Na Mwalimu Oscar Samba wa Ug Ministry. |
Kwa tabasamu Mubashara ninakukaribisha tena
katika mfululizo wa makala yetu hii ikiwa leo ni sehemu ya 4 na kama hukusoma
zilizotangulia ni vyema ukazisoma ili tuweze kwenda sanjari, pia kumbuka ujumbe
huu ni sehemu ya kitabu changu cha NGUVU YA NDOTO KWENYE ULIMWENGU WA ROHO.
(8) Kusikiliza au kufwatilia Hadithi
zenye elementi au chembe chembe za pepo mahaba.
Sikio ni
malango wa rohoni tena hatarishi kama utatumiwa na adui. Elifazi aliota ndoto
ambayo Shetani alitumia mlango wa sikio kupenyeza mathara kathaa ikiwemo hofu,
kutetemeka mifupa na hata nywele kusisimka. Mstari ule wa 12 anasema kuwa
alisikia na kusikia huko ndiko kulikoruhusu hayo mathara. Ona katika kitabu
kile cha Ayubu 4:12-16. Na wewe
kusikiliza hadithi zenye “elementi”/chembechembe za jini Mahaba kutakufanya
kumfungulia mlango maana tayari masikio yameshamruhusu kupenya hali itakayompa
uhalali wa kukutembelea ndotoni.
Kusoma
hadithi hizo kutampa mlango maana unachokisoma chaweza ingia nafsini au moyoni.
Na huko ndiko kuliko na lango la kiroho pia fahamu mtu wa ndani na ndiye
anayeota ndoto kama hizi.
Namna ya Kumshinda Pepo Mahaba.
Katika
ulimwengu wa roho ukiwaona mabinti waliovalia nguo za rangi nyekungu na kwa
nadra waweza vaa za rangi ya zambarau ambazo zipo kama gauni ila lenye mpasuo
mrefu na huonyesha utupu wao, jua ni jeshi la pepo mahaba. Mapepo haya
yanakitengo chao kwa ajili ya kupigana vita ndio maana ni vigumu kuyashinda
bila kanuni stahiki na kiongozi wao Mkuu ni Mama wa Makahaba wa Babeli ama Mama
wa Machukizo ya nchi. Soma Ufunuo wa
Yohana 17:1-18.
1. Muombe Mungu akujulishe milango/mlango alioutumia.
2. Bada ya kuujua mlango, Omba rehema kwa mlango huo
kufunguka. Epuka kujihesabia haki punde ujuapo kuwa huku husika ama huna hatia
iliyofanya mlango huo kufunguka. Rehema ya kumng’o Pepo huyu inapaswa kuwa
kubwa kwani huwa na tabia ya kuwa king’ang’anizi, ndio maana watu wengi
hushindwa kupambambana naye. Rehema hiyo yapaswa ifanyike katika maombi ya
kufunga na kuomba na ya muda mrefu huku yakiwa na mfumo wa maombolezo.
3. Futa uhalali wa Shetani kuutumia huo mlango kwa
kutumia Damu ya Yesu ile imwagikayo ubavuni na mikononi. Omba kwa kumaanisha na
kuzama.
4. Funga mlango huo kwa Maombi ya muda mrefu na yenye
ujazo wa Roho.
5. Fanya maombi malumu ya kufunga mlango huo kabla ya
kulaa. Anza na rehema, pili funga mlango. Pia taja kila lisaa kwa kukemea na
kufunga kuanzia muda unaolala hadi utakapo amka, ukifika muda ambao mara nyingi
huota ndoto hiyo, kemea ama ombea muda huo kwa mzigo zaidi. Mara nyingi mapepo
haya hutumia lango la muda au siku fulani, ndio maana ni muhimu kuandika au
kujua muda ambao mara nyingi huota ndoto za aina fulani. Pia huweza kubadilika
baada ya muda fulani. Kwa mfano ukijua ni saa tisa au saa kumi na moja, wengine
huwa ni saa moja kasoro, muda huo uombee kwa kasi na nguvu zaidi.
6.
Unapoamka
hakikisha unajiombea na kuwaombea wale ambao huweza kufungua mlango wako wa
ndoto kwa siku hiyo wasifanye hivyo, pia jitenge nao rohoni kama watafanya
hivyo. Jiombe ili Shetani asipate nafasi ya kuyatumia macho yako kutamani au
mawazo yako kutafakari upumbavu hali itayomuwezesha kupata nafasi. (Zaidi soma
kipengele cha Usimpe Ibilisi nafasi kilichopo kwenye kitabu changu cha Namna ya Kuishi wakati wa Majaribu au
Mapito)
Katika
kuomba tumia sana Damu ya Yesu na Silaha ya moto, pia na Upanga. Ukisoma sura ya 17 nzima ya
kitabu kile cha Ufunuo wa Yohana, utaona jinsi walivyo mshinda kwa Damu za
watakatifu na ya Mwanakondoo pamoja na moto. Ufunuo 17:14 Hawa watafanya vita na Mwanakondoo, na Mwanakondoo
atawashinda, kwa maana Yeye ni Bwana wa Bwana, na Mfalume wa Wafalume; na hao
waliopamoja nao ndio walioitwa, na wateule na waaminifu. Hapa tunapata pia
Silaha nyingine ya Bwana wa Mabwana, na Mfalume wa Wafalume. Tumia majina hayo
katika kumpinga na kupigana naye, ila kufuta uhalali changanya hapo na Damu ya
Yesu.
7. Vunja hiyo ndoa kwenye ulimwengu wa roho, Mapepo haya
huwa yanafunga ndoa na wahusika kwa hiyo baada ya hatua hizo hapo tangaza
kimaombi kuivunja hiyo ndoa. Pia Vua vitu ambavyo ni alama ya mapepo ulivyovikwa
rohoni, mfano pete mikononi na miguuni, vikuku na hereni na hata mavazi. Fanya
maombi hayo kwa ishara na kwa kumaanisha na yawe maombi ya vita.
8. Futa alama za mapepo
mahaba ambazo hukaa mwilini, kuna mwanaume mmoja wakati anafanya haya maombi
Mungu alimuonyesha kwenye mguu wake eneo la chini kwenye kiungo cha ubavu kuna
alama ya uke. Ikiwa na maana kila aridhi atakayoikanya yenye mapepo haya ni
rahisi kuvamiwa au kutekwa nayo ama kumtumia ndotoni kwani mguuni kuna malango.
Wengine huwa na Ume/Uke wa kimapepo katika sehemu zao za siri ama popote
mwilini, alama hii ni hatarishi kwani mtu kama huyu huweza kuwaka hisia kwa
haraka sana na wengi wao huwa na vitendo vya kujichua/“punyeto” ama ushoga na
usagaji na akiota huweza kuota anazini na mtu wajinsia yake kwani kwenye
ulimwengu wa roho ana alama ya jinsia ningine. Na alama kama hizi zikiongezeka
za jinsia tofauti na kukomaa kwa muda mrefu muhusika kama ni wakike huweza kuwa
namuonekano au tabia kama za kiume na kama ni wakiume huweza kuwa na tabia kama
za kike. (Taadhari: Sio kila mwenye
tabia hizo ana tatizo hili kwani wengine ni matatizo ya kihomo za kibaolojia,
au jinsi alivyojiweka; ingawaje na huyu ni matatizo ya kihomoni kiroho.) Siku
moja nilimuota mtu mmoja mwanaume mwenye maziwa/matiti ya kike kifuani mwake,
na ni ishara ya kwamba mapepo haya yamemkali na huwa mwepesi wa kuzini bila
hiyari yake. Zote zifute na kabla huja zifuta anza na maombi ya rehema ili
kuondoa uhalali wake na kisha futa kwa alama hizo Damu ya Yesu.
NB: maombi haya yafanye kwa muda mrefu, hata ukiona hali
hiyo imeisha usikubali kuacha hadi Mungu akuakikishiye maana Pepo hili huwa na
tabia ya kutulia kwa muda ili usahau na kisha hurudi tena. Ama huweza kuamua
kuamia kwa ndugu yako, watoto au mwanandoa mwenzako pia huwa na utamaduni
wakulipiza kisasi. Kwa hiyo funga pia roho za kisasi na mashambulizi.
Kwa watumishi, Watumishi wa Mungu wanaokemea mtu
mwenye mapepo kama haya wanapaswa kufuga roho za visasa na wao kuishi maisha
matakatifu kwani mara nyingi hupenda kulipiza kisasi kwenye ndoa zao au watoto
pia hata ndugu. Ndio maana watoto wengi wa watumishi hujikuta wakianguka kwenye
Uzizi na bathi ya wake za watumishi hujikuta wakitoka kwenye ndoa zao. Na
watumishi wengi wanaoanguka kiroho husumbuliwa sana na dhambi hii ikiwa ni
matokeo ya kisasi.
Kwenye ndoa, Hakikisha unamuombea mwanandoa
mwenzako kila wakati dhidi ya roho hii ili isimvae. Fungua nami kitabu kile cha
Zaburi, Zaburi 22:20 Uniponye nafsi yangu
na upanga, mpenzi wangu na nguvu za
mbwa. Watu wa kiroho wanafahamu kuwa kiwakilishi cha roho ya umalaya na
ukahaba ama mapepo mahaba kwenye ulimwengu wa roho ni mbwa. Na kwa kulifahamu
hili mtunga Zaburi anamuombea mpenzi wake alindwe na Mungu dhidi ya nguvu za mbwa. Maana yake ipo nguvu kwa
Pepo Mahaba iwezayo kumdhuru mwenzako. Ona pia Zaburi 35:17.
Na kama ndoa
yako imeshavamiwa kwa mujibu wa dalili tajwa hapo juu, ya kupasa kuipeleka
kwenye maombi ili ipone na usikubali makwazo ya mwanandoa mwenzako kukuzuia
maana Shetani huyaleta ili kukupa uchungu utakao kunyima kumuweka kwenye
maombi. Zaidi,
fwatilia somo langu liitwalo Hatari ya Pepo Mahaba.”
Hongera wa
kutufwatilia hadi kufikia hatua hii, na kwa mfululizo kutoka kwenye kitabu
chetu hapo ni mwisho ila kesho nitakupa mwendelezo ambao ni wa ziada sio kwepo
kwenye kitabu na hapo nitatanua matamvua yangu kifikra zaidi ili kukupatia
mambo muhimu yasiyokwemo humu maana ujumbe huo kwa kiasi fulani ulizingatia
maudhui na shabaha ya kitabu ambayo ililenga kwenye nyanja ya Pepo Mahaba.
Tuonane kesho na kusanya Uwezo na Nguvu wakutanabaishwa vyema.
Kama
hujaokoka na unataka kuokoka ama ulirudi nyuma kiroho na unataka kutengeneza na
BWANA kwa upya leo, tafadhali fwatisha nami maneno haya kwa Imani, Sema: BWANA
YESU, NINAKUPENDA, NINAKIRI NA KUAMINI MOYONI MWANGU KUWA WEWE NI MUNGU,
ULIKUFA NA KUFUFUKA KWA AJILI YANGU, INGIA NDANI YANGU KAMA BWANA NA MWOKOZI WA
MAISHA YANGU LEO, AMENI.
Na Huduma ya
UKOMBOZI GOSPLE, Arusha Tanzania, Kwa Maombi, Ushauri, Maswali au Sadaka
wasiliana nasi, Barua pepe: ukombozigosple@gmail.com
Simu: +255 759 859 287 pia waweza itumia kwa M-PESA. Zaidi www.ukombozigospel.blogspot.com #UkomboziGosple #MwalimuOscarSamba
Pia #Like
#Penda Page/Ukurasa wetu au kundi la Fb, ili kupata habari hizi kwa haraka,
zaidi. Ug Ukombozi Gosple,
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni