoka kwa sababu yakutumia vyema kipawa chake
cha kutafsiri ndoto, na kusema na wewe unaweza kutoka kwenye hiyo taabu kwa
kutumia vyema kipawa ulicho nacho.
Pia alibainisha
inawapasa wale ambao hawajaokoka kuhakikisha ya kwamba wanamjua Mungu
iliwatumie vipawa vyao katika kuhubiri Neno la Mungu, maana wasipookoka
wanaweza kutumia vipaji hivyo kubuni vitu vitakavyo wapeleka watu jehanamu kama
Pombe na kadhalika.
Sanjari na
hayo alifafanua kwamba ipo garama ya kutumia kipawa chako hususani kwa watu
waliokoka kwani shetani hulipinga sana jambo hilo. Alitoa mfano wa Yusufu
aliyechukiwa na ndugu zake kwa sababu ya ndoto zake, hatimaye kuuzwa, kuwa
“houseboy”, kupelekwa gerezani pasina hatia yoyote ile, na hiyo ilikuwa ni
garama ya kutumia kipawa chake.
Alikadhalika
kwa watu waliokoka mambo hayo yapo ila yawapasa kuyashinda. Zaidi tazama video
yake kwenye Chaneli yetu ya Youtubu ya Ukombozi Gospel. Ama tembelea www.ukombozigospel.blogspot.com
Ila Mwalimu
alimalizia kwa maombezi kwa watu wote lakini pia kabla ya maombezi aliwataka
watu ambao hawajaokoa kufanya hivyo ili waweze kutumia vyema vipawa vyao maana
wasipokuwa na Roho ya Mungu ndani yao, (alitoa mfano wa Yusufu pale ambapo
Farao alisema Roho ya Mungu inakaa ndani yake na kumuita ni mwenye Akili). Ya
kwamba ni vigumu kuwa na ufanisi katika kipaji chako maana kama ni muimbaji
utaimba nyimbo za dunia na jambo hilo litakuwa ni hatari kwa wewe maana ukifa
utaenda jehanamu ya moto.
Kama
hujaokoka na unataka kuokoka ama ulirudi nyuma kiroho na unataka kutengeneza na
BWANA kwa upya leo, tafadhali fwatisha nami maneno haya kwa Imani, Sema: BWANA
YESU, NINAKUPENDA, NINAKIRI NA KUAMINI MOYONI MWANGU KUWA WEWE NI MUNGU,
ULIKUFA NA KUFUFUKA KWA AJILI YANGU, INGIA NDANI YANGU KAMA BWANA NA MWOKOZI WA
MAISHA YANGU LEO, AMENI.
Hongera kwa
kuokoka na tafuta kanisa la watu waliokoka ukasali hapo.
Na Huduma ya
UKOMBOZI GOSPLE, Arusha Tanzania, Kwa Maombi, Ushauri, Maswali au Sadaka
wasiliana nasi, Barua pepe: ukombozigosple@gmail.com
Simu: +255 759 859 287 pia waweza itumia kwa M-PESA. Zaidi www.ukombozigospel.blogspot.com #UkomboziGosple #MwalimuOscarSamba
Pia #Like
#Penda Page/Ukurasa wetu au kundi la Fb, ili kupata
habari hizi kwa haraka, zaidi. Ug Ukombozi Gosple,
PAGE:
https://www.facebook.com/ugukombozigospel/
Pia kwenye
mtando Mpya wakitanzania wa
2 DAY SKY:
https://www.2daysky.com/home
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni