Mwalimu Oscar Samba |
Na
Mwandishi wetu, Ug Ministry.
Ninayo
furaha murwa kabisa nami bila iyana wala hofu ninakukaribisha katika sehemu ya
nne ya ujumbe wa semina yetu mubashara inayoendelea hapa mkoani Arusha nchini
Tanzania kwenye viwanja vya sokoni Morombo.
Jana Mwalimu
alianza kwa ufafanuzi wa somo ambalo tunaendelea nalo wiki hii yote na katika
hilo alichambua kiundani andiko la msingi ama la semina linalotutaka kuutafuta
kwanza ufalume wa Mbinguni na haki yake na kisha hayo mengine yote
tutazidishiwa. Alisema ni vyema kumtafuta Mungu kwanza kisha katika hapo ndipo
tutapata Hekima, Akili na Moyo wa Maarifa; vitu ambavyo vitatusaidia kufanikiwa
kiuchumi.
Alitanabaisha
kuwa, hakuna mtu anayetaka kuwa dakitari kwa kuanza na kozi ya udakitari ama
kushika sindano na kuvaa joho jeupe kisha kuanza kujiita ama kutaka kuitwa
dakitari.
Mwalimu
alisema inamapasa mtu huyo kuanza masomo ya shule ya msingi, Sekondari na hatimaye
kuisomea kozi hiyo Chuoni. Alikadhalika ndivyo ilivyo kwa mtu aliyeokoka ya
mpasa kuutafuta kwanza ufalume wa Mbinguni ili aweze kufanikiwa kiuchumi.
Aligusia kwa
kifupi mbinu ama kanuni zilizotangulia hapo awali ikiwemo ile ya kuweka akiba,
na kuwataka wakristo kutokula kila wanachokipata badala yake wawe na mfuo
mdhubuti wakujiwekea akiba, pia aliwataka kuwa na ujuzi ama fani maalumu kama udereva
ama ufundi ili kutumia vyema furusa za kiuchumi. Sanjari na hayo aliwataka wale
wenye vipaji kutumia vipaji vyao ili kufanikiwa maishani.
Jana Mwalimu
alizungumzia pwenti moja kuu nayo ni AGANO, Alisema Agano ni mapatano kati ya
pande kuu mbili au zaidi. Kwenye Agano kuna vitu kama vile Ishara au Alama,
kwenye Agano la Ibrahimu na Mungu Ishara ilikuwa ni Toara kwa mtoto wa kiume
atakaye zaliwa, Kwa Agano la Nuhu na Mungu ilikuwa ni Upinde wa Mvua,
alikadhalika yale mapatano ya Rahabu na wapelelezi ilikuwa ni alama ya kamba
nyekundu iliyofungwa dirishani.
Alifundisha;
Kila tu aliyeokoka ni mwana wa Ibrahimu kiimani kama ndivyo basi hili Agano
linatuhusu na alifundisha namna ya kulisimamia kimaombi.
Tulione hilo
Agano, Mwanzo 15: 18 Siku ile Bwana akafanya agano na Abramu, akasema, Uzao wako nimewapa
nchi hii, kutoka mto wa Misri mpaka huo mto mkubwa, mto Frati,
Pia Mwanzo
17: 2 Nami nitafanya
agano langu kati ya mimi na wewe, nami nitakuzidisha sana sana.
3 Abramu akaanguka kifudifudi. Mungu akamwambia, akasema,
4 Mimi, agano langu nimefanya nawe, nawe utakuwa baba wa mataifa mengi,
5 wala jina lako hutaitwa tena Abramu, lakini jina lako litakuwa Ibrahimu, kwani nimekuweka uwe baba wa mataifa mengi.
6 Nitakufanya uwe na uzao mwingi sana, nami nitakufanya kuwa mataifa, na wafalme watatoka kwako.
7 Agano langu nitalifanya imara kati ya mimi na wewe, na uzao wako baada yako, na vizazi vyao, kuwa agano la milele, kwamba nitakuwa Mungu kwako na kwa uzao wako baada yako.
8 Nami nitakupa wewe na uzao wako baada yako nchi hii unayoikaa ugeni, nchi yote ya Kanaani, kuwa milki ya milele; nami nitakuwa Mungu wao.
9 Mungu akamwambia Ibrahimu, Nawe ulishike agano langu, wewe na uzao wako kwa vizazi vyao baada yako.
Mwalimu alisema katika Agano hilo kuna vitu kadha wa kadha kama uzao kuongezeka, kumilikishwa nchi ya Kanani pia lipo jambo ambalo ni la Baraka za kiuchumi ambalo limefichwa kwenye kumiliki nchi ambayo ndani yake kuna aridhi. Na alitoa maandiko yaliyolifumbua jambo hilo ambalo pia kwenye hilo Agano linatajwa kama utajiri huku mataifa yakibarikiwa kwalo.

Mwanzo 22: 16 akasema,
Nimeapa kwa nafsi yangu asema Bwana, kwa kuwa umetenda neno hili, wala
hukunizuilia mwanao, mwanao wa pekee,
17 katika kubariki nitakubariki, na katika kuzidisha nitauzidisha uzao wako kama nyota za mbinguni, na kama mchanga ulioko pwani; na uzao wako utamiliki mlango wa adui zao;
18 na katika uzao wako mataifa yote ya dunia watajibarikia; kwa sababu umetii sauti yangu.

Tunaziona Baraka
hapo za kiuchumi , ikiwa ni matokeo ya Ibrahimu kukubali kumtoa Mwanaye kama
Sadaka. Kwa hiyo Agano hili ukilishika ndani yake ziko Baraka na wewe ni
muhusika ama ni mrithi wa Baraka hizo.
Mwalimu
alituonyesha jinsi ili Agano liliyvo wanufaisha watu na aligusia sana kwa Isaka
na Yakobo.
Tuanze na
Isaka, Kulitokea njaa katika nchi ambayo Isaka alikuwa akiishi na watu walikuwa
wakikimbilia Misiri nae Isaka akataka kufanya hivyo, ila Mungu alimzuia maana
alijua huyu ni mwana wa Agano, kwa hiyo Agano hili linaweza kukusaidia na wewe
kuishi maisha mazuri katikati ya ugumu wa maisha.
Ni Mwanzo
26: 1 Ikawa njaa
katika nchi hiyo, mbali na njaa ile ya kwanza iliyokuwa siku za Ibrahimu. Isaka
akamwendea Abimeleki, mfalme wa Wafilisti, huko Gerari.
2 Bwana akamtokea, akasema, Usishuke kwenda Misri, kaa katika nchi nitakayokuambia.
3 Kaa ugenini katika nchi hiyo, nami nitakuwa pamoja nawe, na kukubariki, maana nitakupa wewe na uzao wako nchi hizi zote. Nami nitakifanya imara kiapo nilichomwapia Ibrahimu baba yako.
4 Nitazidisha uzao wako kama nyota za mbinguni, nami nitawapa uzao wako nchi hizi zote, na katika uzao wako mataifa yote ya dunia watajibarikia.
5 Kwa sababu Ibrahimu alisikia sauti yangu, akayahifadhi maagizo yangu, na amri zangu, na hukumu zangu, na sheria zangu.
6 Isaka akakaa katika Gerari.

Tunaona
sababu kubwa iliyomfanya Isaka kudumishwa hapo ni hili Agano, kwani Mungu
analitaja hapa na anakumbuka kiapo kilichopo kwenye hilo Agano.
Tuzione hizo
Baraka za kiuchumi juu ya Isaka katikati ya mazingira Magumu, Mwanzo
2: 12 Isaka akapanda
mbegu katika nchi ile, akapata mwaka ule vipimo mia kwa kimoja, Bwana
akambariki.
13 Na mtu huyu akawa mkuu, akazidi kusitawi, hata akawa mkuu sana.
14 Akawa na mali ya kondoo, na mali ya ng'ombe, na watumwa wengi...
13 Na mtu huyu akawa mkuu, akazidi kusitawi, hata akawa mkuu sana.
14 Akawa na mali ya kondoo, na mali ya ng'ombe, na watumwa wengi...
Ndivyo
ilivyokuwa kwa Isaka na sasa tumgeukiye Yakobo.
Alikuwa
akisafirikuelekea kwa mjomba ake aitwaye Labani na alipokua njia ndipo Mungu
alimtokea na kumuaidia Baraka tele na sababu kubwa ikiwa ni hili Agano ambalo
Mungu alifnuga na babu yake.
Mwanzo 28:13 Na
tazama, Bwana amesimama juu yake, akasema, Mimi ni Bwana, Mungu wa Ibrahimu
baba yako, na Mungu wa Isaka; nchi hii uilalayo nitakupa wewe na uzao wako.
14 Na uzao wako utakuwa kama mavumbi ya nchi, nawe utaenea upande wa magharibi, na mashariki, na kaskazini, na kusini; na katika wewe, na katika uzao wako, jamaa zote za dunia watabarikiwa.
15 Na tazama, mimi nipo pamoja nawe, nitakulinda kila uendako, nami nitakuleta tena mpaka nchi hii, kwa maana sitakuacha, hata nitakapokufanyia hayo niliyokuambia.

Kama ndivyo
kwao; Na sisi kwetu ndivyo maana hao ni watoto wa Ibrahimu na sisis tulipookoka
punde tu, tulifanyika watoto wake kwa Imani kupitia Yesu Kisto aliye wa uzao
wake.
Tulidhibitishe
hili, ila ukiweza soma sura nzima ya 3 na 4 ya kitabu hiki cha Wagalatia.
Wagalatia 3: 3.29 Na
kama ninyi ni wa Kristo, basi, mmekuwa uzao wa Ibrahimu, na warithi sawasawa na
ahadi.
Kupitia
mtaji huo sasa huna budi kusoma maandiko hayo zaidi na mengineyo ikiwemo yale
ambayo Mungu aliwaambia wana wa Iziraeli kupitia Musa ya kwamba amesikia kilio
chao na amelikumbuka Agano alilofunga na baba yao Ibrahimu, Isaka na Yakobo
akiwa na maana kuwa anawakomboa kwa sababu ya hilo Agano.
Usomaji wa
maandiko hayo yatakuza imani yako na yatamfanya Mungu kufanya njia zaidi maana
hiyo ni kazi ya Imani pia. Inakupasa kuingia kwenye maombi ya kiagano na omba
kwa Jina la Mungu wa Ibrahimu, Isaka na Yakobo ukiwa na falisafa ya kiagano ndani
yako.
Omba hivi, Ee Bwana Yesu, uliniandia kunibariki, kwa
kunifanya kuwa mfanikiwa na mataifa kujitajirisha kwangu na hiki ni kiapo, na
makubaliano yaliyopo kwenye Agano hili, wewe ni Mungu ushikaye maagano, na
hausemi uongo na huwezi kutangua kiapo chako. Sasa ninakuomba unibariki, bariki
biashara hii yangu ya kuuza machungwa, spea/vipuri vya pikipiki, ya kuza magari
na hii ya kuuza maembe.
Uliyembariki Isaka katika mazingira
magumu alikadhalika Yakobo nami pia ninakuomba unionekaniye Bwana wangu.
Hongera kwa
kulifahamu jambo hili liloadimu katika ulimwengu wa leo, zaidi kitabu cha
Mwalimu kiitwacho NGUVU YA AGANO KIROHO, kikitoka hakikisha unakipata pia waweza
soma mafundisho yake ya kitabu hicho yaliyopo kwenye Facebook yake na ukurasa ule
wa huduma wa UG Ukombozi Gospel na web yetu hapo chini. Mungu akubariki ila
Mwalimu pia alikutakuokoka kama hujafanya hivyo maana ukifa leo utaenda Jehanamu
ya Moto na hakika hutaweza pia kunuifaika na Baraka hizi ama na mbinu au kanuni
hii ya AGANO maana jambo hili ni kwa ajili ya hao walio wana wa Ibrahimu
kiimani na wewe yakupasa kuokoa ili uwe hivyo.
Kama
hujaokoka na unataka kuokoka ama ulirudi nyuma kiroho na unataka kutengeneza na
BWANA kwa upya leo, tafadhali fwatisha nami maneno haya kwa Imani, Sema: BWANA
YESU, NINAKUPENDA, NINAKIRI NA KUAMINI MOYONI MWANGU KUWA WEWE NI MUNGU,
ULIKUFA NA KUFUFUKA KWA AJILI YANGU, INGIA NDANI YANGU KAMA BWANA NA MWOKOZI WA
MAISHA YANGU LEO, AMENI.
Hongera kwa
kuokoka na tafuta kanisa la watu waliokoka ukasali hapo.
Na Huduma ya
UKOMBOZI GOSPLE, Arusha Tanzania, Kwa Maombi, Ushauri, Maswali au Sadaka
wasiliana nasi, Barua pepe: ukombozigosple@gmail.com Simu: +255 759 859 287 pia waweza itumia kwa
M-PESA. Zaidi www.ukombozigospel.blogspot.com #UkomboziGosple #MwalimuOscarSamba
Pia #Like
#Penda Page/Ukurasa wetu au kundi la Fb, ili kupata
habari hizi kwa haraka, zaidi. Ug Ukombozi Gosple,
PAGE: https://www.facebook.com/ugukombozigospel/
Pia kwenye mtando
Mpya wakitanzania wa
2 DAY SKY:
https://www.2daysky.com/home
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni