Jumatatu, 12 Juni 2017

NGUVU YA AGANO. Sehemu ya 3.

Na Mwalimu Oscar Samba wa Ug Ministry
Ninakukaribisha katika sehemu ya 3 ya makala hii inayolenga kukujuza Nguvu iliyopo kwenye maagano ili usomapo maandiko uyasome kiagano ukijua kuwa ni sehemu ya maagano mbali mbali ambayo ni msaada mkubwa kwako kama utajua kuyatumia vyema kwa kunjenga hoja mbele za Mungu na kuzisimamia kimaombi vilivyo.
Jana nilikuaidi kuendelea na kipengele cha Isaka ikiwa ni muendelezo wa Agano ambalo Ibrahimu alifunga na Mungu, na ili kujua tulipoanzi yakupasa kusoma sehemu zilizotangulia yaani ya jana na juzi. Nilimalizia kwa kukufahamisha kuwa kwa Isaka Agano hili lilikuwa na Nguvu kubwa sana kwani wakati wengine wakioa kwa taabu kwake mambo yalikuwa ni MSWANO: Na hivi sasa ninakupa Nguvu ya hili Agano kwake kwa ulingo mpana zaidi.
(e) Lili Mpa Kuridhi Mali ya Babaye,Na kufanyika Lango la Uridhi kiahadi; Ni Agano pekee ndilo lililomuwezesha kuipata au kuupata Uridhi wa mali ya baba yake. Kwani maandiko yanamtaja kama mtu pekee aliyekabidhiwa mali ile huku wengine waliokuwa wana wa Masuria wakipewa zawadi tu.

Ni Mwano 25: 5 Ibrahimu akampa Isaka yote aliyokuwa nayo.
6 Lakini wana wa masuria aliokuwa nao Ibrahimu, Ibrahimu a

kawapa zawadi,
naye akawaondoa katika mahali alipokaa Isaka mwanawe, wakati wa uhai wake, waende pande za mashariki, mpaka nchi ya Kedemu.
Jambo hili lilijidhirisha mapema kabisa kipini cha Hajiri;  yule kijakazi na mwanaye Ishumaeli: Ila Sara Alikuwa makini sana na kulidhibiti.
Ni Mwanzo 21: 10 Kwa hiyo akamwambia Ibrahimu, Mfukuze mjakazi huyu na mwanawe, maana mwana wa mjakazi hatarithi pamoja na mwanangu, Isaka.
11 Na neno hilo lilikuwa baya sana machoni pa Ibrahimu, kwa ajili ya mwanawe.
Mungu naye hakukawiya kwani alilidhibitisha mapema, Mstari wa kumi na mbili,  12 Mungu akamwambia Ibrahimu, Neno hili lisiwe baya machoni pako, kwa ajili ya huyo mwana, na huyo mjakazi wako. Kila akuambialo Sara, sikiza sauti yake, kwa maana katika Isaka uzao wako utaitwa.

Jambo hili Paulo analidhiirisha kwenye Agano Jipya, Soma Wagalatia 3:6-29, Na 4:21-31.
Kumbuka pia Uridhi unaotajwa hapa sio wa Mali ama Fedha au Utairi tu, bali ni Ule pia wa Kristo kupitia Isaka maana maandiko hayo ya Wagalatia yanachambua jambo hili bayana,
Tuangaziye Sura ile ya 4: 28 Basi, ndugu zangu, kama Isaka sisi tu watoto wa ahadi.
29 Lakini kama vile siku zile yule aliyezaliwa kwa mwili alivyomwudhi yule aliyezaliwa kwa Roho, ndivyo ilivyo na sasa.
30 Lakini lasemaje andiko? Mfukuze mjakazi na mwanawe, kwa maana mwana wa mjakazi hatarithi kabisa pamoja na mwana wa mwungwana.
31 Ndiposa, ndugu zangu, sisi si watoto wa mjakazi, bali tu watoto wa huyo aliye mwungwana.

Nia yangu kuu ilikuwa ni kukuonyesha ya kwamba Uridhi wa Isaka haukuwa wa kawaida bali ulitokana na Agano, yaani ulipata Nguvu kutoka kwenye Agano.
(f) Lilimtunza, au Kumuwezesha kuishi mahali ama katika Mazingira ambayo kikawaida jambo hilo lisingewezekana. Kuna wakati kulitokea njaa katika nchi ambayo Isaka alikuwa akiishi, na watu walikuwa wakikimbilia Misiri ili kujipatia chakula, Na Isaka alihitaji kufanya hivyo.

Ila Mungu alilitazama Agano lake na kumkataza kwenda ama kuishi katika mfumo wa kawaida ambao watu wengine wanauishi, badala yake alimbarikia katika hiyo Nchi kama ilivyokuwa katika mapatano ya lile Agano.

Mwanzo 26: 1 Ikawa njaa katika nchi hiyo, mbali na njaa ile ya kwanza iliyokuwa siku za Ibrahimu. Isaka akamwendea Abimeleki, mfalme wa Wafilisti, huko Gerari.
2 Bwana akamtokea, akasema, Usishuke kwenda Misri, kaa katika nchi nitakayokuambia.
3 Kaa ugenini katika nchi hiyo, nami nitakuwa pamoja nawe, na kukubariki, maana nitakupa wewe na uzao wako nchi hizi zote. Nami nitakifanya imara kiapo nilichomwapia Ibrahimu baba yako.

Tunamuona Mungu hapo anakumbuka kiapo, na nilikujuza pale awali kuwa miongoni mwa vitu vinavyopatikana katika Agano ni kiapo cha Uaminifu. Na ili kukudhibitishia kuwa kiapo hicho alicho mwapia Ibrahimu ni kile cha kiagano, yatupasa kuendelea na mistari inayofwata.

Nataka tu, kukujuza ya kwamba ukiwa ni mtu wa Agano na Mungu huwezi kuangamia bila kujalisha mazingira hayo yanawaangamiza wengine kwa kiwango gani. Hata ukipitiya magumu ama mazito kiasi gani, watashangaa ukiibuka na Ushindi angali jaribu kama hilo liliwai kuwaangamiza au kuwapoteza wengi.

Tuhakiki jambo hili; 4 Nitazidisha uzao wako kama nyota za mbinguni, nami nitawapa uzao wako nchi hizi zote, na katika uzao wako mataifa yote ya dunia watajibarikia.
5 Kwa sababu Ibrahimu alisikia sauti yangu, akayahifadhi maagizo yangu, na amri zangu, na hukumu zangu, na sheria zangu.
6 Isaka akakaa katika Gerari.


Kumbuka hiyo nchi ni ile ambayo baba yake na mamaye walienda ndipo Mungu akampiga kwa kuwafunga matumbo na kutishia kuwaangamiza, kwa Mfalume kumchukuwa mamaye. Na nilikujuza kuwa ilikuwa ni Ulinzi wa kiagano.

Tuone jinsi Mungu alivyotimiza ahadi hiyo ya kumbariki Isaka mahali palipokuwa na njaa; 12 Isaka akapanda mbegu katika nchi ile, akapata mwaka ule vipimo mia kwa kimoja, Bwana akambariki.
13 Na mtu huyu akawa mkuu, akazidi kusitawi, hata akawa mkuu sana.
14 Akawa na mali ya kondoo, na mali ya ng'ombe, na watumwa wengi.....
Hiyo ni Nguvu ya Agano Mpendwa, fahamu ya kuwa na wewe ni sehemu ya hili Agano kama yasemavyo maandiko kwenye kitabu cha Wagalatia ya kwamba tulio muamini Yesu kwa Imani tunafanyika kuwa wana wa Ibrahimu na pia kuzirithi hizi ahadi kwa njia ya Yesu kwani kwa njia ya Isaka zimeamriwa kutufikia sisi na mataifa yote tutabarikiwa.

Nakutaka kulifahamu hili ili usije kukubali kuyaishi maisha magumu angali wewe ni mwana wa Ibrahimu kwani ulipookoka tu, punde si Punde ulifanyika mwana na kuwa mwana kuna kupa kuzirithi. Tafadhali ungana nami Kesho ili kuendelea na ujumbe huu murwa. Ila kama huja Okoka fahamu ya kwamba hutaweza kuwa mrithi kwa njia hii na ni wangu wito kufanya hivyo, ama kama ulirudi nyuma kiroho tambua ya kwamba umejiengua kwenye hili Agano nami ninakutaka kurejea kwalo.

Kama hujaokoka na unataka kuokoka ama ulirudi nyuma kiroho na unataka kutengeneza na BWANA kwa upya leo, tafadhali fwatisha nami maneno haya kwa Imani, Sema: BWANA YESU, NINAKUPENDA, NINAKIRI NA KUAMINI MOYONI MWANGU KUWA WEWE NI MUNGU, ULIKUFA NA KUFUFUKA KWA AJILI YANGU, INGIA NDANI YANGU KAMA BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YANGU LEO, AMENI.
Hongera kwa kuokoka na tafuta kanisa la watu waliokoka ukasali hapo.

Na Huduma ya UKOMBOZI GOSPLE, Arusha Tanzania, Kwa Maombi, Ushauri, Maswali au Sadaka wasiliana nasi, Barua pepe: ukombozigosple@gmail.com  Simu: +255 759 859 287 pia waweza itumia kwa M-PESA. Zaidi www.ukombozigospel.blogspot.com   #UkomboziGosple  #MwalimuOscarSamba
Pia #Like #Penda Page/Ukurasa wetu au kundi la Fb, ili kupata habari hizi kwa haraka, zaidi. Ug Ukombozi Gosple,                                                                                       PAGE: https://www.facebook.com/Ug-Ukombozi-Gosple                                              
Kikundi: https://www.facebook.com/groups/2268418230050621/
Pia kwenye mtando Mpya wakitanzania wa
2 DAY SKY: https://www.2daysky.com/home








Hakuna maoni:

Chapisha Maoni