Jumapili, 11 Januari 2026

#Muamshe Yesu Kwenye Maisha Yako*

Sikatai ya Kwamba Yesu Unaye, Nakubali Kabisa...

Ila Umemfanya Kukosa Chakukufanyia Kiasi cha Yeye Kutulia au Kunyamaza Kimya...

Ni sawa na wewe kualikwa ugenini alafu mwenyeji wako akawa anafanya kila kitu...hali hiyo inakufanya kukosa jambo la kufanya...

Na unajikuta umekaa mkao wa kusubiri kuambiwa walau nisaidia kukatakata mboga ama kufagia hapo nje...hii ikupe kuhakikisha unamfanya Yesu Kutokutulia katika Maisha Yako...

Siku moja wanafunzi wa Yesu wakapaswa kuvuka  kutoka ng'ambo moja na kuelekea Gerasi...katika boti Yesu hakupewa chakufanya...akalazimika kulala....walipokutwa na Dharuba Majini Ndipo Walijikuta Wakimuamsha....hapo ndipo alipoingia kazini na kuwasaidia....jifunze kitu hapo..

Marko 4:38 Naye mwenyewe alikuwapo katika shetri, amelala juu ya mto; wakamwamsha, wakamwambia, Mwalimu, si kitu kwako kuwa tunaangamia?

39 Akaamka, akaukemea upepo, akaiambia bahari, Nyamaza, utulie. Upepo ukakoma, kukawa shwari kuu.

40 Akawaambia, Mbona mmekuwa waoga? Hamna imani bado?

41 Wakaingiwa na hofu kuu, wakaambiana, Ni nani huyu, basi, hata upepo na bahari humtii?

(Soma pia katika Luka na Mathayo 8 kwenye mistari ya 20 naa.... kwenye vitabu vyote 2).

Unaweza kujiuliza kwa nini Yesu asikusaidie wakati anakuona unataabika?

Nikujibu ya kuwa, wakati Petro anazama Yesu alimuona...lakini alimshika mkono pale alipopiga yowe na kuomba msaada.... tafadhali hili liruhusu Vivyo kwako.... piga yowe ya kuomba msaada sasa ...yashinde mashaka na wasiwasi kwa njia ya Maombi ya Kuhitaji Msaada wa Kiungu...

Mathayo 14:30 Lakini alipouona upepo, akaogopa; akaanza kuzama, akapiga yowe, akisema, Bwana, niokoe .

31 Mara Yesu akanyosha mkono wake, akamshika, akamwambia, Ewe mwenye imani haba, mbona uliona shaka?

Nataka Uone Kitu Katika Mstari Ujao...kisha utajijibu ulichokigundua ukiunganisha na tukio hili la kuzama kwa Petro..

Mathayo 14:32 Nao walipopanda chomboni, upepo ulikoma.

#Umegundua Nini?*

Je, uliwahi kuifahamu kanuni ile ya kuyakanyaga maji ya mto Yordan ndipo ya tindike au ya kauke kwa Makuhani kipindi kile cha Yoshua?

Walipokanyaga maji, ndipo yalipokauka au kusimama kama kichugu...(Wakavuka)

Hilo andiko linatuambia ya kuwa, walipoingia chomboni ndipo bahari au mchafuko wa mawimbi ziwani ulipokoma!

Maana yake ni nini? Kuna vitu kwenye maisha vitakoma pale utakapokaza katika kuliendea kusudi la Mungu....adui hunuia kukuvunja moyo..

Kuna watu wanapata homa au mtoto anaugua, kisha mzazi anajisemea utaponea kanisani...leo lazima niende ibadani...wakifika tu kanisani hata kabla ya maombi Uzima Unajitokeza...kuna upizani kwenye fikra zako hauwezi kukoma hadi umeanza kuchukua hatua!

Kama Bado Hujaokoka na Unatamani Kuokoka, Tafadhali Fanya Vivyo Punde:

#Sema* ; MUNGU BABA, NINAKUJA MBELE ZAKO, MIMI NI MWENYE DHAMBI, NAKUOMBA UNISAMEHE SASA; *Amen* .

*Tafadhali Tafuta Kanisa la Watu Waliokoka Ukasali Hapo..*

Zaidi Endelea Kututembelea na Kuhakikisha UnaiFolo hii Channel Yetu ya Wasapu

Follow the Jipe Moyo 🫀❤️ Utashinda 💪💪🤝 channel on WhatsApp: https://whatsapp.com/channel/0029Vb7ZJLR9hXFGDfQuxT2D

Kwa Kweli #Usiogope

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni