Na Mwalimu Oscar Samba wa Ug Ministry. |
Kwa kifupi
ujumbe huu hulenga kukupa mathara ya kula vyakula visivyosalama kiroho, kwani
wapo wakristo ama watu waliookoka ambao hubugia ama hula kila kitu kilichopo
mbele yao ama huwa na mazoea ya kula vyakula ambayo ni matokeo ya ibada fulani
ama huambatana na ibada ya dini fulani. Na hufaya hivyo bila kujua athari zake.
Leo Bwana amenituma kukupa mathara hayo.
Kwa dini za
wenzetu vyakula ni ibada, kabla ya kupika na wakati wakupika huvunenea na pia
muda wa kula. Hata kwetu ndivyo ilivyo, ndiposa Yesu alikuwa akifanya hivyo
mara kwa mara, kumbuka ile mikate na samaki alishukuru na kuiombea.
Pia katika Luka
22 kabla ya kuumega ule mkate na kunywa maji ya mzabibu alishukuru na kisha
kuwagaiwa wanafunzi wake. (Luka 22.19
Akatwaa mkate, akashukuru, akaumega, akawapa, akisema, [Huu ndio mwili wangu
unaotolewa kwa ajili yenu; fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu.)
Na kwa wale
wanaofanya matambiko pia hufanya hivyo hivyo, kwani hata uchinjaji wao ni kwa
mujibu wa taratibu za mila zao yaani kipepo. Mfano wachaga, humnyonga hadi kufa
kwanza huyo mfugo ndiposa wamchinje, wengine humtemea mate na wapo wanaompa
chakula cha aina fulani. Hata ipo dini ambayo huchinja kwa sheria zao na kuna aina
fulani ya maneno hutamka.
Sasa
unapokula vyakula vyao unajiingiza katika uharibifu wa nafsi yako ama hali yako
ya kiroho kwenye ulimwengu wa roho na kuna hatari pia yakuingia kweye maagano
ya kipepo, na kesho nitakuwekea somo kuhusu jambo hili la maagano ya kipepo
kupitia chakula.
Kuna mtu
mmoja aliniambia ya kwamba aliwai kula chakula cha dini fulani kilichokuwa ni
chaibada ama sherehe au sikuku fulani na baada ya hapo hali yake ya kiroho
ilibadilika. Kwa bahati nzuri alikuwa ni Mchungaji na alifanya hivyo kwa sababu
alidai alikuwa safarini na mazingira yalikuwa magumu kwake. Na kupitia kofia
hiyo ya Utumishi alitumia muda na mbinu za kiroho ili kuondoa na mathara hayo
na hatimaye kufanikiwa.
Wapo watu
wanaojikuta wakiwa na hali ya mapooza kiroho, yaani hawawezi kuomba, kuimba,
ama kusoma Neno kama hapo awali huku sababu ikiwa ni hii hali ya kubugia bugia.
Mtu mmoja akaniambia; “lakini uji wao ni mtamu”. Ila kila
akila anajikuta nakosa amani gafula na huzuni huingia ndani yake.
Mimi
nilimjuza kuwa kukosa huko amani ni ishara ya kuingia kwa roho ya kigeni ndani
yake na roho hiyo inamfanya Roho Mtakatifu kuugua kwani humuhatarishia nafasi
yake kwako.
Tudhibitishe
athari hizi kimaandiko. Ninakupa nukuu ya makala yangu itakayokujia kesho,
yenye dhima ya kukujuza ama kuwakomboa watu wanaoota ndoto za kula vyakula,
tuoe kipengele hiki cha Mithali hapo:
“Mithali 23: 6 Usile mkate
wa mtu mwenye husuda; Wala usivitamani vyakula vyake vya anasa; 7 Maana aonavyo nafsini mwake, ndivyo alivyo. Akuambia,
Haya, kula, kunywa; Lakini moyo wake hauwi pamoja nawe.
AwazavyoNafsini mwake, kwa hiyo
muda unakula au kabla yeye huwana na mawazo mabay ama ya hila dhidi yako na
hukudhuru. Nimetumia neno kukuwazia maana bibilia ya kingereza haijatumia
aonavyo bali imetumia neno afikirivyo ama awazavyo;
(7 For as he thinketh
in his heart, so is he: Eat and drink, saith he to thee; but his heart is not
with thee. ) Hiyo ni ya King James Version,
Tuone ya Basic English; (Proverbs 23:7 For as the thoughts of his heart
are, so is he: Take food and drink, he says to you;but his heart is not with
you.)
{Ni
kama yalivyo mawazo ya moyo wake}
Mathara hayo tunayaona kwenye msatari wa 8 ambapo
hudhiirika mwilini pia; (8 Tonge lile
ulilokula utalitapika, Na maneno yako matamu yatakupotea. )
Mstari wa 6, anataja chakula cha
mtu huyu mwenye husuda, kisha msitari wa 7, Tunayaona mahusiano hayo, kwani mtu
huyu anakupa chakula kwenye mstari wa 6, ila wa saba, anakinenea ama anakiwazia
nafsini mwake na jambo hilo huwa na mathara kwako.
Ninachotaka ukione hapa ni kwamba, mtu huweza kukupa
chakula na moyoni ama nafsini mwake akakuwazia vibaya ama anakunenea vibaya na
chakula hicho kukudhuru ndiposa mstari wa 8 ukasema utakitapika, na
hautaishilia tu hapo bali na maneno matamu yatakutoka.”
Kwa mantiki
hiyo ni kwamba, punde ulapo chakula cha kidini ama kisicho salama kiroho yale
maneno yaliyonenwa ama ile roho iliyobebwa na hicho chakula huambatana nawe.
Kuwa makini
sana na swala hili. Pia kama upo mazingira hatarishi kima hayo na huna uwakika
na kile unachokula hata kama ni hotelini, maana zipo hoteli ambazo hupika
kishirikina kiasi ambacho hukifanya chakula hicho kuwa hatari kiroho yakupasa
kukiombea na kuvunja roho zilizopo ndani ya hicho chakula. Ila njia hii isikuhalalishie
kula chakula ovyo ama kula vile vya ibada ya sanamu, kumbuka hata Paulo ameonya
jambo hilo. Pia epuka vyakula vyote vinavyoambatana na sherehe za dini isiyo salama
kiroho, pamoja na vile vya sherehe za kipepo.
Mfano wapo
watu wanopewa mashariti na waganga hususani wanaofanya biashara za kipepo,
mashariti hayo huwa ni kuandaa sherehe ili kuwalisha watu. KWEPA HAYO ILI UWE SALAMA.
Ilikuwa
nikuage hapa ila ninaguswa kuwapa njia za kuwakomboa wale ambao wameadhirika na
jambo hilo.
NJIA ZA KUWAKOMBOA WALIOATHIRIKA NA
VYAKULA HIVI.
1. Omba rehema yaani fanya maombi ya toba kwa Mungu kwa
kula vyakula hivyo
2. Fanya maombi ya kuondoa hayo mathara, omba huku
ukifanya ishara ya kuyaondoa kwa jina na Damu ya Yesu kivitendo.
3. Rejesha kila kilichoibiwa ama kilichodhurika kutoka
na athari hizo, waweza tumia hili andiko. Yoeli 2: 25 Nami nitawarudishia hiyo miaka iliyoliwa na nzige, na parare, na
madumadu, na tunutu, jeshi langu kubwa nililotuma kati yenu.
4. Mfukuze Shetani kwa maombi ya vita na ikiwezekana
njia hii itumiye kabla ya ile ya nne kadri Roho atakavyokupa kibali.
Ninakutakia
kila la heri katika kuyaishi masomo haya, usikubali kupitwa na ujumbe wa kesho.
Kama
hujaokoka na unataka kuokoka ama ulirudi nyuma kiroho na unataka kutengeneza na
BWANA kwa upya leo, tafadhali fwatisha nami maneno haya kwa Imani, Sema: BWANA
YESU, NINAKUPENDA, NINAKIRI NA KUAMINI MOYONI MWANGU KUWA WEWE NI MUNGU,
ULIKUFA NA KUFUFUKA KWA AJILI YANGU, INGIA NDANI YANGU KAMA BWANA NA MWOKOZI WA
MAISHA YANGU LEO, AMENI.
Hongera kwa
kuokoka na tafuta kanisa la watu waliokoka ukasali hapo.
Na Huduma ya
UKOMBOZI GOSPLE, Arusha Tanzania, Kwa Maombi, Ushauri, Maswali au Sadaka wasiliana
nasi, Barua pepe: ukombozigosple@gmail.com
Simu: +255 759 859 287 pia waweza itumia kwa M-PESA. Zaidi www.ukombozigospel.blogspot.com #UkomboziGosple #MwalimuOscarSamba
Pia #Like
#Penda Page/Ukurasa wetu au kundi la Fb, ili kupata
habari hizi kwa haraka, zaidi. Ug Ukombozi Gosple,
PAGE: https://www.facebook.com/Ug-Ukombozi-Gosple
Pia kwenye
mtando Mpya wakitanzania wa
2 DAY SKY:
https://www.2daysky.com/home
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni