Jumapili, 18 Juni 2017

Mwalimu Oscar Samba: MBINU TEULE ZA KUTOKA KWENYE UMASIKINI KWA WATU WALIOKOKA.

Mwalimu Oscar Samba
 Na Mwandishi wetu, wa Ug Ministry.

Ninakukaribisha sanjari na kukusalimu kwa jina lake Bwana wetu Yesu Kristo aliye pia Mwokozi wetu.Leo ni siku ya saba ya Semina Yetu na kumbuka somo hili ni la jana kwa hiyo kijografia jumapili ya leo ndiyo tunahitimisha semina hii ikiwa ni siku ya nane na ujumbe wa nane utaupata kesho.

Mwalimu jana alitilia tena msisitizo wa kukutaka kuutafuta kwanza Ufalume wake Yesu Kristo na Haki yake kisha hayo mengine utazidishiwa. Pia jana alifundisha mbinu moja kuu ambayo ilikuwa ni mbinu ya Akili, Hekima na Maarifa. Mwalimu alivifafanua vitu hivyo kwa mapana na kukuhitaji kuhakikisha ya kwamba una vifahamu ili uweze kunufaika na vitu hivyo.

Alitoa mfano wa Mfalume Sulemani aliyeomba hivyo vitu, 1 Wafalume 3:4-15, ila alisoma mstari wa12 na kukutaka mingine kujisomea.
12 basi, tazama, nimefanya kama ulivyosema. Tazama, nimekupa moyo wa hekima na wa akili; hata kabla yako hapakuwa na mtu kama wewe, wala baada yako hatainuka mtu kama wewe.

Hapo tunaona akipewa moyo wa hekima na akili, katika kitabu kile cha Mambo ya Nayakati wa pili tunaona akipewa maarifa vitu ambavyo vilimsaidia Mfalume huyu.

2 Mambo ya Nyakati 1:7-13, Ila Mwalimu alisoma mistari ya 10-12 na kukutaka mengine kujisomea.
10 Basi sasa nipe hekima na maarifa, nijue kutoka na kuingia mbele ya watu hawa; kwa kuwa ni nani awezaye kuwahukumu watu wako hawa walio wengi?
11 Naye Mungu akamwambia Sulemani, Kwa sababu neno hili lilikuwamo moyoni mwako, wala hukujitakia mali, wala utajiri, wala utukufu, wala maisha za wakuchukiao, wala hukujitakia maisha ya siku nyingi; bali umejitakia hekima na maarifa, upate kuwahukumu watu wangu, niliokutawaza juu yao;
Kwa hiyo hayo ndiyo mambo ambayo Sulemani Mfalume aliyaomba. Na Mungu kumpatia Utajiri kwa sababu ukivipata hiyo ni umepata kanuni za kuwa tajiri. Mwalimu alifafanua kuwa ukiyakosa mambo hayo utakuwa ni Mpumbavu, hali itakayo kuangamiza kama utafanikiwa, maana maandiko husema kuwa kufanikiwa kwa mpumbavu ni kuiangamiza nafsi yake.
Alisoma pia maandiko ya kitabu cha Mithali 24, yanayozungumzia shamba la Mpumbavu ya kwamba kwa sababu alikuwa hana akili alishindwa kulima na hatimaye kukosa huko akili kukaingiza uvivu ndani yake na hatimaye kujikuta likimea mbigili ama miiba, hapa funzo ni kwamba kukosa akili kunaweza kukufanya usitumiye kipawa chako cha uimbaji, kufundisha ama cha sanaa na kukifanya kumea miiba huku ukilalamika kuwa maisha ni magumu. Kama hili shamba la aliyekosa akili, shamba analo, ila badala ya kume choroko na mahindi ama matunda linamea miiba.

Mithali 24: 30 Nalipita karibu na shamba la mvivu, Na shamba la mizabibu la mtu asiye na akili.
31 Kumbe! Lote pia limemea miiba; Uso wake ulifunikwa kwa viwawi; Na ukuta wake wa mawe umebomoka.
32 Ndipo nilipoangalia na kufikiri sana; Naliona, nikapata mafundisho.
33 Bado kulala kidogo, kusinzia kidogo, Bado kukunja mikono upate usingizi!
34 Hivyo, umaskini wako huja kama mnyang'anyi, Na uhitaji wako kama mtu mwenye silaha.
Baada ya kukupa mtaji huo sasa tutazame Utendaji wa mambo hayo matatu;
Kutoka 35: 25 Na wanawake wote waliokuwa na mioyo ya hekima, walisokota kwa mikono yao, nao wakaleta hizo walizokuwa wamezisokota, nguo za rangi ya samawi, na za rangi ya zambarau, na hizo nyuzi nyekundu, na hiyo nguo ya kitani nzuri.
26 Na wanawake wote ambao mioyo yao iliwahimiza katika hekima wakasokota hizo singa za mbuzi.

Hapa tunaona kuwa watu hao walipewa moyo wa hekima hatimaye kuweza kufanya shuhuli za ustadi wa nguo na singa. Tusone tena misitari ya mbeleni.
Kutoka 35: 30 Kisha Musa akawaambia wana wa Israeli, Angalieni, Bwana amemwita kwa jina lake Bezaleli mwana wa Uri, mwana wa Huri, wa kabila ya Yuda;
31 naye amemjaza roho ya Mungu, katika hekima, na akili, na ujuzi, na kazi ya ustadi kila aina;
32 na kuvumbua kazi za werevu, na kufanya kazi ya dhahabu, na fedha, na shaba,
33 na kukata vito vya kutilia, na kuchora miti, atumike katika kazi za werevu kila aina.
34 Naye amemtilia moyoni mwake ili apate kufundisha, yeye, na Oholiabu mwana wa Ahisamaki, wa kabila ya Dani.
35 Amewajaza watu hao akili za moyoni, ili watumike katika kazi kila aina, ya mwenye kuchora mawe, na kazi ya werevu, na ya mwenye kutia taraza, katika nyuzi za rangi ya samawi, na za rangi ya zambarau, na nyekundu, na kitani nzuri, na ya mwenye kufuma nguo; ya hao wafanyao kazi yo yote, na ya wenye kuvumbua kazi za werevu.


Tunaliona tena jambo hilo hapa likijitokeza, maana yake ni kwamba unapokuwa ni mtu mwenye maarifa, hekima na moyo wa akili unaweza kubuni mafanikio makubwa kwenye biashara yako, kama ulikuwa unauzia nyanya chini utapata ufahamu wa kujenga kichanja ili uziye hapo huku ukitambua ya kwamba wapo wateja wasiopenda kununua vitu vya chini, maana watu wanatofautia kiustarabu na wewe yakupasa kuwapata wote. Pia maarifa hayo yatakufa kutambua ni vyema kuongeza hapo na maembe na pilipili ili kukuza kipato chako.

Ukikosa hekima katika biashara yako ni dhairi kwamba ikipanuka hata muda wako wakumtafuta Mungu utamezwa maana itakuhitaji sana kuitumikia ila ukiwa na hekima unaweza weka mfanyakazi wa ziada katika majira yale au siku zile za ibada na kadhalika. Hutaweza kuchelewa nyumbani au kulaza shuhuli nyingine za kimaendeleo.

Alitoa pia mfano wa Yusufu aliyefanikiwa maishani na pia kuinufaisha nchi ile ya Misiri kutokana na kuwa kwake na akili, na wewe utafanikiwa katika huduma yako kama utakuwa na akili hizo. Alisisitiza, kama una huduma ama biashara ni vyema kumuomba Mungu akupe watendaji wenye akili ili wakusaidiye maana hakuna mtu aliyejaliwa kila kitu, mfano Farao alimuitaji Yusufu na angekwama kama angejiona kuwa yeye ni kila kitu.

Mwanzo 41: 33 Basi, Farao na ajitafutie mtu wa akili na hekima amweke juu ya nchi ya Misri.
34 Farao na afanye hivi, tena akaweke wasimamizi juu ya nchi, na kutwaa sehemu ya tano katika nchi ya Misri, katika miaka hii saba ya kushiba.
Tuone pia maandiko mengine, Farao akidhibitisha kuwa Yusufu ndiye, na ilikuwa kweli maana aliyamudu hayo majukumu.
Manzo 41:38 Farao akawaambia watumwa wake, Tupate wapi mtu kama huyu, mwenye roho ya Mungu ndani yake?
39 Farao akamwambia Yusufu, Kwa kuwa Mungu amekufahamisha hayo yote, hapana mwenye akili na hekima kama wewe.
40 Basi wewe utakuwa juu ya nyumba yangu, na kwa neno lako watu wangu watatawaliwa. Katika kiti cha enzi tu nitakuwa mkuu kuliko wewe.

Farao alinufaika na Yusufu pia na hatimaye taifa zima la Iziraeli, lakini hapo chanzo ni akili za Yusufu, ila alizipata kwa Mungu ndiposa Farao anakiri kuwa ni mtu mwenye roho wa Mungu ndani yake, na wewe muombe Mungu akupe na pia akuinuliye watendaji kama hao. Kuna watu wanabuni mitandao na vitu vingi na vinawapa umaarufu pamoja na kipato.
Jambo lingine akili inafanya ni kukupatia kuridhi mali au utajiri wetu kutoka Mbinguni kwa Baba.
Kupitia Agano la Ibrahimu kwa Njia ya Yesu Kristo sisi ni warithi wa Baraka zote za mbinguni, ila tatizo letu hatuzipati zote ama kwa wakati kwa sababu ya akili zetu kutokuwa na uwezo wa kuzimudu hizo Baraka, na Mungu wetu hawezi kutupa maana zitatuangamiza. Mwalimu alitoa mfano huu nami ninamnukuu.
“Mtoto wa darasa la pili, ama wa miaka nane au tisa ukimpa feha atakimbilia kununua mdoli au pipii alikadhalika wa miaka 18 au 19 atanunua kiatu, ila mtu mzima atanunua kiwanja au nyumba ama usafiri.”
Aliendelea na kusema, ndivyo ilivyo kwenye ulimwengu wa roho, wapo watu Mungu akiwapa elifu 50, jumapili hawaji kanisani hadi ziishe, na wengine wanauwezo wakuimili milioni 2, nakadhalika. Kwa hiyo ili Mungu atupe utajiri au urithi wetu hatuna budi kuwa na uwezo wa kuvimudu hivyo.
Tuone jambo hilo kwenye kitabu kile cha Wagalatia 4:1 Lakini nasema ya kuwa mrithi, wakati wote awapo mtoto, hana tofauti na mtumwa, angawa ni bwana wa yote;
2 bali yu chini ya mawakili na watunzaji, hata wakati uliokwisha kuamriwa na baba.

Mwalimu alitanabaisha kuwa hapa unamkuta mtu ana mali tayari katika hazina ya Mungu ila Mungu ameweka chini ya wasimamizi ili atakapo pevuka au kukua kiakili aweze kumpatia. Na alitoa mfano huu;

Wanasheria wanafahamu, kwamba baba anaweza kuandika urithi kwa mtoto wake mdogo ila akaagiza apewe hiyo mali baada ya kufikia umri fulani aidha mika 16, au 20. Kwa hiyo huyu mtoto mdogo ni tajiri ila mali yake ipo chini ya wakili ama mwanasheri na atakapofikisha umri ulio amriwa na babaye ataipata.”

Aliongeza, jambo hili ni halisi kwetu leo mbele za Mngu, ni lazima tukuwe ndipo atupe maana akikupa angali akili zetu hazijakuwa ni fika tutapotea kiroho kama mwana mpotevu na akuna mzazi anayetaka kuona mwanaye akipotea.

Alimalizaia kwa kutoa sababu za watu kutokukua kiroho huk akisema ni kutokuyatamani maziwa ya Akili yasiyogoshiwa, maana humo dimo kuliko na kaili
1Petro 2: 2.2 Kama watoto wachanga waliozaliwa sasa yatamanini maziwa ya akili yasiyoghoshiwa, ili kwa hayo mpate kuukulia wokovu;
2.3 ikiwa mmeonja ya kwamba Bwana ni mwenye fadhili.
Na kama na wewe Umeona mfundisho haya ni yenye fadhili na adili kwako ya kupasa sasa kutamani kukua kiakili na kupata vitu yvote hivo, Tuendelee.
 Pia alisema yeye mweyewe alilipata somo hilo ama kitabu hiki chaTajirika kibibilia ikiwa ni matokeo ya yeye kutamani kufahamu ni kwanini watu wengi waliookoka wanaishi maisha magumu angali wananena kwa lugha na Mungu wanaye na maandiko yanasema ya kwamba Mungu ametubariki kwa baraka zote za rohoni na mwalini huku yakisema kuwa Yesu      alifanyika masikini ili sisi tuwe matajiri ila akitazama mambo hayo alikuwa hayaoni kwa wapendwa.

Kila la heri katika kutazama video yake ambayo inapatika kwenye channeli yetu ya Youtubu ambayo tutakupatia hapo mwishoni, sajari na hayo mwalimu alikutaka kuokoka kama bado huja fanya hivyo huku akisema ya kwamba hiyo ndiyo njia pekee itakayokuwezesha wewe kuziridhi ama kuzipata hizo Baraka kiuwalisia zaidi huku ukiwa na uwakika wa kwenda mbinguni mara baada ya kufa.

Kama hujaokoka na unataka kuokoka ama ulirudi nyuma kiroho na unataka kutengeneza na BWANA kwa upya leo, tafadhali fwatisha nami maneno haya kwa Imani, Sema: BWANA YESU, NINAKUPENDA, NINAKIRI NA KUAMINI MOYONI MWANGU KUWA WEWE NI MUNGU, ULIKUFA NA KUFUFUKA KWA AJILI YANGU, INGIA NDANI YANGU KAMA BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YANGU LEO, AMENI.
Hongera kwa kuokoka na tafuta kanisa la watu waliokoka ukasali hapo.

Na Huduma ya UKOMBOZI GOSPLE, Arusha Tanzania, Kwa Maombi, Ushauri, Maswali au Sadaka wasiliana nasi, Barua pepe: ukombozigosple@gmail.com  Simu: +255 759 859 287 pia waweza itumia kwa M-PESA. Zaidi www.ukombozigospel.blogspot.com   #UkomboziGosple  #MwalimuOscarSamba
Pia #Like #Penda Page/Ukurasa wetu au kundi la Fb, ili kupata habari hizi kwa haraka, zaidi. Ug Ukombozi Gosple,  
 PAGE: https://www.facebook.com/ugukombozigospel/
Pia kwenye mtando Mpya wakitanzania wa
2 DAY SKY: https://www.2daysky.com/home               




Hakuna maoni:

Chapisha Maoni