Na
Mwandishi wetu, Ug Ministry.
Hakika kwetu
Jehova Jire ni Ebeneza maana sio kwa uweza wetu bali ni kwa nguvu zake ndiposa
tunayanena hayo. Jana tulifanikiwa kuhitimisha semina yetu huku nguvu za Mungu
zikishuka mahali pale, watu wakifunguliwa na hakika semina ilikuwa ya Baraka
maana licha ya watu kunufaika na mafundisho pia wapo waliookoka.
Kama ilivyo
ada Mwalimu jana alianza kwa kuwaimiza wakristo kumtafuta Mungu kwanza na haki
yake kisha hayo mengine yote wanayoyahitaji kutoka kwake Yeye atawajaza.
Siku ya jana
Mwalimu alihitimisha kwa Mbinu ya 9, nayo ni ; Kufahamu athari za kuwa na Mali
isiyo na Yesu. Katika hili alisisitiza mathara yanayoweza kujitokeza kwa mtu
mwenye mali kisha akamkosa Yesu kwenye Uchumi wake.
Alinza na andiko lile la Ufunuo
wa Yohana
3: 17 Kwa kuwa wasema, Mimi ni tajiri, nimejitajirisha, wala sina haja ya kitu;
nawe hujui ya kuwa wewe u mnyonge, na mwenye mashaka, na maskini, na kipofu, na
uchi.
18 Nakupa shauri, ununue kwangu dhahabu
iliyosafishwa kwa moto, upate kuwa tajiri, na mavazi meupe upate kuvaa, aibu ya
uchi wako isionekane, na dawa ya macho ya kujipaka macho yako, upate kuona.
19 Wote niwapendao mimi
nawakemea, na kuwarudi; basi uwe na bidii, ukatubu.
Maandiko
hayo yanamzungumzia mtu mwenye kiburi cha fedha, na yanamtaka aje kwa Mungu maana
yu Uchu avikwe vazi jeupe ambalo ni wokovu, na anajiona ni tajiri ila Bibilia
inamuona kuwa ni mnyonge, masikini na kipofu, mwisho anatakiwa kutubu maana
maandiko yanasema anampenda ndio maana anamuonya au kumkemea. Andiko hili liwe
lako wewe mwenye hali hiyo, uliyepandisha mabega kwa sababu ya mali yako.
Tutazame
kitabu cha Yeremia 17: 11 Kama
kware akusanyaye makinda asiyoyazaa, ndivyo alivyo mtu ajipatiaye mali, wala si
kwa haki, katikati ya siku zake zitaachana naye, na mwisho wake atakuwa
mpumbavu.
Hapa Yesu
anawazungumzia wale wanaojipatia mali kwa njia ya udhalimu, wanataka rushwa,
utapeli ama njia zilizo za hila, na anawaita ni wapumbavu kisha hufanana na
kware ambaye ni ndege anayekusaya watoto asiyowazaa, maana yake mtu kama huyu
anafanya kazi bure kwani watoto wasio wako hawawezi kukuita baba ama mama, labla
udogoni ila wakikua watagundua wewe sio mzazi wao, alikadhalika hiyo mali
haitakuwa ya kwako.
Tugeukiye
kitabu kile cha Mithali 15: 16 Kuwa na
mali chache pamoja na kumcha Bwana; Ni bora kuliko mali nyingi pamoja na taabu.
Andiko hilo
linatutaka tumche Bwana katika chumi zetu hata kama uchaji huo utatupelekea
kuwa na mali chache kwani ni heri zaidi, kuliko kuwa na mali nyingi kisha
ukakosa kwenda kanisani, ukashindwa kuudhuria maombi na mbaya zaidi hali yako
ya kiroho ikafa, mwishowe ukaenda jehanamu ya moto.
Tuone tena
jambo hilo katika Mithali 16: 8 Afadhali
mali kidogo pamoja na haki, Kuliko mapato mengi pamoja na udhalimu.
Ni afadhali
kutenda haki ile ya kibibilia katika kuitafuta mali kuliko njia haramu kama za
hongo ili kuipata mali nyingi.
Ona tena
hapa; Zaburi 37: 16 Kidogo alicho nacho mwenye haki ni bora Kuliko wingi wa mali wa wasio haki
wengi.
Dhima ya andiko
hili ni kukutaka kutokuwa na tamaa katika kuitafuta mali, pia sio kusudio lake
kukutaka kuwa masikini au mwenye mali chache bali yakupasa kuitafuta mali au
kuwa na bidii katika Kriso Yesu na sio tamaa ya mali ama mali bila Yesu.
Turejee tena
kwenye Mithali, Mithali 30: 8 Uniondolee ubatili na uongo; Usinipe umaskini wala utajiri; Unilishe
chakula kilicho kadiri yangu.
9 Nisije nikashiba nikakukana, Nikasema, Bwana ni nani? Wala nisiwe maskini sana nikaiba, Na kulitaja bure jina la Mungu wangu.
9 Nisije nikashiba nikakukana, Nikasema, Bwana ni nani? Wala nisiwe maskini sana nikaiba, Na kulitaja bure jina la Mungu wangu.
Maandiko
haya ni ya ajabu sana kwani yana upekee wake, muombaji anaukataa umasikini,
kwani athari zake ni mbaya mno, maana huweza kumpelekea kuiba, pia anaukataa
utajiri usio na Yesu ndani yake kwani huweza kumpelekea kumkana ama kumkufuru
Mungu ama kutokumcha Yeye maana huweza kujikuta anaota kiburi ambacho
kitamfanya hadi kusema kwa kejeli kuwa Mungu ni nani?
Ndiposa na Mwalimu
akakutaka kuwa na kiu ya kuwa tajiri ila hakikisha katika mali zako unakuwa na
Yesu, kumbuka Mwalimu siku za nyuma aliwai kutoa mfano wa kijana yule tajiri
jinsi mali yake ilivyomzuia kumtumikia Mungu.
Na jana alisema
kuwa ukimuona Mpendwa ambaye yupo tayari kutoa laki moja kwenye harusi ila
mchago wa ujenzi wa kanisa anatoa elufu tano jua mali yake inampeleka au imeshamfikisha
pa baya, na hiyo ni dalili ya mali isiyo na Yesu kikamilifu, au kabisa.
Nikutakiye
siku njema na majira mazuri na hari kuukatika kumfwatilia Mwalimu wetu kwenye
masomo mengine na huenda kesho tukaendelea na sehemu ya 4, ya ile makala yetu ya
NGUVU YA AGANO, Ikiwa ni sehemu ya kitabu chetu cha TAJIRIKA KIBIBILIA. Pia
usiache kutazama video ya mafundisho yote ikiwemo ya somo ili kwenye Channel
yetu ya Youtubu hiyo hapo chini. Hapo pia utanufaika na maombezi maalumu ya
Uchumi ya jana na siku nyinginezo.
Kama
hujaokoka na unataka kuokoka ama ulirudi nyuma kiroho na unataka kutengeneza na
BWANA kwa upya leo, tafadhali fwatisha nami maneno haya kwa Imani, Sema: BWANA
YESU, NINAKUPENDA, NINAKIRI NA KUAMINI MOYONI MWANGU KUWA WEWE NI MUNGU,
ULIKUFA NA KUFUFUKA KWA AJILI YANGU, INGIA NDANI YANGU KAMA BWANA NA MWOKOZI WA
MAISHA YANGU LEO, AMENI.
Hongera kwa
kuokoka na tafuta kanisa la watu waliokoka ukasali hapo.
Na Huduma ya
UKOMBOZI GOSPLE, Arusha Tanzania, Kwa Maombi, Ushauri, Maswali au Sadaka
wasiliana nasi, Barua pepe: ukombozigosple@gmail.com
Simu: +255 759 859 287 pia waweza itumia kwa M-PESA. Zaidi www.ukombozigospel.blogspot.com #UkomboziGosple #MwalimuOscarSamba
Pia #Like
#Penda Page/Ukurasa wetu au kundi la Fb, ili kupata
habari hizi kwa haraka, zaidi. Ug Ukombozi Gosple,
PAGE: https://www.facebook.com/ugukombozigospel/
Pia kwenye mtando
Mpya wakitanzania wa
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni