Jumanne, 30 Mei 2017

PAKUWA, DOWNLOAD BIBILIA TAKATIFU YA KISWAHILI, SWAHILI HOLY BIBLE

BONYEZA HAPA

Tumebadlisha anuani yetu ya blogu sio www.ukombozigosple.blogspot.com bali ni www.ukombozigospel.blogspot.com

NAMNA YA KUJINASUA KWENYE VIFUNGO VYA PEPO MAHABA. Sehemu ya 1.

 Na Mwalimu Oscar Samba #Ug Ministry 
 #SHARE  #SAMBAZA Ili kueneza injili hii Zaidi.
Kuna watu wanasumbuliwa kwa kuota ndoto wakiwa na Wanazini na mapepo Mahaba aidha kwa muonekano wa watu wanaowajua ama wasio wajua. Pia wapo wanaofanya ukahaba, Uzizi na hata vitendo vya kinyume na maumbile huku wakiwa hawapendezwi na hali hiyo na wamejaribu kutafuta msaada bila mafanikio.

Baya zaidi wapo wanandoa wenye kusumbuliwa na hali kama hiyo na tatizo hili linaiweka ndoa yao njia panda kwani hufanya ama huleta ugumu hata kwenye tendo la ndoa kwa mwenzi wake. Usiogope ama usiendele kulia tena kwani Mungu amesikia kilio chako na leo amenituma kukunasua hapao.

Jumatatu, 29 Mei 2017

WANAFUNZI MLIOKOKA NISIKILIZENI.

Na Mwalimu Oscar Samba #Ug Ministry
Nina wasalimu katika jina lenye Uweza na Furaha ya hali ya juu la Bwana wetu Yesu Kisto, Leo nimeandaa ujumbe mahususi kwa ajili ya wanafunzi waliokoka katika ngazi zote za Elimu hususani vyuoni ila wazazi walimu, walezi na watumishi pia ni wahusika wa ujumbe huu ili kutimiza adhima hii.

Kusudi kuu la ujumbe huu, Ni kuwataka wanafunzi kutokuacha utayari wao wakumtumikia Mungu pindi waendapo ama wamalizapo vyuo.

Kuna tatizo kubwa sana linawakumba wanafunzi hawa nalo ni hili, Kabla ya kwenda vyuoni katika makanisa walipotokea walikuwa ni watumishi wa zuri sana ila baada ya kwenda wanaacha kumtumikia MUNGU.

Wengine wanajitaidi pindi wa wapo chuoni ila wakimaliza na kupata kazi huacha kabisa kufanya utumishi na baya zaidi wengine wana WITO na kusudi la Mungu kuwapeleka vyuoni ni ili wamtumikiye.

Kama watafanya utumishi baada ya kuhitimu, wengi ni wakati wanasubiria majibu aidha ya chuo, vyeti ama yale ya Kazi.
Inamsikitisha sana Mungu kuona jambo hili linatokea, kwani Utumishi wake haukusudiwi kufanywa tu na watu ambao hawajafika kiwango hicho cha Elimu bali hata wasomi wana Nafasi kubwa kwake kwani Paulo Mtume alikuwa Msomi na aliifanya kazi yake kwa umakini na weledi mkubwa .

Kinachotokea ni hiki, Wanapokuwapo chuoni uwanapoteza utayari wakumtumikia MUNGU, ambao huwakilishwa na viatu kwenye ulimwengu wa roho.
Tuone kwenye kitabu kile cha Wefeso;  WAEFESO 6: 15 NA KUFUNGIWA MIGUU UTAYARI TUUPATAO KWA INJILI YA AMANI.
Na sababu inayopelekea hayo ni kuweka kando Fikra za kutumia elimu yao ili kuujenga ufalume wa mbinguni badala yake huzijaza nafsi zao na fikra za kufanikiwa kimwili kwa elimu yao.
Jambo hili maandiko yamelizungumzia kwenye mfano wa Mpanzi na yanalifananisha na mbegu iliyodondoka kwenye miiba na kusongwa nayo, ambapo tafsiri yake ni mtu aliyesongwa na shuhuli nyingi na udanganyifu wa mali. Kwenye shuhuli nyingi ni hizo fikra na udanganyifu wa mali ni huo udanganyifu wa mafanikio ya kielimu.

Ukiwahitaji kumtumikia MUNGU huwa na kisingizio cha “ubize” ama ratiba ni nyingi, kumbuka jibu la huo mfano wa Mpanzi linasadifu majibu yao. Tuhakiki hilo jambo.
Mathayo 13:22 Naye aliyepandwa penye miiba, huyo ndiye alisikiaye lile neno; na shuhuli za dunia na udanganyifu wa mali hulisonga hilo neno, likawa halizai.

Rai yangu kwao ni kuwakumbusha jinsi MUNGU alivyowatoa mbali kipindi ambacho ada ilikuwa ikisumbua walivyomlilia kwa magoti, walipofukuzwa shule kwa kukosa karo za shule walivyoombolezana kuwaendea watumishi ila wakati huu imefika hatua ya kuwakwepa na wakipigiwa simu kuhusu changizo za huduma huzima hata simu ama huona wanasumbuliwa.
   Kumbuka ulipokosa msaada YESU alikupigania, kabla hujasoma ulivyokuwa na nia ya kuifanya kazi ya MUNGU tena kwa mzigo. Kumbuka siku ile ulipokuwa kwenye taabu kubwa kimaisha ulivyomuaidia Mungu kama atakutoa hapo kwa kumuwekea nadhiri ya jambo utakalolifanya kwenye utumishi wake.

Fanya hima sasa kumrejea yeye.
Ni kweli sio kila mtu ameitwa kuwa Mchungaji ama Mwalimu ila wapo walio waimbaji, wapiga vyombo, wanaodeki kanisani na cha ajabu wanaofanya usafi siku hizi sio wale wasomi wa chuo tena bali wasomi wameweka Elimu yao mpaka kwa MUNGU. Paulo alisoma ila alijishusha na Mungu kumuinua.

Mshahara wako utumiye kuifanya kazi yake, masomo ama kazi ikichukuwa muda mwingi ama kukupa ubize epeleke msalabani kwa maombi na sadaka maalumu ukimsihi MUNGU akupe hekima ya namna ya kumtumikia pia kukupa muda katika hiyo shuhuli.

Rudia enzi zile za maombi yako ya kufunga na kuomba, usiombe tu siku ukiwa na jaribu ama uliyokosa amani. Mungu akutiye nguvu pia #Share ujumbe huu na uweneze kwa wengine ikiwemo kwenye vikundi vya wanafunzi ili waliokoka wapone kiroho.

Kama hujaokoka na unataka kuokoka ama ulirudi nyuma kiroho na unataka kutengeneza na BWANA kwa upya leo, tafadhali fwatisha nami maneno haya kwa Imani, Sema: BWANA YESU, NINAKUPENDA, NINAKIRI NA KUAMINI MOYONI MWANGU KUWA WEWE NI MUNGU, ULIKUFA NA KUFUFUKA KWA AJILI YANGU, INGIA NDANI YANGU KAMA BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YANGU LEO, AMENI.
Hongera kwa kuokoka na tafuta kanisa la watu waliokoka ukasali hapo.

Na Huduma ya UKOMBOZI GOSPLE, Arusha Tanzania, Kwa Maombi, Ushauri, Maswali au Sadaka wasiliana nasi, Barua pepe: ukombozigosple@gmail.com  Simu: +255 759 859 287 pia waweza itumia kwa M-PESA. Zaidi www.ukombozigosple.blogspot.com   #UkomboziGosple  #MwalimuOscarSamba
Pia #Like #Penda Page/Ukurasa wetu au kundi la Fb, ili kupata habari hizi kwa haraka, zaidi. Ug Ukombozi Gosple,                                                                                       PAGE: https://www.facebook.com/Ug-Ukombozi-Gosple                                              
Pia kwenye mtando Mpya wakitanzania wa                                                                       2 DAY SKY: https://www.2daysky.com/home





Jumapili, 28 Mei 2017

MAJIRA YA FARAO ASIYEMJUA YUSUFU.

Na Mwalimu Oscar Samba #Ug Ministry
Yapo majira ya Kuingia, kuishi na hatimaye kutoka Misiri huku ukiyakabili majira mapya ya Jangwani ama nyika isiyopandwa kitu kwani haina umande, pia yapo majira ya kuingia ama kuishi Kanani.

Na majira hayo yote yamegawanyika katika majira kadhaa, na leo ninakujuza kuhusu Majira ya Farao Asiyemjua Yusufu. Ni kweli wana wa Iziraeli waliingia Misiri na Mungu alihaidi kuwabariki ama kuwazidisha huko kupitia ahadi ya Ibrahimu; Mwanzo 15:13. Andiko hilo pia lilitaja muda wa kuishi huko ikiwa ni miaka 400.

Na kipindi cha Mzee Yakobo jambo hili lilitimia pale Mungu alipomtaka kushuka huko Misiri na ajenda iliyowasukuma ilikuwa ni njaa; Mwanzo 46. Baada ya hapo maisha yalikuwa mazuri mno kwani Kijana wake Yusufu alipata kibali na kibali hicho kikawa juu ya Iziraeli yote.

Lakini ili ahadi ya Mungu ya kuwatoa Misiri itimiye ni lazima wapitiye Jangwani, na maisha ya jangwa ni magumu mno, na Mungu alilazimika kuhakikisha ya kwamba anatengeneza mazingira yakuwafanya wayaone walau maisha ya jangwani ni bora kuliko ya utumwani. Kwani lazima wapitiye shule iitwayo jangwa ili kuweza kuishi vyema katika jiji la raha liitwalo Kanani.

Ndiposa Mungu akaruhusu majira mazuri mno kiroho ila magumu sana kimwili ya itwayo; “MAJIRA YA FARAO ASIYEMJUA YUSUFU.” Kwani Mungu alitazama jinsi walivyoyafuraia yale maisha ya masufuria ya nyama na matango na matikiti ukizingatia walikimbia njaa kule Kanani.

Tuyadodose hayo majira kwa mapana zaidi: Kutoka 1:8 Basi akainuka mfalume mpya kutawala Misiri, asiyemjua Yusufu.
Huyu ndiye Huyo Farao, Tutizame atakayotenda.
9 Akawaambia watu wake, “Angalieni watu wa wana wa Iziraeli ni wengi tena wana nguvu kuliko sisi. 10 Haya! na tuwatendee kwa akili, wasije wakaongezeka; tena, kukitokea vita wao nao wasije wakashikamana na adui zetu na kupigana nasi, na kutoka katika nchi hii.” 11 Basi wakaweka wasimamizi juu yao wawatese kwa mizigo yao. Nao wakamjengea Farao miji yakuwekea akiba, Pithomu na Ramesesi.
 Mstari wa kumi na mbili unadhibitisha faida yangu moja wapo ya majira haya kwani unasema ya kwamba; “Lakini kwa kadri ya walivyowatesa ndivyo walivyoongezeka na kuzidi kuenea. Nao walichukiwa kwa sababu ya wana wa Iziraeli.”  Na wewe kadri wanavyokutesa ndivyo unavyozidi kuongezeka kiroho na upako unajaa huku mafuta ya Mungu yakikutiririkia mara dufu huku ukaribu wako na Mungu ukipanuka kila Uchwao.

Natumai umeanza kujionea kuhusu ugumu au majira haya, ila sio huo tuu bali tujionee zaidi.
13 Wamisiri wakawatumikisha wana wa Iziraeli kwa ukali; 14 wakafanya maisha yao kuwa uchungu kwa  kazi ngumu; kazi za chokaa na matofali, na kila namna ya kazi za mashamba; kwa kazi zao zote walizowatumikisha kwa ukali.
Mateso hayakuishia hapo bali yalizidishwa makali kama ule moto wa mfalume Nebkadreza kwa wakina Azaria ulivyochochewa mara 7 zaidi, tumulike mstari wa 15.
15 Kisha mfalume wa Misiri akasema na wazalishaji wa waebrania, … 16 akasema, “Wakati mwazalishapo wanawake wa Kiebrania na kuwaona wa katika kuzaa, ikiwa ni mtoto mwanamume, basi mwueni, bali ikiwa ni mtoto mwanamuke basi na aishi.”

Hakika hayakuwa majira mepesi kwao lakini Mungu aliyaachia kwa makusudi na hili ndilo kusudi lake: Alitaka kuwatengenezea msuli wa kuweza kuimili mikikimiki ya jangwani, pili alilenga kuwafanya watambuwe kuwa hiyo sio nchi yao kwani hatuwaoni mahali wakiwa na kiu yakurejea kama ilivyokuwa kwa Yusufu ambaye alitamani kurejea kiasi chakuwataka kutokuacha hata mifupa yake huko.

Tatu, alilenga kutengeneza hoja itakayowafanya wana wa Iziraeli kuishikilia na kuisimamia ili kuwa na umoja wakutoka katika nchi hiyo na itamfanya Farao na taifa lake kutamani ama kutaka kuwaachiilia huku ikikumbwa kwamba wamisiri walishaonyesha chuki juu yao. Na fahamu kuwa mtu unayempenda kumuachuilia ni ngumu hata kama ni hatari kwako ila ukisha mchukia waweza muachilia ingawaje bado unamuitaji.
Nne, alitafuta namna yakuwatoa ambayo itamfanya akumbuke Agano lake na awatowe kiagano maana aliwapeleka kiagano.

Katika njia hii Mungu alifanikiwa mno, Wana wa Iziraeli walilia kwa sauti iliyo kuu katika majira haya, na kumlilia Mungu. Maombi yaliyomfanya Mungu kutokutulia na hatimaye kumtuma Musa huku akilikumbuka Agano. Kwa moyo mkunjufu ninakufunulia maandiko hayo.

Kutoka 6:2-8, 4 Tena nimelidhibitisha agano langu nao, la kuwapa nchi ya Kanani, nchi ya kukaa kwao hali ya ugeni. 5 Na zaidi ya hayo nimesikia kuugua kwao wana wa Iziraeli, ambao wa misiri wanawatumikisha, nami nimelikumbuka agano langu.

Musa anatumwa kwa ajili ya ukombozi, Na fahamu anatumwa katika majira ya FARAO ASIYEMJUA YUSUFU, kwa hiyo Mpendwa mwenzangu yamkini unapita katika mazingira magumu sana kimaisha na hali hiyo inakupa kusononeka sana ila fahamu ya kwamba hayo ni majira ya Frao asiyemjua Yusufu na Mungu amesikia kilio chako ndiposa mimi nikatumwa kama Musa ili kukutangazia ukombozi wako hivi leo.

Yamkini hapo awali ulikuwa na kibali sana kwa Mchungaji wako, Shemasi ama kiongozi fulani kanisani na uwenda ikawa ni kwenye kwaya ila hivi sasa kimetoweka. Ulipendwa na kukubalika mno kazini ila kwa sasa ni kama umepoteza mvuto.

Mume ama mke alikupenda na kukudhamini, wazazi na hata wakwe walikuona ni mwenye dhamani ila muda huu wamekunyanyapaa.

Nisikilize, hayo ni majira mapya kwako kwani ilikuwa hivyo hata kwa wana wa Waebrania kwani kiti ama cheo au nafasi ile ile ya Farao iliyompa kibali ama kumpongeza Yusufu kipindi kile ndiyo iliyokuja kugeuka na kuwa adui ama sehemu ya utumwa kwa wanae na nduguze.
Tazama Farao aliyemjua namna alivyomkubali na kumpa Heshima hii sanjari na sifa kemukemu ama kedekede;
Mwanzo 41:38 Farao akawaambia watumwa wake, “Tupate wapi mtu kama huyu, mwenye roho ya Mungu ndani yake?” 41 Farao akamwambia Yusufu, “Tazama, nimekuweka juu ya nchi yote ya Misiri.” 42 Farao akavua pete yake ya mhuri mkononi mwake, akaitiya mikononi mwa Yusufu; akamvika mavazi ya kitani kizuri, na kumtia mkufu wa dhahabu shingoni mwake.

Yamkini na wewe hapo awali walikuona hivyo, kwani walisema; “Tupate wapi mtu kama huyu, mwenye roho ya Mungu ndani yake” Ila kibao kwa sasa kimegeuka na kuwa hivi:
Haya! na tuwatendee kwa akili, wasije wakaongezeka” ama “Wamisiri wakawatumikisha wana wa Iziraeli kwa ukali.” Walikuona mtumishi mzuri tena mwenye heshima, muimbaji bora, kijana mcha Mungu. Walikushirikisha kila jambo kipindi cha majira ya Farao aliyekujua ila majira yamebadilika.

Wewe mtazame Yesu kwani kubadilika kwa majira hayo ni kwa ajili ya kukutoa katika nchi ya utumwa, na ninakuhakikishia ya kwamba muda wa ukombozi wako umekaribia. Wewe mliliye Mungu na punde mambo yako yatakaa sawa kwani ninakwambia hili kama Musa aliyekwisha kukutana na Mungu  pale kijiti kilipokuwa kikiwaka moto na ujumbe wangu ni huu.
“Kwa sasa lia mbele za Mungu ili alikumbuke agano lake ulilofunga na Ibrahimu kwani wewe ni sehemu ya hilo agano tangu pale ulipoamua kuokoka. (Mwanzo 15:16 Siku ile Bwana akafanya agano na Abrahamu, akasema, “Uzao wako nimewapa nchi hii, kutoka mto wa Misiri mpaka huo mto mkubwa, mto Frati.”)
Pili hakikisha haupambani na huyo Farao bali wewe muachiliye kwa Bwana naye atashuhulika naye kwa maana yapo mapigo kumi kwa ajili yake na wewe bahari ya Shamu itafunguka kwa ajili yako.”

Hongera kwa kuwa pamoja na mimi na ni yangu imani ya kwamba wakati wako wakutoka hapo utumwani umefika na hautatoka kwa kutoroka bali mpaka umempata Musa wako maana ukifika Masa yeye ndiye atakayeupiga mwamba wa Horebu ili ukupatiye maji na pale Shamu fimbo yake ndiyo itakayo ugawa mwamba. Ukimpata Musa basi na Yoshua unaye maana ndiye atakayekurithisa Kanani yako.

Kama hujaokoka na unataka kuokoka ama ulirudi nyuma kiroho na unataka kutengeneza na BWANA kwa upya leo, tafadhali fwatisha nami maneno haya kwa Imani, Sema: BWANA YESU, NINAKUPENDA, NINAKIRI NA KUAMINI MOYONI MWANGU KUWA WEWE NI MUNGU, ULIKUFA NA KUFUFUKA KWA AJILI YANGU, INGIA NDANI YANGU KAMA BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YANGU LEO, AMENI.
Hongera kwa kuokoka na tafuta kanisa la watu waliokoka ukasali hapo.

Na Huduma ya UKOMBOZI GOSPLE, Arusha Tanzania, Kwa Maombi, Ushauri, Maswali au Sadaka wasiliana nasi, Barua pepe: ukombozigosple@gmail.com  Simu: +255 759 859 287 pia waweza itumia kwa M-PESA. Zaidi www.ukombozigosple.blogspot.com   #UkomboziGosple  #MwalimuOscarSamba
Pia #Like #Penda Page/Ukurasa wetu au kundila Fb, ili kuupta habari hizi kwa haraka, zaidi. Ug Ukombozi Gosple,                                                                                       PAGE: https://www.facebook.com/Ug-Ukombozi-Gosple                                              






Jumamosi, 27 Mei 2017

BONDE LA KUKATA MANENO.

Na Mwalimu Oscar Samba #Ug Ministry 
Kwa furaha isiyo na kifani wala uzani ninakukaribisha ndugu yangu katika Bwana wetu Kristo kwenye safu hii ya makala za kiroho zenye dhima ya kukuinua kiroho, langu jina ni Mwalimu Oscar mwana wa Flora Samba kipenzi cha Mzee Prospa.

Katika makala hii sehemu ya kwanza nitakujuza athari ya maneno huku sehemu ya pili nikikupa mbinu za kupambambana na silaha hii ya maneno yenye nguvu kuliko bunduki ama mabomu yatengenezwayo na wanadamu.

Awali ya kukuletea uhodo huo natamani nikujuze maana ya bonde la kukata maneno. Huu ni ufunuo nilioupata na unamaanisha ya kwamba mtu yupo kwenye mazingira magumu ya kiroho kivita huku hali hiyo ikiwa ni matokeo ya maneno mabaya anayosemwanayo kutoka kwa watesi wake na nguvu ya vita hivyo ni ukaribu wa watu hao aidha kimwili au kiroho.

Ijumaa, 26 Mei 2017

NYAMAZENI NI VUKE.

Na Mwalimu Oscar Samba #Ug Ministry
Ayubu 13:13a Nyamazeni, niacheni, ili nipate kunena.) Hayo ni maneno ya Shujaa Ayubu aliyoyanena mbele ya adui zake. Na wewe leo ujumbe huu ni wa kwako kwani ninakutaka kutokutishwa ama kubabaishwa na maneno au mtazamo mbovu wa adui dhidi yako bali wewe mtazame Yesu aliyebingwa wakuwafunga vinywa kwa Utukufu atakao kutendea.

Adui zako walinena kila lilobaya vinywani mwao, huku wakimtuhumu ya kwamba ametenda dhambi.Ndio maana mabaya yanampata, tutizame sehemu ya maneno ya Elifazi.
Ayubu  4: 7 “Kumbuka, tafadhali: ni nani aliyeangamia akiwa hana hatia? Au hao waelekevu, walikatiliwa mbali wapi? 8Kama mimi nilivyoona, hao walimao maovu, na kupanda mathara, huvuna yayo hayo. 9 Kwa pumzi ya Mungu huangamia, na kwa kuvuma kwa hasira yake humalizika. ”

Ona tena kebei hii katika mstari wa 11; “Simba mzee huangamia kwa kukosa mawindo, nao watoto wa simba mke wametawanyika mbalimbali.”

NYAMAZA KIMYA MUNGU AKUTETEE.

Na Mwalimu Oscar Samba #Ug Ministry
Ayubu akawaambia  adui zake; Laiti mnge nyamaza kabisa, hilo lingekuwa hekima kwenu. Ayubu 13:5.
Kumbe Ukimya ni Hekima? Na wewe fanya hima kuipata Hekima hii. Yaamkini adui zako wamekusonga na maneno kila kona, ukigeuka kulia unasikia, Eti Umefilisika, Kushoto wanasema; Huna tena Upako, Ukitaka kusonga mbele masikio yako husikia haya, “Alijiona kapata kumbe kapatikana.” Unafika mahali unataka kukata tamaa kwa kurudi nyuma, Looh! Kumbe Nyuma nako hakurudiki kwani yapo manongono haya; “Mwaka huu lazima atembee na viraka.”

Basi unajilazimisha kubaki hapo ulipo, napo hapakaliki kwani kila uchwao wanakuwinda kwa ndimi zao ili wakumalize, tena cha ajabu ni watu wako wa karibu na yamkini ni viongozi wako kanisani.

SHINDA VIKWAZO TUKUTANE NG’AMBO YA YORIDANI.

  Na Mwalimu Oscar Samba #UgMinistry  
Maziwa na Asali, hayapatikani Misiri wala jangwani hakuna malisho yawezeshayo ng’ombe kutoa Maziwa ama maua ya mimea ili nyuki wazalishe Asali. Bali ukiyataka yakupasa Kufika Kanani kwani ndiko kwenye mizabibu na tini na zaituni zenye maua mazuri ya wezeshayo nyuki kutanda hapo na kisha kufwonza na hatimaye kuunda Asali.

Maziwa ama majani yatoayo maziwa hustawi kando ya mito na karibu na chemichemi za maji, na vitu hivyo hupatika kanani ambapo ndipo paitwapo; “NG’AMBO YA YORIDANI.”
Huku hawaingi, Waoga, Wasioamini ahadi za Mungu, yaani wasiochanganya ahadi za Mungu na imani, Wanung’unikaji, kwani hao hufa kwa nyama za kware kuwatokea puani; Hesabu 11. Ama kwa nyoka wa Moto; Hesabu 21.

Jumanne, 23 Mei 2017

HAYUPO KABURINI AMEFUFUKA.

Mwalimu Oscar Samba
Tatizo lako halipo tena kaburini bali limefufuka na Bwana YESU, Wakati watu wakikuona wanakuona kama mtu aliyepoteza matumaini ama wengine wakikumbuka jinsi ulivyokuwa mfanikiwa ila kwa sasa maisha ni kama yamekupiga wewe tambua ya kwamba matatizo hayo ni kweli yalikwepo  ila kwa sasa yamekwisha kufufuka na YESU WALA HAYUPO TENA KABURINI. 
Mtazamo wa wengine usikutishe kwani hadi leo huko Uyaudi zipo dini zinazongonja masiya wakiamini kuwa hajaja na wapo wachache wanaoamini ya kwamba YESU hakufufuka kama viongozi wa mafarisayo na wakuu wa makuhani walivyowahonga wale walinzi na kuwataka kusema ya kwamba watangaze eti wanafunzi wamemuiba na haja fufuka.  Hakiki hilo jambo hapa, Matahyo 28:11-15.
Naguswa kukudokezea walau kidogo, 13 wakisema, “Semeni, ya kwamba wanafunzi wake walikuja usiku, wakamuiba, sisi tulipokuwa tumelala.” 15….Na neno hilo likaenea kati ya Wayahudi hadi leo.

USILIYE.

Mwalimu Oscar Samba wa huduma ya Ukombozi Gosple
Najua umekuwa na wakati mgumu sana maishani mwako, na umelia vyakutosha, ila sasa ninakwambia usiliye tena maana Yesu amekusikia na kukuhurumia.
Kitabu kile cha Luka 7:11-17, Kinaeleza kisa cha mwanamke mjane aliyefiwa na kijana wake wa pekee, na Yesu alipoukaribia huo mji wa Naini alimuona na kisha kumuhurumia na hakuishia kumuhurumia tu, bali alimwambia; “USILIYE.”
Mara baada ya maneno hayo alitenda mujiza wa kumfufua mwanaye. Bila iyana nakufunulia maandiko hayo ili ujidhibitishiye mwenyewe.

13 Bwana alipomuona alimuonea huruma, akamwambia, “Usiliye.” 14 Akakaribia, akaligusa jeneza; wale waliokuwa wakilichukuwa wakasimama. Akasema, “Kijana nakuamuru: Inuka.” 15 Yule maiti akainuka, akaketi, akaana kusema. Akampa mama yake.

BELIVE ON YOUR DREAMS, AMINI KATIKA NDOTO ZAKO.

Na Mwalimu Oscar Samba #Ug Ministry
Ni nani unataka kuwa, Dakitari, Mwanasiasa, Mwimbaji wa Nyimbo za Injili, Muhubiri fulani mwenye Upako wa hali ya Juu? Whom one you what to be, a Doctor, A Singer, Politician or a Preacher. God Never lie. Mungu kamwe hasemi uongo.
AMINI KATIKA NDOTO ZAKO, Usiruhusu Mtu mwingine yeyote akwambiye kuwa hauwezi, wala mazingira yasikuaminishe hiyvo. Wewe amini tu ya kwamba inawezekana kuwa unayehitaji kuwa kesho bila kutazama wewe wa leo. Belive on You are Dreams.

Tumtizame Yusufu kijana wa Mzee Yakobo, aliamini kuwa ipo siku anachokiona kitageuka uhalisia. Mwanzo 37:7 Tazama sisi tulikuwa tukifunga miganda shambani, kumbe! Mganda wangu ukaondoka ukasimama, na tazama, miganda yenu ikazunguka ikainama mbele ya mganda wangu.
Hiyo ndiyo iliyokuwa ndoto yake, ambayo ilibeba ukuu katika maisha yake, na wewe tazama ndoto yako kisha, amini katika hiyo wala sio katika kitu kinginecho.

YATOSHA.

 
   Na Mwalimu Oscar Samba #UgMinistry 
Ni fika na bayana ya kwamba mapito yapo, mateso, dhiki na taabu, kulala njaa na kutengwa ama kukataliwa na ndugu ama wapendwa.
Ila yapo majira ya mambo hayo kukoma, na ndiposa Yesu pale msalabani akasema IMEKWISHA, na Mungu akawaambia wana wa Iziraeli wakati wanazunguka ile milima ya Seiri yakwamba YATOSHA.  “Mlivyouzunguka mlima huu yatosha; geukeni upande wa kasikazini.”  Ni Torati 1:2.
Na wewe imetosha sasa kuteseka kulala njaa, Nasema imetosha kulialia kwani majira ya furaha yako yamekwisha kutimia. Kwa waliyokosa watoto kwa muda mrefu ninaachilia Neno la kinabii kwao ya kwamba majira kama haya mwakani watapakata wana na kama ilivyokuwa mwisho wa machozi ya Hana kwa kumpata Samweli na kwao itoshe hivyo.

NYUMA YA MLIMA.

Na Mwalimu Oscar Samba #Ug Ministry 
Baraka zako ama majibu ya maombi  yapo nyuma ya mlima mpendwa kwa hiyo usichoke kuupanda huo mlima kwani ukiumaliza  utakutana na majibu yako.

Ninakuhakikishia ya kwamba PITO hilo ulilonalo ni kama mlima maishani mwako na uhakikisho ni huu; Ukilimaliza salama utakumbana na majibu ya maombi yako.

Wana wa Izirali waliizunguka milima ya Seiri siku za kutosha ila mara baada ya kumaliza kuizunguka nyuma yake walikutana na majibu yao yaliyolenga kuwapitisha salama na Mungu kufungua ukurasa wa kanuni za kuishi nchi ya ahadi sanjari na kuwawezesha kuifikia Kanani yao kwa wepesi zaidi.
kumbukumbu la Torati  2:1 “Ndiposa tukageuka, tukashika safari yetu kwenda jangwani kwa njia ya Bahari ya Shamu, kama alivyoniambia Bwana; tukawa tukiizunguka milima ya Seiri siku nyingi. 2Bwana akanena akaniambia                             3 Mlivyouzunguka mlima huu yatosha; geukeni upande wa kasikazini.

YESU KAMA MTULIZA MAWIMBI AU DHORUBA.

Na Mwalimu Oscar Samba #Ug Ministry 
Siku moja wanafunzi wa Yesu walikuwa wakisafiri majini ama ziwani na walilenga kufika nga’ambo ya ziwa ili kufanya jambo fulani, lakini walipokuwa katika safari yao, Punde si Punde bahari ili kumbwa na Mawimbi makubwa yaliyoambatana na Upepo mkali.

Hali hiyo iliwapa hofu kubwa mno, Lakini katika mazingira yote hayo hawakukubali kukwama safarini bali walimwamsha Yesu aliyekuwa akipiga usingizi, Hii ina maana kubwa sana na hapo mbeleni nitaifafanua.

NGAMBO YA YORIDANI, Sehemu 2.

Na Mwalimu Oscar Samba  Ug Ministry 
Yesu akawambia wanafunzi wake, “Natuvuke mapaka ng’ambo ya ziwa” Luka 8:22. Kisha mbele yake kukatoke dhoruba kali iliyolenga kuwazuia wateule hawa wa Mungu kulifikia kusudi la Mungu lilopo ng’ambo ya Ziwa.

Mariko 4:37Ikatokea dhoruba kuu ya upepo, mawimbi yakakipiga chombo hata kikaanza kujaa maji. 38 Naye mwenyewe alikuwapo katika Shetri, amelala juu ya mto; wakamwamsha, wakamwambia, Mwalimu sii kitu kwako kuwa tunaangamia?” 39 Akaamka, akaukeme upepo, akaiambia bahari, “Nyamaza utuliye!” Upepo ukakoma, kukawa shwari kuu.

NGAMBO YA YORIDANI Sehemu ya 1

                Na Mwalimu Oscar Samba #Ug Ministry 
Ni kweli Maziwa na Asali ni Ahadi ya Mungu maishani mwako, lakini kabla ya kuuvuka mto Yoridani, nilazima ukutane na bahari ya Shamu, Kisha ugumu wa jangwa.

Yesu aliwaambia wanafunzi wake na tuvupe mpaka ng’ambo, lakini kabla ay kuvuka walikumbana na dhoruba kali baharini, Upepo ambao uliwapa hofu kuu. Petro alitamani kutembea juu ya maji ili  amfike alipo Yesu. Ila kabla ya kumkaribia wimbi lilifanyika kikwazo kwake.

Jumatano, 17 Mei 2017

MAREHEMU WALIOGEUKA JESHI KUBWA, (MIFUPA MIKAVU).

 Na Mwalimu Oscar Samba Ug Ministry
Nabii Ezekieli alionyeshwa bonge lilojaa mifupa ya wafu na aliitabiria mara mifupa ikageuka na kuwa maremu, kisha marehemu wakapata uhai kwa kufufuka. Na wewe leo hicho kilichokufa maishani mwako na kusaulika, kitafufuka kwa JINA LA YESU na kisha kuwa hai tena.

Kama ile maiti ilivyogusana na mifupa ya Nabii Elisha ndivyo itakavyokuwa kwako leo, kwa hicho kilicho kufa kugusana na YESU KRISTO MTENDA MIUJIZA. Aliyemfufua Lazaro, Binti wa mama yule mjane wa mji wa Naini, Kijana aliyekuwa amekufa na Yesu kusema amelala, kisha watu kumcheka. Ila punde si punde, maiti alifufuka. Yamkini na wewe unapowambia nitaolewa, wanakucheka sana, kwani umri umesonga, ama unapowaambia ya kwamba, utasoma, utajenga, utamiliki magari na hata majumba, hucheka sana. Wewe endelea kumuamini Yesu aliyemfufua huyu mfu sanjari na mifupa ile mikavu, ikawa mibichi, marehemu na kisha WALIO HAI.

Jumanne, 16 Mei 2017

Mwalimu Oscar Samba wa Ug Ministry aandaa Mkutano Mkuwa wa Semina ya Neno la Mungu kwa Morombo Arusha Tanzania.

Mwalimu wa Neno la Mungu Oscar Samba,wa Huduma ya Ug Ministry, anakuletea Semina kubwa ya Mkutano wa Neno la Mungu. Itakayofanyika hapa kwa Morombo Mkoani Arusha kuanzia tare 11-19/6/2017. Walete viwete, vipofu na viziwi pamoja na wagonjwa wote ikiwemo wa UKIMWI na Wakoma. Yesu Mtenda miujiza atakwepo katika Mkutano huo. Watu wote mnakaribishwa.

LAZARO HAJAFA, AMELAA NA WEWE AMINI TU.


 Na Mwalimu Oscar Samba Ug Ministry
Wakati Dada yake  Lazaro anasema, Lazaro amekufa na ni siku ya nne sasa, na kunuka ananuka, Jemedari YESU anasema, “Lazaro ajafa bali amelala.” Na kumtaka dada huyu amini tu, ili mujiza utendeke.

Na kwako wakati wanasema kuwa, ndoa yako, imekufa,Uchumi wako umedidimia, Eti ndoto zako za kuwa mbunge, kiongozi, msomi ama dakitari na hata zile za kuwa na huduma kubwa zimekufa, mimi ninakwambia kwa jina la Yesu aliye hai hazijafa bali zimelala tu, na siku ya leo zitaamka kama Lazaro na kijana walivyo fufuliwa.

Jumatatu, 15 Mei 2017

USITISHWE NA MAZINGIRA, MUNGU AKISEMA AMINI TU.

Na Mwalimu Oscar Samba #UgMinistry
Kuna wakati ukitazama mazingira uliyonayo na kulinganisha na ahadi ya Mungu maishani mwako, unapata vitu tofauti ama visivyowezekana. Mungu alimuaidia Ibrahimu na Mkewe Sara kuwafanya taifa kubwa, cha ajabu aliwapa mtoto mmoja.  Kimazingira ilikuwa ngumu kwani tungalitarajia kupewa watoto wengi.

Isaya 51:2 Mwangaliye Ibrahimu, baba yenu, na Sara aliyewazaa; kwa maana alipokuwa mmoja tu nalimwita, nikambariki, nikamfanya kuwa wengi.
Mazingira haya yalikuwa hayasadifu ahadi hii ya Mungu ila Ibrahimu na mkewe waliishika kwa Imani iliyo kuu kwani licha ya kupewa mtoto mmoja pia walikuwa hawajapata mtoto huyo hadi kufikia uzeeni ambapo Ibrahimu alimpata Isaka akiwa ni mtu wa miaka mia na ushee, jambo hili halikuwa dogo kwake maana yeye na mkewe walicheka wakati ahadi hii inatokea kwa kudhibitishwa.

KWA NINI UJINYONGE, KWA NINI UJIUWE, KWA NINI UKATE TAMAA? WAKATI YESU ANAWEZA.

 Na Mwalimu Oscar Samba #UgMinistry
Ipo nguvu ya ajabu ipatikanayo katika msalaba wa Yesu Kristo iwezayo kukupa majibu ya masumbuko unayoyahitaji. Na kama msaada upo basi haipaswi kukata tamaa ama kuendelea kufadhaika bali wewe uhitaji huu msaada ili uwe salama.

Kuna kisa kimoja kwenye Bibilia nacho ni cha Petro ambaye alitembea juu ya maji, ila punde mara baada ya kuanza tendo hili la Imani alianza kuzama. Petro hakunyamza, wala hakufikiria kuzijizamisha kama wengine hivi leo wanavyofikiria kujiua, kwa kujinyonga ama kunywa sumu. Bali rafiki yangu huyu alimuita Yesu. Na Yesu alimsaidia.

EPUKA KUYAFANYA HAYA PUNDE UMUONAPO MUNGU YUPO KIMYA.

Kijana mmoja akasema, “Sitowi tena sadaka maana kila nikitoa ndo kama matatizo yanaongezeka”
Wengine wameanguka kwenye uzizi na uasherati huku sababu ikiwa ni kumuona Mungu kama awasikii ama amechelewa kuwaletea majibu yao, aidha ya kuolewa ama mtoto.
Sarai akamwambia Abrahamu/Ibrahimu, “Basi sasa, Bwana amenifunga tumbo nisizae, umwingiliye mjakazi wangu, labla nitapata uzao kwa yeye.” Abrahamu akaisikiliza Sauti ya Sarai. Mwanzo 16:2.

Baada ya hapo kilichofwata ni Ibrahimu kuzaa na kijakazi huyo wa bibi Sarai na hatimaye kumpata Ishmaeli ambaye

MUNGU ANAPOKUWA KIMYA FANYA YA FWATAYO. Sehe. 2.

Inaumiza kuwa katika pito gumu na unamtumaini Mungu kisha kumuona Yupo kimya, Ingawaje wakati mwingine huongea ila hatuelewi ila kiukweli upo wakati anakuwa kimya kama wakati ule wa Yesu pale msalabani.

Wengine hujifariji kuwa alinyamza kwa sababu Yesu alikuwa amebeba dhambi na Mungu hachangamani na wenye dhambi. Hoja hii kwangu ni dhaifu kwani kama aliweza kuzungumza na Petro katikati ya dhambi yake ya kumkana Yesu kwa ishara ya jogoo kuwika huku Yesu akimgeuki na kumkumbusha moyoni maneno yale ya kwamba kabla ya jimbi kuwika atamkana, alishindwaje kunena na mwanaye aliyemtuma kwa kusui hilo?

Ila katika yote hayo haipaswi kukata tamaa ama kutafuta njia za mkato kama wengine wafanyavyo baada ya hali kama hii.

MUNGU ANAPOKUWA KIMYA FANYA YA FWATAYO. Seh. 1


Ni rahisi kunena kinyume na mtazamo huu ya kwamba Mungu hawezi kunyamaza ila wasomaji wa maandiko na watu wanaopitia mapito magumu na ya muda mrefu ni wepesi wa kukubaliana na Falisafa hii.

Ila kumbuka hali hii ilimkuta hata Yesu, “Mungu wangu, Mungu wangu mbona umeniacha?”, Mathayo 27:46. Kiukweli Mungu alikuwa Kimya. Hatumuoni akiongea naye wala kumjibu lolote baada ya kukamatwa kwa Yesu.
Kuna taswra kuu mbili za Mungu kunyamaza kimya, ya kwanza ni ile ya mtu kutenda dhambi na Mungu kumuacha, na ya pili ni ile ya mtu kuwa katika hali ya pito huku Mungu akipima subira yake iliyondani ya Saburi ya Kimungu ama Mungu akimsubiria achukuwe hatua fulani ndipo amjibu.

YASIYOWEZEKANA KWA WANADAMU KWA MUNGU YANAWEZEKANA.

Mwalimu Oscar Samba
Uhali gani mpenwa mwenzangu katika Bwana? Natumai u buheri wa afya.

Leo nimekuandalia ujumbe mahususi kwa ajili ya kukujuza ukubwa na Uweza wa Yesu Kristo katika mambo yaliyoonekana ni magumu kama mlima ama bahari katika maisha yako.

Ni kweli hitaji ama jambo lilopo mbele yako ni kubwa kuliko wewe na hata mimi mwenyewe ni kweli siliwezi, ila Yesu tunayemuamini analiweza. Amini tuu kama alivyomwambia dada yake na Lazaro rafiki yake kuwa anapaswa kuamini tu.

MTAZAME NYOKA WA SHABA.

Ndugu yangu, wasalamu katika Bwana Yesu Kristo, Ewe unayepita katika mapito magumu usifadhaike wala kukata tamaa badala yake mtazame Yesu kama Nyoka wa Shaba.
Kama Musa alivyomuinua yule nyoka wa shaba jangwani ndivyo Mwana wa Adamu hanabudi kuinuliwa.”
Katika maandiko matakatifu yaliyopo kwenye kitabu kile cha Hesabu yanaitaja nyoka ya shaba kama ishara ya ushindi katika nyakati zilizo ngumu kimaisha. Kwani kipindi hiki wana wa Iziraeli walikuwa wakiumwa na nyoka wa moto ama wenye sumu kali na walipoteza maisha punde.
Ila Musa alipata maelekezo kutoka kwa Mungu ya kwamba ainuwe nyoka ya shaba kwa kuitundika juu ya mti na kila aliyeng’ata na nyoka ya moto alipomtazama nyoka huyu alipokea uponyaji.
Musa akafanya nyoka ya shaba, akaiweka juu ya mti: hata ikiwa nyoka amemuuma mtu, alipoitazama ile nyoka ya sahaba, akaishi”.Hesabu 21:9.
Nami leo hii ninakuta kutokukata tamaa ama kuacha WOKOVU kwa sababu ya ugumu wa maisha ama mateso kwenye ndoa, uchumi ama biashara kuwa ngumu, magonjwa, kukataliwa au vita kwenye ulimwengu wa roho.
Bali inua macho yako ya Imani na kwa Imani; umtazame Yesu aliyeinuliwa kwenye ulimwengu wa roho kama yule nyoka wa shaba jwangwani na hakika hapo utapata majibu yako.
Kumbuka walioshindwa kumtizama yule nyoka wa shaba walipoteza maisha yaani walikufa hali iliyowafanya washindwe kufika Kanani. Na wewe ukilitazama tatizo lako utakwama maana ni kubwa kuliko wewe bali mtazame Yesu aliye dawa ya tatizo lako nawe utashinda, tena na zaidi ya kushinda.

Na Huduma ya UKOMBOZI GOSPLE, Arusha Tanzania, Kwa maombi, Ushauri, Maswali au Sadaka wasiliana nasi, Barua pepe: ukombozigosple@gmail.com Simu: +255 759 859 287 pia waweza itumia kwa M-PESA. Zaidi www.ukombozigosple.blogspot.com

Jumapili, 7 Mei 2017

Mwalimu Oscar Samba KUKAA KWENYE NAFASI

Mwalimu Oscar Samba, MAMBO MUHIMU KATIKA KUMTUMIKIA MUNGU

Wanafunzi wa Vyuo na Shule, Usimwache Yesu mfikapo vyuoni/Shuleni

Mwalimu Oscar Samba
+255 759 859 287  Kumekuwa na wimbi kubwa la wanafunzi kuyaacha maadili ya kikristo pindi wa fikapo shuleni ama vyuoni.

Jambo hili ni hatarishi kwao kwani mazingira ya masomo hufananishwa na eneo la kivita kwenye ulimwengu wa roho. Katika maeneo kama haya ndipo hujitokeza wanafunzi waliozoezwa kutumia ushirikina au wenye ujuzi katika mambo hayo. Na wewe ukiyumba kiroho maana yake ni kwamba utashindwa na mambo hayo na kujikuta ukididimia kiroho na kimwili huku maono au ndoto zako zikikwamia njiani.

Pia wachawi na waganga wa kienyeji ama washirikina hupenda kudhuru maeneo hayo kwenye ulimwengu wa roho ili kuiba nyota za wanafunzi, kuwachezea ama kuwatumikisha kichawi na hata kujipatia wajumbe wao hapo.

Ndio maana katika maeneo ya mashule ama yvuo hakuishi vituko vya kishirikina hususani kwenye vyoo na hata mabweni. Ukiwa na Yesu utayashinda haya kirahisi na wewe hawatakuweza.

Na sababu zifwatazo ndizo huwafanya wanafunzi wengi kumuacha Yesu punde wafikapo katika mazingira kama haya; 
1. Kufwata mkumbo, wanafunzi wengi hujikuta wakifwata mkumbo kwa kuiga mambo yasiyofaa, ikiwemo vitendo vya ulevi na hata ukahaba. Pamoja na mavazi.

2. Kukosa ujasiri wa kumtaja Yesu ama kuona wokovu kama ni aibu, Nisikilize kwa bidii ili upone, Yesu sio mzigo wala sio aibu kuwa naye bali ni sehemu ya Ushindi. Kumbuka msalaba kwao wapoteao ni upuzi bali kwetu siye ni ushindi, uzima, na nguvu tele maishani mwetu. Usikubali kuona haya kumtangaza Yesu maana anasema atakayemkana mbele ya watu naye atamkana mbele ya Baba.

3. Kuwa na marafiki waovu, siku zote rafiki wa mtu ni mtu, na unapojifanyia marafiki wasiofaa ni kwa uaribifu wa nafsi yako na maisha, na maono yako kwa ujumla. Mithali 18:24a Ajifanyiaye marafiki wengi ni kwa uaribifu wa nafsi yake.. 
Mithali 22: 24 Usifanye urafiki na mtu mwenye hasira nyingi, wala usiende na mtu wa gadhabu nyingi.

Bibilia inatupa muongoza sahihi wa namna ya kuwa na marafiki kwani ukiwa na rafiki mwizi na wewe utakuwa kama yeye, aliye kahaba ama mwenye tabia ya kuchuna wanaume "Mabuzi" ama mwenye macho ya kutamani mabinti, "Mademu" hakika na wewe utafanana naye. 
Katika hili ninakuta kuwa makini sana na marafiki, ingawaje dhumuni langu sio kukunyima kushirikia nao kimasoma, ila shabaha yangu ni kukuondolea ukaribu nao.

4. Kuwa na gelifrend au Boyfrendi, Kitendo hiki cha mwananfunzi kuamua kuwa na mpenzi kabla ya wakati wa kibibilia ama nje ya mpango wa kimungu ni dhambi na jambo hili hufungua mlango kwa Shetani unaomuwezesha kunyonya hali yako ya kiroho polepole na kujikuta ukianza kuwa na Wokovu wa mazoea ama wa kidini na hatimaye kuwa debe tupu litoalo upatu. 

Usidanganywe eti huo ni uchumba, hii ni hila ya Shetani kwani uchumba wakibibilia haufanyiki hivyo, na huwa na utaratibu ufwatao , Mchungaji wako ajue, Wazzzi wafahamishwe, kisha mchakato wa mahari ufanyike na utangazwe kanisani.
Kama hayo hayajafanyika ama hakuna rathi hiyo fahamu kuwa mpo mtegoni.
Na huku ni kumkosea Mungu Mpendwa, Wimbo uliobora 3:5 Nawasihi, enyi binti za Yerusalemu, kwa paa na kwa ayala wa porini: msiyachoche mapenzi, wala kuyaamsha, hata yatakapoona vyema yenyewe.

Ndugu yangu kiimani ninakutaka kumshika Yesu kwa bidii unapokuwa katika masomo yako na endelea na misingi ya kiroho ili kufanikiwa vyema. Usikubali kuwa mlokole ukienda likizo ila kibaka ama mwizi au mtukanaji ukiwa shueni. Achana na utamaduni wa kumwa mwema mbele ya wazazi ila muovu mbali ya upeo wa macho yako.

Swala la kiroho ni lako wewe na Mungu wako. Wakina Meshaki, Shedraki na Aberinego na Danieli walipofika uamishoni kule Babaeli na kuingizwa katika iamaya ya kifalume huku wakipelekwa darasani ili kuijua lugaha ya wazawa na maarifa ya kifalume kwa shabaha ya utumika kwa mfalume Nebukadreaza hawakumwacha Yesu; Badala yake waliongeza bidii na hatimaye Mungu wao kutukuzwa hapo.

Na wewe hapo ulipo inahitajika Mungu wako atukuzwe na kila mtu amptambuwe huyo uliye naye kama wakina Meshaki na Aberinego, Shedraki na Danieli kipindi kile. 

Pia kama hujaokoka fanya hima umpokee huyu Yesu kwani ndiye atakayekuwezesha kuishi maisha mazuri chuoni maana bila Yeye wachawi, walozi na wasoma nyota wanaweza kukuibia mafanikio yako na kujikuta unafukuzwa shule bila sababu za msingi ama kuishilia kwenye vitendo vya ulevi na ukahaba na hatimaye kuvurugikiwa maishani.

Kumbuka kuwa sio kila anayetenda mambo ya ajabu ama maovu vyuoni ama mashuleni amependa bali wengine wamelogwa au kuchezewa kwenye ulimwengu wa roho na watu wenye husuda, wivu na hata wenye nia mbaya. Wapo walioibiwa nyota, na waibao hutupa tabia za ulevi, ukahaba ama mwenendo mbaya pia magonjwa ili mshuhulike na hayo badala ya kugundua wizi huo wa nyota ama huwa kama bumbuzi kwa kutokuja kuwa ameibiwa.

Yesu pekee ndiye awezaye kumuweka huyu mtu salama,

Kama huja Okoka na unataka kuokoa ama ulikuwa umeokoka na ukalega kiroho ama wakati huu upotayari kurejea tafadhali fanya sala hii ya toba.

Sema, Mungu Baba, nipo mbele zako, Nimetambua yakuwa mimi ni mwenye dhambi, Na nipotayari kukufwata, Na ninakuamini na kukupokea kama Bwana na Mwokozi wa maisha yangu, ninakupenda Yesu, nilinde kiroho na kimwili. Ameni .

Hongera kwa kuokoka na tafuta kanisa la kihoho mahali ulipo ukaabudu, Ameni.

Na Huduma ya Ukombozi Gosple, kwa maombezi ama ushauri na sadaka Ya M-pesa tumia +255 759 859 287.  


USIFIYE JANGWANI MPENDWA

Na Mwalimu Oscar Samba
Ndugu yangu mpendwa katika Bwana ninakutaka kutokukata tamaa na maisha ya wokovu, kwani haijalishi ni jambo gani unalolipitia, mbele upo ushindi.

Wana wa Iziraeli walisafiri kutoka nchi ya utumwa ya mateso ya Misiri ili kuelekea nchi ya Maziwa na Asali kama Bwana alivyo waaidia, ila iliwalazimu kupita jangwani. Haikuwa safari nyepesi kutokana na ugumu na manthari ya Jangwa.

Ila wale walioshinda walifanikiwa kuingia Kanani na hatimaye kuyaishi maisha yale ambayo Mungu aliwaaidia. Na wewe yakupasa kushinda.

Ijumaa, 5 Mei 2017

Wasifu, Mjuwe Mwalimu Oscar Samba.

Mwalimu Oscar Samba
Ni Mwalimu wa Neno la Mungu na Muasisi wa Huduma ya Ug, yenye kirefu cha UKOMBOZI GOSPLE. Na yenye tafsiri ya Injili ya Ukombozi.

Pia ni mwandishi wa vitabu vya Neno la Mungu, na kitaaluma ni mwandishi wa habari mwenye elimu ya ngazi ya Diploma/Stashahada na ngazi ya Cheti cha Juu. Amesomea kwenye chuo cha AJTC kilichopo mkoani Arusha.

Ana elimu ya Thielojia ngazi ya cheti aliyoipata kwenye chuo cha kupanda makanisa Makuyuni mkoani Arusha kikiwa ni tawi la chuo cha TAG cha BIBILIA ARUSHA, kwa hivi sasa ni Chuo cha Bibilia Kanda ya Kasikazini.

Pia amehitimu shule ya Msingi Maharo na ya sekondari ngareni zilizopo mkoni Kilimanjaro. Kabila lake ni mchaga wa maeneno ya Rombo. Na Dini yake ni Mlokole.

Baba yake ni Prospa, Mama yake ni Flora. Na Ukoo wake ni Samba.  Ni mtoto wa pili katika familia ya Mzee Prospa.
Kuzaliwa ni 6/6/1989,
Anaishi mkoani Arusha na kiasili ni mtu wa mkoani Kilimnjaro.

Pia Kabla ya kuingia kwenye wito wa kitumishi aliwai kufanya Siasa na alikuwa mwanachama wa vyama viwili ambapo chama cha kwanza alikitumikia kwa muda mrefu zaidi na hatimaye kuhamia kingine kutoka na masilai ya kisiasa.

KUTOA MIMBA NI DHAMBI

Na Mwalimu Oscar Samba
Kumekuwa na matukio mengi ya watu kutoa mimba huku baathi yao wakijifariji kuwa kufanya hivyo sio mauaji.

Ninataka kukufahamisha bayana ya kwamba utoaji wa mimba ni mauaji, na kibibilia hakuna muuaji mwenye uzito zaidi ila ukubwa ama kipimo cha kosa hilo la umwagaji damu ni sawa.

Yaani aliyeua mtoto aliyetumboni na aliyeumuua mtu wa miaka kumi ama zaidi wote hukumu yao inalingana.

Kwa kifupi aliyetoa mimba na aliyeshiriki wote ni kundi la wakina kaini.

Ikumbukwe kuwa kibibilia mtoto ama mtu hutambulika toka tumboni, Na hapo Mungu umuhesabu sawa na aliyezaliwa.

Ndio maana akamwambia Yeremia kuwa "Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, na kabla hujatoka tumboni, nalikutakasa..." Yeremia 1:5

Yohana mbatizaji alicheza akiwa tumboni mara baada ya mama yake kukutana na mama yake na Yesu. Hii ni ishara kwamba kusudi la Mungu lilidhirishwa ndani yake angali tumboni mwa mamaye, sanjari na hapo kwaYeremia.

Kwa hiyo epuka kushiriki dhambi hii kwa namna ya aina yoyote ile na kama ulishashiriki tubu haraka.

USIKATE TAMAA YESU ANAWEZA

Mwalimu Oscar Samba
Yaliyoshindikana kwa wanadamu, Kwa Yesu yote yanawezekana.

Hivyo ndugu yangu ninakutaka kutokukata tamaa na maisha kwa namna ya aina yoyote ile kwani Yesu anayaweza yote.

Yeye aliyefanya njia kwenye bahari ya Shamu atafanya njia pia katika mapito yako.

Yeye aliyemfufua Lazaro, aweza fufua leo Uchumi wako, Ndoa yako na hata kukurejeshea afya yako.

MAOMBI YANGU KWAKO:
Mungu wangu na akuponye na magonjwa yako yote na kukuondelea mateso yako leo. Amen.

Mwalimu Oscar Samba, MTUMAINI BWANA KATIKA PITO LAKO

MWALIMU OSCAR SAMBA NAFASI YA IMANI KATIKA MAISHA YA UOKOVU

Jumatano, 3 Mei 2017

Nukuu iliyopo kwenye Kitabu cha Sadaka Kama Mbegu cha Mwalimu Oscar Samba

 "Ni jambo la hatari sana kufikia hatua ya kula Sadaka ambayo Mungu amekupa kama Mbegu na umejua fika kabisa alikupa kuitoa ila kwa sababu una hitaji fulani ukalazimika kuitumia. Nisikilize kwa ukaribu na utulivu: Maana hitaji na uhiitaji wa mwadamu hauishi, na Mungu anapotaka umtolee Sadaka kama Mbegu haimaanishi kuwa haioni shida yako, laa! Asha! Anaiona na amepanga kuitatua kwa kukupa njia ya upandaji.
Hivi kama una uhitaji wa mahindi kilogramu 30 na una mbegu ya mahindi kilo mbili. Itakufaidia nini kula mbegu hizo leo na kubakiwa na uhitaji wa kilogramu 28? Ni ya heri kuzifukia mbegu mchangani kama Yesu alivyosema kwenye Mariko 4:26-29. Na hatimaye kukupatia mavuno yatakayokidhi mahitaji yako.
Masikini wegi ni masikini kwa sababu walikwepa garama za kutoka katika umasikini. Na matajiri wengi ni matajiri kwa sababu walikuwa majasiri wa kuzikabili gharama za kutoka katika umasikini huku wakiwa wanajua faida za kuwa tajiri.
"