Na Mwalimu Oscar Samba wa Ug Ministry. |
Hakika ni
jambo la fanaka kukutana tena katika safu hii ya makala za kiroho na ikiwa ni
sehemu yetu ya mwisho ya mfululizo wa makala hii, leo nimekuandalia mambo
kadhaa kuhusu hadhari za huyu Pepo mahaba na ni ombi langu Mungu akupe kibali
cha kukuletea ujumbe kama huu katika sura nyingine maana hakika Mungu amenipa hazina
ya maarifa kuhusu roho hii hatarishi.
Moja kwa
moja nianze kwa kukujuza ya kwamba hii ni miongoni mwamambo ama roho
inayoitessa dunia mno. Ikumbukwe kuwa katika historia ya Bibilia Mungu aliwai
kuiangamiza dunia kwa maji kipindi cha Nuhu na kwa moto mji ule wa Sodoma na
Gomora na sababu kubwa ikiwa ni roho hii.
Utumishi wa
Daudi na Samsoni uliingia doa na sababu kubwa ikiwa ni roho hii. Ilimtesa pia
Musa na Joshua sanjari na Kalebu kule Jangwani. Kumbuka baada ya matokeo yale
ya upelelezi ya nchi ile ya ahadi Mungu anasema ya kwamba wamefanya uzizi na aina
inayotajwa pale sio ya kukutana kimwili bali ni taswira nyingine ya utendaji
kwa upande waibada za miungu na imani inayotajwa kiroho na lipo somo litakalo
gusia taswira hiyi nami nimekuonjesha mwishoni mwa makala hii. Tuone adhari
moja wapo ya roho hii.
HUTIA JERAHA, KUKUVUNJIA HESHIMA, Kitabu kile cha Mithali
kimebainisha jambo hili vyema. Mithali 6: 32 Mtu aziniye na
mwanamke hana akili kabisa; Afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake. 33 Atapata jeraha na kuvunjiwa heshima; Wala fedheha yake
haitafutika.
Kwa mantiki
hiyo unapotenda dhambi hii ni fika kwamba unaijerui nafsi yako na kwenye nasi
kuna vitu vikuu vifwatavyo, 1. Hisia,
utajikuta uwezo wako wakumwambudu Mungu katika roho na kweli unatoweka huku
ukipoteza upendo kwa Mungu na kwa mwanandoa wenzako ama mchumba maana Upendo ni
matokeo ya hisia itokayo katika Nafsi. 2.
Akili, hiki ni kitua muhimu sana na hakipatikani kwenye ubongo bali ni
kwenye nafsi, na jambo hili linaudhibitisho kibibilia katika kitabu changu cha
SAIKOLOJIA YA MTU WA NDANI, nitalidadavua zaidi. Kwa hiyo
unapotenda hiyo dhambi
akili zako zinadhoofika ndio maana utamkuta mtu akiwa radhi kuwalisha watoto
wake dagaa ama kisamvu pamoja na mkewe
huku nyumba ndogo wakila nyama choma. Yuko tayari watoto warudishwe ada huku hawara
akila vizuri. Ukiona hivyo jua ni akili zimeshaharibiwa, ndiposa pia hilo
andiko likasema ya kwamba hana akili mtu huyu.
3. Makusudi, Pia yamo kwenye nafsi. 4. Dhimiri, Tunafahamu kuwa jambo hili
huusika sana katika kutoa ama kuachilia hukumu kwenye moyo na ndiposa Roho
Mtakatifu akihitaji kumgeuza mtu huugua kupitia Dhamiri, ila dhambi hii
inaiadhiri na kuifanya ife kwa haraka zaidi. Mtu aliyemzizi ama mwasherati huwa
na moyo mgumu sana kutubu. Au kujinyeyekesha.
5. Nia, Yesu alitutaka tuwe na nia ile ile
kama aliyokuwa nayo yeye, katika kitabu kile cha Wafilipi. Nia ni kama kiini
cha uhai wa jambo fulani katika maisha ya mwanadamu na ndicho huzalisha , Malengo,
mikakati na hatimaye kufanikisha maono ama jambo fulani na kwa ujumla huweza
kuziita njia. Maandiko yanapotutaka tuwe na nia moja tusitangetange katika nia
mbili pia yanatutaka kwa tafsiri rahisi tuwe na nia moja maana vitu hivyo
vilivyopo kwenye nia huitwa njia kwenye ulimwengu wa roho, sanjari na mawazo
huzalishwa ama aina fulani ya Nia huzalisha mawazo ya aina yake na ndiyo huunda
aina fulani ya moyo na yakipanuka huadhiri makusudi katika moyo, ambayo huwa na
madhara katika njia za mtu. Ukiona mahali pameandikwa ya kwamba acheni njia
zenu mbaya maana yake anza kwanza kubadili Nia na kisha mambo yaliyomo ndani
yake. Ukimkuta mtu anahubiri Injili ili watu waokoke lakini ndani yake analenga
kupata fedha jua huyo yupo kwenye utumishi wa Mungu na Nia isiyokuwa ya Kristo.
Ba Nia yake ni kupata fedha. Ili
kumbadilisha ni msaada wa maandiko yafwatayo.
Wafilipi 2:.5 Iweni na nia iyo hiyo
ndani yenu ambayo ilikuwamo pia ndani ya Kristo Yesu; 6 ambaye yeye mwanzo
alikuwa yuna namna ya Mungu, naye hakuona kule kuwa sawa na Mungu kuwa ni kitu
cha kushikamana nacho;
Pia Yakobo na
mistari yote hii imebeba kanuni kuhusu namna ya kujikwamua hapa ikiwemo
Kumpinga Shetani aliyekamata hiyo Nia, Kumtii Mungu ili kuifwata Nia yake, Kuusafisha
Moyo, Kutakasa Mikono ikiwa na tafsiri ya kazi ama mambo uyafanyayo. Huku Mungu
akielekeza namna ya kuomba na anatuambia kuwa ni maombi ya Kuomboleza, Kulia,
pamoja Kujinyenyekesha, hii pia inapatika katika kitabu hicho cha Wafilipi na
ukitaka picha kamili endelea na maandiko yanayoendelea hapo utamuona jinsi Yesu
alivyojishusha na kuikubali hata mauti ya msalaba huku akiiacha Mbingu. Jambo
hili ni Muhimu sana kwako maana kwa Mtumishi kuwa na Nia mbli (Double Mind), Ni
jambo hatarishi sana na ni matokeo ya kukosa unyeyekevu. (Zaidi fwatilia Somo
langu la Nia ama kitabu cha Saikolojia ya Mtu wa Ndani kikitoka)
Bila iyana nakufungulia
maandiko hayo; Yakobo 4:7 Basi mtiini Mungu. Mpingeni Shetani, naye atawakimbia. 8
Mkaribieni Mungu, naye atawakaribia ninyi. Itakaseni mikono yenu, enyi wenye
dhambi, na kuisafisha mioyo yenu, enyi wenye nia mbili.
9 Huzunikeni na kuomboleza na kulia.
Kucheka kwenu na kugeuzwe kuwa kuomboleza, na furaha yenu kuwa hamu. 10
Jidhilini mbele za Bwana, naye atawakuza.
Kwa mantiki
hiyo ni kwamba dhambi hii huweza kuugeuza moyo wako na kukujengea nia isiyotoka
kwa Mungu na kujikuta unakuwa na utumishi tofauti na ule uliyoanza nao hapo
awali.
Alikadhalka
katika maisha ya kawaida dhambi hii huweza kubadili Nia ya muhusika ambayo hapo
awali ilikuwa ni kununua viwanja, kuipenda familia ama kuwa na Nia njema kuhusu
nduguze na mara baada ya kuanza jambo hili anabadilika na kuwa mtu mwingine na
unashangaa anavaliwa na Nia ya ukali, hasira na kadhalika.
6. Maamuzi, uwezo wa maamuzi wa huyu mtu
unabadilika, Samsoni alipokubali kukaa kwenye mapaja ya Delila kilichomtokea ni
maamuzi yake kujikuta yakitekwa. Mtu anayefanya dhambi hii huwa na maamuzi
yasiyokuwa shupavu na mara nyingi hutawaliwa na roho hii.
Ni fika na
bayana ya kwamba nalitamani kuendele na somo hili katika sehemu ya 6, ila
tukutane siku nyingine katika ujumbe kama huu kwenye somo liitwal HATARAI YA
PEPO MAHABA. Na hapo nitakujuza kiunaga ubaga jinsi roho hii inavyofanya kazi
hadi kwenye siasa na dini na mtaji wangu mmoja wapo utatoka kwenye kitabu kile
cha Ufunuo wa Yohana sura ya 17 anapomtaja yule mwanamke kahaba wa Babeili mwenye
jina la siri la Babeli Mkuu mama wa makahaba na machukizo ya nchi pia anahusika
na maangamivu.
Anasema
wafalume wamezini naye na kujipatia utajiri na kadhalia. Nitakufafanulia sababu
za andiko hilo kusema kuwa alilewa, na nafasi ya Damu ya Yesu katika kupigana
naye ambayo husimama sehemu kama ya mvinyo umleweshao na namna ya kutumia
kikombe cha gadhabu ili kupigana naye ambacho maandiko husema ya kwamba ni
kikombe chenye kulevywa na fahamu kikombe hicho ni Agano. Ndiposa katika Luka
22 Yesu akatanaibasha ya kwamba kikombe hiki ni Agano Jipya, (22.20
Kikombe nacho vivyo hivyo baada ya kula; akisema, Kikombe hiki ni agano jipya
katika damu yangu, inayomwagika kwa ajili yenu.]) Sasa nitakuelekeza
namna ya kuchukuwa KIKOMBE+AGANO kama silaha.
Na fahamu
pia maandiko yanasema waliokaa juu ya nchi wamelewa kwa mvinyo wake wa
uasherati, ndiposa miziki ya dunia yenye kubeba roho hii inawabamba wengi.
Pamoja na uvaaji wa mavazi ya roho hii ambayo mitindo yake hutoka kuzimu moja
kwa moja yakiratibiwa na kitengo ama idara hii pamoja na “staili” za kucheza
kwenye miziki yao na maudhui ya filamu zilizo nyingi ndiposa nyingine
hazikamiliki bila kuonyesha vitendo vya kikahaba na miziki yao na bila mavazi
ya kimalaya huku kanisa likijikuta likiiga mavazi na uchezaji wao na kwa upofu
wachungaji wamefumbia macho uchezaji huo na uvaaji huo kwa kuwa na Falsafa
zilizokufa kiroho za “Eti atuangalii mwili bali ni roho”, NINANI ALIYE WALOGA
HAWA? Paulo Mtume anasema ya kwamba sisi ni barua, na maandiko hututaka tuvae
mavazi ya Staha ama yatusitirio huku wanaume wakivaa mavazi ya kiume na
wanawake wakivaa mavazi ya kike.
(Tafadhi
naona Upako wakiinjilisti unatiririka, tukutane kwenye programu yangu mpya ya
Tv on Line ikiwa ni Mwanzo wa Ug Tv, ambayo itagusia maswala haya na nitavaa
pia kofia ya kiinjilisti.)
Nitajibu pia
hoja ya watu wanaodai kwamba walipokuwa watumishi na kujikuta wamaetoka kwenye
mstari wa Mungu kwa kuhitaji nguvu za kihuduma kwa upande wa shetani walijikuta
wakiwa baharini na kuhitajika kuzini na mwanamke aliyetoka baharini (Kwenye
maji, na andiko hilo la Ufunuo humtaja Mama huyu wa Machafuko kuwa anatoka
majini: Hakiki jambo hili,
Ufunuo wa Yohana
17.1 Akaja mmoja wa wale malaika
saba, wenye vile vitasa saba, akanena nami, akisema, Njoo huku, nitakuonyesha
hukumu ya yule kahaba mkuu aketiye juu ya maji mengi;) na nitakwambia ni huyu au jirani
yake. Na hapo hapo nitakupa jibu la kiumbe kiitwacho Nguva na siri ya
wanamuziki na waigiza filamu ama watu wakisirikina kutumia picha za wanawake
warembo wakiwa baharini na namna ishara ya samaki inavyomuwakilisha Pepo Mahaba,
na nitagusia kitengo ama idara ya vita ama jeshi la Pepo Mahaba linavyofanya
kazi kwenye ulimwengu wa roho.
Langu jina
ni mwalimu Oscar Samba wa Ug Ministry mtoto wa pili wa Mama Flora wa Mzee
Samba. Tukutane kesho kwenye makala nyingine iliyo Murwa na hakika itakujenga
vilivyo.
Kama
hujaokoka na unataka kuokoka ama ulirudi nyuma kiroho na unataka kutengeneza na
BWANA kwa Upya leo, tafadhali fwatisha nami maneno haya kwa Imani, Sema: BWANA
YESU, NINAKUPENDA, NINAKIRI NA KUAMINI MOYONI MWANGU KUWA WEWE NI MUNGU,
ULIKUFA NA KUFUFUKA KWA AJILI YANGU, INGIA NDANI YANGU KAMA BWANA NA MWOKOZI WA
MAISHA YANGU LEO, AMENI.
Hongera kwa
kuokoka na tafuta kanisa la watu waliokoka ukasali hapo.
Na Huduma ya
UKOMBOZI GOSPLE, Arusha Tanzania, Kwa Maombi, Ushauri, Maswali au Sadaka
wasiliana nasi, Barua pepe: ukombozigosple@gmail.com
Simu: +255 759 859 287 pia waweza itumia kwa M-PESA. Zaidi www.ukombozigospel.blogspot.com #UkomboziGosple #MwalimuOscarSamba
Pia #Like
#Penda Page/Ukurasa wetu au kundi la Fb, ili kupata habari hizi kwa haraka,
zaidi. Ug Ukombozi Gosple,
PAGE: https://www.facebook.com/Ug-Ukombozi-Gosple
Pia kwenye
mtando Mpya wakitanzania wa
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni