Jumanne, 27 Juni 2017

NGUVU YA AGANO, Sehemu ya 8.

Na Mwalimu Oscar Samba wa Ug Ministry.
Nami sina shida kwani ni kweli waswahili husema kuwa ahadi ni deni, nami leo sina budi kulipa deni hili, Ndugu yangu katika Kristo kumbuka kuwa leo ni siku ya 8 ya makala yetu hii ya Nguvu ya Agano nami tokea siku kadhaa zilizopita nalikuaidia kukuonyesha kitu muhimu ambacho Ibrahimu alijuzwa na Mungu na hatimaye kuja kutokea kipindi cha Yakobo yaani Iziraeli ikiwa ni Jambo la Kiagano.

Ukisoma kutoka kitabu kile cha Mwanzo sura ile ya kumi na tano utamuona Mungu akimwambia Ibrahimu kuwa uzao wake utaenda kuishi Misiry ama utakuwa mgeni huko na kusudi kubwa la Mungu ni kuwazidisha ama kuwaongeza, na kuwatajirisha huko maana walitabiriwa kutoka na mali nyingi, huku muda wao ukiwa ni miaka 400, muda ulioamariwa na Mungu, ingawaje walikaa mika 430, na sababu za kuongezeka kwa hiyo miaka nimezielezea kwenye kitabu changu cha Namna ya Kuishi Wakati wa Majaribu au Mapito, na pia Mungu akinipa kibali nitaligusia kwenye kitabu kile cha Wito wa Kitumishi ili kukusaidia ujuwe umuhimu wa kumuombea Musa wako ili asichelewe kuitika ama asikimbiliye Midiani badala yakukukomboa kwa wakati.

Tusonge mbele na Agano, Sasa leo tunaona utimiajia wa jambo hilo ila awali ya yote ninawiwa kulidhibitisha jambo hilo ama kuliweka bayana mbele ya macho yako.

Kwa Furaha ya Moyo Fungua nami kitabu kile cha Mwanzo 15: 13 Bwana akamwambia Abramu, Ujue hakika ya
kwamba uzao wako utakuwa mgeni katika nchi isiyo yake, watawatumikia watu wale, nao watateswa muda wa miaka mia nne.
14 Hata na taifa lile, watakaowatumikia, nitawahukumu; baadaye watatoka na mali mengi.
15 Lakini wewe utakwenda kwa baba zako kwa amani, utazikwa katika uzee mwema.
16 Na kizazi cha nne kitarudi hapa, maana haujatimia uovu wa Waamori bado.



Ili kukudhibitishia kuwa ilikuwa ni taarifa ya Kiagano soma mstari wa 18 na 19 pia wa 20; Utaona Mungu akifunga Agano na Ibrahimu linalohusisha mambo muhimu ambayo ni Uzao wake, Kuirithi Nchi, na Utajiri pia.
Hapo awali na katika mfululizo wa makala hii twaweza sema hapo jana, tuliona jinsi Yusufu alivyokuwa beba kwa bega na ndugu zake ikiwa ni matokeo ya yeye kupata kibali kwa Farao na nikakujuza kuwa kilikuwa ni kibali cha kiagano kwani alimiliki lango la baraka la Misiry.

Nataka kukuonyesha Nguvu iliyopo kwenye Agano inavyoweza kutimiza ahadi zake katika mazingira yoyote yale ili nikusaidiye na wewe unayeona mambo ni kama vile hayawezekani angali unakumbuka kuwa Mungu alishakuaidia kwa kinywa chake mwenyewe ama cha Nabii wake. Tuanze na Farao mwenyewe.
Mwanzo 45: 16 Habari ikasikika nyumbani mwa Farao kusema, Ndugu zake Yusufu wamekuja. Ikawa vema machoni pa Farao, na machoni pa watumwa wake.
17 Farao akamwambia Yusufu, Uwaambie ndugu zako, Fanyeni hivi; wachukuzeni mizigo wanyama wenu, mwondoke mwende nchi ya Kanaani;
18 kisha mkamtwae baba yenu, na watu wa nyumbani mwenu, mkanijie; nami nitawapa mema ya nchi ya Misri, nanyi mtakula unono wa nchi.

Sasa nataka kukuonyesha Kwa Mzee Yakobo ama Iziraeli, hapa Mungu anajidhiirisha kwake kama Mungu wa baba zake,  (Mungu wa hili Agano). Na anataja mambo muhimu yaliyopo kwenye Agano hili, 1. Uzao; Kumzidisha ama kumfanya kuwa Taifa kubwa, (kumtajirisha,) na 2. Kumrudisha katika hiyo nchi ikiwa ni ahadi ya kuirithi ama kuwarithisha nchi ya ahadi.

Tudodose hayo maandiko ya kiagano, Mwanzo 46: 2 Mungu akanena na Israeli katika ndoto ya usiku, akasema, Yakobo, Yakobo. Akasema, Mimi hapa.
3 Akasema, Mimi ni Mungu, Mungu wa baba yako, usiogope kushuka mpaka Misri; maana nitakufanya uwe taifa kubwa huko.
4 Mimi nitashuka pamoja nawe mpaka Misri; nami nitakupandisha tena bila shaka; na Yusufu ataweka mkono wake juu ya macho yako.

Nataka uone kuwa ni kweli yeye na uzao wake walielekea Misiry kama Mungu alivyomjuza Ibrahimu kiagano. Ni mistari inayofwata;
5 Yakobo akaondoka kutoka Beer-sheba; wana wa Israeli wakamchukua baba yao na watoto wao wadogo, na wake zao katika magari aliyoyapeleka Farao ili kumchukua.
6 Wakatwaa na wanyama wao, na mali zao walizokuwa wamezipata katika nchi ya Kanaani, wakaja
Misri, Yakobo na uzao wake wote pamoja naye.
7 Wanawe, na wana wa wanawe, pamoja naye, binti zake na binti za wanawe, na uzao wake wote, aliwaleta pamoja naye mpaka Misri.
Ukiendelea mbele utayaona majina. Ni hakika hata kwako kile ambacho Mungu aliwai kunena na wewe katika sura kama hii ama na wazazi wako kinawezekana na kilicho cha msingi ni wewe kumtizama Mungu.

Tuendelee na tukio hili kwani hata kuishi kwao hapo ni kiagano na mwishoni katika hili tutaona kuwa hata kutoka kwao pia ilikuwa ni Kiagano.
Najua kiu uliyo nayo yakusonga mbele nami kuhusu hili ni kubwa ila iweke kiporo ama akiba kwani kesho pasina shaka na kwa majaliwa yake Mola ama Maulana tutakutana tena katika safu hii Mubashara.

Ila kiukweli kabisa ni kwamba mambo hayo tuliyoyanena hayataweza kuwa halisi kwako kama hujampa Yesu maisha yako, nafahamu fika kwamba umefurai na umejengwa kiroho na kinafsi pia lakini sina budi kukueleza ukweli ya kwamba waliookoka ndio wana wa Ibrahimu kiimani ama kiroho na wewe kama unataka kuwa mwana ili unufaike na Agano hili, huna budi kuookoka sasa.
Kama hujaokoka na unataka kuokoka ama ulirudi nyuma kiroho na unataka kutengeneza na BWANA kwa upya leo, tafadhali fwatisha nami maneno haya kwa Imani, Sema: BWANA YESU, NINAKUPENDA, NINAKIRI NA KUAMINI MOYONI MWANGU KUWA WEWE NI MUNGU, ULIKUFA NA KUFUFUKA KWA AJILI YANGU, INGIA NDANI YANGU KAMA BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YANGU LEO, AMENI.
Hongera kwa kuokoka na tafuta kanisa la watu waliokoka ukasali hapo.

Na Huduma ya UKOMBOZI GOSPEL, Arusha Tanzania, Kwa Maombi, Ushauri, Maswali au Sadaka wasiliana nasi, Barua pepe: ukombozigospel@gmail.com  Simu: +255 759 859 287 pia waweza itumia kwa M-PESA. Zaidi www.ukombozigospel.blogspot.com   #UkomboziGospel  #MwalimuOscarSamba
Pia #Like #Penda Page/Ukurasa wetu au kundi la Fb, ili kupata habari hizi kwa haraka, zaidi. @ugukombozi Gospel 
 PAGE: https://www.facebook.com/ugukombozigospel/
Pia kwenye mtando Mpya wakitanzania wa
 Pia TAZAMA VIDEO ZETU HAPA  https://www.youtube.com/channel/UCv1tghnugOSpbmb5h6ebJtA  (Ukombozi Gospel)


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni