Jumatano, 26 Agosti 2026

#UMUHIMU WA KUFANYIKA KWA TENDO LA NDOA (Kibiblia)

Na _Mwl Oscar Samba_ . Ningepewa nafasi ya kuandika au kuandikwa kwa amri kumi za ndoa, ningeanza na Mosi, #Msinyimane ; 1 Kor. 7: 5. Pili Na Malazi Yawe #Safi; Waebrania 13:4..(Usafi wa Uaminifu Katika Ndoa). Tatu #Hakikisha Mwenzi Wako #Ametosheka, Ukiwiwa kuniongezea basi shiriki nami katika eneo la maoni au "comment". Kwa moyo mkunjifu kabisa ninawiwa kukaribisha katika makala hii fupi *(eBook)* inayozungumzia umuhimu na thamani pamoja na sababu za tendo la ndoa. Imizo kubwa lipo kwa wanandoa kukutana; nje ya wanandoa ni chukizo na uovu mkubwa mbele za Mungu. Katika somo hili au makala hii, jiandae kufahamu kiupana zaidi kuhusu vita, au ni kwa nini Shetani hufanya vita katika tendo hili la ndoa. Lakini utafahamu kiupana na kiunaga ubaga nini huwa kinatokea kipindi cha tendo la ndoa! Hali itakayokuimarisha zaidi katika kufahamu kiundani sasa ni kwa nini Shetani analipinga au anapiga vita sana jambo hili la tendo la ndoa. Kiroho tendo hili lina maana gani? Hakika jiandae kutokuwa mtu wa kawaida mara baada ya kulifahamu hili jambo. Maarifa ambayo yatakuongezea thamani katika tendo hili. Ufanisi wake ni dawa, ni tiba, ni kiungo katika kuleta umoja; linatimiza dhima ya mwili mmoja. Naungana na wanasaikolojia kadhaa kuhusu mitazamo yao katika thamani ya tendo hili. Mmoja aliwahi kusema ya kwamba, tendo hili likifanywa kwa ufanisi, huijenga ndoa kwa asilimia 15 na likikosekana au ufanisi ukipungua huwezakuibomoa ndoa kwa asilimia 85. Kwa hayo na mengine mengi nikukaribishe. Lakini pia, ukitulia katika ujumbe huu; utaweza kufahamu japo kwa sehemu ni kwa nini majini mahaba au mapepo mahaba hupenda kuzini au kufunga ndoa za kiroho na wanadamu! Kuna jambo gani wananufaika nalo? Hata vita vingi vya kiutumishi, huhusisha maswala ya kuota au kuzini katika ndoto. Ambapo kama kesho mhusika ana hudumu mahali, basi akiota hivyo anajikuta nguvu katika ile huduma hazipo kabisa. Kwa nini? Kuna jambo lipo katika maingiliano ya namna hii. Na sababu za watu baadhi wanapotaka kumuadhiri mtu, au kuiba mafanikio yake kwa jinsi ya kishirikina; kupewa masharti ya namna hii..ikiwemo kuzini na mtu husika, na hata kuwatumia mapepo ya kuzini nayo! Na hii ndiyo inayompa au inayowapa mapepo mahaba kuwa vinganganizi sana katika maisha ya mtu. Maana wanajua siku akifunguliwa hapa, na mipaka yake ya kiutumishi, kiuchumi au kibiashara ama katika mahusiano itafunguka. Ipo siri kubwa tu hapa. Karibu Tujifunze; #Muktadha wa Tendo la Ndoa na Tendo Lenyewe Kiroho. 1. Huijenga Nafsi. Kama Biblia inalitaja kama tendo linaloweza kubomoa nafsi, kuijerui au kuweza kuifikia nafsi na kuidhuru: endapo litafanyika katika mazingira ya nje ya ndoa; basi uwe na hakika likifanyika katika mazingira sahihi, huijenga nafsi. Huwa na dhima ya kuiimarisha hiyo nafsi. Tujione katika mazingira ya tendo hili pale linapofanywa katika njia haramu, au njia isiyokuwa sahihi. Mithali 6:32 Mtu aziniye na mwanamke hana akili kabisa; Afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake. 33 Atapata jeraha na kuvunjiwa heshima; Wala fedheha yake haitafutika. Atapata jeraha na kuvunjiwa heshima! Kinyume chake ni kwamba, tendo hili huleta uponyaji wa moyo au ndani, na kujenga heshima. Sasa heshima hii huweza kuwa katika ndoa, yaani baina ya mume na mke, lakini pia huwa miongoni mwa jamii. Hutumia neno kibali katika maana ya namna hii. Mke akimheshimu mumewe, kiroho ni anamtengenezea kibali. Tukio la malikia Vashtii kumdharau mfalme, sio kwamba lilikuwa linawafanya wanaume wengine kudharauliwa tu, bali lilikuwa na lengo pia la kuivunja au kuishusha heshima ya mfalme kwa watu wake wa karibu na jamii pia. #Tendo la ndoa limewekwa ili kujenga na kudumisha heshima. Sijasema wale wanawake wanodharau waume zao sabau ni kukosekana au kuzorota kwa tendo hili. Na wala sijasema ya kwamba likikosekana au kukiwa na udhaifu basi heshima lazima ipotee. Ila hii haiwezi pia kuondoa ukweli ya kwamba jambo hili likifanyika katika ufanisi wake; heshima haikosekani. Hali inayozaa kibali. Katika mke kuna kibali, ambapo huchipuza kutoka kwake na kuonekana kwa jamii. Adui akitaka mara nyingi kukukosesha kibali kwa watu, huanzia ndani. Na kutoka ndani, huweza kukikuza kwa nje, yaani kwa jamii. #Tazama Hapa; Mithali 18:22 Apataye mke apata kitu chema; Naye ajipatia kibali kwa BWANA. Hapa anasema kwa Bwana, uwe na hakika hata kwa wanadamu pia. Mke si mtu, ingawaje anyeolewa ni mtu wa jinsia ya kike yaani mwanamke. Ila anapokuwa mke, sio swala la mtu. Bali ni swala la nafasi. Ndoa ndiyo inayozaa nafasi itwayo mke (wife). Kwa hiyo, swala la heshima ya tendo la ndoa ni muhimu katika nafasi ya mke (ambayo amepewa mwanamke). Nakufundisha hili, ili uwe mwepesi wa kuelewa ni kwa nini adui Shetani anapotaka kupigana na kibali kilichopo juu yako mara kwa mara hukimbilia kwanza kwenye ndoa. Na akikwama hapo ni amekosa kitu kikubwa sana. #Muhimu : Ni muhimu kufahamu ya kuwa sii kila heshima inazalishwa na tendo la ndoa. Maana heshima ni heshima kwa sababu ni heshima. Lakini ukweli ni kwamba, kuna aina ya heshima inayozalishwa katika tendo la ndoa. Sio swala la kumridhisha au kumfikisha tu mwenza wako kileleni; (japo ni muhimu sana) bali ni swala la yeye kulifurahia tendo hilo na kuridhika. Kwa maana kwamba, jambo la uaminifu ni muhimu. Maana nafsi ikigundua mwenzake sio mwaminifu; hujeruhiwa. Na heshima ya namna hii haiwezi kuzalishwa kutoka katika nafsi ya mwenzako (iliyoumia) wala nafsi yako (ambayo pia dhambi hii imeijerui). Lakini pia, kwa wale wanandoa ambao wameoa au kuolewa ama wenye vifungo vya mapepo mahaba, ni vigumu kufikia aina hii ya utoshelevu. Kileleni anaweza kufika, ila ile hali ya kuridhika ndani yake isifanikiwe kufikika. Nawiwa pia ujifunze, Shetani anapoleta upinzani au pingamizi katika tendo la ndoa, ni kitu gani anakiwinda! Ili ikupe kujifunza kupambana naye, usiuchukuli udhaifu wowote kama sehemu au jambo la kawaida. Badala yake ujifunze kuukabili kiroho. #Atapata #Jeraha! Tumeangazia eneo la heshima, sasa tuangalie eneo la jeraha. Kinyume chake ni uponyaji. Wanandoa watakubaliana na mimi kabisa ya kwamba kati ya eneo ambalo huwaunganisha watu vizuri na kuwafanya warudi katika upendo wa awali, ni suluhisho linaloletwa au kuzalishwa kitandani. Tendo la ndoa, hujenga ndoa, huunganisha wanandoa. Huponya ndoa. Ndio maana mtu anapozini, yaani anapotoka nje ya ndoa, inafananishwa na kujaribu kuziachanisha karatasi mbili zilizounganishwa au kuambatanishwa pamoja kwa kupitia gundi. Hali ambayo huzifanya kuraruka na kuzalisha jeraha. Ndoa huunganisha nafsi, unapotoka nje ya ndoa ni unajaribu kuzitenganisha. Agano la ndoa ni kama gundi. Kwa hiyo, kunapotokea mikwaruzano midogo midogo na hata ile mikubwa mikubwa; tendo hili hutumika katika kuleta suluhisho. Kwa hiyo, likikosekana au likikosa ufanisi; uwe na hakika ni mnapokonywa mahakama ya amani ndani ya nyumba. Mungu ametupa hakimu mwema, ambaye hukumu yake ni mapatano bila adhabu. Ndio maana wanandoa wanashauriwa hata wakikwazana haipaswi kunyimana. Maana katika kupeana ndiko kunakozalisha hali ya kuelewana au kupatana. Adui Shetani asingetamani kuiona mahakama hii huru ikiendesha kazi zake vizuri. Maana anajua tu itakwamisha mipango yake. Ndio maana wanandoa wengi, husani mama zetu, wakikwazika hawataki hata kusogelewa! Hili ni tatizo. Ananuna katika kuongea hadi kufungua duka. Duka linafungwa na huduma hakuna. Inakulazimu mwanaume ubadilishe mboga ya dagaa na kuleta nyama, uvunje bajeti na kuja na zawadi ya kitenge au wigi jipya! Hapo ndipo duka litafunguliwa. Zawadi haipaswi kuwa kipatanishi! Kitanda kina nafasi hiyo. Wenye akili, wakiona tu siku haijashinda vizuri, basi wanaimalizia ishee salama na kwa wema kabisa. Siri ni matumizi mazuri ya sita kwa sita. Hakimu huyu hana hukumu ya hila. Ukiona unategemea zawadi, basi umekuwa hakimu mla rushwa. (Sipingi zawadi, ila zawadi sio mbadala). 2. Huimarisha Akili. Kumbuka katika andiko lile, husema aziniye na mwanamke hana akili kabisa. Kwa hiyo jambo la kuzini, linaadhiri akili. Kwa lugha nyingine ni kwamba, tendo la nje ya ndoa au tendo haramu huhusisha akili au ni tatizo la kiakili. Na kwa lugha sahihi ni kwamba tendo la ndoa hujenga akili, ama ni matokeo ya akili njema. Ninachotaka kusema ni kwamba, tendo la ndoa huchangia kujenga afya ya akili. Sio katika eneo la kumuondolea mtu tu msongo wa mawazo, bali ni katika kumjengea pia uwezo wa kufikiri, na kupanga mipango yake vizuri. Ukimnyima, usilalamike uchumi ndani kuwa mgumu au usijilaumu kwa mwenzio kuwa na matumizi mabaya ya fedha. Kwa maana kisababishi ni wewe. Uchoyo wako ndio uliompelekea ashindwe kufikiri vizuri. Kile ni sawa na kiburudisho au tukio la utalii, mandhari nzuri hujenga afya ya akili. Ni sawa na kumtoa mtu "out" ni unajenga saikolojia njema. Ukitaka mwenza wako afikiri vizuri, wewe zidisha tu dozi ya sita kwa sita. Hakikisha inafanyika kiufanisi. Utashangaa hata uso wake umeanza kuondoa mikunjo. Wewe ndie uliyeshikilia funguo za kutokuzeeka kwake kabla ya wakati. Mahasira ya mara kwa mara, majibu ya mkato kwako na kazini ama jaziba za ovyo kwa watoto; ni matokeo ya afya mbaya ya akili. Dakitari ni wewe. Tendo hili sio mahakama huru tu; bali ni dakitari mzuri na mwenye tiba ya akili njema. Mpe bila kumbania bania. Utaona matokeo tu. Jambo hili linaiokoa pia nafsi; Mithali 6:32 Mtu aziniye na mwanamke hana akili kabisa; Afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake. Kuiangamiza nafsi ni nje ya tendo halali. Maana yake lililo halali huwa na dhima ya kuiponya nafsi. Lazima kutaka sana kujua kwenye nafsi kuna nini na nini? (Kitabu chetu cha SABABU ZA MUNGU KUTUTAKA TUSIJILIPIZIE KISASI na kile cha IMANI INAPOJARIBIWA), vitakusaidia kuifahamu nafsi kiundani. Mosi kwenye nafsi kuna akili, pili kuna hisia, ambapo ni hisia kama za kimapenzi, hasira, furaha, chuki na hata hisia za tamanio la tendo la ndoa. Maana kuna mahusiano ya karibu sana kati ya mfumo wa fahamu na nafsi. Akili ni kiungo muhimu katika mfumo wa fahamu na kipo katika nafsi. Ubongo upo katika mwili, viungo vya uzazi vina mishipa au upo mshipa wenye mawasiliano ya moja kwa moja na uti wa mngonau ubongo. Pia katika nafsi kuna maamuzi au utashi. Katika nafsi pia kuna fikra. Uwezo wa kufikiri. Lakini neno fikra lina upana kuliko neno mawazo, maoni au kufikiri. Fikra kwa kingereza hutumika neno "mindset" lenye maana ya kwamba mtu jinsi alivyo ni matokeo ya fikra zake. Hutengeneza mfumo wa maisha kwa mtu. Ukisikia kufikiri ni kuishi; basi kufikiri au mkusanyiko wa mawazo ambayo yanafanyika kama mfumo; ndio huitwa fikra. Kwa hiyo, tendo hili la ndoa salama huijenga nafsi. Sasa unaweza kuelewa ni vitu gani humo huweza kujengeka. Ndio maana mchungaji akinyimwa, usishangae na jumapili upako unakuwa mzito! Kwa nini? Katika nafsi kuna kiunganishi cha mbingu. Nafsi ni daraja la ulimwengu wa roho. Mambo ya Walawi hutuambia ya kuwa huo upatanishi kwa njia ya damu hunuia kuhuisha uhai katika nafsi. Uhai wa ndoa pia upo katika nafsi. Nafsi ni pumzi ya Mungu. Alipotuumba akatupulizia pumzi yake ndipo tulipokuwa nafsi hai. Sasa basi, kama ni daraja kati ya Mungu na sisi, uwe na hakika nafsi ikiwa vizuri, na daraja litafanya kazi vizuri. (Ndio maana Shetani katika ndoa za watu waliokoka hufanya vita sana katika tendo hili..ni ili nini? Avunje au adhoofishe kufikiri kwetu, akili ibada au avunje daraja kati yetu na Mungu). Na utaelewa sasa ni nini kinatokeaga, adui au mapepo mahaba yanapozini na mtu? Hususani aliyeokoka..kuna kitu kinapandwa, kuna daraja linanajisiwa...kuna roho ya mauti inapandwa ili kupingana na uhai wa ndoa, uhai wa mahusiano yetu na Mungu...ama uhai wa ustawi wa kimaisha.... Uchumi au utajiri ni nguvu...ndivyo Kumbukumbu la Torati 8, inatuambia. Inasema ya kwamba Mungu ndie anayetupa hizo nguvu za kupata la utajiri. Kwa hiyo, utajiri ni nguvu. Na nguvu hizi hazikai katika mwili, maana sio nguvu za kula ugali hizi. Kibali, heshima...fikra nyepesi kiuchummi (ni sehemu ya nguvu hizi) uwezo wa kuteka, kutawala na kumiliki katika ulimwengu wa roho ni sehemu pia. Kwa maana kwamba, sehemu zinapokaa ni katika eneo la nafsi. Ukitaka kujua ni kweli, tazama kipindi ambacho mhusika anaota ndoto za namna hii. Lazima mbele kuna jambo..ndipo utakapogundua ya kwamba sio ndoto au kuzini kwa kawaida, bali ni zinaa kama vita. Shetani hupigana na wewe kwa lengo la kukudhoofisha ili akushinde. Ananua fika ya kuwa, ukiwa dhaifu humuwezi. 3. Ni Tendo Linalofanyika au Kufanywa na Mtu wa Ndani na Mtu wa Nje. Wasomaji wazuri wa Biblia watakubaliana nami ya kwamba, zinaa ni miongoni mwa dhambi mbaya sana; maana hufanywa nje na ndani ya mwanadamu. Kati ya mafundisho mengi, hili ni moja wapo linalodhibitisha jambo hili; 1 Wakorintho 6:18 Ikimbieni zinaa. Kila dhambi aitendayo mwanadamu ni nje ya mwili wake; ila yeye afanyaye zinaa hutenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe. Mtu amegawanyika katika sehemu kuu mbili, mtu wa nje, ambaye ni huu mwili wa damu na nyama au huu unaoonekana. Yupo pia mtu wa ndani. Ambaye huhusisha nafsi na roho. Sasa ukizini ni umefanya kosa dhidi ya mwili wako wa ndani na wa nje. Dhidi ya mtu wa ndani na mtu wa nje. Nikikupa zawadi, nikakupiga kibao, au fimbo ni matendo dhidi ya mtu wa nje. Lakini zinaa huhusisha maeno yote mawili. Je, nataka kukwambia nini hapo? Kama zinaa hufanywa nje na ndani. Basi uwe na hakika na ndivyo ilivyo katika tendo la ndoa. Mtu wa ndani na mtu wa nje wote wawili hushiriki jambo hili. Hii ni faida kubwa sana na dhima muhimu katika musudio la Mungu kuliweka tendo la ndoa. Na laiti kama kanisa lingelijua jambo hili. Upande wa pili wanalijua sana, ndio maana hujigeuza na kulala na watu kwa njia za kimapepo mahaba. Wanajua wanachopanda ndani ya nafsi zao na jinsi silaha hii ilivyo sehemu kubwa ya mafanikio yao sio katika kuharibu tu maisha ya watu, ama kuitawala dunia; bali katika kulidhoofisha kanisa pia. Nasema kulidhoofisha kanisa maana kati ya keshi nyingi na za kisiri sana ni watu wa kanisani kusumbuliwa na zinaa katika ndoto. Na wengi wamedumbukia na kuzama kabisa, katika wimbi kubwa la kutazama picha za utupu; pamoja na kupiga punyeto. [Punyeto ni hali ya mtu kujichua au kujitosheleza mwenyewe kimapenzi aidha kwa kutumia vifaa au vidole vyake mwenyewe au mikono]. (Adui ana mhadhiri mtu nje na ndani.) Ndani kuna nafsi na roho yake. Unapolala na mwenzi wako, ni unafanya tendo ndani ya mwili na nje ya mwili wako. Viungo hivi ama tendo hili limepewa hiyo nafsi. Nasikitika kanisa linajua sana hatari ya dhambi ya uzinzi ama uasherati. Mtu kuanguka kiroho tunajua ni kosa kubwa sana. Lakini naumia kwa kanisa hili, hili kutokujua umuhimu wa tendo la ndoa linapopatikana katika usahihi wake kwa wanandoa na jamii. Pamoja na athari zake kunapokuwa na mushkeli dhidi yake. Mimi huwa nikiletewa malalamiko yoyote kuhusu ndoa, mara kadhaa sehemu yangu ya kuanzia utafiti wangu ni kutaka kujua kama tendo hili linafanyika katika hali ya ufanisi! Maana mtu wa ndani akipokea chakula hiki, kuna baadhi ya matatizo yatajitatua juu kwa juu. Mtu mwenyewe minyoo akiwa na njaa, anasumbua sana; lakini mtu huyu huyu mwenye minyoo akishiba; hutaona usumbufu. 4. Unafanyika Kuwa Mwili Mmoja na Mmke au Mume Wako. Maandiko yapo wazi kabisa ya kwamba, unapolala na kahaba unakuwa mwili mmoja pamoja naye. Kumbe tendo lililo haramu huweza kumuuunganisha mtu na kahaba. Basi ndivyo ilivyo kwa tendo sahihi, huweza pia kumuunganisha mtu na mwenza wake. Nao wakawa mwili mmoja. Wengi wanafikiri hii ni dhana ya kiapo cha kiagano cha ndoa tu. Mimi sikatai hilo, ila kuna maana pana zaidi ya hapo. Ambapo utimilifu wake upo katika tendo hili. Sheria za ndoa haitambui ndoa bila tendo la ndoa. Ndoa ni tendo la ndoa, (hiyo ni lugha ya kisheria). Sasa utaelewa ni nini huwa kinatokea kama Shetani akifanikiwa kuwafarakanisha wana ndoa katika hili tendo la ndoa? Hapana Shaka ni anafanikiwa kuwanyima umoja. Mshikamano, wnasalia kuwa wawili na sio mwili mmoja tena! Kwa hiyo, kuna hatari ya kuwa na ndoa ambazo ni wawili na sio wamoja. Nataka pia nikudokezee na swala ambataniahi hapa katika muktadha wa haya maandiko. *Tazama* ; 1 Wakorintho 6:15 Je! Hamjui ya kuwa miili yenu ni viungo vya Kristo? Basi nivitwae viungo vya Kristo na kuvifanya viungo vya kahaba? Hasha! Jambo lenyewe ni hili hapa, adui akifanikiwa kukuingiza katika wimbi la dhambi hii ya zinaa, uwe na hakika ni anamnyima Kristo Yesu kuwa na utawala katika mwili wako! Maana ndicho Paulo Mtume anajaribu kutudokesea hapa...na kwa wale wanaoota hizo ndoto, maana yake moja wapo ni kwamba; adui anapingana na umiliki wa Kristo katika miili yetu. Ukisoma maandiko yote utatambua anazungumzia kuhusu sisi kununuliwa na kuwa mali ya Kristo. Unajisi huu unanuia kuadhiri jambo la namna hii. Kwa lugha nyingine ni kwamba, Shetani anapigania umiliki wa mwili wako. Ili nini? Ni ili afanikiwe lile analolikusudia! Anauliza bapo katika huo mstari ya kwamba, je, avitwae viungo vya Kristo na kuwa viungo vya kahaba? Ufafanuzi ni kwamba, je atwae viungo hivyo ya Kristo na kuvifanya vimikiwe na roho iliyopo ndani ya kahaba! Sasa inategemea ni roho gani, kuna wengine wamebeba roho za kuua huduma au kipawa chako. Wapo waliobeba roho ya madeni. Wengine wananuia kukuibia kibali au kudhuru mbaraka wako (wanaita nyota). Wapo waliobeba magonjwa na kadhalika. _Tuendelee_ ; 1 Wakorintho 6:16 Au hamjui ya kuwa yeye aliyeungwa na kahaba ni mwili mmoja naye? Maana asema, Wale wawili watakuwa mwili mmoja. Hapa ndipo pale penye kiini chetu; natamani sana uelewe na unufaike na thana hii ya kukufanya kuwa mwili mmoja na mkeo au mwenza wako. Ukikwama hapa ni umekwama eneo kubwa sana, sana. 17 Lakini yeye aliyeungwa na Bwana ni roho moja naye. Katika sura ile nyingine, ni kwamba wale wanaozini, wanaungwa na kuwa roho moja na Shetani. Hili ni agano au patano katika uharibifu. Kwa hiyo, unapoota unazini katika ndoto ni muhimu kutaka kujua unaungwa na roho gani. Mfano, wapo wanaoota wanazini na baba, bibi au babu. Mama, mzazi shangazi na hata mjomba au mama mdogo na kadhalika. Wengine ni binamu, dada ama kaka na hata mpwa. Fahamu wazi ya kwamba kuna aina ya roho ya kifamilia au kutoka sio kwa mwanafamilia bali ni kutoka katika nafasi husika ya kifamilia unaunganishwa nayo. Kama ni roho ya kutokupata mtoto sawa, ni roho ya umaskini au kutokuolewa pia ipo. La muhimu ni kutaka kufahamu ni roho gani unaunganishwa nayo. (Roho Mtakatifu atakusaidia kuijua.) 1 Wakorintho 6:18 Ikimbieni zinaa. Kila dhambi aitendayo mwanadamu ni nje ya mwili wake; ila yeye afanyaye zinaa hutenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe. Maandiko yanapotoa agizo la wewe kuikimbia, ujue na kwenye ndoto akili zako zinatakiwa kufanya hivyo. Ukiona katika ndoto unaridhia kiwepesi, au ni hata ni wewe ndie unayetaka au kufurahia; uwe na hakika ya kwamba kiwango chako cha kuwa mateka au cha kukamtwa na hii roho ni kikubwa zaidi. (Mtu anapolala akili zake hazilali, maana nafsi pamoja na roho ndivyo huota ndoto; na akili zipo katika nafsi. Sasa nafsi iliyo mateka na fahamu za mhusika huwa mateka pia.) Ulimwengu wa roho ni wa kiroho, lakini nafsi yako ina nafsi ya kimaamuzi kama ingali huru.) Ndoto za kuota unakula vyakula zinahusika sana katika kubana akili au kuifanya nafsi iwe mateka. 19 Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe. Roho Mtakatifu anadhima ama jukumu la kuifanya miili yetu isiwe mali yetu wenyewe (maana ndio chapa au harabuni ya rohoni yaani anatupiga mhuri na kuwa hakikisho la Kristo katika kutumiliki). Kwa upande mwingine, ile roho inayokumiliki au uliyounganishwa nayo ina nafsi ya kukufanya kuwa mali ya roho husika. Ndio maana tuna wakristo wanaofanana na sanamu ya mfalme Nebukadreza. Huku shaba, kule udongo, huku chuma na kule dhahabu. Ibada wanapenda, uongo wanao. Kanisani wapo, usiku wanatazama picha za ngono. Uasherati haachi, na kushuhudia wanafanya. Uwe na hakika, wana wamiliki wengi. Na ishara wana wamiliki wengi, tazama aina ya ndoto wanazoota! Kama sio za kuzini basi ni za vyakula. Kuota unakula katika ndoto, ni unaunganishwa na vyakula vilivyotolewa sadaka kwa sanamu au mashetani. Kwa lugha nyingine ni vyakula ambavyo ndani yake vina roho nyingine. Ni meza ya mashetani. Vyakula vya kichawi. Kama meza ya Bwana ni chakula chema cha uzima, ndivyo ilivyo na meza ya mashetani. (Ndoto ni mlango wa kiroho). Na huwa mbaya zaidi kama utakula vyakula vya matambiko, vyakiganga au vya futari ya dini fulani. Hivyo huwa na nguvu zaidi. 20 maana mlinunuliwa kwa thamani. Sasa basi, mtukuzeni Mungu katika miili yenu. Kati ya kitu anachonyimwa mtu wa namna hii, ni Mungu kutukuzwa katika mwili wake. Usishangae hata uvaaji na unyoaji wake au mtindo wake wa nywele, na mavazi havimpi Mungu utukufu. (Usininukuu vibaya, sijasema kuvaa nguo fulani ni dhambi, wala kugusia unyoaji fulani...nimesema havimpi Mungu utukufu. Mimi kulala na nguo ya ndani chumbani kwangu sio dhambi...ila nikitoka nayo nje na kwenda nayo sokoni nina mnyima Mungu utukufu. Japo pia sio dhambi, ila ninamnyima Mungu utukufu. Maana halina heshima jambo hilo mbele za jamii, watu watajikwaa...na watu wakijikwaa Mungu hana utukufu. ) Mungu akikosa utukufu, na wewe utakosa utukufu. Hilo lishike daima. Ili ujue adhari za kuvaa na kunyoa kiholela holela. Nimesema Mungu akikosa utukufu na wewe utakosa utukufu...na utukufu wa Mungu ukipungua katikati yako...(Simalizii)... Watu wengi fundisho la mavazi wamekuwa wakilihukumu kiutofauti sana. Lakini nikufikirishe tu, kama katika dunia hii ungekuwa upo mwenyewe; kwani kutembea na nguo moja ingekuwa ni dhambi au tatizo? Naamini hata kutembea uchi kusingekuwa ni tagizo! Lakini kwa sababu ya watu wengine, tunalazimika kuishi katika namna fulani. Ukipuzia hapo; sawa: ila nakushauri sasa ungetafuta sayari yako mwenyewe ukaishi huko ili sasa uwe na uhuru wako binafsi. Mtu mmoja akasema nanyoa au navaa hivi kwa sababu mume au mke wangu anapenda. Mie namshauri, mvaliye mkeo au mmeo mkiwa wawili. Nyoa ukiwa naye, ukitoka mbele yetu hivyo, ujue sisi tutakwazika...na huo utukufu utakuondokea...(Sijaweka fundisho la mavazi hapa...na wala sio kusudio langu hata kidogo....nimeguswa tu kulichomekea hilo na wala lisikukwaze tafadhali maana nami sio wale wa misimamo mikali..... 5. Humnyima Adui Shetani Nafasi...andiko la kututaka tusinyimane...linakamilisha dhima na thana muhimu ya kwamba, kama hatutanyimana...Shetani anakosa nafsi ya kuipiga au kuivamia ama kuijaribu ndoa na hata familia. ...(Inaendelea..) 6. 7. 8. KITABU KINAENDELEA: Nikushukuru kwa Kuungana Nami Hadi Wasaa Huu... Kitabu Hiki Hakijafikia Tamati...Bado Kinaendelea...Ukikihitaji Utalazimika Kulipia Fedha za Kitanzania Shilingi Elfu 5....Nawe Utatumiwa kwa njia ya PDF kikiwa Kamili na Kikiprintiwa Tutawajulisha Pia... Àsante: Namba ya Mawasiliano: +255759859287 Oscar Samba Kama Bado Hujaokoka na unaguswa kufanya hivyo, Fuatisha Pamoja Nami Sala Hii ya Toba. #Sema; MUNGU BABA, NINAKUJA MBELE ZAKO, MIMI NI MWENYE DHAMBI, NAKUOMBA UNISAMEHE: AMENI. Hakikisha unatafuta kanisa la Watu Waliokoka Ukaabudu Hapo. Tumeunda Channel ya WhatApp, Tufolo; https://whatsapp.com/channel/0029Va827LBJENy9u6Enke1h Kwa Maombi: +255759859287 http://www.ukombozigospel.blogspot.com Kundi letu la WhatsApp https://chat.whatsapp.com/E0eD0xegh1eIGMjRykPyRD Telegram https://t.me/+fft3GHXC9xIzYjhk Subscribe YouTube yetu: https://www.youtube.com/@ukombozigospeltv Kwa Maombi +255759859287 Usiache Kutembelea na Ku-Like Page Yetu Ya Mafundisho ya Neno la Mungu Facebook: https://www.facebook.com/MafundishoyanenolaMungunamwalimuoscarsamba?mibextid=ZbWKwL UWE NA AMANI

Jumamosi, 6 Juni 2026

#MILANGO au #MAMBO 5 AMBAYO ADUI SHETANI HUYATUMIA KUVURUGA NDOA au AMANI KATIKA NYUMBA

1. #Hasira ...ni Mlango Hatari sana Pamoja na Uchungu...Vikikaa muda mrefu...Shetani Hupata Nafasi..(hugeuka na kuwandhambi)...Waefeso 4:26 Mwe na hasira, #lila msitende dhambi; jua lisichwe na uchungu wenu bado haujawatoka; 27 *wala msimpe Ibilisi nafasi . 2. #Kuzira au Kununa ...Wanawake wengi (wanaume pia wapo ila wachache) huwa na tabia ya kununa muda mrefu na hata wiki na wengine mwezi...Biblia huita ni upumbavu na kila penye upumbavu Shetani hupata mlango..Mithali 19:3 Upumbavu wa mtu hupotosha njia yake; Na moyo wake hununa juu ya BWANA. Ambapo hukupotosha njia zako...kwa wanawake wengi hufanya njia hii kama fimbo ya kumchapia mwanaume...lakini Mithali pia huita ni fimbo ya Kiburi...kila anayezira ana kiburi...(Huu ni Utafiti Nilioufanya wa Kisomi na Kitaaluma Kabisa...na katika Roho Mtakatifu...ukiendelea hivyo baada ya muda utajikuta mwenzako anapunguza upendo nawe...maana hali hii humuathiri katika nafsi yake...) Mithali 14:3 Katika kinywa cha mpumbavu mna fimbo ya kiburi, Bali midomo ya wenye hekima huwahifadhi. (Unamsemesha aongei...na wengine wanaweka mgomo hadi kwenye haki za msingi...UJINGA Kabisa huo). 3. #Kunyima au Kunyimana Haki ya Tendo la Ndoa ...tendo hili limewekwa na Mungu kama kiunganishi...maana kama anayeungana na kahaba anakuwa mwili mmoja naye...uwe na hakika anayeungana na mke au mume wake huwa kitu kimoja pia...sasa adui akifanikiwa kuwavuruga hapo ujue kashafanikiwa kuwatenganisha tayari...Paulo alishaonya hili...1 Wakorintho 7:5 Msinyimane isipokuwa mmepatana kwa muda, ili mpate faragha kwa kusali; mkajiane tena, Shetani asije akawajaribu kwa kutokuwa na kiasi kwenu. Adui Shetani Anapata Nafasi ya Kuwajaribu... 4. #Migogoro au Malumbano... Magomvi huondoa uwepo wa Mungu ...maana Roho wake ni wa Amani...Amani ni Tunda la Roho lakini Amani ni Yesu mwenyewe maana ni mfalme wa Amani yaani Salemu...Salemu ni Yerusalemu...ambapo hubeba pia Yerusalemu Mapya kama Mji na Nchi Mpya...Ufalme wa Mbinguni ni Sasa na Utimilifu wake ni Baada ya Unyakuo...kwa hiyo Utawala wa Kristo wa Amani Upo Sasa Kati Yetu...Ndoa ni Sehemu ya Kristo Yesu Kutawala...(Ni Kibiblia Kabisa). Fujo ni tunda la Shetani yaani tabia zake. 5. #Kukosa au Kukosekana kwa Ibda ya Pamoja ...umoja wa Roho ni Ulinzi...kumbuka ndoa ni wito...katika kila wito kuna kifungo cha amani...na Roho Mtakatifu ndiye msimamizi mkuu wa kifungo hiki...ndio maana kanisa au dhehebu likipoteza kifungo hiki...kuna namna umoja utatoweka tu...Soma maneno haya kwa sura ya ndoa kama wito...fahamu kabla ya dhambi kuingia ulimwengu ndoa ndilo kanisa la kwanza...mifumo mingine ya kikanisa ni matokeo ya dhambi kutuviruga....lazima ndoa ibebebkitu cha kikanisa kwanza ndipo iweze kufanikiwa...Soma; Waefeso 4:1 Kwa hiyo nawasihi, mimi niliye mfungwa katika Bwana, mwenende kama inavyoustahili wito wenu mlioitiwa; 2 kwa unyenyekevu wote na upole, kwa uvumilivu, mkichukuliana katika upendo; 3 na kujitahidi kuuhifadhi umoja wa Roho katika kifungo cha amani. 4 Mwili mmoja, na Roho mmoja, kama na mlivyoitwa katika tumaini moja la wito wenu. #Tutaendelea Wakati Mwingine Tukipata Neema .. _Imeandikwa na Mwl Oscar Samba Mwanza Tz Kama Bado Hujaokoka na unaguswa kufanya hivyo, Fuatisha Pamoja Nami Sala Hii ya Toba. #Sema ; MUNGU BABA, NINAKUJA MBELE ZAKO, MIMI NI MWENYE DHAMBI, NAKUOMBA UNISAMEHE: AMENI. Hakikisha unatafuta kanisa la Watu Waliokoka Ukaabudu Hapo. Tumeunda Channel ya WhatApp, Tufolo; https://whatsapp.com/channel/0029Va827LBJENy9u6Enke1h Kwa Maombi: +255759859287 http://www.ukombozigospel.blogspot.com Kundi letu la WhatsApp https://chat.whatsapp.com/E0eD0xegh1eIGMjRykPyRD Telegram https://t.me/+fft3GHXC9xIzYjhk Subscribe YouTube yetu: https://www.youtube.com/@ukombozigospeltv Kwa Maombi +255759859287 Usiache Kutembelea na Ku-Like Page Yetu Ya Mafundisho ya Neno la Mungu Facebook: https://www.facebook.com/MafundishoyanenolaMungunamwalimuoscarsamba?mibextid=ZbWKwL UWE NA AMANI

Ijumaa, 5 Juni 2026

MTAZAMO WA MUNGU/KIBIBLIA DHIDI YA ADUI AU WATESI WAKO.

Na Mwl Oscar Samba Ujumbe huu ni Sehemu ya Kitabu Chetu cha KWA NINI MUNGU ANATUTAKA TUSIJILIPIZIE KISASI? Nia kuu ya mada au kipengele hiki ni kukuwezesha ama kukujengea aina sahihi ya fikra dhidi ya aina ya watu wanaokutesa kutoka katika kona ya mbingu. Kwa nini? Itakusaidia kutokupambambana nao, kutokuwawekea kisasi wewe na kumuachia Mungu; lakini pia hutateseka kwa nini Mungu bado anawapenda (angali kwako ni mwiba). Ama kwa nini Mungu anakawia kuwaadhibu. Sababu za kukawia kwake zitakuwa wazi mbele ya fikra zako. Na hata sababu za Yeye kuwaruhusu kukutesa. Nakumbuka mie mwenyewe binafsi nilikuwa sijalielewa sana hili andiko la Yesu, lakini ipo siku nilikuja kulifahamu. Kuna jambo nililipitia kutoka kwa mkuu wangu la kuzuiliwa kuhudumu (kwa miezi kadhaa); na siku hiyo kuna namna nilipaswa kuchangia katika muda fulani kanisani: kumbe tayari barua ya kufurumushwa kazini ilishaandikwa: sikupata hiyo nafasi kabisa. Nikiwa nimekaa pale kwenye eneo letu maalumu: ndipo Roho Mtakatifu akanisemesha haya maneno. Ni andiko la Yesu dhidi ya mtu aliyepaswa kuitumia mamlaka yake kipindi cha kuteswa kwake. Lilinipanua kufikiri sana andiko hili; Yohana 19:10 Basi Pilato akamwambia, Husemi nami? Hujui ya kuwa mimi nina mamlaka ya kukufungua, nami nina mamlaka ya kukusulibisha? Yohana 19:11 Yesu akamjibu, Wewe hungekuwa na mamlaka yo yote juu yangu, kama usingepewa kutoka juu; kwa hiyo yeye aliyenitia mikononi mwako yuna dhambi iliyo kubwa zaidi. Nikajifunza kuyaona mapenzi ya Mungu katika ukatili ule. Ama nikajifunza kuuona mkono wa Bwana dhidi yangu au ukiwa upande wangu katika kipindi cha mateso ama moto ule. Kwa kifupi nilipata fikra pana zaidi kuanzia pale. Na ndipo nilipoelewa alipokuwa anapitia Yesu, na kitu ambacho Yesu alikuwa akikimaanisha. (Maandiko yanaposema mamlaka hutoka kwa Mungu, haina maana ya moja kwa moja kwa kila aliyeteuliwa au kuchaguliwa hutokakwa Mungu. Bali maana yake kubwa ni kwamba Mungu ndiye mwanzilishi wa mfumo wa uongozi na utawala. Swala la kiongozi kutoka wapi, na anamtumikia nani ni jambo jingine). Na Mungu huweza aidha kukuondoa katika mamlaka zao, au kuiondoa/kumuondoa mtumiaji wa mamlakanasiyeitumia kwa haki. Ile amekuacha hapo bado, endelea kumshukuru; maana pia angeweza kuhakikisha huo mfumo unapokea mtu ambaye angeendana na kusudi hilo japo maombi hayo ni muhimu sana kwa kanisa siku za leo: Asante. 1. Biblia Husema Yesu Aliteswa na Mungu. Kati ya jambo la ajabu na lenye maajabu yake lililowahi kunishangaza ni hili; eti maandiko hukiri wazi ya kwamba Yesu hakuteswa na waliomsulubisha! Hakika ilinishangaza sana hii. Tunafahamu waliopanga njama za kumkamata na kisha askari waliotumwa walitoka upande gani, waliomsulubisha na kupiga kelele asulubiwe, asukubiwe. Lakini katika mateso hatimaye kifo cha msalaba mbingu zinajinadi hizo ndizo zilizohusika na sio Wayahudi kadhaa na Shetani nyuma yao! Tazama; Isaya 53:4 Hakika ameyachukua masikitiko yetu, Amejitwika huzuni zetu; Lakini tulimdhania ya kuwa amepigwa, Amepigwa na Mungu, na kuteswa. Kwa wasomaji wa hicho kifungu wanafahamu kinazungumza habari za mateso ya Yesu Kristo. Maandiko yako wazi hapo kabisa ya kwamba ni Mungu. Sasa basi, kama mbingu zinajitwika tukio la wewe kuteswa, uwe na hakika hazina haraka kukuondoa kwenye mateso. Kama zinasema huo moto ni wangu; usijaribu kwenda kuita zima moto waje, (jeshi la zima moto na uokoaji). Maana watagoma na kusema tunaona mkuu wetu ndiye anayesimamia tukio la nyumba yako kuungua moto. Wanaishilia kukupa ile Isaya 43 ya kwamba maji mengi hayatakugarakiisha wala mwali wa moto hautakuunguza. Watakwambia ni moto kweli, ila hautakuteketeza; maana hata tofali la kuchoma lazima lipitie moto ili liimarishwe. Sasa yamkini unajiuliza ni kwa nini mbingu zinakuwa na lugha ya namna hii? Mosi ni kwamba, ndizo zilizoruhusu tukio hilo. Mungu asingeruhusu lisingekujilia. Kivipi? Nami nakuuliza kama unajua maana ya andiko hili? Soma;1 Wakorintho 10:13 Jaribu halikuwapata ninyi, isipokuwa lililo kawaida ya wanadamu; ila Mungu ni mwaminifu; ambaye hatawaacha mjaribiwe kupita mwezavyo; lakini pamoja na lile jaribu atafanya na mlango wa kutokea, ili mweze kustahimili. (Ukiwa katika jaribu zito; hilo neno Mungu ni Mwaminifu unaweza lisoma mara mbili mbili....) #IngawaNiKweliNiMwaminifu Nataka ujikite katika A, jaribu lililo ndani ya uwezo wako, B; kujaribiwa kwa kiasi au kipimo utakachoweza kustaimili na kisha C, Mungu ndiye mfanyaji wa huo mlanago au mratiibu wa namna ya wewe kutoka. (Nakupa "Home Work" ya kutafiti kwa nini neno uwezo na kiasi vimetumika pamoja, tafuta sababu...ukiweza nenda hadi katika lugha ya asili, pia soma tafsiri mbalimbali za Biblia.) Tuendelee: Hapo sasa, unijubu...je, huyu anayeweza kupima kiwango cha moto unaoweza kuivisha vizuri tofali anashindwa kuuzima huo moto? Uliwahi kupika chapati au wali katika jiko la gesi au umeme? Si kuna kiwango cha moto huwa unapima? Je, unayeweza kufanya hivyo unashindwa kuuzima huo moto kweli? Jibu ni kwamba Mungu angeweza kuzuia jaribu hilo. Anayeweza kufanya mlango au kuratibu namna ya wewe kutoka katika pito hilo unathani angeshindwa kukuzuilia usiingie katika hilo jaribu? Yaani aweze kuwa na mipango ya kukutoa, alafu akose mipango ya kukuzuilia usiingie! Laiti kama ungejua ni majaribu mangapi yanaandaliwa kwa ajili yako lakini BWANA Mungu huwa anayazuilia! Maana anajua hayana utukufu kwake, ama huyawezi au muda wake bado. Pili, Hataki Utukufu Umuendee Shetani ama Washirika Wake. Kati ya kitu muhimu katika Biblia ni kuhakikisha utukufu wote ni wa Mungu. Mbingu haziwezi kushiriki utukufu na Shetani hata siku moja. Kwa hiyo, hauwezi zisikia zikimsifia Shetani kwa kumpiga Yesu. Au kwa kukupitisha wewe, badala yake zitautaja mkono wa Bwana. Naye Shetani huwa mkimya maana anajua kama sio Bwana usingaliweza kutoka katika mikono yake salama. 2. Kinachokufanya Wakutese ni Kusudi Ulilobeba. Hii nayo ni ajabu nyingine. Ndio maana mtazamo wa mbingu ni tofauti kabisa na wawalio wengi inapofika eneo la namna hii. Mungu hawatazami sana watesi wako, badala yake hujikita katika kulitazama kusudi ulilobeba. Na anachokiona ni wewe kupitishwa kwa ajili ya aidha kuandaliwa kuwa mtu sahihi katika kuweza kuubeba huo mpango wa Mungu; ama kupitia huko kuna mchango gani katika kukamilishwa kwa kusudi. Yesu aliteswa kwa ajili ya kuzalisha ukombozi wa wanadamu. Kupigwa kwake kulifanya damu kuvuja. Damu ilipomwagika ndipo kusudio lilipotimia. (Umejionea hiyo siri hapo?) Ndio maana maandiko hayakumuona Shetani wala kikundi kile cha Wayahudi wakorofi kilichomkamata na kumsulubisha. Bali kiliona kusudi la ukombozi ndani ya yale mateso. Na kwako, mbingu haziwaoni watesi wako, bali zinaliona lile kusudi lilokufanya kupita hapo. Soma Tena Andiko Hili Katika Sura Hii na Mtazamo Huu; Isaya 53:5 Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu, Alichubuliwa kwa maovu yetu; Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona. 6 Sisi sote kama kondoo tumepotea; Kila mmoja wetu amegeukia njia yake mwenyewe; Na BWANA ameweka juu yake Maovu yetu sisi sote. (Ukiijua siri hii, kuna aina tofauti sana za fikra zitakufunika...utajifunza kulinda heshima ya mbingu pamoja na kusudio linalokupitisha hapo. Heshima ya mbingu kwa maana kwamba, kuna namna utamzuilia Shetani kupata utukufu. Kuvuka kwako kutakuwa kipaumbele kikubwa ili mbingu zipate heshima yake. Kisasi hakiwezi kuwa sehemu ya kipaumbele chako hata kidogo. Na badala yake utakiacha kwa Bwana Yesu Kristo mwenyewe...Amina) NB: Katika kuunganisha pointi iliyopita na hii, mistari hii ijayo, inatuambia mambo muhimu sana. Anasema Bwana aliridhia...umeliona hilo neno hapo? Ni kwamba mbingu zilikubali...kukubali ni ni? Yaani kuteswa kwa Yesu hakukuwa kwa bahati mbaya...kuna kikao kilikaa na kupitisha ajenda hiyo. Kama una Biblia yako hapo tafadhali pigia mstari hayo maneno Bwana aliridhia. Na mstari huo upige moyoni mwako ya kwamba Bwana ameridhia pia wewe kupita hapo unapopita... Tazama; Isaya 53:10 Lakini BWANA aliridhika kumchubua; Amemhuzunisha; Utakapofanya nafsi yake kuwa dhabihu kwa dhambi, Ataona uzao wake, ataishi siku nyingi, Na mapenzi ya BWANA yatafanikiwa mkononi mwake; 11 Ataona mazao ya taabu ya nafsi yake, na kuridhika. Kwa maarifa yake mtumishi wangu mwenye haki Atawafanya wengi kuwa wenye haki; Naye atayachukua maovu yao. (Swala la ukombozi lilikuwa na thamani kuliko mateso ya msalaba kwa Yesu. Na kwako ndivyo ilivyo...ya kwamba kesho ya utumishi wako ina thamani kubwa kuliko leo unayoitesekea....niamini mimi...kama tu kitabu hiki kinakusaidia...uwe na hakika nisingepita utukufu huo usingalikuwa juu yako.) Kumbuka tena...Mungu aliridhia....Kati ya kitu Shetani angetamani usione, ni wewe kumuona Mungu katika kupitishwa kwako. Huwa anatamani umuone yeye Shetani katika pito hilo ili azidi kujitutumua zaidi.....ila fahamu Mbingu Zimeridhia kupita kwako hapo....na ni jambo la muda kitambo tu. 3. Wanaokutesa Hawakutesi Wewe, ni Wanamtesa Yesu Mwenyewe. Kati ya maajabu niliyoyagundua katika Biblia kipindi cha somo hili; basi pointi hii nayo ilinishangaza mno. Yesu anamwambia Paulo Mtume mbona unaniudhi...Biblia ya Kingereza ikatumia neno mbona unanitesa...Paulo akauliza u nani wewe Bwana...Yesu akamwambia ni mimi Yesu unayenitesa...! Maajabu na kweli, tukitazama tunamuona Paulo akilitesa kanisa, akiwatesa watakatifu wa Yerusalemu na hata hapo alikuwa akiwafuata walipotawanyikia...lakini Yesu haoni hivyo. Anamuona Paulo aliyekuwa Sauli akimtesa...kumbe wanapokufanyia mabaya hawakufanyii wewe, bali humfanyia Mungu mwenyewe aliye mbinguni! Hii ni ajabu kabisa, kabisa. Tazama; Matendo ya Mitume 9:4 Akaanguka chini, akasikia sauti ikimwambia, Sauli, Sauli, mbona waniudhi? And he fell to the earth, and heard a voice saying unto him, Saul, Saul, why persecutest thou me? In simple terms we cana say, why do you perscute me? Kwa nini unanitesa...Kwa kiswahili neno linalotumika ni kuniudhi...kingereza ni kunitesa. Matendo ya Mitume 9:5 Akasema, U nani wewe, Bwana? Naye akasema, Mimi ndimi Yesu unayeniudhi wewe. Umeuona huo mtazamao? Ndiposa kisasi unapaswa kukiruhusu kuwa cha Bwana, maana mateso hayo ni ya Bwana na sio yako wewe hapo. Mwewe anaponyemelea banda la vifaranga, pigo hilo ni lako wewe, ingawaje kinachowindwa ni kifaranga; na ingawaje kifaranga na mama yake na kuku wengine utawasikia wakipiga kelele. Fisi anapowinda kondoo au mbuzi wako, pigo hilo ni lako wewe; ingawaje anayekuwa hatarini ni huyo mfugo wako. Na ndivyo ilivyo kwa Mungu wetu, alivyo dhidi ya pigo au teso lolote juu y tu. (Kumbuka tusingekuwa wake, tusingeteswa...kwa hiyo tunateswa kwa ajili yake na kwa sababu sisi ni wake Yeye.) Soma Hapa; Luka 10:16 Awasikilizaye ninyi anisikiliza mimi, naye awakataaye ninyi anikataa mimi; naye anikataaye mimi amkataa yeye aliyenituma. Unaniambia Mwalimu Oscar lakini adui hawa wamenitenda moja mbili tatu..! Ni kweli, maana hata Sauli alilitawanya kanisa kule Yerusalemu, aliwaua wateule wengi na kuwatesa kabisa kabisa....na hata Stefano alikufa mikoni mwake...lakini kwa kazi hiyo injili ilienea zaidi.(Vua mtazamo wako na utazame kimbingu zaidi...) 4. Anayepigana na Kusudi la Mungu Ndani Yako, Ni Anajaribu Kuupiga Mwiba au Kitu Chenye Ncha Kali Mateke. Yesu anamwambia Paulo (Sauli) neno gumu kabisa, ya kwamba hawezi kufanikiwa kuendelea kulitesa kanisa. Na anachokifanya ni anajiumiza yeye mwenyewe. Anamwambia ni sawa na kujaribu kuupiga mchokoo teke. Wengine husema ni mti wenye miiba mikali sana, ukija katika lugha kadhaa utaambiwa pia ni kitu chenye ncha kali kama sindano, na kwa wengine ni kifaa cha kulimia au kuchimbua aridhini ambacho hukokotwa aidha na wanyama au gari maalumu ambacho huwa na ncha kali sana....sasa ndicho ambacho Sauli anajaribu kukipiga mateke. Kikawaida kabisa ni nani anayeweza kupiga mateke au kupigana na mti wenye miiba? Haiwezekani hata kidogo, kabisa kabisa. Mungu ndivyo anavyowaona adui zako. Ndio maana kila mara wanakuchukia tu! Hata wakikutesa mara baada ya hapo unafikiria wataridhika kumbe badala yake chuki ndo inazidi kuendelea...! Ni kwa nini? Kwa sababu walipokupiga, kuna kitu kimewachoma...walipokurushia teke wamekutana na mchokoo ukawadunga...sasa maumivu yake yanawapa hasira....(Ni ukweli nakueleza...hili ndilo jibu lake.) Tazama; Matendo ya Mitume 26:14 Tukaanguka nchi sote, nikasikia sauti ikisema nami kwa lugha ya kiebrania, Sauli! Sauli! Mbona waniudhi? Ni vigumu kwako kuupiga mateke mchokoo. 15 Nami nikasema, Wewe u nani, Bwana? Bwana akaniambia, Mimi ni Yesu, ambaye wewe unaniudhi. 5. Wapende Adui Zako, Waombee na Uwatendee Yaliyo Mema. Biblia inatutaka kuwapenda adui na wale wanaotutesa au kutuudhi. Hili nalo ni jambo la kushangaza katika hali ya kawaida. Lakini ndivyo ilivyo na inavyopaswa kuwa. Mosi kisaikolojia itakusaidia kuepukana na makosa ya hasira na hamaki. Mtu anapokuwa mtesi, kuna hatari ya kukufanya kukosea. Majibizano ya maneno, kinyongo na hata kujikuta umeingia mwilini na kupigana au kutumia upanga kama Petro wakati wa kukamatwa kwa YESU. Lakini Biblia pia inatoa sababu zake muhimu...kwanza tulione andiko na kisha sababu zake.. Andiko; Mathayo 5:44 lakini mimi nawaambia, Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi, Anaendelea n kutoa Sababu; 45 ili mpate kuwa wana wa Baba yenu aliye mbinguni; maana yeye huwaangazia jua lake waovu na wema, huwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki. A. Tupate kuwa wana wa Mungu wetu aliye mbinguni. Kwa hiyo, ukiwatendea hivyo adui zako, ni unakuwa mtoto wa Mungu. Kwa maana kwamba, kama ukitenda kinyume chake kwa kuwachukia, kuwawekea kinyongo na hata kunilipizia kisasi ni unakuwa mtoto wa nani vile...? Ni mtoto wa Shetani aliye wapi...? Aliye kuzimu...na ukiwa mtoto wa huyo jamaa uwe na hakika utatenda yampendezayo huyo baba yako wa kambo..ambapo ni husuda, chuki, kulipiza kisasi na kadhalika... B. Anatuambia ili Tuweze Kumfanania Mungu Kitabia...anasema ya kwamba Yeye huwanyeshea mvua wema na wabaya...jua lake huwaangazia watu wote. Sijui kama unajua maana yake hii? Kuna viongozi ambao huwapandisha vyeo watu ambao wanawataka wao, watu ambao ni marafiki zao...ila wale ambao huwapinga na kuwakosoa hawawezi kupata kibali kwao hata kidogo. Wale wanao wasifia hata katika makosa yao, hao ndio ambao zikija nafasi za marupurupu hutumwa...kazi za sulubu hupewa wale ambao hunyoosha sentensi, ambao nyeupe ni nyeupe na nyeusi ni nyeusi huwa katika kundi la kifo...kundi la mateso na upinzani mkali...kundi la sulubu. Ila Yesu kwake sivyo, watu wote ni sawa. Hata ambao ni watenda dhambi...ndio maana tunapaswa kuwa na mtazamo sahihi sio dhidi ya adui zetu tu, bali hata maasimu wetu. Hili ni swala muhimu sana kulifahamu. Tabia ya namna hii ingekwepo kwa viongozi wetu wa kisiasa leo, makanisani, makazini na kadhalika; kuna aiana ya mateso ambayo watu hupitia wasingeyapitia kabisa, kabisa. C. Ni ili tuweze kujipatia thawabu. Tuzo au kutuzwa na Mungu. Kuna aina ya neema au baraka kutoka kwa Bwana inakuwa juu yetu. Kwa maana kwamba kama hutendi hivyo, kuna aiana fulani ya hii neema utaikosa. Soma;Mathayo 5:46 Maana mkiwapenda wanaowapenda ninyi mwapata thawabu gani? Hata watoza ushuru, je! Nao hawafanyi yayo hayo? D. Sehemu B ya hilo andiko hutujuza kuwa ni ili Tusifanane na Watu Wasio Mjua Mungu. Yakwamba wapagani hutenda kama hayo. Sasa nasi tunapaswa kufanana na kundi la Mungu. Hii nayo ni siri muhimu sana katika kanisa la leo. Na kiukweli ni kwamba viongozi wengi wa kiroho wamekuwa na kasumba za namna hii. Kanisa lina hali mbaya sana... Mathayo 5:47 Tena mkiwaamkia ndugu zenu tu, mnatenda tendo gani la ziada? Hata watu wa mataifa, je! Nao hawafanyi kama hayo? F. Inatupatia Ukamilifu wa Kiungu. Sijui kama unaelewa fundisho la ukamilifu wa Kristo? (The Doctrine of Perfecion in Jesus Christ or Doctine of Christ Likeness). Waefeso ile 4 ndiyo inayotupatia mtaji wa namna hii muhimu. Ya kwamba tukue katika kimo na cheo cha kumfahamu Yesu Kristo, ili tuweze kumfikia Yeye. Kila mkristo kipimo chake muhimu ni kumfikia Kristo Yesu. Hapo ndipo tunapotaka kufika. Sasa maandiko hutuambia ya kwamba, kama tukimjua Yesu kwa "staili" ya namna hii katika kuchukuliana na adui zetu, basi tutafanikiwa kukua kiroho. Kumbe maisha ya kinyongo, kisasi na hata husuda ni matokeo ya uchanga kiroho! Hii ni siri kubwa sana ambayo huachi kuijua. Tazama Andiko; Mathayo 5:48 Basi ninyi mtakuwa wakamilifu, kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu. 6. Ni Mtumishi Wake Mteule. Wakati wewe unamuona ni mtesi, (kweli ni adui sikatai) muda huo, huo mbingu zinatazama kilichomo ndani yake. Wanadamu tuna tabia ya kutazama sana madhaifu ya watu, mapungufu na hayo maudhi kutoka kwa mtu hufanyika zuio kwetu. Tunamuweka mtu katika kundi la kukataliwa moja kwa moja. Lakini Mungu hutazama mambo yote mawili. Sura zote mbili ni muhimu sana kwa Mungu. Na hiki ndicho kinachomfanya kuwavumilia watu, na kuzidi kuwavuta na neema yake iokoayo. Kuna watumishi wa Mungu hivi leo, lakini hapo awali walikuwa wauaji, watesaji,.majambazi na wengine ni wachawi ama waganga walioua na kutesa watu wengi sana. Sasa unaonaje katika nyakati kama hizo kama Mungu angewafutilia mbali! Yamkini hata wewe kabla ya neema uliwahi kuwa mtu wa hivyo. Na inawezekana hata baada ya neema kuna maisha ya kikatili uliwahi kuishi; ulikuwa mtu wa ovyo kabisa. Aidha kwa mkeo, mumeo, watoto, ndugu, mshirika, mpendwa; na yamkini ni mfanyakazi wako na kadhalika. Lakini leo Bwana amekubadilisha, nikuombe kuwapa muda wa kubadilika na hao watesi wako. (Swala la kutokubadilika liweke kwa Mungu; ndio maana tukaimizwa sana ya kwamba kisasi kisiwe juu yetu...maana Yeye ndiye ajuaye ya kwamba huyu ni sikio la kufa ama huyu ni wa kupona.) Sauli aliyekuja kuitwa Paulo alikuwa mtu wa ovyo na hatari sana kwa kanisa la Mungu kwa wakati ule. Lakini neema ya Bwana iokoayo haikuwahi kumkatia tamaa. Mungu alimbadilisha na hatimaye kuwa mtu anayefaa. Unaposoma Warumi, Wagalatia, Wakolosai na Wathesaloni...jaribu kujiuliza kama tungalimosa mtu huyu! Kuna adui ukonao leo, lakini ndani yao kuna nyaraka muhimu kwa kanisa; Waefeso, Barua kwa Filomoni, Timotheo na hata Tito vimo ndani yao. Unapojaribu kumlipizia kisasi uwe na hakika ni unapigana na Bwana mwenyewe, maana kwa Mungu mtu huyo ni chombo kiteule chake. Na unapojaribu kumpinga, na kumfanyia fitina mbingu zinakuona na wewe ni sehemu ya adui wa mapenzi makamilifu ya Mungu. (Kumbuka jicho la Kiungu linatofauti sana na letu. Sisi hutazama mtu wa leo, mbingu zinamjua huyo mtu miaka kadhaa ijayo ni nani?) Nikwambie ukweli kwenye madanguro kuna wahubiri wengi wakubwa! Je, madanguro yote ya chomwe moto! Katikati ya wachawi walioua watoto wako kuna watumishi muhimu sana humo! Je, wachawi wote wafe leo, leo? Jibu ni la! Na utaelewa sasa ni kwa nini mbingu sii nyepesi kujibu maombi unayomuomba Mungu usiku na mchana ya kuwa huyo adui yako anapaswa kufa. Kwa sababu jicho la Kiungu lipo tofauti sana, sana. Anania alimtazama Paulo kama muuaji na mtesi wa kanisa (ni kweli kabisa) lakini Mungu wakati huu alimtazama kama chombo chake kiteule. Mungu alishampa mashitaka yake ya kwamba mbona unaniudhi Sauli! Na wakamalizana hapo, hapo. Anania anajaribu kumtaja Sauli muuaji, Mungu anamuona Sauli muhubiri wa injili. Hiki kwa Mungu ni cha thamani kubwa sana...maandiko husema ya kwamba hatamani watu waangamie, ila wote waifikiliye toba kwanza...nalicha ya kuifikilia toba, bali hutamani tena ya kwamba kile kilichowekezwa ndani yao kitumike kuujenga ufalme wa mbinguni. Huyo adui yako, yamkini ni chombo kiteule cha Bwana...(Sikuzuilia kuendelea kumsihi Mungu kuhusu watesi wako, la hasha! Silo lengo langu...ila nanjia kukupa taadhari na kukupanua uelewa wako kuhusu mtu huyo na kukutaka kuona yamkini kama Mungu anavyomuona...ili kukuzuilia kutoka katika masumbufu ya kwamba mbona adui wanachanua angali ni adui wako na mbingu...) Soma kisa hili; Matendo ya Mitume 9:13 Lakini Anania akajibu, Bwana, nimesikia habari za mtu huyu kwa watu wengi, mabaya mengi aliyowatenda watakatifu wako Yerusalemu; 14 hata hapa ana amri itokayo kwa wakuu wa makuhani awafunge wote wakuitiao Jina lako. 15 Lakini Bwana akamwambia, Nenda tu; kwa maana huyu ni chombo kiteule kwangu, alichukue Jina langu mbele ya Mataifa, na wafalme, na wana wa Israeli. 7.

Jumamosi, 23 Mei 2026

. Chuki Ina Nguvu Kama Mauti. Kati ya jambo la ajabu sana nililojifunza na ningependa ulifahamu; ni hili la nguvu ya chuki. Ni hakika chuki ina nguvu sawa na roho ya mauti. Lakini pia chuki hutenda kazi kama ilivyo roho ya mauti. Sio jambo jepesi kulielewa kama halijawahi kukuta ama kama hujawahi kujifunza somo hili kwa sura ya namna hii. Na Mwl Oscar Samba Ujumbe huu ni sehemu ya kitabu Chetu cha IMANI INAPOJARIBIWA; Karibu... Walipomchukia Yusufu na kumuuza; ni wazi alishakufa ndani ya mioyo yao. Katika kujifunza hili somo nilijikuta nawaza hivi ilikuaje wakati Yakobo analia na kuomboleza wale ndugu wakawa kimya sana, na wakamuacha baba yao akiwa analia siku zote na kukaa hali ya ukiwa? Liliwezekanaje jambo hili! Yaani katika maombolezo makuu namna hii hawa ndugu bado wapo kimya tu! Tazama; Mwanzo 37:34 Yakobo akararua mavazi yake, akajivika gunia viunoni, na kumlilia mwanawe siku nyingi. 35 Wanawe wote, na binti zake wote, wakaondoka wamtulize, lakini akakataa kutulizwa, akasema, La! Nitamshukia mwanangu, nikisikitika, hata kuzimu. Baba yake akamlilia. Maneno kama haya, waliyashuhudia: "Nitamshukia mwanangu, nikisikitika, hata kuzimu. Baba yake akamlilia." Katika kumtuliza baba yao nao hao waliomuuza walikwepo. Huo mstari anaposema binti na wana, uwe na hakika Biblia ya Kingereza imetumia neno "sons" ikiwakisha wana wa kiume. Nao wanahusika katika kumtuliza, angali ndio waliomuuza; Mwanzo 37:35 Wanawe wote, na binti zake wote, wakaondoka wamtulize, lakini akakataa kutulizwa, akasema, La! Nitamshukia mwanangu, nikisikitika, hata kuzimu. Baba yake akamlilia. And all his sons and all his daughters rose up to comfort him; but he refused to be comforted; and he said, For I will go down into the grave unto my son mourning. Thus his father wept for him. (Neno wote limetumika.) Nalijiuliza sana huu ujasiri ulitoka wapi; Mwanzo 37:32 Wakaenda nayo ile kanzu ndefu, wakamletea baba yao, wakasema, Tumeona hii; basi, utambue kama kanzu hii ni ya mwanao, ama siyo. 33 Akaitambua, akasema, Ndiyo kanzu ya mwanangu, mnyama mkali amemla; bila shaka Yusufu ameraruliwa. Baada ya kufikiri sana mahali huo ujasiri ulipotoka, ndipo nilipokuja kutambua ya kwamba, chuki ina nguvu kama mauti. Kwa maana kwamba, waliposema tumue, alikuwa ameshakufa kwanza kwenye mioyo yao. Wanasaikolojia wanasema hivi; kabla mtu hajamua mtu, anaanza kuiuwa dhamiri yake kwanza, ndipo auwe mtu. (Kifo cha kukusudia.) Yusufu ni kweli alishakufa kwenye mioyo yao. Hapa ilikuwa ni madhiirisho tu! Tazama; Mwanzo 37:20 Haya, twende, tukamwue na kumtupa katika birika mojawapo, nasi tutasema, Mnyama mkali amemla; kisha tutaona zitakuwaje ndoto zake. Ndio maana waliweza kumuuza na wakamsahau kabisa. Haya ni majibu ya swali nililokuwa najiuliza, ya kwamba ilikuaje wakamuuza sawa; ila wakaweza kumsahau kabisa kwa muda wa miaka 27? Na "actually" walishamsahau kabisa, kabisa. Maana kama asingalisimama mbele yao wakati wamekimbilia Misri, bado kumbukumbu lake lisingali kwepo. Kumuuza ni sawa, labla ni matokeo ya kughafilika tu; lakini kumsahau kabisa, kabisa! Hili sii jambo dogo hata kidogo. Tena ndugu wa damu! Nilikuwa nawaza mimi binafsi ya kwamba hawa watu ni kweli wamenifukuza kazi, tena bila kunisikiliza au kupewa nafasi ya kujibu mashitaka yao...lakini wanawezaje kunisahau namna hii! Sizioni hata fadhili za kanisa, ni kama vile sikuwahi kusimama mbele yao kabisa kabisa. Ndipo Roho Mtakatifu akanisemesha kwa ndani; chuki ina nguvu kama mauti. Kwenye moyo wao ulishakufa. Haiwezekani kumsahau Yusufu kana kwamba kweli kafa, kumbe angali hai. Ukiona hivyo, ndani yao ni kweli amekufa. Nilijifunza pia chuki ina tabia ya kukua na kuambukizwa. Sasa eneo la kuambukizwa sitalisemea, maana kuna wengine wanashiriki kukuchukia angali hukuwahi kuwakosea lolote. Nataka kukugusia eneo la kukua. Hapo awali walikuwa wanamchukia kwa kiwango fulani, lakini hapa; chuki ilizidi kukua. Maana chuki inayolandana na mauti, ni chuki yenye kiwango kikubwa kabisa. Na kwangu tukio la kuoa, lilikuza chuki kwa kiwango kikubwa sana. Usiniulize kwa nini? Kwa Yusufu ni hili hapa; Mwanzo 37:5 Yusufu akaota ndoto, akawapa ndugu zake habari, nao wakazidi kumchukia. Hiyo ndoto ilileta chuki, hapana shaka kabisa ilikwepo ikaongezeka. Lakini mstari ujao linaongezeka neno na maneno yake. Ina maana wazi kabisa Yusufu kwa kuwa alikuwa na ujuzi wa kutafsiri ndoto, aliwapa na tafsiri yake. Kitu kilichokuza chuki zaidi, na zaidi. Mwanzo 37:8 Ndugu zake wakamwambia, Je! Kweli wewe utatumiliki sisi? Nawe utatutawala sisi? Wakazidi kumchukia kwa ajili ya ndoto yake, na kwa maneno yake. Ndoto ya pili iliongeza au ilikuza tena kiwango cha chuki; Mwanzo 37:11 Ndugu zake wakamhusudu; bali baba yake akalihifadhi neno hili. Watu wengi hawajui ya kuwa azimio na kikao rasmi cha kumua Yesu kilizaliwa au kuja mara baada ya muujiza wa kufufuka kwa Lazaro. Ni kweli awali walikuwa wakimuwinda, ila hapa ndipo chuki ilipokuwa na kufikia ukomo. Hatua isiyovumilika kabisa kabisa. Sifa ya chuki iliyofikia hatua hii, ni mtu kuwa radhi kufanya lolote ili tu akuangamize. Hatajali hatima yako, maana mauti ina tabia za namna hiyo. Tazama; Yohana 11:45 Basi wengi katika Wayahudi waliokuja kwa Mariamu, na kuyaona yale aliyoyafanya, wakamwamini. 46 Lakini wengine wakaenda zao kwa Mafarisayo, wakawaambia aliyoyafanya Yesu. 48 Tukimwacha hivi, watu wote watamwamini; na Warumi watakuja, watatuondolea mahali petu na taifa letu. 49 Mtu mmoja miongoni mwao, Kayafa, aliyekuwa Kuhani Mkuu mwaka ule, akawaambia, Ninyi hamjui neno lo lote; 50 wala hamfikiri ya kwamba yafaa mtu mmoja afe kwa ajili ya watu, wala lisiangamie taifa zima. Chuki kwa Daudi ilikwepo, lakini ilikua zaidi kutoka kwa Sauli mfalme, kwa sababu ya tukio hili; 1 Samweli 18:6 Hata ikawa, walipokuwa wakienda, hapo Daudi aliporudi baada ya kumwua yule Mfilisti, wanawake wakatoka katika miji yote ya Israeli, kwa kuimba na kucheza, ili kumlaki mfalme Sauli; wakatoka na matari, na shangwe, na vinanda. 7 Nao wale wanawake wakaitikiana wakicheza, wakasema, Sauli amewaua elfu zake, Na Daudi makumi elfu yake. 8 Basi Sauli akaghadhibika sana, na maneno haya yakamchukiza; akasema, Wamempa Daudi makumi elfu, na mimi wamenipa elfu tu; kuna nini tena awezayo kupata, isipokuwa ni ufalme? 9 Sauli akamwonea Daudi wivu tangu siku ile. 10 Ikawa siku ya pili yake, roho mbaya kutoka kwa Mungu ikamjilia Sauli kwa nguvu, naye akatabiri ndani ya nyumba. Basi Daudi alikuwa akipiga kinubi kwa mkono wake kama siku zote; naye Sauli alikuwa na mkuki mkononi mwake. 11 Mara Sauli akautupa ule mkuki; maana alisema, Nitampiga Daudi hata ukutani. Daudi akaepa, akatoka mbele yake, mara mbili. Shetani ana tabia ya kupanda chuki ndani ya moyo wa mtu pole-pole, anajua anachokifanya. Kuna siku anafahamu itakuwa, na kisha kubeba mimba, itazaa mwana tu. Kiufupi ni kwamba, chuki ina tabia ya kupasuka kama nyongo. Nimepita mikononi mwa wachunguji na viongozi kadhaa. Mkuu wangu akinichukia huwa na mpa muda tu. Najua asipotumbua hilo jipu na kukamua mapema; litakuja kupasuka tu. Ndio maana nimekuwa nikiishi kama mgeni katika mazingira ya namna hii. Hili ni jambo nililojifunza tangu awali. Kuwa makini sana na mtu anayekuchukia. Huwa nasema hivi, kuna watu wakikosa uchafu chumbani kwako; wanaenda kwenye "dustbin" au chombo cha takataka cha hapo ndani ama nje na kupekua. Wakikosa na hapo huwa wanaenda jalalani, kisha wanachukua uchafu na kuja kuumwaga sebleni kwako. Wanapiga picha na kusema ushahidi huu hapa tunao kumuhusu huyu mtu. Epuka sana watu wanaokaa kikao cha kuuwa, kisha ndipo wanatafuta makosa yako. Sio kosa linawasukuma kukuuwa, bali ni chuki. Kisha hiyo chuki inahalalishwa kwa makosa waliojiokotea. Ndivyo ilivyokuwa kwa Yesu. Yaani, unahukumiwa kabla hata ya kukutwa na kosa. Na ndivyo viongozi wetu wengi wa kidini walivyo. Lakini ashukuriwe Mungu ambaye hatuachi tuwe mateka wa adui zetu. Wanandaa mauti, lakini Bwana anaigeuza na kuwa ushindi. Ingawaje ni kweli majira haya yanaumiza sana. Ila ndio njia ambayo mashujaa wengi hupita. Nimejikuta nikimuomba Mungu awaondoe moyoni mwangu kama walivyoniondoa wao. Anipe kuwasahau kama walivyo nisahau. Wafe kwenye nafsi yangu, kama nilivyotangulia kufa ndani yao. Maana nikifikiria jinsi nilivyojitoa, moyo unaumia kama ule wa Daudi katika Zaburi. Maana sio jambo la kawaida hata wazee wa kanisa kwa umoja wao waseme tumjuliye hali mchungaji, jamani hata mashemasi nao! Mshirika mmoja akaniambia baba, nimeambiwa eti hapa ndio utamaduni wetu ya kwamba mchungaji akishaondoka ndo ameondoka, hairuhusiwi hata kumpigia simu! Ninachojua ni kwamba chuki imewaambukiza lakini kila penye chuki kuna sheria. Ukishangaa sheria kwenye chuki nenda katika Danieli, mashujaa watatu na Danieli wenyewe ilibidi ipitishwe sheria ili kuwatia hatiani. Lakini sheria ya kulinda chuki utaikuta kwa Mafarisayo, walishatangaza kuwatenga watu na sinagogi kama watamkiri Yesu kama Masihi na kadhalika. Na kweli hata sasa watu huwa katika kundi fulani kama wataambana na mtu ambaye mkuu kwa hila zake mwenyewe kaamua kumchukia. Sauli alipomchukia Daudi, alisababisha ufa mkubwa. Kukawa na kundi la Daudi na la Sauli. Watu walilazimika kujipendekeza kwa mfalme ili kulinda ugali wao. Kuna sheria za "wananzengo" (kwa kanda ya ziwa ni wana jamii wa mtaa mmoja,) ya kwamba mtu akitengwa na "nzengo" alafu wewe ukashirikiana naye, au ukaenda kwake; na wewe unatengwa. Hii ni tabia ya roho ya chuki. Ikusaidie kukujibu mbona hadi fulani na fulani nao wamenichukia! Nimemuomba Mungu pia ya kwamba, nafsi yangu iweze kutambua ya kuwa Bwana ameshanitenga nao. Hii itanisaidia kuniondolea maumivu na kutokuwatazama tena moyoni mwangu. Hakiki hapa kuhusu nguvu ya chuki kimauti: nikuonye tena; kuwa makini na mtu anayekuchukia; 1 Yohana 3:15 Kila amchukiaye ndugu yake ni mwuaji: nanyi mnajua ya kuwa kila mwuaji hana uzima wa milele ukikaa ndani yake

Kati ya jambo la ajabu sana nililojifunza na ningependa ulifahamu; ni hili la nguvu ya chuki. Ni hakika chuki ina nguvu sawa na roho ya mauti. Lakini pia chuki hutenda kazi kama ilivyo roho ya mauti. Sio jambo jepesi kulielewa kama halijawahi kukuta ama kama hujawahi kujifunza somo hili kwa sura ya namna hii. Na Mwl Oscar Samba Ujumbe huu ni sehemu ya kitabu Chetu cha IMANI INAPOJARIBIWA; Karibu... Walipomchukia Yusufu na kumuuza; ni wazi alishakufa ndani ya mioyo yao. Katika kujifunza hili somo nilijikuta nawaza hivi ilikuaje wakati Yakobo analia na kuomboleza wale ndugu wakawa kimya sana, na wakamuacha baba yao akiwa analia siku zote na kukaa hali ya ukiwa? Liliwezekanaje jambo hili! Yaani katika maombolezo makuu namna hii hawa ndugu bado wapo kimya tu! Tazama; Mwanzo 37:34 Yakobo akararua mavazi yake, akajivika gunia viunoni, na kumlilia mwanawe siku nyingi. 35 Wanawe wote, na binti zake wote, wakaondoka wamtulize, lakini akakataa kutulizwa, akasema, La! Nitamshukia mwanangu, nikisikitika, hata kuzimu. Baba yake akamlilia. Maneno kama haya, waliyashuhudia: "Nitamshukia mwanangu, nikisikitika, hata kuzimu. Baba yake akamlilia." Katika kumtuliza baba yao nao hao waliomuuza walikwepo. Huo mstari anaposema binti na wana, uwe na hakika Biblia ya Kingereza imetumia neno "sons" ikiwakisha wana wa kiume. Nao wanahusika katika kumtuliza, angali ndio waliomuuza; Mwanzo 37:35 Wanawe wote, na binti zake wote, wakaondoka wamtulize, lakini akakataa kutulizwa, akasema, La! Nitamshukia mwanangu, nikisikitika, hata kuzimu. Baba yake akamlilia. And all his sons and all his daughters rose up to comfort him; but he refused to be comforted; and he said, For I will go down into the grave unto my son mourning. Thus his father wept for him. (Neno wote limetumika.) Nalijiuliza sana huu ujasiri ulitoka wapi; Mwanzo 37:32 Wakaenda nayo ile kanzu ndefu, wakamletea baba yao, wakasema, Tumeona hii; basi, utambue kama kanzu hii ni ya mwanao, ama siyo. 33 Akaitambua, akasema, Ndiyo kanzu ya mwanangu, mnyama mkali amemla; bila shaka Yusufu ameraruliwa. Baada ya kufikiri sana mahali huo ujasiri ulipotoka, ndipo nilipokuja kutambua ya kwamba, chuki ina nguvu kama mauti. Kwa maana kwamba, waliposema tumue, alikuwa ameshakufa kwanza kwenye mioyo yao. Wanasaikolojia wanasema hivi; kabla mtu hajamua mtu, anaanza kuiuwa dhamiri yake kwanza, ndipo auwe mtu. (Kifo cha kukusudia.) Yusufu ni kweli alishakufa kwenye mioyo yao. Hapa ilikuwa ni madhiirisho tu! Tazama; Mwanzo 37:20 Haya, twende, tukamwue na kumtupa katika birika mojawapo, nasi tutasema, Mnyama mkali amemla; kisha tutaona zitakuwaje ndoto zake. Ndio maana waliweza kumuuza na wakamsahau kabisa. Haya ni majibu ya swali nililokuwa najiuliza, ya kwamba ilikuaje wakamuuza sawa; ila wakaweza kumsahau kabisa kwa muda wa miaka 27? Na "actually" walishamsahau kabisa, kabisa. Maana kama asingalisimama mbele yao wakati wamekimbilia Misri, bado kumbukumbu lake lisingali kwepo. Kumuuza ni sawa, labla ni matokeo ya kughafilika tu; lakini kumsahau kabisa, kabisa! Hili sii jambo dogo hata kidogo. Tena ndugu wa damu! Nilikuwa nawaza mimi binafsi ya kwamba hawa watu ni kweli wamenifukuza kazi, tena bila kunisikiliza au kupewa nafasi ya kujibu mashitaka yao...lakini wanawezaje kunisahau namna hii! Sizioni hata fadhili za kanisa, ni kama vile sikuwahi kusimama mbele yao kabisa kabisa. Ndipo Roho Mtakatifu akanisemesha kwa ndani; chuki ina nguvu kama mauti. Kwenye moyo wao ulishakufa. Haiwezekani kumsahau Yusufu kana kwamba kweli kafa, kumbe angali hai. Ukiona hivyo, ndani yao ni kweli amekufa. Nilijifunza pia chuki ina tabia ya kukua na kuambukizwa. Sasa eneo la kuambukizwa sitalisemea, maana kuna wengine wanashiriki kukuchukia angali hukuwahi kuwakosea lolote. Nataka kukugusia eneo la kukua. Hapo awali walikuwa wanamchukia kwa kiwango fulani, lakini hapa; chuki ilizidi kukua. Maana chuki inayolandana na mauti, ni chuki yenye kiwango kikubwa kabisa. Na kwangu tukio la kuoa, lilikuza chuki kwa kiwango kikubwa sana. Usiniulize kwa nini? Kwa Yusufu ni hili hapa; Mwanzo 37:5 Yusufu akaota ndoto, akawapa ndugu zake habari, nao wakazidi kumchukia. Hiyo ndoto ilileta chuki, hapana shaka kabisa ilikwepo ikaongezeka. Lakini mstari ujao linaongezeka neno na maneno yake. Ina maana wazi kabisa Yusufu kwa kuwa alikuwa na ujuzi wa kutafsiri ndoto, aliwapa na tafsiri yake. Kitu kilichokuza chuki zaidi, na zaidi. Mwanzo 37:8 Ndugu zake wakamwambia, Je! Kweli wewe utatumiliki sisi? Nawe utatutawala sisi? Wakazidi kumchukia kwa ajili ya ndoto yake, na kwa maneno yake. Ndoto ya pili iliongeza au ilikuza tena kiwango cha chuki; Mwanzo 37:11 Ndugu zake wakamhusudu; bali baba yake akalihifadhi neno hili. Watu wengi hawajui ya kuwa azimio na kikao rasmi cha kumua Yesu kilizaliwa au kuja mara baada ya muujiza wa kufufuka kwa Lazaro. Ni kweli awali walikuwa wakimuwinda, ila hapa ndipo chuki ilipokuwa na kufikia ukomo. Hatua isiyovumilika kabisa kabisa. Sifa ya chuki iliyofikia hatua hii, ni mtu kuwa radhi kufanya lolote ili tu akuangamize. Hatajali hatima yako, maana mauti ina tabia za namna hiyo. Tazama; Yohana 11:45 Basi wengi katika Wayahudi waliokuja kwa Mariamu, na kuyaona yale aliyoyafanya, wakamwamini. 46 Lakini wengine wakaenda zao kwa Mafarisayo, wakawaambia aliyoyafanya Yesu. 48 Tukimwacha hivi, watu wote watamwamini; na Warumi watakuja, watatuondolea mahali petu na taifa letu. 49 Mtu mmoja miongoni mwao, Kayafa, aliyekuwa Kuhani Mkuu mwaka ule, akawaambia, Ninyi hamjui neno lo lote; 50 wala hamfikiri ya kwamba yafaa mtu mmoja afe kwa ajili ya watu, wala lisiangamie taifa zima. Chuki kwa Daudi ilikwepo, lakini ilikua zaidi kutoka kwa Sauli mfalme, kwa sababu ya tukio hili; 1 Samweli 18:6 Hata ikawa, walipokuwa wakienda, hapo Daudi aliporudi baada ya kumwua yule Mfilisti, wanawake wakatoka katika miji yote ya Israeli, kwa kuimba na kucheza, ili kumlaki mfalme Sauli; wakatoka na matari, na shangwe, na vinanda. 7 Nao wale wanawake wakaitikiana wakicheza, wakasema, Sauli amewaua elfu zake, Na Daudi makumi elfu yake. 8 Basi Sauli akaghadhibika sana, na maneno haya yakamchukiza; akasema, Wamempa Daudi makumi elfu, na mimi wamenipa elfu tu; kuna nini tena awezayo kupata, isipokuwa ni ufalme? 9 Sauli akamwonea Daudi wivu tangu siku ile. 10 Ikawa siku ya pili yake, roho mbaya kutoka kwa Mungu ikamjilia Sauli kwa nguvu, naye akatabiri ndani ya nyumba. Basi Daudi alikuwa akipiga kinubi kwa mkono wake kama siku zote; naye Sauli alikuwa na mkuki mkononi mwake. 11 Mara Sauli akautupa ule mkuki; maana alisema, Nitampiga Daudi hata ukutani. Daudi akaepa, akatoka mbele yake, mara mbili. Shetani ana tabia ya kupanda chuki ndani ya moyo wa mtu pole-pole, anajua anachokifanya. Kuna siku anafahamu itakuwa, na kisha kubeba mimba, itazaa mwana tu. Kiufupi ni kwamba, chuki ina tabia ya kupasuka kama nyongo. Nimepita mikononi mwa wachunguji na viongozi kadhaa. Mkuu wangu akinichukia huwa na mpa muda tu. Najua asipotumbua hilo jipu na kukamua mapema; litakuja kupasuka tu. Ndio maana nimekuwa nikiishi kama mgeni katika mazingira ya namna hii. Hili ni jambo nililojifunza tangu awali. Kuwa makini sana na mtu anayekuchukia. Huwa nasema hivi, kuna watu wakikosa uchafu chumbani kwako; wanaenda kwenye "dustbin" au chombo cha takataka cha hapo ndani ama nje na kupekua. Wakikosa na hapo huwa wanaenda jalalani, kisha wanachukua uchafu na kuja kuumwaga sebleni kwako. Wanapiga picha na kusema ushahidi huu hapa tunao kumuhusu huyu mtu. Epuka sana watu wanaokaa kikao cha kuuwa, kisha ndipo wanatafuta makosa yako. Sio kosa linawasukuma kukuuwa, bali ni chuki. Kisha hiyo chuki inahalalishwa kwa makosa waliojiokotea. Ndivyo ilivyokuwa kwa Yesu. Yaani, unahukumiwa kabla hata ya kukutwa na kosa. Na ndivyo viongozi wetu wengi wa kidini walivyo. Lakini ashukuriwe Mungu ambaye hatuachi tuwe mateka wa adui zetu. Wanandaa mauti, lakini Bwana anaigeuza na kuwa ushindi. Ingawaje ni kweli majira haya yanaumiza sana. Ila ndio njia ambayo mashujaa wengi hupita. Nimejikuta nikimuomba Mungu awaondoe moyoni mwangu kama walivyoniondoa wao. Anipe kuwasahau kama walivyo nisahau. Wafe kwenye nafsi yangu, kama nilivyotangulia kufa ndani yao. Maana nikifikiria jinsi nilivyojitoa, moyo unaumia kama ule wa Daudi katika Zaburi. Maana sio jambo la kawaida hata wazee wa kanisa kwa umoja wao waseme tumjuliye hali mchungaji, jamani hata mashemasi nao! Mshirika mmoja akaniambia baba, nimeambiwa eti hapa ndio utamaduni wetu ya kwamba mchungaji akishaondoka ndo ameondoka, hairuhusiwi hata kumpigia simu! Ninachojua ni kwamba chuki imewaambukiza lakini kila penye chuki kuna sheria. Ukishangaa sheria kwenye chuki nenda katika Danieli, mashujaa watatu na Danieli wenyewe ilibidi ipitishwe sheria ili kuwatia hatiani. Lakini sheria ya kulinda chuki utaikuta kwa Mafarisayo, walishatangaza kuwatenga watu na sinagogi kama watamkiri Yesu kama Masihi na kadhalika. Na kweli hata sasa watu huwa katika kundi fulani kama wataambana na mtu ambaye mkuu kwa hila zake mwenyewe kaamua kumchukia. Sauli alipomchukia Daudi, alisababisha ufa mkubwa. Kukawa na kundi la Daudi na la Sauli. Watu walilazimika kujipendekeza kwa mfalme ili kulinda ugali wao. Kuna sheria za "wananzengo" (kwa kanda ya ziwa ni wana jamii wa mtaa mmoja,) ya kwamba mtu akitengwa na "nzengo" alafu wewe ukashirikiana naye, au ukaenda kwake; na wewe unatengwa. Hii ni tabia ya roho ya chuki. Ikusaidie kukujibu mbona hadi fulani na fulani nao wamenichukia! Nimemuomba Mungu pia ya kwamba, nafsi yangu iweze kutambua ya kuwa Bwana ameshanitenga nao. Hii itanisaidia kuniondolea maumivu na kutokuwatazama tena moyoni mwangu. Hakiki hapa kuhusu nguvu ya chuki kimauti: nikuonye tena; kuwa makini na mtu anayekuchukia; 1 Yohana 3:15 Kila amchukiaye ndugu yake ni mwuaji: nanyi mnajua ya kuwa kila mwuaji hana uzima wa milele ukikaa ndani yake

Jumatano, 6 Mei 2026

KUUJENGA UKUTA KUNA GHARAMA na Shujaa Hushinda Vita

Nehemia alighamua nia ya yule nabii mke na mwovu na alichonuia kukifanya. Alitaka kumjengea hofu kwa kupitia aina fulani ya maneno ili aweze kumuondoa katika kusudi. Adui Shetani alipoona wakina Tobia na Sanbalati wameshindwa kuzuia ukuta kwa njia mbalimbali, aliamua moja kwa moja kutumia njia hii. Lazima ujifunze hatari ya maneno unapokuwa unavikabili vita. Yawe yanatoka kwa adui au mtu mwingine. Na yakitoka kwako huwa mabaya zaidi. Maana Shetani atakufanya kama kiwanda cha kuzalisha hofu itokayo ndani mwako. Mawazo ya kushindwa yatakutawala nawe utazungukwa na kushindwa muda wote. Tazama; Nehemia 6:11 Nami nikasema, Je! Mtu kama mimi nikimbie? Naye ni nani, akiwa kama nilivyo mimi, atakayeingia hekaluni ili kuponya maisha yake? Sitaingia. 12 Nikatambua, na tazama, siye Mungu aliyemtuma; lakini amefanya unabii huu kinyume changu; nao Tobia na Sanbalati ndio waliomwajiri. :13 Kwa sababu hii aliajiriwa, ili mimi niogope, nikafanye hivyo na kutenda dhambi, kisha wao wawe nazo habari mbaya, ili wanishutumie. 14 Uwakumbuke, Ee Mungu wangu, Tobia na Sanbalati sawasawa na hayo matendo yao, na yule nabii mke Noadia, na hao manabii waliosalia, waliotaka kuniogofya. 15 Basi huo ukuta ukamalizika siku ya ishirini na tano ya mwezi wa Eluli, katika muda wa siku hamsini na mbili. 16 Ikawa adui zetu wote waliposikia, ndipo makafiri wote waliotuzunguka wakaogopa, nao wakakata tamaa sana machoni pao wenyewe; maana waliitambua kazi hiyo ilivyotendwa na Mungu wetu. Alitumwa mjumbe, mwenye ujumbe! Sii kila maneno unapaswa kukubaliana nayo. Shujaa huwa makini sana anapokuwa vitani. Sii kila mwanajeshi aliyevaa nguo na zenye nembo kama yako unapaswa kumuamini! Wengine wameajiriwa na wakina Sanbalati ili wakuogofye. Nia yao ni kukutia hofu. Wanajifanya wana mpango mzuri wa kukusaidia, kumbe ni baada ya wao (kama Sanbalati) kukwama katika kukuzuilia kuujenga ukuta. Watakupa maneno mengi ya kwamba huyu ana misimamo mingi sana; ni mtu wa misimamo mikali...wewe usijali. Mimi huwa nasema ya kwamba asiye na misimamo ni maiti pekee. Lakini baadae nafikiria nakusema hata maiti ina misimamo maana imeshachagua upande wa kufa. Na uzima sio sehemu yake tena. Ukiumaliza ukuta ndipo watakapokuja kukuelewa. Usilazimishe kueleweka mapema na kila mtu. Unajua, anayeona unakoelekea ni wewe mwenyewe; kwa hiyo epuka kuwalazimisha wasiona waone kama wewe. Kama kila mtu atafanikiwa kuona kama unavyoona wewe basi hayo sio maono tena. Maono sifa yake moja wapo ni aidha mtu mmoja ama watu wachache kuona kwa niaba ya wengine. Na usikubali wasiona wakalie nafasi ya maamuzi yako. Wengine ni kweli uko nao ila ni wakina Tobia na Sanbalati, hili lazima ulielewe daima. Ukiona mtu unakataa ushauri wake na anakukasirikia au anakuwa mkali kama pilipili; uwe na hakika haukuwa ushauri bali yalikuwa ni maamuzi au maelekezo aliyokuwa anakupatia. Na inapendeza sana kama ukifanikiwa kujua roho iliyo ndani yake kama Nehemia dhidi ya Noadia nabii mke. Maana kama ingelikuwa ni ushauri kusingekuwa na haja ya yeye kukasirika. (Kuna watu fulani waliwahi kunifanyia fitina, moyoni mwangu nikajisemea wanafikiri mimi ni dhaifu kiasi hicho. Ningekuwa dhaifu nisingefika hapa). Nehemia asingekaza katika kusudi ukuta usingejengwa. Utakutana na Ujumbe Huu Katika Kitabu Chetu Kipya cha KUJARIBIWA KWA IMANI

Ijumaa, 10 Aprili 2026

Falsafa ya Mwalimu Oscar Samba ya Kuwa Marehemu Anayeishi

Kijana Mmoja Akaniuliza; Mwalimu Nini Siri ya Mafanikio Yako ? Nataka Kuwa Mwalimu Mzuri Kama wewe. Nami Nikamjibu, "Mimi ni Marehemu Anayeishi." Kuna Watu Wengine Ukiishi Nao, Ukiwa Hai, Watakuuwa: Suluhu Ni Kuwa Marehemu Anayeishi.

Alhamisi, 26 Machi 2026

Aina za Upako

Pichani ni Mwl. Oscar Samba, akiwa anatoka Shambani akijikinga mvua kwa njia ya Asili: anatumia jani la gimbi kujifunika.
 Huku ikisadifu maudhi haya kwa kutuonyesha alipokuwa anapitia. Ambapo utapaelewa katika kitabu chake cha IMANI INAPOJARIBIWA na Kile cha KWA NINI MUNGU ANATUTAKA TUSIJILIPIZIE KISASI?.

 #AINA ZA #UPAKO

1. Upako Unaotokana na Mahali Unapopitia

2. Upako Unaotokana na Maombi

3. Upako Unaotokana na Neema au Karama. Au Unao ambatana na Wito ama Mafuta. (Ingawa kuna ambaye ana Mafuta ya Wito 'kila aliyeitwa hupewa.' Na kuna yule mwenye mafua hayo pamoja na neema ya ziada ambapo huitwa Karama.

4. Upako Unaotokana na Utii wako kwa Mungu katika Maelekezo aliyokupatia. Mfano aina ya ujumbe, kibali cha kuhudumu eneo au mahali husika na kadhalika. (Mapenzi Makamilifu ya Mungu.)

5. Upako Unaotokana na Kuombewa, au Kubandikwa Mikono na Muhubiri au mtumishi fulani. Paulo anamueleza Timotheo ya kwamba kuna aina ya mafuta aliyapata kwa kuwekewa mikono na wazee. (Uwe makini sio kila mzee amebeba roho sahihi.) 

Aina Nyingine

 6.Tukio Maalumu la Kutembelewa na Nguvu za Mungu Katika Ibada. 

7. Uwezo wa Kufuata Maelekezo Maalumu Yanayokuja Saa hiyo hiyo Unapokuwa Madhabahuni.

Jumatano, 28 Januari 2026

Karibu katika Mfululizo Wetu wa 1, wa Kitabu Chetu Hiki Kipya cha #KUJARIBIWA KWA IMANI katika Mada ya Cha Kufanya #Unapotupwa Kwenye Shimo, Pointi ya 1.

Na Mwl Oscar Samba

1. Cha Kufanya Unapotupwa Kwenye Shimo

1. Uwe Utayari na Ufahamu ama Akili ya Kukubali Kuishi Katika Shimo. Lugha ya kutupwa katika shimo ina maana ya kushushwa au adui kunuia kukuua. Ni aina ya pigo la kukung'oa au kukuangamiza kabisa kabisa. Mfano vijana wale wa tatu wa Yuda alipotupwa katika tanuru la moto; Meshack, Shedraka na Aberinego. Danieli katika shimo lenye simba wakali. Alikadhalika Yusufu gerezani, maana alitolewa katika maisha ya utukufu, na kisha kushushwa chini ghafla. Alikadhalika pia alipotupwa katika shimo na nduguze, na kisha kuuzwa utumwani. Maisha ya utumwa kwake bado yalikuwa ni kama shimo, maana anatolewa katika familia ya

Jumatatu, 26 Januari 2026

Karibu Katika Mfululizo Wetu wa 10, katika Kitabu Chetu Hiki cha CHA #KUFANYA UNAPOKUWA NJIA PANDA. Pointi ya 8-10

Mwl. Oscar Samba

8. #Uwe na Utulivu Moyoni. Nimekujuza kuwa kama hujui cha
Kufanya usifanye chochote, ila na hapa nakutaka pa kuhakikisha ya
kuwa unakuwa na utulivu moyoni. Ukapata kibali cha kusoma kitabu
chetu kinacho uelezea nafasi ya mwili wa mwandamu au viungo vyake katika kumtumikia Mungu; kuna jambo muhimu sana utalipata
pale.

Jambo hilo lipo katika tukio la Nuhu akiwa katika Safina. Alimtuma
kunguru na kugundua kuwa muda bado wa kutoka safinani. Mara
baada ya muda kadhaa kupita, akamtuma njiwa: mara ya kwanza na
alirudi na jani la mti bichi. Napo kuna kitu aligundua ya kwamba bado
hakujakauka. Mara ya mwisho akamtuma na hakurudi tena; ndipo
alipogundua ya kuwa nchi imekauka!

Hakuwa na haraka, hakuchukua maamuzi hadi alipojiridhisha; sio

Jumatano, 21 Januari 2026

Karibu katika Mfululizo wa 9 wa Kitabu Chetu cha CHA KUFANYA UKIWA NJIA PANDA . Katika Pointi ya 7. Na Mwl Oscar Samba 7. Kama Hujui cha Kufanya Usifanye Chochote

 Watu wengi wamejikuta wakiwa katika njia isiyo sahihi mara baada ya kupitia 

kipindi cha ukimya wa Mungu. Kuna kipindi Mungu huwa kimya kama 

sehemu ya jaribu kwetu. Ikiwa imani yetu kwake inapimwa, jambo la 

sabra na hata nidhamu, utii na hofu kwake; ni kwamba ni kweli 

tunamtegema na kumtumaini Yeye! 

Japo wakati mwingine anaongea lakini hatuelewi, na pia kuna muda 

anaona hata akiongea hatutamuelewa. Usisau pia ukimya wake, huweza 

kuwa ni matoke ya hasira yake juu yetu. Maana hata mfalme Sauli kuna 

wakati Mungu hakusema naye; baada ya kukorofishana naye, na 

kujikuta akigeukia msaada kwa mganga wa kienyeji. Na alilalamika 

kuwa Mungu hasemi naye hata kwa ndoto.

Sasa, Nisikilize; Mungu anapokua kimya, au unapofikia katika hatua 

Jumamosi, 17 Januari 2026

Usiogope Na Uwe Mwaminifu Hadi Kifo

Uwe Mwaminifu hadi kifo maana yake uwe na msimamo ambao utakuwa tayari kulipa gharama yoyote ile.

Pia tunaambiwa ya kuwa, ukishinda kuna madhara utaepukana nayo; hii inatupa kufahamu bayana ya kuwa, zipo faida za ushindi.

 Tazama Andiko : Ufunuo wa Yohana 2:10 Usiogope mambo yatakayokupata; tazama, huyo Ibilisi atawatupa baadhi yenu gerezani ili mjaribiwe, nanyi mtakuwa na dhiki siku kumi. Uwe mwaminifu hata kufa, nami nitakupa taji ya uzima. 

11 Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa. Yeye ashindaye hatapatikana na madhara ya mauti ya pili. 

Ninalowiwa kukupatia Majira haya ni kukutia moyo ya kwamba USIOGOPE na nikutake kuwa Mwaminifu huku ukijua mwisho wake kuna ushindi tele.

Maumivu nyakati kama hizi ni muhimu, ila mwisho wake umejaa mafanikio tele...kuna majira unalazimika kuingia gharama kwa ajili ya kulinda kile ulichokibeba ....

Jumatano, 14 Januari 2026

Karibu Katika Mfululizo wa 8 wa Kitabu Chetu cha CHAKUFANYA UKIWA NJIA PANDA, Pointi ya 5.

 Na Mwl. Oscar Samba

 5. Omba Mpenzi ya Mungu Yatimie.* Unajua maana yake ni nini?

Ni kwamba, umefikia mahali ambapo kwa akili na fahamu zako, 

hujui mpango wa Mungu, ama unajua lakini huna ujasiri na uwezo 

wakuukukabili! Sasa mwambie Mungu sio kama mimi nitakavyo bali 

mapenzi au mpango wako, ama njia yako ndiyo niiendee, sio njia 

nyingine. Yaombe haya kwa mzigo mkubwa sana, na kwa kumaanisha 

kwa viwango vikubwa mno.

22:41 Mwenyewe akajitenga nao kama kiasi cha kutupa jiwe, akapiga magoti akaomba, 

42 akisema, Ee Baba, ikiwa ni mapenzi yako, uniondolee kikombe hiki; 

walakini si mapenzi yangu, bali yako yatendeke. 

Jumanne, 13 Januari 2026

Jifunze Kubariki na Kubarikiwa Katika Swala la Uzao, na Kuoa au Kuolewa

Watu wengi hawaijui hii siri...ndio maana sio wepesi wa kuzidai baraka hizi iwe ni kutoka Madhabahuni, (kwa watumishi wa Mungu) Wazazi na Kadhalika...

Hata wao wanaopaswa kuzitoa wengi wao hawana weledi wa kutosha kuwahusu au kuzihusu....

Nikiwa katika mkoa ambao hivi sasa nipo, nimejikuta nashangaa kuona sherehe za SendOff hata za watu walio okoka zisizokuwa na ibada ndani yake.

Sherehe hizo unakuta nyingine zinaudhuriwa hata na wachungaji na zinafanyikia kanisani ama mazingira hayo...lakini hata muda wa neno la Mungu haupo...(Hawajui kilichotokea kwa Rebeka saa anaagwa).

Jumapili, 11 Januari 2026

#Muamshe Yesu Kwenye Maisha Yako*

Sikatai ya Kwamba Yesu Unaye, Nakubali Kabisa...

Ila Umemfanya Kukosa Chakukufanyia Kiasi cha Yeye Kutulia au Kunyamaza Kimya...

Ni sawa na wewe kualikwa ugenini alafu mwenyeji wako akawa anafanya kila kitu...hali hiyo inakufanya kukosa jambo la kufanya...

Na unajikuta umekaa mkao wa kusubiri kuambiwa walau nisaidia kukatakata mboga ama kufagia hapo nje...hii ikupe kuhakikisha unamfanya Yesu Kutokutulia katika Maisha Yako...

Siku moja wanafunzi wa Yesu wakapaswa kuvuka  kutoka ng'ambo moja na kuelekea Gerasi...katika boti Yesu hakupewa chakufanya...akalazimika kulala....walipokutwa na Dharuba Majini Ndipo Walijikuta Wakimuamsha....hapo ndipo alipoingia kazini na kuwasaidia....jifunze kitu hapo..

Jumamosi, 10 Januari 2026

Mfululizo wa 7, Katika Kitabu Chetu cha CHAKUFANYA UKIWA NJIA PANDA, Pointi ya 4.

Na _Mwl. Oscar Samba_ 

 4. Tafuta Ushauri Sahihi.

Hapo juu nimekupa mfano wa huyu baba ambaye alifikia mahali

pagumu sana kimaamuzi, ila mkewe alimshauri asimwache Mungu.

Badala yake waombe, nukuu moja wapo inamtaja au inamkariri huyu

baba akiwa anasema kuwa, Mungu amempa mke mzuri sana maana

alimshauri vyema!


Katika nyakati kama hizi ni muhim kujua umhimu wa namna ya

kukabiliana na shauri mbalimbali, maana wapo marafiki wataabishaji

ambao hawataacha kuja kwa nia ya kukuyumbisha kiushauri.

Kwenye fikra zako ni alzima kuwa na akiba ya hekima na maraifa ya

namna ya kukabilina na mamabo au amsuari au hali amahizi;

Ndipo mkewe akamwambia, Je! Wewe hata sasa washikamana na

Jumanne, 23 Desemba 2025

Mfululizo wa 6 Katika Kitabu Chetu cha CHAKUFANYA UKIWA NJIA PANDA.

Mada ya 2 ya Mambo Mengine ya Kufanya au Kuepuka Ukiwa Njia Panda.

Na _Mwl. Oscar_ Samba 

Pointi  ya 3. Ingia kwenye Maombi ya Muda Mrefu. Yanaweza pia yasiwe 

ya muda mrefu, ila yakawa ya kina na mazito au yenye mzigo mzito. 

Lakini imizo la maombi ya muda mrefu sio la kupuuza, ni muhimu sana 

kulizingatia. Yanaweza kuwa ya siku tatu kavu, masaa 24, au ya wiki 

moja. Huweza kuwa katika mfumo wa masaa 12 au 24 kwa 24 ama 

masaa 36 na kadhalika. Ni kadri Roho wa Bwana atakavyo kuongoza.

Kuna baba mmoja alikuwa akipitia mahali pa gumu sana, aliingia ubia 

wa kibiashara na mtu ambapo ilimbidi aweke dhamana mali zake 

muhimu. Na Yule mtu baadae akajakukimbia na ile fedha; alifikia hatua 

ya kutaka kujiua. Maana ilikuwa ni fedha nyingi, mkewe alimshauri 

asijidhuru badala yake wa mgeukiye Bwana.

Jumatatu, 22 Desemba 2025

3⃣ SERA YA UFALME WA MBINGUNI KUHUSU UJENZI WA NYUMBA YA KUISHI KWA “RAIA” WAKE WALIOKO DUNIANI 🖊 Mwl.CHRISTOPHER MWAKASEGE.

Bwana Yesu asifiwe sana!

Masomo ya wiki mbili mfululizo zilizopita, juu ya Sera ya ufalme wa Mungu kuhusu ujenzi wa nyumba za kuishi, yamezaa maswali kadha kutoka kwa wasomaji.


Maswali hayo yalihusu kupata ufahamu zaidi, juu ya sera hii ya ufalme wa Mungu. Tumeyapokea hayo maswali, ingawa si rahisi tukayajibu yote, kwa sababu ya “ufinyu” wa nafasi ya kufanya hivyo.

Lakini kwa leo tunataka tujibu swali moja, kati ya maswali mengi yaliyoulizwa, – na tunaamini majibu hayo yataongeza ufahamu zaidi juu ya utekelezaji wa sera hii.

Swali lenyewe lenyewe liliulizwa hivi: “Je, unatushauri kuweka wakfu au kuitakasa ardhi kabla ya sijajenga?”

Majibu yake ni haya:

Kuna tofauti kati ya kutakasa kitu,

Alhamisi, 18 Desemba 2025

Mfululizo wa 1 wa Kitabu Chetu cha CHAKUFANYA UNAOOKUWA NJIA PANDA

Tunaanza na Utangulizi (kinapatikana Google Bure)

 Na Mwl. Oscar Samba

 Utangulizi

Kitabu hiki kimenuia kumsaidia mtu ambaye yupo katika mazingira

magumu ya kimaamuzi, na mbele yake kuna aina zaidi ya moja ya

maamuzi ambayo anahatarishwa kuyachukuwa au yanayomkabili,

inawezekana lililo hatari ni moja, au salama ni moja ila kuna zaidi ya

aina mbili au moja na kadhalika.

Kitabu hiki ni matokeo ya sehemu ninayopitia sasa kuhusu ndoa yangu.

Ikumbukwe sasa ni mwaka unaokaribia wa nane toka mwenzangu

tuoane na kujikuta ananiacha kwa talaka mahakamani hali inayonipa au

kunipelekea kuwa njia panda. Njia panda yangu inaweza isiwe na tija

sana kwako ila la muhimu ni wewe kufahamu mazingira ya kitabu

hiki ili kikusaidia. (Wakati nakitoa, imetimia miaka 10/11, “2015-

2015”.)

Unaweza usione umuhimu wake kwa leo ila nikuhakikishie kuwa

chakula hiki ni kama akiba, kuna muda tunakula leo lakini chakula

hicho kinatusaidia kesho; sio kwamba tuliingia kwenye mfungo la! Bali

homa ya ghafula imetukuta na kutunyima hamu au uwezo wa kula. Ila

kwa akiba ya jana ambayo hatukuwa hata na wazo la kula tumevuka leo

salama!

….Nikikuongezea ni kwamba, mara baada ya kuandika

utangulizi huu, na nikiwa tayari nimeshaanza kukiandika hiki

kitabu, njia panda nyingine ilijitokeza kama sio moja basi ni

zaidi, licha ya swala la ndoa, lakini pia limeibuka swala la

kusimamishwa masomo chuoni. Kumbuka nipo katika chuo cha

Biblia Dodoma cha CBC; mara baada ya kutofautiana na

kiongozi wangu mmoja wapo katika swala fulani, nilijikuta

nikipewa adhabu ya kusimamishwa masomo mwaka mmoja.

Nikiwa tu nimetoka kuchukuwa barua zangu, (ikiwa moja yangu na ya

mchungaji wangu kingozi,) ndipo nilipokutana na mchungaji mmoja wa

dhehebu jingine akiniambia kuwa nihamie kwake. Maana huku

kumekuwa kugumu kwangu na katoa sababu kadhaa: zingeweza

kuonekana ni zenye mashiko maana nyuma ya pazia jambo langu

limeonekana ni matokeo ya mimi kuwa na tabia ya kutetea na kudai haki. Pamoja na kusema ukweli pale ambapo ninapoona mambo

hayajaka sawa.

Wazo hili halikwepo kabisa kichwani mwangu, maana nilishapitia

mahali kama hapa mara baada ya uongozi wangu wa sehemu huko

Arusha kutofautina nami na kunichukulia mamuzi ambayo sikuyapenda

maana sikusikilizwa kimapana!