Na Mwalimu Oscar Samba wa Ug Ministry.
Sifa na Utukufu ni kwa Bwana wetu Yesu Kristo, nami kwa
salamu hizo ninakukaribisha katika safu hii murwa na mubashara ya makala ambapo
leo tupo kwenye mfululizo wa 6, wa somo
letu la NGUVU YA AGANO, Ikiwa ni sehemu ya kitabu changu cha NGUVU YA AGANO
KWENYE ULIMWENGU WA ROHO.
(i) Liliamua
Mustakabali wa Maisha yao kindoa au kimahusiano, Tunafahamu
Isaka alichaguliwa mke na babaye, huku naye akimchagulia Yakobo ama
akimuelekeza mahali pakwenda kuoa, hii ikiwa na maana kwamba mwana wa Agano
haulewi na kila mtu ama haowi kila mahali kiolela.
Alikadhalika jambo hili liliendelea hadi kwa watoto wa
Yakobo yaani Iziraeli. Ukisoma katika Kitabu hiki cha Mwanzo sura ile ya 34,
utamuona binti Lea aitwaye Dina alivyochukuliwa na mtu wa ile nchi aitwaye
Shekemu mwana wa Hamori wa kabila la Hivi ama Muhivi.
Ndugu zake wakakasirika, na awali ya yote walitoa shariti
la kutahiriwa kwa wanaume wa lhlo eneo ikiwa na maana ya kwamba kwao hawezi
kuolewa mtu ama wao kuoa katika jamii isiyotairiwa.
Kumbuka kutairiwa ni
Ishara ya Agano hili kwa wale tulioanza nao toka mwanzo; Wakati Mungu anafunga
hili Agano na Ibrahimu alimwambia kuwa Ishara yake ni Tohara. Tujikumbushe na
kuhakiki pia.
Mwanzo 17: 10 Hili ndilo agano langu
utakalolishika, kati ya mimi na wewe, na uzao wako baada yako, Kila mwanamume
wa kwenu atatahiriwa.
11 Mtatahiriwa nyama ya magovi yenu, na jambo hilo litakuwa ishara ya agano kati ya mimi na ninyi.
11 Mtatahiriwa nyama ya magovi yenu, na jambo hilo litakuwa ishara ya agano kati ya mimi na ninyi.
Kwa hiyo katika swala hili la Mwanzo 34, la kuolewa kwa Dina hawa nduguze wanaposema kuwa binti
yao hawezi kuolewa na mtu asiyetairiwa maana yake ni kwamba hawezi kumruhusu
dada yao kuolewa na mtu wa nje ya Agano.
Mwanzo 34: 14 wakawaambia, Hatuwezi kufanya
neno hili, tumpe umbu letu mtu asiyetahiriwa; ingekuwa aibu kwetu.
Umeona hicho kipengele hapo? Ingawaje mbeleni waliwapa
hilo shariti la kuwatairi watu wa mji wao walio wakiume, lakini bado tohara
hiyo haikuwa na nguvu ya kiagano kwa
kiwango cha kulihalalisha jambo hilo maana ishara ni matokeo ya mapatano kati
ya pande mbili yenye makubaliano, ni kweli walipatana na hawakukubaliana. Kuna mambo
ambayo hukamilisha Agano hayakuingizwa hapo.
Mbeleni Simeoni na Lawi waliwaendea usiku na kuwaangamiza
wote na ksha kuwateka nyara. Sina kusudio la kuhalalisha kilichofanywa na wana
hawa wa Mzee Yakobo ila nataka ujionee Nguvu iliyopo kwenye Agano hili
ilivyoamua swala la Dina na Shekemu mwana wa Hamori.
(h) Liliamua
Mahali Yakobo na Famili yake yaani Iziraeli inapaswa kuishi,na Kuabudu. Maisha ya Mwana wa Agano
yaani wewe uliyeokoka yanaamuliwa na Agano, nikiwa na maana kwa mtu
anayelitambua hili Agano hawezi kuishi nyumba ni nyumba ama kuishi mji ambao
Mungu hakumpangia.
Ndivyo ilivyokuwa kwa Yakobo, Mwanzo 35: 1
Mungu akamwambia Yakobo, Ondoka, panda uende Betheli, ukakae huko; ukamfanyie
Mungu madhabahu huko; yeye aliyekutokea ulipomkimbia Esau, ndugu yako.
Kwa wale wanafunzi wangu niliokuwa nao toka awali
wanakumbuka vyema ya kwamba Betheli ndio mahali ambapo Mungu alifunga Agano
hili ama alimuingiza Yakobo kwenye Agano hili la Ibrahimu kama iliyokuwa kwa
Isaka na kwa babu yake Ibrahimu. Hapo ndipo Mungu alipomtokea Yakobo kwa mara
ya kwanza kwa sura ya kiagano.
Na kwako wewe mpendwa ipo dhamani kubwa sana ya kuishi
eneo sahihi ikiwemo kuabudu sehemu sahihi ambayo Mungu ameikusudia kwako
ndiposa ninakuwa mwepesi wa kuwataka watu waliokoka kutokuhama makanisa
kiholela kwa sababu za makwazo ama vita au hila za ibilisi. Sehemu ambayo Mungu
amekupanda ndipo hapo palipo na madhabau sahihi ya kukubariki. Na jambo hili ni
lakiagano, na hili ni shariti muhimu sana kwenye hili Agano.
Na kujuza hili mapema kwa maaana kama hutaabudu sehemu
sahihi maana yake ni hii, hutaweza kutembea na nguvu za hili ya kiagano, badala
yake utaishia kuomba maombi yakiagano ya Mungu wa Ibrahimu, Isaka na Yakobo
uliyetubariki kwa baraka zote za rohoni na mwalini na uliyenitaka nibarikiwe na
kufanikiwa katika mambo yangu yote na kuwa na afya yangu kama vile roho yangu
ifankiwavyo bila mafanikio.
Jaribu kufikiri kama Yakobo angegoma kwenda El-Betheli
nini kingetokea? Ama kama asigeliitambua sauti ya Mungu iliyomtaka kwenda hapo?
Ni kweli kwa weza kuibua vita katika sehemu ama madhabahu
ambayo Mungu amekuweka ila fahamu fika ya kwamba vita hivyo vinalenga kukutoa kwenye
madhabahu ya El-Betheli. Zaidi kuhusu hili soma kwenye kitabu changu
cha NAMNA YA KUISHI WAKATI WA MAJARIBU AMA MAPITO, kwenya mada ya mwisho ya Faida
za Majaribu pwenti ya EDENI YAKO.
Tuone jinsi Yakobo alivyofanikiwa katika hili. Mwanzo
35: 6 Basi Yakobo akafika Luzu, ulio katika
nchi ya Kanaani, ndio Betheli, yeye na watu wote waliokuwa pamoja naye.
7 Akajenga huko madhabahu, akapaita mahali pale, El-Betheli; kwa sababu huko Mungu alimtokea, hapo alipomkimbia ndugu yake.
7 Akajenga huko madhabahu, akapaita mahali pale, El-Betheli; kwa sababu huko Mungu alimtokea, hapo alipomkimbia ndugu yake.
Pamoja na mengineyo nilitaka uione hiyo Madhabau, kumbuka
madhabau inawakilisha sehemu ya Ibada, yaani mahali ambapo utamwambudu Mungu
katika roho na kweli, kutolea sadaka zako na kisha kumsikia Mungu akinena nawe.
Yamkini unaniambia Mwalimu; Ni kweli ila nimejeruhiwa
sana, ni kweli ila swala hilo lisikutoa El-Betheli
maana utakosa baraka zako na pia kuhusu waliokujerui wewe muachiye BWANA maana
maandiko yanasema kuwa vita ni vya BWANA wala sio vyako, aliyekuja kuwalipa
Wamaleki baada ya mamia ya mika maana waliwadhuru wana wa Iziraeli wakati
wanatoka Misiri kisha akaja kuwalipa kipindi cha Mfalume Sauli ikiwa ni mamia
ya mika, atawalipa na hao.
Ninakwambia hili nikiwa ni shuhuda wa maswala kama haya,
labla nikupe mfano. Mwaka huu mwanzoni kuna mpendwa mmoja nilienda kumtia moyo
na aliniambia kuwa anataka kuhama kanisa, kwa sababu mahali alipo amekwazwa na
aliyemkwaza ni kiongozi ama mtu wa heshima kiutumishi hapo kanisani kwao. Mimi
nilimpa mafano wa “Meeting Pwenti,”
Nikiwa na maana ya eneo la kukutania na Mungu. Nalimwambia kuwa Mungu amepanga
kukutana na wewe hapo kanisani na kitu shetani anafanya ni kukubadilshia kituo
nami nilimuuliza hivi:
Ukikubaliana na mtu kukutana naye muda fulani katika
kituo A kisha wewe kusimama kituo B muda huo mtaonana kweli? Alijibu laa!; Nami
nikamwambia kuwa Shetani anataka usimame kituo B angali miadi yako na Mungu ni
kukutanaye kito A.
Kuwa makini na swala hili kwani Shetani ni bingwa
wakucheza na kanuni. Nina kwambia hata kama ni Mchungaji, Mama Mchungaji, ama
Shemasi au Askofu yupo kinyume nawe, haupaswi kufanya haraka kwa kuchukuwa
maamuzi ya kubadili madhabahu bila kibali cha Mungu wako maana hasara ni ya kwako
na utapitwa na Mungu wa El-Betheli.
Sisemi kuhama kanisa ni Dhambi, La! Asha! Ni vyema upatapo kibali cha Mungu.
Tuendelee na tumuone Yakobo alivyokuta na majibu yake
hapo El-Betheli, Mwanzo
35: 9 Mungu akamtokea Yakobo tena, aliporudi
kutoka Padan-aramu akambariki.
10 Mungu akamwambia, Jina lako ni Yakobo; hutaitwa tena Yakobo, lakini Israeli litakuwa jina lako. Akamwita jina lake, Israeli.
11 Mungu akamwambia, Mimi ni Mungu Mwenyezi, uzidi ukaongezeke. Taifa na kundi la mataifa watatoka kwako, na wafalme watatoka viunoni mwako.
12 Na nchi hii niliyowapa Ibrahimu na Isaka nitakupa wewe, na uzao wako baada yako nitawapa nchi hiyo.
13 Mungu akakwea juu kutoka kwake mahali hapo aliposema naye.
10 Mungu akamwambia, Jina lako ni Yakobo; hutaitwa tena Yakobo, lakini Israeli litakuwa jina lako. Akamwita jina lake, Israeli.
11 Mungu akamwambia, Mimi ni Mungu Mwenyezi, uzidi ukaongezeke. Taifa na kundi la mataifa watatoka kwako, na wafalme watatoka viunoni mwako.
12 Na nchi hii niliyowapa Ibrahimu na Isaka nitakupa wewe, na uzao wako baada yako nitawapa nchi hiyo.
13 Mungu akakwea juu kutoka kwake mahali hapo aliposema naye.
Hayo mazungumzo ya Mungu ni yakiagano, natumai unakumbuka
vyema kama ungali mwanafunzi wangu mwaminifu kuwa vitu vilivyomo kwenye hili
Agano la Ibrahimu na Mungu ni Uzao, Baraka za mataifa, Kuirithi nchi na
Kubarikiwa kwa huo uzao. Mambo hayo yote Mungu anayataja kwa Yakobo na kumbuka
yanatajwa wapi? Sio Padan-aramu wala Kwa Labani bali ni El-Betheli, mahali ambapo
Mungu alipachagua Yeye kama Mungu sio Yakobo, na mastari wa 13, uanonyesha kuwa
Mungu alishuka kabisa kwenye hiyo madhabahu yaani hakuongea akiwa mbinguni
ndiposa andiko linasema kuwa alirejea katika makazi yake.
Ni kweli jana mpendwa nilikuaidia kukuonyesha jambo la utofauti
kwa wana wa Iziraeli lililoanzia kwa Ibrahimu ila nikitazama muda wangu unaniwashia
taa yenkundi yenye ishara ya kwamba Muda umekwisha, ingalikuwa njano ama kijani
hakika ningalikumegea walau kiduchu. Ila usife moyo kwani kesho pia ni siku, na
panapo majaliwa yake Mwenyezi Mungu Mwenye Enzi nitakujuza kiunaga ubaga pasina
Shaka, ila jambo muhimu kwako ni kusika mashariti ya Agano ili uwe na Nguvu ya kiagano itokanayo na kanuni
za Agano .
Na Mwisho kama hujaokoka yaani Yesu sio Bwana na Mwokozi
wako ni fika mafundisho haya hayatakuwa na tija kwako bali ili yawe na tija
yakupasa sasa kufanya hivyo ili pia ukifa umuone Baba, yaani uende Mbinguni, na
kama ni mgonjwa atakuponywa.
Kama
hujaokoka na unataka kuokoka ama ulirudi nyuma kiroho na unataka kutengeneza na
BWANA kwa upya leo, tafadhali fwatisha nami maneno haya kwa Imani, Sema: BWANA
YESU, NINAKUPENDA, NINAKIRI NA KUAMINI MOYONI MWANGU KUWA WEWE NI MUNGU,
ULIKUFA NA KUFUFUKA KWA AJILI YANGU, INGIA NDANI YANGU KAMA BWANA NA MWOKOZI WA
MAISHA YANGU LEO, AMENI.
Hongera kwa
kuokoka na tafuta kanisa la watu waliokoka ukasali hapo.
Na Huduma ya
UKOMBOZI GOSPEL, Arusha Tanzania, Kwa Maombi, Ushauri, Maswali au Sadaka
wasiliana nasi, Barua pepe: ukombozigospel@gmail.com Simu: +255 759 859 287 pia waweza itumia kwa
M-PESA. Zaidi www.ukombozigospel.blogspot.com #UkomboziGospel #MwalimuOscarSamba
Pia #Like
#Penda Page/Ukurasa wetu au kundi la Fb, ili kupata habari hizi kwa haraka,
zaidi. @ugukombozi Gospel
PAGE: https://www.facebook.com/ugukombozigospel/
Pia kwenye mtando
Mpya wakitanzania wa
2 DAY SKY: https://www.2daysky.com/ukombozigospel
Pia TAZAMA VIDEO ZETU
HAPA https://www.youtube.com/channel/UCv1tghnugOSpbmb5h6ebJtA
(Ukombozi Gospel)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni