Na Mwalimu Oscar Samba #Ug Ministry |
Ni nani unataka
kuwa, Dakitari, Mwanasiasa, Mwimbaji wa Nyimbo za Injili, Muhubiri fulani
mwenye Upako wa hali ya Juu? Whom one you what to be, a Doctor, A Singer,
Politician or a Preacher. God Never lie. Mungu kamwe hasemi uongo.
AMINI KATIKA
NDOTO ZAKO, Usiruhusu Mtu mwingine yeyote akwambiye kuwa hauwezi, wala mazingira
yasikuaminishe hiyvo. Wewe amini tu ya kwamba inawezekana kuwa unayehitaji kuwa
kesho bila kutazama wewe wa leo. Belive on You are Dreams.
Tumtizame
Yusufu kijana wa Mzee Yakobo, aliamini kuwa ipo siku anachokiona kitageuka uhalisia.
Mwanzo 37:7 Tazama sisi tulikuwa
tukifunga miganda shambani, kumbe! Mganda wangu ukaondoka ukasimama, na tazama,
miganda yenu ikazunguka ikainama mbele ya mganda wangu.
Hiyo ndiyo iliyokuwa ndoto yake, ambayo ilibeba ukuu katika maisha
yake, na wewe tazama ndoto yako kisha, amini katika hiyo wala sio katika kitu
kinginecho.
VIKWAZO KWA
YUSUFU. 1. Ndugu kumchukia, 2. Kutupwa Gerezani.
Mwanzo 37:5 Yusufu akaota ndoto,
akawapa ndugu zake habari, nao wakazidi kumchukia. Mstari wa 8 unaonyesha
kauli za kumchukia huyu kijana. 8
Ndugu zake wakamwambia, “Je, kweli wewe utatumili sisi? Nawe utatutawala,”
Wakazidi kumchukia kwa ajili ya ndoto yake na maneno yake.
Bila kosa
Yusufu alitupwa Gerezani mara baada ya kukataa kutenda dhambi ya kulala na mke
wa bwana ama mwajiri wake Potifa. Mwanzo 39:20-23. Cha ajabu hapo ukisoma hayo
maandiko utakuta kuwa Yusufu alipata kibali hata huko gerezani na mkuu wa
gereza hakutazama maneno ama mashitaka dhidi yake.
#Usitazame
vikwazo, tazama Furusa, na geuza matatizo ama changamoto kuwa furusa kama
Yusufu. Kijana huyu alikuwa gerezani na mazingira ya gereza yangeweza kuwa
kikwazo tosha katika safari ya ndoto zake ila aliyageuza matatizo na vikwazo
hivyo kuwa furusa kwani humo gerezani ndiko alikotafsiri ndoto hali iliyomfanya
kutambulika kwa Farao na kisha Farao kumtoa na kumfanya kuwa mkuu sana hali
iliyompa Mwanya wa kutimia kwa maono yake.
Fungua nami
kwa mwendo wa pole kama twiga nyikani kitabu kile cha Mwanzo ili ujione ujasiri
huu wakuyafanya mazingira yasiyowezekana kuwa mtaji ama daraja la kufika
ng’ambo.
Mwanzo 40:1-22, 12
Yusufu akamwambia tafsiri yake ndiyo hii, “Matawi matatu ni siku tatu. 13 Baada
ya siku tatu Farao atakiinua kichwa chako, atakurudisha katika kazi yako; nawe
utampa Farao kikombe mkononi mwake, kama desturi ya kwanza, ulipokuwa
mwenyeshaji wake”
Baada ya
hapo huyu Mweshaji kwa mikono yake mwenyewe anatengeneza daraja ili Kijana
Mbeba maono apite. Mwanzo 41 Sura yote. Ila miye nitakupitisha katika maandiko
kadhaa.
Mwanzo 41:12 Na huko
pamoja nasi palikuwa na kijana Mwebrania, mtumishi wa mkuu wa askari,
tukamhadithia, naye akatutafsiria ndoto zetu; akamtafsiri kila mtu kama
ilivyokuwa ndoto yake.
Baada ya
daraja kujengwa Farao hakuweza kunyamaza bali alihitaji daraja kuzinduliwa na
uzinduzi huo ni kwa Yusufu kutoka Gerezani, Tazama nami.
Mwanzo 41:14 Ndipo
Farao akapeleka watu, wakamwita Yusufu, wakamtoa haraka kutoka gerezani.
Akanyoa, akabadili nguo zake, na kuingia kwa Farao.
Kijana
aliingia kazini, na Mungu akiwa pamoja naye. Kama alivyofanya Mwebrania huyu
kwa kumshika Mungu na kuendelea kuamini katika ndoto zake nawe fanya hivyo
kwani ukiyumba kwa kupoteza mwelekeo utakwama mahali. Tuendelee ili kutazama
kilichotokea. Utaona aliyekuwa Mfungwa namna anavyopewa heshika kubwa kama
mwana wa kifalume.
Mwanzo 41:41 Farao
akamwambia Yusufu, “Tazama, nimekuweka juu ya nchi yote ya Misiri.” 42
Farao akavua pete yake ya mhuri mkononi mwake, akaitiya
mikononi mwa Yusufu; akamvika
mavazi ya kitani kizuri, na kumtia mkufu wa dhahabu shingoni mwake. (Unafikiri Mungu huyu wa Yusufu amekufa? Jibu ni
laa, yaani Yungali hai na atatenda hivyo kwako ila wewe amini tu katika ndoto
zako ya kwamba ipo siku utakuwa unayetaka kuwa hata kama huko kwako ama katika
taifa hili hajawai kutokea mtu kama wewe. Wewe amini tu, ipo siku You will
become Some One as You Wish.)
Mpendwa! Na
wewe Geuza gereza ulilonalo kuwa mtaji ama njia ya kutokea kama Yusufu. Ni jambo gani
linalofanyika kikwazo kwako? Je, Unaona Bahari ya Shamu mbele yako? Kulia na
kusho milima? Nyuma Jeshi kubwa la Farao?
Lisikiye Neno la Bwana, Kutoka 14:13 Musa akawaambia watu,
“Msiogope! Simameni tu, mkauone wokovu wa Bwana atakao wafanyia leo; kwa maana
hao Wamisiri mliowaona leo hamtawaona tena milele.14 Bwana atawapigania ninyi,
nanyi mtanyamaza kimiya”
Ni
jambo gani la kumshinda Yesu? Halipo.
Tukutane kesho kwenye somo la SHINDA VIKWAZO TUKUTANE NG’AMBO YA YORIDANI.
Ulikuwa na Mwalimu mwana wa Flora Samba, katika familia ya Mzee wa Hekima Mzee Prospa.
Kwa Busu takatifu lenye upako wa kutimiza maono ninakuaga.
Kama hujaokoka na unataka kuokoka ama
ulirudi nyuma kiroho na unataka kutengeneza na BWANA kwa upya leo, tafadhali
fwatisha nami maneno haya kwa Imani, Sema: BWANA YESU, NINAKUPENDA, NINAKIRI NA
KUAMINI KUWA WEWE NI MUNGU, ULIKUFA NA KUFUFUKA KWA AJILI YANGU, INGIA NDANI
YANGU KAMA BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YANGU LEO, AMENI. Hongera kwa kuokoka na
tafuta kanisa la watu waliokoka ukasali hapo.
Na Huduma ya
UKOMBOZI GOSPLE, Arusha Tanzania, Kwa Maombi, Ushauri, Maswali au Sadaka
wasiliana nasi, Barua pepe: ukombozigosple@gmail.com
Simu: +255 759 859 287 pia waweza itumia kwa M-PESA. Zaidi www.ukombozigosple.blogspot.com #UkomboziGosple #MwalimuOscarSamba
Pia #Like
#Penda Page/Ukurasa wetu au kundila Fb, ili kuupta habari hizi kwa haraka,
zaidi. Ug Ukombozi Gosple, PAGE:
https://www.facebook.com/Ug-Ukombozi-Gosple
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni