Jumatano, 21 Januari 2026

Karibu katika Mfululizo wa 9 wa Kitabu Chetu cha CHA KUFANYA UKIWA NJIA PANDA . Katika Pointi ya 7. Na Mwl Oscar Samba 7. Kama Hujui cha Kufanya Usifanye Chochote

 Watu wengi wamejikuta wakiwa katika njia isiyo sahihi mara baada ya kupitia 

kipindi cha ukimya wa Mungu. Kuna kipindi Mungu huwa kimya kama 

sehemu ya jaribu kwetu. Ikiwa imani yetu kwake inapimwa, jambo la 

sabra na hata nidhamu, utii na hofu kwake; ni kwamba ni kweli 

tunamtegema na kumtumaini Yeye! 

Japo wakati mwingine anaongea lakini hatuelewi, na pia kuna muda 

anaona hata akiongea hatutamuelewa. Usisau pia ukimya wake, huweza 

kuwa ni matoke ya hasira yake juu yetu. Maana hata mfalme Sauli kuna 

wakati Mungu hakusema naye; baada ya kukorofishana naye, na 

kujikuta akigeukia msaada kwa mganga wa kienyeji. Na alilalamika 

kuwa Mungu hasemi naye hata kwa ndoto.

Sasa, Nisikilize; Mungu anapokua kimya, au unapofikia katika hatua 

ama “point” ya kutokuelewa cha kufanya: ni sawa na mtu aliyeko njia 

panda. Njia ziko nyingi, na hajui anaelekee wapi! Wewe tulia, usiwe na 

haraka.

Wakati ufunuo hu unanijia, ulinijia na kujikuta najiambia kuwa; njia 

panda nyingi zinakuwaga na eneo la kupumzikia, au lililotengwa na 

kuwekwa vitu fulani, fulani: kama mau au bustani. Nyingine zinakuwa 

na eneo la duara na katikati kuna kuwa na mnara au nembo au alama 

fulani. Aidha kiwakilishi cha maji na kadhalika. Ya pale Moshi Mjini 

Kilimanjrao Tanzania; kwa sasa moja wapo ina “kichuguu” cha mlima 

Kilimanjro. Nyingine sanamu ya mwanajeshi mwenye sila, ile ya 

Ufaransa ina mnara mkubwa tu. Huku ya Mwanza ikiwa na Samaki. Pia 

ya Arusha mjini nayo ina mnara wa Mwenge ile iliyopo mkaba na 

Azimio la Arusha. Nyinge ina mnara wa Saa ile iliyopo karibu na ofisi 

ya mkuu wa Mkoa au tawi la Benki Kuu ya Tanzania.

Kwa hiyo, kama upo katika njia panda kama hiyo, kuliko 

uamuwe kufuata njia ni njia, utapotea! Na gharama ya kupotea 

ni kubwa: na kurudi huwa gharama kubwa sana: na kuna kuwa 

na kutokurudi kabisa; kwa hiyo, ni bora upumzike kwenye hilo 

eneo lenye nafas tajwa hapo juu. Jifanye hata kama unangolea 

majani au muhudumuwa bustani ama maua yaliyopo hapo. 

Hata kama hakuna maua, au mnara, basi kuna uwezekana kukawa na 

eneo la kusimama; hapo simama! 

Kama hakuna, simama katikati kabisa, na magari yatakupisha tu maana 

hapo katikati huwa hayapiti! 

 Epuka kuendea njia ni njia! Nimewaona wengi wakisema 

kuwa nimesubira mume vyakutosha, mwezi hu ukipita, asipokukuja 

mtu kunichumbia aliyeokoka; basi. Nimevumilia vyakutosha, akija hata 

mlevi nitaoana naye! Hata mwisilamu maadamu ni mwanaume nitaona 

naye! Huku ni kuhatarisha maisha kwa viwango vikubwa sana! Wengi 

tumewapoteza na hakuja tena kuirudia njia ya wokovu, waliziendea njia 

nyingine moja kwa moja.

Unakuta mtu katafuta kazi muda wa kutosha, na baada ya muda, 

anavunjika moyo. Anakata tamaa, hajui mbele yake kuna njia panda. 

Anafika hapo, kuna njia ya kwanza imeandikwa au inatwa; vumilia 

utapata kazi katika mpango wa Mungu: japo utakawia kulingana na 

mtazamo wako. Ingawa mimi Mungu sikawii maana ni na muda 

nilioupnga. Ya pili inatwa, kubali kutoa rushwa ya ngono, yaani weke 

wokovu pembeni alafu upate kazi na utaanza kesho. Na utapewa na 

kiasi fulani cha fedha cha kuanzia maisha, ila uwe na uhakika uwokovu ndo umeuacha hivyo.

Nyingine ya tatu inatwai, kubali kusilimu, yaani uwe mwisilamu, au 

kuolewa kama mke wa pili alafu nitakupatia maisha mauzri. Lakini 

huyo Yesu wako muweka pembeni.

Mtu kwa kuwa amechoka kiroho, na amemuona Mungu kama

hajamjibu, anajikuta anaangukia katika njia ambayo si sahihi! Maamuzi 

kama haya huwa hayafanywi ghafula. Ila ni jambo ambalo linakuwa 

katika hali ya mgogoro kwenye nafsi ya mtu kwa muda kitambo! 

Fahamu kuwa maamuzi hufanywa kwenye nafsi. Ndiposa 

unampoyasikia maneno ya mtu aliyevunjika moyo; au kukata tamaa 

unapaswa kuwa makini sana.

Jifunze kuisemesha nafsi yako, na kujiambia kuwa, muamini 

Mungu. Kama wakina Kalebu, Musa na Yoshua walivyozungumza na 

ndugu zao. Wakiwambia kuwa msimwasi Bwana: nawe ongea na nafsi 

yako, iambie; Ee nafsi yangu; usimwasi Bwana. Maana atabaki kuwa 

Mungu hata kama hakujibu; ni bora kufia au kuzalilika kwenye mikono 

ya Bwana kuliko nje ya hapo.

Huwezi kumuelewa Musa, kama hukuwahi kupitia hapo. Mungu alikuja 

na pendekezo la njia, ambayo Musa alilikataa; kwamba niwauwe hawa 

watu wote alafu wewe uwe taifa kubwa. Musa aliipangua hoja ile, kisha 

Mungu akakubali waende, ila Yeye hatakuwa pamoja nao! Napenda 

sana maneno haya kuwa, “kama hutaenda pamoja nasi, nasi hatatoka 

hapa!” Ifike mahali na wewe, kaa pembeni kwenye eneo la njia panda; 

alafu mwabie Mungu, sichukui maamuzi yoyote yale kama 

hutaninyesha njia sahhi!

Unajua kilicho waangusha wana wa Israeli na kujikuta 

wanajitengenezea ndama ya kuyayusha na kuiabudu kama Mungu! Ni 

pale walipoona Musa amekawia sana mlimani! Adui akawafikisha njia 

panda ya kimawazo! Kisha akawaonyesha njia isiyo ya kweli 

aliyoikusudia, Haruni naye akajikuta anawasikiliza wale watu!

Nakujulisha hili maana eneo la kumngoja Bwana, limefanyika kuwa 

gumu sana kwenye maisha ya watu wengi; Hata watu walipoona ya 

kuwa Musa amekawia kushuka katika mlima, wakakusanyana 

wakamwendea Haruni, wakamwambia, Haya! Katufanyizie miungu itakayokwenda mbele yetu, kwa maana Musa huyo aliyetutoa katika 

nchi ya Misri hatujui yaliyompata. Kutoka 32:1

Sijui kwako ni jibu lako lipi lililokawia kuja! Ila kumbuka na 

fahamu sana hata Mithali husema; kuwa jambo likikawia moyo 

huugua! Usipojifunza kuongeza imani yako; ya kumngoja 

Bwana kwa Saburi, uwe na hakika unakabiliwa na hatari ya kuwa njia panda. 

Musa alionekana amekawia machoni pao! Na wao kujikuta wakichukua 

maamuzi yasiyo sahihi! Sio hao tu, kuna makosa pia kwa mfalme 

Sauli. Hapa ni mwanzoni tu mwa ufame wake, alikwena kutoa sadaka, 

na watu walijikusanya kwa ajili ya jambo hili, ila Samweli alikawia, na 

alipokawia, watu waanza kuondoka. Alipoona wanaondoka naye moyo 

wake ukavunjika. Kwa jeuri na kiburi akaisongeza yeye ile sadaka.

Ile amemaliza tu, Samweli kuhani huyo mbele yake! Sijui kama 

unajifunza kitu hapo, unapokuwa unasoma haya maandiko! Ni kwamba 

ile mtu amenaguka au kuiendea njia nyinge, tu, hukumu ya Mungu 

inamjili punde. Mungu ambaye alifikiri yupo mbali, anamuona sasa 

anamjilia ila sio katika kumpatia, majibu bali ni katika kumpatia hukumu! 

Hali kama hii utaiona pia kwa Adamu na mkewe. Wakati wakiwa njia 

panda ya mamuzi ya kwamba wakubaliane na onyo la Mungu au 

waambatane na ushawishi wa Shetani Mungu alikuwa kimya. Alitulia 

kama vile hayupo, ila walipoanguka tu! Ndipo walipomuona huyo 

ajitokeza, na uwepo wake walianza kuuhisi, baada ya anguko: ndiposa 

uliwapatia hukumu na kujificha!

Mungu sio kwamba yupo mbali, yupo karibu, ila njia 

panda wakati mwingine zipo ili kutupima kama kweli 

tunampenda, au kumtegemea Mungu!

Mfano hapa kwa mfalme Sauli, vumilvu ulikuwa ukipimwa, na utii pia. 

Kumbuka kinyume cha utii ni kiburi! Na hapo kilijidhiirsha. Yamkini 

alijisemea moyoni, mwake kukwa ba Samweli ni nani! Hata mimi 

naweza kutoa sadaka hii, mimi ni mfalme, nami ni mpakwa mafuta wa 

Bwana! Watu wengi Mungu anazungumza nao, kuhusu jambo fulani, 

ila kuhusu utekelezaji wake anakawia kusema. Hapo wengi huanza 

kulitekleza, baada ya muda wanakuja kugundua kuwa wakati wa 

Mungu ulikwa bado. Hapo ni baada ya maumivu mengi! Fahamu, hata wachezaji na waimbiji, hawaanzi bila kusikia kipenda au filimbi ama 

mlio fulani !

Na sisi tunapswa kujifunza pia. Jionee maandiko haya kisha ujifunze 

jambo hapa. 1 Samweli 13:

8 Akangoja siku saba, kwa kadiri ya muhula uliowekwa na Samweli 

lakini Samweli hakuja Gilgali; na hao watu wakatawanyika mbali naye.

9 Sauli akasema, Nileteeni hapa sadaka ya kuteketezwa na sadaka za 

amani. Akaitoa sadaka ya kuteketezwa.

10 Hata mara alipokwisha kuitoa hiyo sadaka ya kuteketezwa, kumbe!

Samweli akatokea. Naye Sauli akatoka kwenda kumlaki na kumsalimu.

11 Samweli akasema, Umefanya nini? Naye Sauli akasema, Ni kwa 

sababu naliona ya kuwa watu wanatawanyika mbali nami, na wewe 

hukuja siku zile zilizonenwa; nao Wafilisti wamekusanyika pamoja 

huko Mikmashi;

12 basi nikasema, Wafilisti watanishukia sasa mpaka Gilgali, kabla 

sijaomba fadhili za Bwana; kwa hiyo nalijishurutisha, nikatoa sadaka ya 

kuteketezwa.

13 Naye Samweli akamwambia Sauli, Umefanya upumbavu; 

hukuishika amri ya Bwana, Mungu wako, aliyokuamuru; kwa maana 

Bwana angaliufanya ufalme wako kuwa imara juu ya Israeli milele.

14 Lakini sasa ufalme wako hautadumu; Bwana amejitafutia mtu 

aupendezaye moyo wake, naye Bwana amemwamuru yeye kuwa mkuu 

juu ya watu wake, kwa sababu wewe hukulishika neno lile Bwana 

alilokuamuru. 1 Samweli 13:8-14. 

{Mstari wa 13 na 14, unalenga kutujulisha ya kuwa, kuna jambo jaribu 

hili lililenga. Nyuma yake anatujulisha kuhusu yeye Sauli kupimwa na 

kukutwa na hatia/kosa la kukosa utii. Lakini; kitu Mungu alikusudia ni 

kwamba, ufalme wake udumu milele. Na hauwezi kudumu, kama 

hatashinda mtihani. Tazama mara baada ya kufeli; utakuta 

anapokonywa ufalme!}

Tuendelee: Kama Samweli angetokea siku ya kwanza, lisingekuwa 

jaribu kwa mfalme Sauli, lakini hata ya pili, tatu na ya sita mfalme bado 

moyo wake ungeweza kuimili. Ila zaidi ya hapo uvumilivu ulimshnda!

Matokeo yake namabiw ana samweli kuhani kuwa hajaitii sauti au mari 

ya Bwana! Na kwkao inawezekana kuw amajib yangekukuta mwaka wa kwanza, wa pli au awatat, bado isingekuw ajaribu kwkao, ilalimekaa 

hadi sasa kwawa nee ayua wa sita, limeanza kufanyiajaribu kwkao. 

Kitendo cha wengine kuole, au kufanikiwa a kukuacha kinakuumiza 

kama ilivyokwa kwa Sauli mfalme ilehali yawat kundkana 

kumuachahuku kukiw ana shindikiz la Waflisi! Nikwmabie tu kwmaba, 

majira ya Mungu ni ya thamani kulko harakaharaka zako. Na ni nnai 

amekwmabia kwua umeitiwa kfanaikwia katika mda unaofanna na 

wenzako! Ibrahimualipata mdtoto Isaka katika muda ulikinza na watu 

wengi! 

 Fahamu : Shindikizo, ni njia ya adui ya kukusukuma au 

kukuharakisha. “Presha” kutoka nje, au msukumo fulani; Shetani 

huutumia sana kukuharakisha. Vitu kama umri umeenda, tazama jinsi 

wenzako wanavyofanikiwa na kukuacha. Na kadhalika.

Kuna sentesi moja muhimu sana kutoka kwa mfalme Sauli tunapaswa 

kuidodosa kwa kina hapo juu. Na kabla ya kukupatia hiyo, nataka uione 

hali ya watu kuanza kuondoka! Watu walipoanza kutawanyika, au 

kurudi majumbani kwao katika ile siku ya saba; ndipo na moyo wa 

mfalme ulipoanza kutetereka.

Maana yangu ni nini? Adui akiona umeweza kuliimili jaribu, atatumia 

kelele za wana wa Israeli; ili kukushindikiza wewe Haruni uwachongee 

ndama. Maana ameshajua, ameshindwa kukupigia kelele nafsini 

mwako; sasa anatumia kelele za watu wengine.

Kitendo hicho, kiliuteteresha moyo wa mfalme. Lakini pia; hofu ya ujio 

wa adui ambao ni Wafilisti; ilimteteresha mara dufu. Lazima ujifunze 

namna ambavyo adui hufanya kazi. Tazama sentesi hii kutoka kwa 

Sauli; mara baada ya kuulizwa na Samweli: basi nikasema, Wafilisti 

watanishukia sasa mpaka Gilgali, kabla sijaomba fadhili za Bwana; 

kwa hiyo nalijishurutisha, nikatoa sadaka ya kuteketezwa. 1 Samweli 13:12.

Tafadhali Usikose Sehemu Ijayo, inayobeba pointi ya 8 isemayo UWE NA UTULIVU MOYONI...

Kama Bado Hujaokoka na unaguswa kufanya hivyo, Fuatisha Pamoja Nami Sala Hii ya Toba.

 Sema ; MUNGU BABA, NINAKUJA MBELE ZAKO, MIMI NI MWENYE DHAMBI, NAKUOMBA UNISAMEHE: AMENI.

Hakikisha unatafuta kanisa la Watu Waliokoka Ukaabudu Hapo.

Tumeunda Channel ya WhatApp, Tufolo; https://whatsapp.com/channel/0029Va827LBJENy9u6Enke1h 

Kwa Maombi: +255759859287 

http://www.ukombozigospel.blogspot.com


Kundi letu la WhatsApp https://chat.whatsapp.com/E0eD0xegh1eIGMjRykPyRD

Telegram https://t.me/+fft3GHXC9xIzYjhk

Subscribe YouTube yetu: https://www.youtube.com/@ukombozigospeltv

Kwa Maombi +255759859287 

Usiache Kutembelea na Ku-Like Page Yetu Ya Mafundisho ya Neno la Mungu Facebook: https://www.facebook.com/MafundishoyanenolaMungunamwalimuoscarsamba?mibextid=ZbWKwL


UWE NA AMANI

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni