Karibu tena
katika muendelezo wa makala hii ya kiroho na leo tunaendelea na dalili za mtu
anayesumbuliwa na Mapepo Mahaba ikiwa ni somo lenye dhima ya kukunasuma na mateso
hayo na nisehemu ya kitabu chang cha NGUVU YA NDOTO KWENYE ULIMWENGU WA ROHO.Pia
kama hujasoma sehemu ya kwanza jitaidi uisome ili kujua tutokapo na tuendapo.
Kushindwa kujizuia, kutazama au
kufwatilia kitu chenye kushawishi kufanya ngono. Aliyetawaliwa na Roho wa Mungu huwa
mwepesi kufwatilia mambo ya Kiungu. Alikadhalika aliyevaliwa na roho ya mpira
pia huwa mwepesi wa kufwatilia na hushindwa kujizuia kuacha kufwatilia maswala
ya kimpira. Na hii ni matokeo ya roho hizo kukamata uwezo wa maamuzi yao,
fahamu kuwa uwezo wa maamuzi upo kwenye nafsi, na nafsi ndiyo inayoratibu
shuhuli na matendo ya mtu kwa kivuli cha moyo.
Kwa hiyo mtu
aliyekaliwa na Mapepo Mahaba hujikuta akilazimika kutizama picha za Utupu,
Maumbile ya yatamanishayo ama sehemu zake kwa mshichana/mvulana.
Hata
kutizama baadhi ya miziki kwa lengo la kuona hayo maumbile ama kukodolea macho
magazeti au majarida yenye picha za mapepo za watu walio katika mkao wa
kimapepo mahaba.
Hutamani
hata kushika mkono na mtu aliyemtamani, au kuongea naye huku akiwa hana hoja ya
msingi, ama kuingia gharama yoyote ile ikiwemo kununua vocha na kumpigi ama
kuwasilia na mtu kwa dhumuni la kupiga hadithi za kimahaba bila kujali gharama
atakayo itumia na kulinganisha na uwezo wake kiuchumi, ndio maana wengine
hufanya kazi za sulubu na kupata kipato kidogo lakini huweza kuishia kuhonga
bila kufanya jambo la msingi na fedha hiyo. Miongoni mwa tabia ya Pepo Mahaba
ni kuleta Umasiki/Utumwa kifikra au
kimaisha.
Unakuta mtu
anafwatilia hadidhi kama hizi aidha kwenye intanenti au jarida fulani ama
filamu au tamfilia kwa gharama kubwa na kwa kupoteza muda mwingi. Utumwa huu ni mbaya maana hupoteza muda,
fedha na huathiri uwezo wa mhusika kufikiri huku ukifungua milango ya dhambi na
ndoto za kishetani.
Kuwa mwepesi wa kifkra za kimahaba
hata kwa jambo au mambo yasiyoendana. Maandiko kwenye kitabu kile cha Mithali hutamka bayana
kuhusu jambo hili, Mithali 23:7a maana aonavyo nafsini mwake ndivyo alivyo..
Bibilia ya kingereza imetumia neno afikirivyo (think) badala ya neno aonavyo,
kwa huyo liweke hapo ilo neno na usome kwa upya msatari huo. “maana
awazavyo/afikirivyo nafsini mwake ndivyo alivyo”. Kwa mantiki hiyo ni
kwamba nafsi ya mtu iliyovaliwa na Mapepo Mahaba, hufikiri kimapepo mahaba ama
kufikiri kwa huyu mtu ni matokeo ya Pepo huyu kukaa ndani yake.
Unaweza
ukatoa maneno ambayo hayahusiani na mahaba ila unashangaa mtu fulani akicheka
au kutabasamu na ukichunguza unakuta alifikiria jambo jingine. Uonapo hilo jua
ndani yake ipo kambi ya Jini Mahaba.
Mfano
unaweza kuzungumzia juu ya tunda la mti wa katikati ya Edeni ila yeye fikra
zake huenda kwenye maeneo ya katikati ya mwili.
Ugumba au Utasa, Mapepo haya huwa na tamaduni za
kumzuia mtu kupata mtoto ingawaje kibaolojia huweza kuwa na uwezo huo. Kumbuka
kila pepo mahaba humkalia mtu akiwa na shabaha fulani na miongoni mwayo yaweza
kuwa hii ya utasa ama ugumba.
Matatizo katika siku za mwezi, Pia mapepo haya huusika katika
kuleta maumivu yasiyo ya kawaida katika siku za hethi ama mwezi kwa mwanamke.
Ya weza kuwa maumivu ya kiuno, kichwa ama tumbo. Pia kwa wengine hushidwa
kuziona siku zao kabisa ama kupitiliza nje ya sababu za kibaolojia. Kumbuka
swala la mwezi la weza kusumbua kikawaida ila hapa silizungumzii kwa taswira
hiyo.
Ndoa:
108
|
Unaweza
ukaona taswira hiyo kwamba Mapepo haya yana mathara makubwa kiasi gani katika
kusambaratisha ndoa za watu.
Namna ya
kuishi na Mwanadoa mwenzako mwenye Pepo Mahaba.
Inakupaswa
wewe unayenyimwa kuwa mvumilivu huku
ukilifanyia maombi swala hilo.
Sehemu sahihi zaidi ni kwa Mungu. Pia kama mwenzako ni muelewa kwamba hiyo siyo
hali ya kawaida bali inahitaji maombi ili mshirikiane kwa pamoja. Mapepo haya
pia huweza kumfanya hata mwenzako kutokupika au kufua, yaani kutimiza wajibu
wake kama mwanandoa na ukimuliza huwa mkali na mwenye majibu ya umizayo,
ingawaje baadaye hujijutia ila hurudia tena. Na kwa mwanaume huweza kuwa mkali
bila sababu ya msingi kumpiga mke, kumtukana au kuchelewa kuja nyumbani na pia
kupoteza mvuto mkewe. Lakini katika kupoteza mvuto au upendo huweza kuchangiwa
na matendo ya mwezake kama ndiye mwenye mapepo hayo. Zaidi soma kipengele cha Dalili ya ndoa yenye mapepo mahaba kilichopo
kurasa zinazofwatia.
Mara baada ya kuota hujikuta
unamchukia mwenzako bila sababu za msingi. Jini Mahaba huwa na tabia ya wivu sana na hii ndiyo
inayochangia kumfanya mhusika kuwa na chuki kuu kwa mwenzi wake.
Kutamani kufanya tendo hilo na mtu
mwingine angali mwenzako yupo. Pepo hili huwa na tabia za kumtamani mtu yeyote limpendalo
na huambukiza au hutumia mwili wa aliyeukalia. Utamkuta mtu ana upendo wakipepo kwa mtu fulani wakati ndani mwenzake
yupo. Na hata sio mwanandoa hujikuta akitamani watu ambao sio utashi wake
kufanya hivyo
Kuishiwa nguvu au hamu ya kufanya
tendo hilo na mwenzako. Kuna mwanaume mmoja aliyekuwa na hali hii ambayo kiungo chake husika
kilishindwa kuwa katika hali ya tendo. Ila mke wake alikuwa ni mtu wa kiroho na
kusema “hali hii sii ya kawaida”. Alikishika na kufanya maombi, mara baada ya
muda hali ikarejea na kuwa kawaida.
Ikimkuta
mwanamke hali hii huweza kumfanya kutokuwa na ladha na tendo husika na pia
kumuona mwenzake kama anamsumbua au kumpotezea muda. Hali hii ikiongezeka au
kukomaa huweza kusababisha ugomvi wakati wa tendo au mmoja wapo anapohitaji na
Pepo hili likikomaa ndani ya mtu muhusika huweza kumtharau mwingine au kumtusi
kwa maneno.
Pamoja na Utasa ama Ugumba, Kumekuwa na kilio kikubwa kwa
wanandoa kukosa watoto na mara nyingi tatizo hilo huwa ni matokeo ya ndoa hiyo
ama mwanandoa kutawaliwa na Pepo mahaba. Linaweza kupata uwalali kwa njia
nitakazokujuza kwenye kipengele kijacho ama kwa mtu kumwendea mwenzake kwenye
njia za kishirikina ili kumfunga ikiwemo kwa waganga wakienyeji ama kumloga.
Katika hayo yote ipo Damu ya Yesu iwezayo kumkomboa huyu mtu na kumbuka katika
sehemu yangu ya kwanza ya makala hii nilimtaka mlengwa anayesumbuliwa na Mapepo
haya kuokoka kwani ni njia kuu ya ukombozi na kama ameshaokoka ya mpasa
kusimama kiroho na kupambambana kimaombi. Pia nitakuelekeza namna ya kuomba
ndio maana nikakwambia ni somo la NAMNA AYA KUJINASUA.
MLANGO
UNAOWEZA KUIFUNGUA NDOTO YA MAPEPO MAHABA.
(1) Uhalali wa kuridhi, Kitovu chako hakikukatwa, wala
kuoshwa kwa maji na kutiwa chunvi, maana yake ipo nguvu ya kurithi
inayoyasumbua maisha yako. Kwani kitovu huwakilisha hali ya kuridhi maana mtoto
hulishwa na mamaye kupitia kitovu. Na maji ni utakaso wa Roho Mtakatifu na
chunvi huondoa mapooza. Kwa hiyo kama nyumbani kwenu kuna tatizo litokanalo na
Pepo mahaba ama roho ya Pepo huyu inakalia jamii ya kwenu ama kabila au eneo
ulilopo ni fika adui huyu huweza kukusumbua ndotoni na mlango mkubwa ikiwa ni
hali hii.
Dalili/Ishara
zitakazokujulisha uwepo wa Pepo Mahaba kwa njia ya Uridhi.
(….Tuonane Kesho)
Pasina shaka umependezwa na kujengwa
na ujumbe huu katika sehemu hii ya pili, kipengele nilichokudokezea hapa
mwishoni ndiho tutakacho anza nacho kesho katika sehemy ya 3 ya ujumbe huu. Kwa
hiyo hakikisha unatufwatilia. Na Mungu akubariki.
Hongera kwa
kuokoka na tafuta kanisa la watu waliokoka ukasali hapo.
Na Huduma ya
UKOMBOZI GOSPLE, Arusha Tanzania, Kwa Maombi, Ushauri, Maswali au Sadaka
wasiliana nasi, Barua pepe: ukombozigosple@gmail.com
Simu: +255 759 859 287 pia waweza itumia kwa M-PESA. Zaidi www.ukombozigospel.blogspot.com #UkomboziGosple #MwalimuOscarSamba
Pia #Like
#Penda Page/Ukurasa wetu au kundi la Fb, ili kupata habari hizi kwa haraka,
zaidi. Ug Ukombozi Gosple,
PAGE: https://www.facebook.com/Ug-Ukombozi-Gosple
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni