Alhamisi, 22 Juni 2017

NGUVU YA AGANO SEHEMU YA 5.

Na Mwalimu Oscar Samba wa Ug Ministry.
Ninakusalimu katika jina la Bwana wetu Yesu Kristo ndugu msomaji wa makala hii ikiwa ni sehemu ya tano, na jana nilikuaidi kuendelea na kipengele kinachoonyesha jinsi Yakobo alivyobarikiwa katika Agano hili.
(h) Kubarikiwa kimali na kurudishwa katika nchi ya Nyumbani, Kumbuka kuwa Yakobo alikuwa akiishi katika nchi isiyo yake ama ya baba zake naye alikuwa kwa Labani ama kwa mjomba ake, ila majira haya Mungu anatumia Agano hili kumtoa huko pamoja na kumpa mali.
Tutayatazama hayo maandiko lakini nataka uyaone kwa sura ya kiagano. Yaana anza kwa Yakobo kuanza mipango ya kuondoka mara baada ya Mungu kumpa kibali na hapo anaongea na wake zake, katika hayo mazungumzo kunatajwa kitu kama mimi ni Mungu wa Betheli, katika mstari wa 13.( 13 Mimi ni Mungu wa Betheli, huko ulikotia mafuta nguzo, na kuniwekea nadhiri. Sasa ondoka, toka katika nchi hii, urudi mpaka nchi ile uliyozaliwa.) 
Maana yake hapo ni Mungu analienzi Agao lake, ambapo lilifanywa Imara kwa Yakobo pale Betheli, kumbuka katika sehemu yetu ya 4, uliona kuwa sehemu hiyo ilikuwa ikiitwa Luzu, na Mungu alimtokea Yakobo na kujitambulisha kama Mungu wa Isaka na Ibrahimu, na alilitaja Agano lake hapo, kisha kumuaidia kumzidisha, kumrejesha salama na kumtajirisha pia. Na hayo yote yanapatika kwenye hili Agano la Ibrahimu; Kwa walioanza sehemu ya kwanza ya makala hii wanakumbuka ama kufahamu hivyo. Tuyadodose hayo maandiko sasa.
Mwanzo 31: 6 Nanyi mmejua ya kwamba kwa nguvu zangu zote nimemtumikia baba yenu.
7 Na baba yenu amenidanganya, akabadili mshahara wangu mara kumi; lakini Mungu hakumwacha kunidhuru.
8 Aliposema, Walio na madoadoa watakuwa mshahara wako, wanyama wote wakazaa madoadoa. Aliposema, Walio na milia watakuwa mshahara wako, ndipo wanyama wote wakazaa wenye milia.
9 Hivi Mungu akamnyang'anya mali yake baba yenu, na kunipa mimi.
10 Ikawa, wakati wale wanyama walipochukua mimba, naliinua macho yangu nikaona katika ndoto, na tazama, mabeberu waliowapanda hao wanyama walikuwa na milia, na madoadoa, na marakaraka.
11 Na malaika wa Mungu akaniambia katika ndoto, Yakobo! Nikasema, Mimi hapa.
12 Akasema, Inua, basi, macho yako, ukaone; mabeberu wote wanaopanda wanyama wana milia, na madoadoa, na marakaraka; maana nimeona yote aliyokutendea Labani.
13 Mimi ni Mungu wa Betheli, huko ulikotia mafuta nguzo, na kuniwekea nadhiri. Sasa ondoka, toka katika nchi hii, urudi mpaka nchi ile uliyozaliwa.


Kwa mantiki hiyo ni kwamba bila hili Agano kulikuwa na uwezekano mkubwa sana kwa Yakobo kutoka bila mali (kapa) katika arihi ya mzee Labani.
Tutazame jambo jingine ambalo jana nilikuaidia kukujuza nalo ni lile la Penueli, katika safari yake Yakobo kuna mahali alifika akapumzika na hapo alipopumzika Mungu alijitokeza kwake. Ndiposa Yakobo kwakujijua kuwa yeye ni mwana wa hili Agano hakuwa na haja ya kupoteza Muda bali alimng’ang’ania Malaika wa Bwana hadi ambariki. Na alikuwa na uwalali maana tayari Mungu wa Betheli yupo pamoja naye.
Fungua
Mwanzo 32: 24 Yakobo akakaa peke yake; na mtu mmoja akashindana naye mweleka hata alfajiri.
25 Naye alipoona ya kuwa hamshindi, alimgusa panapo uvungu wa paja lake; ukateguka uvungu wa paja la Yakobo alipokuwa akishindana naye.
26 Akasema, Niache, niende, maana kunapambazuka. Akasema, Sikuachi, usiponibariki.
27 Akamwuliza, Jina lako n'nani? Akasema, Yakobo.
28 Akamwambia, Jina lako hutaitwa tena Yakobo, ila Israeli, maana umeshindana na Mungu, na watu, nawe umeshinda.
29 Yakobo akamwuliza, akasema, Niambie, tafadhali, jina lako? Akasema, Kwa nini waniuliza jina langu? Akambariki huko.
30 Yakobo akapaita mahali pale, Penueli, maana alisema, Nimeonana na Mungu uso kwa uso, na nafsi yangu imeokoka.
Hapo tunaona kitu cha ajabu sana, kwamba Yakobo alibadilishiwa hadi jina, kumbuka jina hili liliwakilisha mataifa kumi na mawili, yaliyokuwa au yaliyoanzia kwa wana wake 12, na wana hao ndio kabila 12 za Iziraeli.
Nataka ufahamu kitu hapo, natumai unakumbuka kuwa katika hili Agano la Ibrahimu miongoni mwa vitu vinavyotajwa hapo ni Uzao, na hapa tunaona utumizwaji wa ahadi hiyo kwa mara ya kwanza kwa nyanja yenye mapana zaidi kutoka kwa Isaka aliyekuwa mmoja kisha Yakobo na sasa ni Kumi na wawili yaani Iziraeli.
Kingine hapo ni Malaika kumbariki, pale Mwanzo 22, baada ya Ibrahimu kumtoa Isaka kama Sadaka kwenye ulimwengu wa roho, tuliona Mungu akimtamkia dhairi baraka, Betheli tumeliona hilo na hata pale Mwanzo 15, na 17 pia. Hapa jambo hilo linatimia kwa Yakobo ama Iziraeli.
Kwa kweli ni yangu kiu kuendelea nawe ila kihakika muda wangu sio rafiki, na ninakutaka kuungana nami kesho majira kama haya nitakapokuwa nikiendelea na sehemu ya 6, na kesho Mungu akinijalia nitakujuza jambo la utofauti kwa wana wa Iziraeli linaloanzia kwa mzee Yakobo likiwa ni chimbuko kwa Ibrahimu pale Mwanzo 15.
Ninafahamu fika kuwa ujumbe huu umekuwa mzuri kwako ila kama hujaokoka ni ukweli kwamba baraka hizi haziwezi kuwa halisi kwako, kwa hiyo yakupasa kuhakikisha ya kwamba unafanya hivyo ili kuwa sehemu ya hili Agano.
Na Huduma ya UKOMBOZI GOSPEL, Arusha Tanzania, Kwa Maombi, Ushauri, Maswali au Sadaka wasiliana nasi, Barua pepe: ukombozigospel@gmail.com Simu: +255 759 859 287 pia waweza itumia kwa M-PESA. Zaidi www.ukombozigospel.blogspot.com #UkomboziGospel#MwalimuOscarSamba
Pia #Like #Penda Page/Ukurasa wetu au kundi la Fb, ili kupata habari hizi kwa haraka, zaidi. @ugukombozi Gospel
PAGE: https://www.facebook.com/ugukombozigospel/
Kikundi: https://www.facebook.com/groups/2268418230050621/
Pia kwenye mtando Mpya wakitanzania wa
2 DAY SKY: https://www.2daysky.com/ukombozigospel
Pia TAZAMA VIDEO ZETU HAPAhttps://www.youtube.com/channel/UCv1tghnugOSpbmb5h6ebJtA(Ukombozi Gospel)

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni