Ninakukaribsha
katika jina la Bwana wetu Yesu Kristo aliye Bwana na Mwokozi wa maisha yetu
katika safu hii ya ujumbe wa Semina ya Neno la Mungu ikiwa ni siku ya sita kama
ilivyofundishwa jana na Mwalimu.
Mwalimu
alianza kwa msisitizo kwamba ili kufanikiwa Kiroho na kiuchumi ama kufikia
mafanikiao ya kutajirika kiuchumi katika Kristo Yesu yatupasa kuutafuta kwanza
Ufalume wa Mbinguni na Haki yake na kisha hayo tunayaoyahitaji tutayapata.
Jana alifundisha
mbinu moja nayo ilikuwa ni KULIJUA KUSUDI LA MUNGU LA KUKUTAJIRISHA, katika
mbinu hii Mwalimu aliwataka walio matajiri kufahamu jambo hili na kuliishi huku
akiwafundisha wale wenye nia au kiu ya kutajirika kupitia mfumo wa kimbingu
kuhakikisha wanalifahamu na kuliisha kusudi hili ili Mungu awatajirishe na
akisha kuwatajirisha wahakikishe wanalitimiza hili kusudi ili mali ama fedha
zisiwatowe kwake.
Mwalimu
aliendela kubainisha ya kwamba siku hizi kumekuwa na tatizo kubwa sana siku za
leo ya kwamba watu kabla hawajawa matajiri au kipindi wakiwa hawana kazi
walikuwa wakijitoa mbele zake kwa kufanya usafi makanisani au kuwa wana maombi
ila mara baada ya mafanikio hali hiyo imeyayuka ndani yao.
Tulitazame hilo kusui, Ni 1Timotheo
6:17 Walio matajiri wa ulimwengu wa sasa uwaagize wasijivune, wala
wasiutumainie utajiri usio yakini, bali wamtumaini Mungu atupaye vitu vyote kwa
wingi ili tuvitumie kwa furaha.
18 Watende mema, wawe matajiri kwa
kutenda mema, wawe tayari kutoa mali zao, washirikiane na wengine kwa moyo;
19 huku wakijiwekea
akiba iwe msingi mzuri kwa wakati ujao, ili wapate uzima ulio kweli kweli.
Kwa mujibu
wa hayo maandiko tunapata ya kwamba jambo la kwanza Mungu anawataka WASIJIVUNE, Maana yake utakapokuwa na
mali haikupasi kujivuna ama kuiringia hiyo mali. Pili Kutokuutumaini huu Utajiri, Mwalimu alisema ya kwamba wapo
watu walioweka tumaini lao kwenye utajiri ama mali zao ndio maana wakisikia duka
limeungua ama gari limepata ajali nao hupata presha ama kushindwa kuendelea
vyema na maisha, na alisema athari yake kubwa likija jaribu na kupiga hizo mali
hakika utamwacha Mungu au hutaweza kupita hapo.
Ayubu
alishinda kwa sababu aliweka tumaini lake kwa Mungu ndio maana kuna mahali anasema
kama alizitumainia hizo dhahabu, nalitokee jambo fulani akiwa na maana
hakuutumainia utajiri wake na kwako ikiwa hivyo likija jaribu utasema Bwana
Ametoa Bwana Ametwaa, Jina lake lihimidiwe.
Jambo la tatu ni kuvitumia kwa furaha, sio kusudi la Mungu la kutupa fedha
kisha sisi tushindwe kuzitumia hizo fedha kwa furaha, bali ni kusudi lake
tuzitumiye bila masikitiko, haifai kuwa tajiri huku watoto au jamaa yako
ikiishi maisha magumu.
Nne watende Wema, Wawe Matajiri kwa kutenda wema, wema
ya kwanza hapo ni ya tajiriri binafsi na ile ya pili ni kutenda wema kupitia
utajiri wake. Wewe kama mtu binafsi unapaswa kuhakikisha unakuwa mwema, Ukiona
jambo jema lifanye ukiona uhitaji wa tendo la kiungwana mahali litende kama
wewe. Pili kukiwa na uhitaji wa tendo lolote linalohitaji fedha wewe litendo
katika wema.
Tano, Unapaswa kuwa tayari kutoa mali
zako, utoaji ndilo
kusudi kuu la Mungu katika kukubariki na anahitaji ufanye hivyo kwa ajili ya kuitegemeza
kazi yake na kuwasaidia wenye uhitaji mbali mbali. Kuna watu walimuomba Mungu
magari kisha akawapa ila magari yao hayakuwai kubeba hata kipaza sauti kwa
ajili ya kuhubiri injili, huku wakishindwa hata kuandika neno YESU ANAOKOA
nyuma ya magari yao.
Wengine
walimuomba vyombo vya Injili cha ajabu havitumiki katika kumtukuza Bwana badala
yake vinapiga miziki isiyofaa kwenye masherehe ya kidunia huku vikitumika
kuwapeleka watu jehanamu ya moto.
Sita, Washirikiane na wengine kwa
Moyo, hapo maandiko
yanawataka matajiri kuwa na ushirika na watu wote bila kubagua au kuchagua tena
kwa moyo wala sio kwa kuigiza ama kujionyesha kwenye magazeti au mbele ya
waandishi wa habari bali jambo hilo la paswa kufanywa kwa moyo wakupenda na
wakujitoa. Shiriki misiba, wenzako wakichimba kaburi na wewe chimba.
Saba ni ili wajiweke akiba kama
msingi mzuri wa baadaye, kumbuka katika siku za awali ya kwanza ama ya pili tulichambua jambo
hili la akiba kiundani sana na ndiposa Mwalimu akakutaka kumuiga chungu ama
kujifunza kwa sisimizi ambaye Mithali 6:6-8 ina mataja kama ni
mwenye akili na hujiwekea akiba kwa ajili ya majira ya njaa, na wewe kukutaka
kufanya hivyo huku akitaja aina nyingine ya akiba kuwa ni ile ya wema au
ukarimu, na kusema unapokarimu wengine ndiposa na Mungu atakukarimu na wewe
hata kama yule uliyemkarimu hata kuwepo muda huo Mungu atakuinulia mtu mwingine
ikiwa ni matokeo ya wewe kutumia hiyo akiba. Akiba nyingine ilikuwa ni ile ya Sadaka,
alifafanua vyema ya kwamba unapotoa Sadaka unajiwekea akiba Mbinguni kusiko
haribika, kwa nondo wala hakuna kutu na jambao hilo ni la msingi sana.
Shabaha kuu ya Mungu kuyafanya hayo
yote ni ili wewe upate Uzima Kweli Kweli, hapo zipo kweli mbili, ya kwanza ni ile ya kuhesabiwa
haki kulingana na utajiri wako na ya pili ni ile ya wewe kuurithi ufalume wa
Mbinguni mara baada ya kufa yaani kuwa mwana wa Mungu na kuepukana na ile
falisafa ya kwamba ni ngumu matajiri kuurithi ufalume wa Mbinguni.
Awali ya
kukupa mbinu hiyo teule na kisha
kukutaka kulitumia au kuliisi hilo kusudi la Mungu la kukutajirisha Mwalimu
Oscar alikutaka kufahamu kuwa usipolijua kusudi hilo la Mungu ni rahisi sana
kukumbwa na mambo ya fwatayo;
Fungungua
nami kitabu hicho cha 1 Timotheo 6:9 Lakini hao watakao kuwa na
mali huanguka katika majaribu na tanzi, na tamaa nyingi zisizo na maana, zenye
kudhuru, ziwatosazo wanadamu katika upotevu na uharibifu.
Pia sio hilo
tu bali, Mstari wa 10, 6:10
Maana shina moja la mabaya ya kila namna ni kupenda fedha; ambayo wengine hali
wakiitamani hiyo wamefarakana na Imani, na kujichoma kwa maumivu mengi.
Katika hayo
yote alitoa sababu kubwa inayopatikana kwenye mfano ule wa Mpazi tafsiri ya
aliyepandwa kwenye miiba ni mtu aliyekuwa yupo vizuri kiroho na kisha Shuhuli
nyingi, taama na udanganyifu wa mali vikamsonga. Maana yake mali ni roho ndio
maana huweza kumdanganya mtu. Na ili uishinde yakupasa kulifahamu vyema hilo
kusudi la Mungu.
Ni Matahayo 13: 13.22
Naye aliyepandwa penye miiba, huyo ndiye alisikiaye lile neno; na shughuli za
dunia, na udanganyifu wa mali hulisonga lile neno; likawa halizai.
Katika kuhitimisha kwa maombi ya Baraka Mwalimu
na Mwinjilisti aliyekuwa ni mtumishi Mgeni Sixmoni, aliwataka wapendwa kutokuwa
wasikiaji tu wa Neno bali wawe pia ni watendaji wa hilo Neno.
Na kabla
hajamkaribisha Mtumishi huyo Mgeni ili kufunga ibada kwa maombi, Mwalimu Oscar
aliwataka wale ambao hawajaokoka kuhakikisha wanafanya hivyo kwani hawajui ni
lini watakufa na wakifa katika hali hiyo ya dhambi ni fika wataenda jehanamu ya
moto maana bado hawajampokea Bwana na wale wanaotaka kutajirika kibibilia
kupitia mfumo huu wanapaswa kuliishi jambo hili kiusahihi zaidi, na ili kufanya
hivyo hawana budi kuokoka ili Roho Mtakatifu awasaidiye kutimiza jambo hilo.
Kama
hujaokoka na unataka kuokoka ama ulirudi nyuma kiroho na unataka kutengeneza na
BWANA kwa upya leo, tafadhali fwatisha nami maneno haya kwa Imani, Sema: BWANA
YESU, NINAKUPENDA, NINAKIRI NA KUAMINI MOYONI MWANGU KUWA WEWE NI MUNGU,
ULIKUFA NA KUFUFUKA KWA AJILI YANGU, INGIA NDANI YANGU KAMA BWANA NA MWOKOZI WA
MAISHA YANGU LEO, AMENI.
Hongera kwa
kuokoka na tafuta kanisa la watu waliokoka ukasali hapo.
Na Huduma ya
UKOMBOZI GOSPLE, Arusha Tanzania, Kwa Maombi, Ushauri, Maswali au Sadaka
wasiliana nasi, Barua pepe: ukombozigosple@gmail.com Simu: +255 759 859 287 pia waweza itumia kwa
M-PESA. Zaidi www.ukombozigospel.blogspot.com #UkomboziGosple #MwalimuOscarSamba
Pia #Like
#Penda Page/Ukurasa wetu au kundi la Fb, ili kupata
habari hizi kwa haraka, zaidi. Ug Ukombozi Gosple,
PAGE: https://www.facebook.com/ugukombozigospel/
Pia kwenye mtando
Mpya wakitanzania wa
2 DAY SKY:
https://www.2daysky.com/home
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni