Ndugu yangu,
wasalamu katika Bwana Yesu Kristo, Ewe unayepita katika mapito magumu
usifadhaike wala kukata tamaa badala yake mtazame Yesu kama Nyoka wa Shaba.
“Kama Musa alivyomuinua yule nyoka wa shaba
jangwani ndivyo Mwana wa Adamu hanabudi kuinuliwa.”
Katika
maandiko matakatifu yaliyopo kwenye kitabu kile cha Hesabu yanaitaja nyoka ya
shaba kama ishara ya ushindi katika nyakati zilizo ngumu kimaisha. Kwani
kipindi hiki wana wa Iziraeli walikuwa wakiumwa na nyoka wa moto ama wenye sumu
kali na walipoteza maisha punde.
Ila Musa
alipata maelekezo kutoka kwa Mungu ya kwamba ainuwe nyoka ya shaba kwa
kuitundika juu ya mti na kila aliyeng’ata na nyoka ya moto alipomtazama nyoka
huyu alipokea uponyaji.
“Musa akafanya nyoka ya shaba, akaiweka
juu ya mti: hata ikiwa nyoka amemuuma mtu, alipoitazama ile nyoka ya sahaba, akaishi”.Hesabu 21:9.
Nami leo hii
ninakuta kutokukata tamaa ama kuacha WOKOVU kwa sababu ya ugumu wa maisha ama
mateso kwenye ndoa, uchumi ama biashara kuwa ngumu, magonjwa, kukataliwa au
vita kwenye ulimwengu wa roho.
Bali inua
macho yako ya Imani na kwa Imani; umtazame Yesu aliyeinuliwa kwenye ulimwengu
wa roho kama yule nyoka wa shaba jwangwani na hakika hapo utapata majibu yako.
Kumbuka
walioshindwa kumtizama yule nyoka wa shaba walipoteza maisha yaani walikufa
hali iliyowafanya washindwe kufika Kanani. Na wewe ukilitazama tatizo lako
utakwama maana ni kubwa kuliko wewe bali mtazame Yesu aliye dawa ya tatizo lako
nawe utashinda, tena na zaidi ya kushinda.
Na Huduma ya
UKOMBOZI GOSPLE, Arusha Tanzania, Kwa maombi, Ushauri, Maswali au Sadaka wasiliana
nasi, Barua pepe: ukombozigosple@gmail.com Simu: +255 759 859 287 pia waweza
itumia kwa M-PESA. Zaidi www.ukombozigosple.blogspot.com
Somo zuri lenye kuturejesha kwenye misingi ya kumtegemea Bwana wetu Yesu Kristo, Ubarikiwe sana, kwa kuongeza maarifa zaidi juu ya NYOKA WA SHABA, karibu tujifunze hapa fuata link hii >> https://wingulamashahidi.org/2019/05/22/nehushtani-nyoka-wa-shaba/
JibuFuta