Na Mwalimu Oscar Samba #Ug Ministry |
Dalili/Ishara
zitakazokujulisha uwepo wa Pepo Mahaba kwa njia ya Uridhi.
(..Mpendwa Kesho ya jana
ni leo, na ahadi ni deni kama waswahili wanenavo, nami sina budi kuendelea pale
nilipo ishia jana. Kumbu hii ni sehemu ya 3 kwa hiyo kama uipitwa na zilizopita
zitafute ili tuweze kwenda sanjari)
1. Wazazi au babu
zako watakuwa na mafarakano kwenye ndoa, yaani migogoro au kutokuelewana na
hali hiyo huwa kwa ndoa za ndugu zako pia.
2. Baathi ya ndugu wa kwenu kuwa na
watoto wa nje ya ndoa.
Ukiona mama au baba alikuwa na tabia hiyo na hatimaye watoto/mtoto kuiridhi jua
roho hii ipo miongoni mwao.
3. Wanandoa kutengana, huyu kuishi huku na yule kule ni
dalili kubwa sana ya Pepo Mahaba, na jambo hilo kuwa katika jamii husika.
4. Wazazi kugawana watoto, unakuta katika familia kuna watoto
wa wapendwao zaidi na baba na wale wa mama. Na jambo hili huwa katika familia
za kwenu yaani zaidi ya moja. Dalili hii imejificha sana na kwa bahati mbaya
wengi hawaitambui kuwa ni ya uwepo wa Pepo Mahaba.
Hatua za kuchukuwa: Nimekwisha kukuorotheshea mbinu
kadhaa za kumshinda huyu pepo kwenye kipengele kilichopo hapo mbeleni ila hapa
ninakutaka kufanya ya fwatayo.
Zipo njia kuu mbili za
kufanya.
Ingawaje wataalamu ama wa mambo ya kuvunja
madhabahu ama kujinasua katika matatizo kama haya hupendekeza kwa anayetaka
kutumia njia zote kuanza na ya pili ili kujikomboa yeye kwanza na kisha
kuwakomboa wengine kwa madai kwamba mfungwa ni ngumu kumkomboa mfungwa ama ni
vigumu kusukuma gari angali ukiwa upo ndani ni shariti ushuke kwanza nami
ninakubaliana nao.
(a) NI ILE YA KUVUNJA MADHABAHU. Faida
yake: Ni kwamba utawakomboa ndugu zako wote ama watu wote waliopo chini ya
hiyo madabahu, aidha ni ukoo au kabila ama eneo fulani.
Gharama yake: Maombi yake ni magumu na huchukuwa
muda mrefu.
(b) NJIA YA PILI, KUJITENGA
NA MADHABAU. Njia hii ni pale muhusika atakapofwata hatua zote za kuvunja
madhabahu ila maombi yake hayata lenga kuivunja bali kujitenga yeye na huweza
kuitenga pia na familia yake au kikundi kidogo cha watu. Hufananishwa na kukata
tawi la mti huku yale ya kuvunja madhabahu yakifananishwa na kung’oa mti. Kwa
mfano huo natumai utaelewa utofauti wake. Pia unaweza kulitoa jina lako kwenye
maagano ama viapo ulivyoingizwa aidha na mababu, wazazi ama mtu yeyote
aliyekuwa na uhalali huo ikiwemo viongozi wakimila, kabila, jadi ama
kisiasa/kiseikali.
Gharama yake: Huchukuwa muda mfupi kulinga na
bidii ya muombaji.
Hasara yake: Jamii iliyosalia itaendelea kuteseka
na madhabahu hiyo huku wewe ukiwa salama ila kuna baadhi ya vitu hutavipata kwa
haraka au ukamilifu hususani vile vya kurithi vilivyo vizuri yaani Baraka za
wazazi au zilizopo kwenye eneo husika ambavyo ni halali yako kuvipata kwa
mujibu wa bibilia.
Katika namna
ya kuvunja madhabahu fwatilia mbinu hizo kwenye kitabu changu cha Namna ya
Kuishi wakati wa Majaribu au Mapito kwenye mada ya kujitia nguvu, kipengele cha
huzuni mada ndogo ya kuifunga dhambi katika madhabahu.
Naguswa
kukupa mfano wa njia hizo mbili za kujikomboa. Mfano wa njia (a), Nilikuwa katika maombi ya kuvunja
madhabahu kipindi fulani na niliota ndoto ya kuwa nimeung’oa mti mkubwa uliopo
kijijini kwetu, ila bado ulikuwa hai na ulikuwa upo chini huku ukiwa na
uhalisia wa mtu na sura ya miongoni mwa babu yetu mmoja wa kale aliyekwisha
kufariki. Kung’oa mti maana yake ni kuvunja madhau na kuendelea kuwa hai angali
ukiwa chini umeng’olewa maana yake ni kwamba hatua za kuharibun
kuangamiza/kuteketeza zinaitajika, kwani kuung’oa ni ishara ya kung’oa na kubomoa,
kama lisemavyo hili andiko: Yeremia 1:10.
Katika mfano
(b) wa kujitenga, kuna rafiki yangu
mmoja aliye mtumishi mwenzangu alinisimulia kuwa wakati akifanya maombi fulani
mlimani yaliyomgarimu miaka kama miwili, aliona dhairi kwamba kuna kisu kimempita
na kwenda kukata tawi fulani la mti na tawi lile kudondoka chini. Kisha Mungu
akamwambia kuwa “tawi hilo ni wewe”.
Maana yake mtu huyu alikuwa kwenye maombi ya kujitenga na roho za kwao kwani
pia Mungu alimwambia mti huo ni ukoo wa kwao na tawi ni yeye. Kwa hiyo yeye
yupo salama ila ndugu zake bado wapo hatarini/matesoni. Tuendele na mlango mwingine;
(3) Vitendo vya Uzizi/Uasherati. Dhambi hii maandiko yanatamka
bayana ya kwamba hufanyika nje na ndani ya mwili wa mwanadamu. Nje ni kwa huu
mwili na ndani humuwakilisha Mtu/Utu wa ndani na mtu wa ndani ndiye anayeota
ndoto. Nikiwa na maana nafsi yako, roho na moyo. Kwa hiyo ufanyapo hivyo ni
dhairi kwamba mapepo haya hupata nafasi ya kuweka makao kwako na kuketi panapo
mlango wa ndoto ambao upo kwenye nafsi. Kumtoa pepo aliyepenya kwa njia hii
kuna hitaji maombi ya rehema makubwa
na yale ya utakaso wa nafsi na moyo pamoja na upatanisho wa nafsi ambao hufanywa kwa Damu ya Yesu na Ujazo wa
Roho Mtakatifu.
(3) Kutizama Picha za Utupu/Uchi. Macho ya mfalume Daudi alipomtizama
yule mwamke aliyekuwa katika pozi la kuoga na ndani yake yaani kwenye ulimwengu
wa roho Pepo Mahaba ilipata nafasi, na kupitia dhambi ile maisha yake na ya
Taifa lake yaliyumba mno. 2Samweli 11:2
Ikiwa wakati wa jioni, Daudi akaondoka kitandani, akatembea juu ya dari la
jumba la mfalume; na alipokuwa juu ya dari aliona
mwanamke anaoga; naye huyo mwanamke
alikuwa mzuri sana, wakupendeza macho. Kupitia Macho Daudi
alianguka dhambini, kwani mistari inayofwata anaanza kupeleleza habari za huyo
mwanamke, na wewe unayetazama picha za
utupu kupitia macho utaanza kupeleza kutenda dhambi na hapo hapo mapepo yatakupeleleza
ili kukupata na madamu mlango huu wazi yataingia na kufunga ndoa nawe rohoni.
Kumbuka
kupitia macho yako waweza fungua mlango kwa adui huyu kuingia ndani yako na
kukuvuruga kupitia ndoto. Kitendo cha kutizama picha hizo kina mpa Shetani
nafasi kwa kufungua mlango kwani macho yako na mawazo yako moyoni ni mlango.
(4) Kutamani Mke/Muwe wa Mtu ama
Binti/Mvulana (Tamaa ya Ngono). Katika kitabu kile cha Kumbukumbu
la Torati 5:21 Wala usimtamani mke wa jirani yako.. Mungu alijua
fika ya kwamba kutamani kwa aina hii hufungua mlango kwa Pepo Mahaba na kwa
njia hiyo huweza kukusumbua ndotoni.
Ukisoma mada
ile ya Usimpe Ibilsi nafasi na ya Namna ya kuifunga dhambi kwa kamba
madhabauni kwenye kitabu changu cha Namna
ya Kuishi wakati wa Majaribu au Mapito nimeelezea jinsi ya kujinasua na
kukwepa jambo hili. Ila hapa ninakudokezea kwa kifupi.
Jitaidi sana
kuchunga macho yako kwa kumsihi Mungu pia akusaidiye, Ayubu 31:1 “Nimefanya agano na
macho yangu: basi nawezaje kumuangalia msichana? Na Daudi aliomba hivi; Zaburi 119:37 Unigeuze macho yangu
nisitazame visivyofaa, unihuishe katika njia yako. Mungu akishageuza macho yako mwambiye pia
avifanye viungo vyako kupita katika njia yake kama Daudi aombavyo, “unihuishe
katika njia yako”
(5) Mwanandoa mwenzako kupoteza
uaminifu, Natuma
tupo pamoja nisemapo kuwa mtu mke na mtu mume waliowana ni mwili mmoja. Kama
ndivyo basi rohoni pia ndoa yao hutumia mlango mmoja. Kosa la mwanadoa mmoja
linaweza kufungua mlango kwa Pepo Mahaba na akija atakaa juu ya ndoa yenu na
akikaa hapo atawavuruga sana. Ila mmoja wapo akiwa yupo vizuri kiroho na kwa
kujua jinsi ya kufunga mlango, Pepo huyu hawezi kukaa juu ya ndoa hiyo badala
yake atakaa kwa mhusika aliyefungua mlango au aliyedhaifu kiroho. Yaani anaweza
kufungua mlango mume na akatubu na kuendelea vyema kiroho ila Pepo likakaa kwa
mke ambaye hakufungu mlango ila amelega kiroho maana ameshindwa kulifukuza.
Tutazame
jinsi pepo linavyoweza kukaa juu ya ndoa kwakutizama mfano huu wa jinsi lilivyo
wai kukaa juu ya Taifa la Iziraeli. 1Mambo
ya Nyakati 21:1 Tena Shetani akasimama juu
ya Iziraeli, akamshawishi Daudi
kuwahesabu Iziraeli.
Ukifwatilia
kisa hiki utaona jinsi Mungu alivyokasirika na kuachilia adhabu yake kwa Taifa
hili. Nataka utizame nami hapo kwa akili za rohoni: Ni kwamba Shetani amekaa
juu ya Iziraeli na matokeo yake akapata nafasi ya kumshawishi mfalume Daudi na
kumtumbukiza dhambini. Na kwenye ndoa yako akikaa juu ya hiyo ndoa ni hakika
hakuna namna mtakavyoweza kuelewana na mwenzako au wote mnaweza kujikuta
mnatafuta “nyumba ndogo” na kufanya vitendo visivyofaa. Na
kupoteza uaminifu kwa mwanandoa mwenzako kwa weza kuwa kwa kutoka nje ya ndoa,
kumtamani mtu wingine kingono na kadhalika.
(6) Mahusiano ya Uchumba Bubu au
“Uboyifrendi/Ugelifrendi”, ama Ahadi ya kukuoa/Kuolewa nawe.
Kupitia pia
ahadi ya mtu aliyewai kukutamkia kukuoa au kuolewa na wewe na jambo hilo
kutokutimia, huweza kufanyika mlango kwa pepo huyu. Ndio maana baada ya muda
ukiota unafanya tendo hilo unaiona sura ya huyo mtu. Ni jambo la hatari kwa
vijana kujihusisha kwenye mapenzi kabla ya wakati wake nikiwa na maana
“Uboyifrendi” na “Ugelifredi” ni dhambi pia uchumba usio na lengo la kuoana ni
dhambi pia. Maandiko yanaunga nami dhairi bila kificho, Wimbo uliobora 3:5 Nawasihi,
enyi binti za Yerusalemu, kwa paa na kwa ayala wa porini: msiyachoche mapenzi, wala kuyaamsha, hata yatakapoona vyema
yenyewe.
Kuona vyema
yenyewe maana yake mahusiano ya kimapenzi yana wakati wake. Kwa hiyo kufanya
hivyo kabla ya wakati wake ni hatari ndio maana punde ufanyapo hivyo Shetani
anapata mlango wakuyavuruga maisha yako na miongoni mwa vitu anavyopenyeza ni
ndoto. Na njia hii ni miongoni mwa njia kuu zinazowasumbua wengi hususani
wanandoa na watumishi, maana Shetani ni ngumu kuipata njia nyingine kwako kwa
hiyo hulazimika kuifwatilia historia yako ya zamani ili kukutesa leo.
(7) Miziki/Nyimbo za kidunia. Bibilia huziita nyimbo za upuzi, Amosi 6:5. Nyimbo hizi zimeingiliwa na
kutawaliwa na Mapepo Mahaba ndio maana “staili” zao za kucheza na mavazi yao
walio wengi hususani wanawake ni yakimapepo mahaba. Watacheza kama watu
wanaofanya tendo la ndoa au kuchezesha viungo vya mwili vyenye mvuto kimapenzi
na kuvaa mavazi ya nusu na hata uchi kamili.
Mauthui ya
nyimbo zao walio wengi huwa ya kimapepo mahaba. Utakuta wanaimba mapenzi na
kuhimiza au kusifia jambo hilo kwa shabaha za kuwadondosha wengi katika dhambi
hiyo. Muonekano wa waimbaji baathi ya wakiume huchocheoa vitendo vya Ushoga
kwani wapo waimbaji wakiume wanaovaa hereni na kufunga suruali chini ya kiuno.
Hizo zikiwa ni alama za Ushoga. Pia kwa wanawake wapo wanaoonyesha vitendo vya
kuchochea usagaji kwa kucheza kwao na hata kuvionyesha atharani. Unapo tazama
ama kusikiliza nyimbo kama hizo ni fika una fungua mlango kwa mapepo hayo
kukuingia kwani nyimbo huweza kuimba moyoni kwa muda mrefu na picha hizo kukaa
katika macho ama nafsini kwa muda. Epuka hili kwa gharama yoyote ile na kumbuka
ni dhambi kwa aliyeokoka kuimba au kutiza na hata kucheza nyimbo hizo.
(8) Kusikiliza au kufwatilia Hadithi
zenye elementi au chembe chembe za pepo mahaba.
Sikio ni
malango wa rohoni,… (..Tuonane tena Kesho). Nakusihi kuendelea kunifwatilia
tena kesho na panapo majaliwa tutaendelea na kipengele hiki na vinginevyo. Kama
hujaokoka na unataka kuokoka ama ulirudi nyuma kiroho na unataka kutengeneza na
BWANA kwa upya leo, tafadhali fwatisha nami maneno haya kwa Imani, Sema: BWANA
YESU, NINAKUPENDA, NINAKIRI NA KUAMINI MOYONI MWANGU KUWA WEWE NI MUNGU,
ULIKUFA NA KUFUFUKA KWA AJILI YANGU, INGIA NDANI YANGU KAMA BWANA NA MWOKOZI WA
MAISHA YANGU LEO, AMENI.
Hongera kwa
kuokoka na tafuta kanisa la watu waliokoka ukasali hapo.
Na Huduma ya
UKOMBOZI GOSPLE, Arusha Tanzania, Kwa Maombi, Ushauri, Maswali au Sadaka
wasiliana nasi, Barua pepe: ukombozigosple@gmail.com
Simu: +255 759 859 287 pia waweza itumia kwa M-PESA. Zaidi www.ukombozigospel.blogspot.com #UkomboziGosple #MwalimuOscarSamba
Pia #Like
#Penda Page/Ukurasa wetu au kundi la Fb, ili kupata habari hizi kwa haraka,
zaidi. Ug Ukombozi Gosple,
PAGE: https://www.facebook.com/Ug-Ukombozi-Gosple
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni