Inaumiza
kuwa katika pito gumu na unamtumaini Mungu kisha kumuona Yupo kimya, Ingawaje
wakati mwingine huongea ila hatuelewi ila kiukweli upo wakati anakuwa kimya
kama wakati ule wa Yesu pale msalabani.
Wengine
hujifariji kuwa alinyamza kwa sababu Yesu alikuwa amebeba dhambi na Mungu
hachangamani na wenye dhambi. Hoja hii kwangu ni dhaifu kwani kama aliweza
kuzungumza na Petro katikati ya dhambi yake ya kumkana Yesu kwa ishara ya jogoo
kuwika huku Yesu akimgeuki na kumkumbusha moyoni maneno yale ya kwamba kabla ya
jimbi kuwika atamkana, alishindwaje kunena na mwanaye aliyemtuma kwa kusui
hilo?
Ila katika
yote hayo haipaswi kukata tamaa ama kutafuta njia za mkato kama wengine
wafanyavyo baada ya hali kama hii.
Wapo walioamua kuolewa nje ya utaratibu
wakibibilia ama wengine kwenda kwa waganga kama Sauli ili kusaka utajiri ama
majibu fulani.
Nataka
ujifunze uvumilivu aliokuwa nao Ayubu, hakika mwanume huyu aliyeishi miaka
kadhaa iliyopia alikumbana na majaribu ya ajabu na kinachonipa kumshangaa Ayubu
ni pale alipoweza kustaimili ukimia wa Mungu kuanzia sura ya kwanza anapoanza kupatwa
na majaribu, Mungu hakunena lolote hadi sura ya 38. Na hapo anaanza na kumuhoji
maswali ila majibu yake yanatokea sura ya mwisho ya 42. Kisha Bwana akageuza
uteka wa Ayubu, hapo alipowaombea rafiki zake; Bwana akampa Ayubu mara mbili
kuliko hayo aliyokuwa nayo kwanza. Ayubu 42:10.
16
Kisha baada ya mambo hayo Ayubu akaishi miaka mia na arubaini, naye akawaona
wanawe, na wana wa wanawe, hata vizazi vinne. 17 Basi Ayubu akafa, mzee sana
mwenye kujawa siku.
Kumbe hata
Mungu akiwa kimya kwa kiasi gani inafika wakati anatujibu, ni kweli kwa Ayubu
ukimia huu haukuwa mwepesi kwake kwani ulimtesa kama anenavyo hapa. Ayubu 312:35 Laiti ningekuwa na mtu
wakunisikia! –Tazama sahihi yangu ni hii! Mwenyezi na anijibu!-Laiti ningekuwa na hayo mashitaka
yaliyoandikwa na adui yangu! 36 Hakika ningeyachukuwa mabegani ningejifunga
mfano wa kilemba; 37 ninge mwambia hesabu ya hatua zangu, ningemkaribia kama
vile mkuu.
Lakini
katika yote hayo Ayubu hakumtenda Mungu dhambi bali alimngoja yeye kwa saburi,
nataka kukuonyesha siri iliyopo kwenye saburi kama nilivyoifafanua kwenye
kitabu changu cha Namna ya kuishi wakati wa majaribu au mapito.
“Yakobo 1:2 Ndugu zangu hesabuni ya kuwa ni furaha tupu mkiangukia katika majaribu mbalimbali. 3 mkifahamau ya kwa kujaribiwa kwa
imani yenu huleta saburi.
Yamkini ulijiuliza kama mimi
saburi ni nini? 4 Saburi
na iwe na kazi kamilifu, mpate
kuwa wakamilifu na watimilifu bila kupungukiwa na neno.
Ona neno hili Saburi kwenye
kitabu kile cha Warumi 5:3 Wala sii
hivyo tu, ila na tufurai katika dhiki pia;
tukijua ya kuwa dhiki, kazi yake
ni kuleta saburi; 4 na kazi ya saburi
ni udhabiti ya moyo; na kazi ya udhabiti
wa moyo ni tumaini.
Saburi, inazaa, udhabiti wa
moyo ikiwa na maana ya uhodari au ushujaa ulio jawa na uvumilivu pamoja na
ujasiri, kisha inazaa tumaini. Na kitabu hiki cha
warumi
kimelielezea kama dhiki ila ufahamu dhiki ni aina ya pito au jaribu lenye
makali mno na mara nyingi huwakuta watumishi wa madhabauni na huwa ni jaribu la
muda mrefu huku likiwa na sifa ya upweke kijamii.”
Hiyo ni
nukuu iliyopo kwenye hicho kitabu, natumai imeona dhamani ya Uvumilivu aina ya
Saburi ambayo hukuwezesha kuvuka mahali pa gumu kama ilivyokuwa kwa Ayubu.
Ninakuletea
somo hili nikiwa ni shuhuda wa wahanga waliowai kukwama mahali kama hapa, Yupo
mtu mmoja ambaye alikuwa ni mtumishi wa Mungu na alilazwa hosipitalini kwa muda
fulani, aliombea wagonjwa wengine pale hosipitalini na walipona ila yeye bado
alikuwa amelazwa. Aliumia sana kwa Mungu kuponya wengine ila kumuacha yeye.
Mie mwenyewe
ni shuhuda miongoni mwa huu ushuhuda. Kuna kipindi nilikuwa kwenye hali ngumu
sana ya hitaji la fedha na cha ajabu nilikuwa nikiwaombea wengine ikiwemo ndugu
zangu walikuwa wakifanikiwa angali nikijiombea mimi ni kama Mungu anijibu na alikuwa
kimiya hadi kulazimika kuomba msaada kwao.
Nkimuliza
Mungu kuhusu mambo mengine hunijibu kwa haraka ila kuhusu uchumi yupo kimya. Na
hili limewakuta wapendwa wengi sana, kwani unakuta anahitaji fulani na
ameliombea kwa muda mrefu sana hadi kufikia hatua ya kuishiwa nguvu za kusonga
mbele na inafika wakati anajikaza tena na kuinuka kiroho ila bado Mungu Yu kimya.
Akiombea
mengine anajibiwa ila katika hilo ni kama Mungu amsikii. Inafika hatua mtu
anahitaji hata jibu la njia ya ndoto ila na hapo tena Mungu Yu kimiya. Baada ya
Ibrahimu kumpata Ishmaeli Mungu alikaa kimya bila kuzungumza nae kuhusu
kumpatia majibu yake kwa kipindi cha miaka 14, Alimpata Ishmaeli akiwa na miaka
86, Mwa16:15-15, na malaika
walipomletea majibu ya Isaka alikuwa na miaka 100, Mwa 17:17.
Hakikuwa
kipindi cha kawaida, bali ni kigumu, Yusufu mwana wa mzee Yakobo mara baada ya
kutafsiri zile ndoto mbili za mwokaji na mwenyeshaji mkuu alikaa gerezani tena
miaka 2 na hapo hatuoni mahali Mungu akizungumza naye. Fahamu bado hakikuwa
kipindi kizuri ama rahisi kwake.
Ila mara
baada ya majira ya watu hao kupita, Ibrahimu alimpokea Isaka wake na hatimaye
kuwa ni nderemo na kicheko, Yusufu alipokea mujiza wake na hatimaye kuwa ni
mwingi wa furaha kwa kutimiza maono.
Huo ndio wakati ninaotaka
uangaliye wewe kama mpendwa. Ni kweli leo upo gerezani ila tazama wakati Farao
akisema, Mwanzo 41:38 Frao akawaambia
watumwa wake, “Tupate wapi mtu kama huyu, mwenye roho ya Mungu ndani yake?” 39
Farao akamwambia Yusufu, “Kwa kuwa Mungu amekufahamisha hayo yote, hapana
mwenye akili na hekima kama wewe.
40 Basi wewe utakuwa
juu ya nyumba yangu, kwa neno lako
watu wangu watatawaliwa…”
Huo ndio
wakati wa kuutazama, usitazame wakati wa mke wa Potifa wakukusingizia na
kutupwa gerezani ama wakati wa mkuu wa wanyweshaji kukusahau angali ulimtedea
mema na amefanikiwa kwa mema yako.
Yamkini kuna
watu uliwasaidia maishani nao wamefanikiwa na kukuacha wewe ungali unatafuta
mpenyo, wewe mtazame Yesu atakuinulia Samweli wako atakayekupaka mafuta ama
Barinaba wako atakayekutambulisha kama ilivyokuwa kwa Paulo. Cha msingi ni
Uvumilivu wenye Saburi.
Baada ya
uvumilivu tuangaziye njia nyingine, Na hii ni ya maombi na utoaji sadaka.
Usikubali kukaa kimiya wakati ambao unamuona Mungu ni kama hakujibu ama asemi
na wewe na unauwakika ya kwamba haujatenda dhambi. Na kama ni dhambi rejea pale
awali kwenye sehemu ya kwanza ya makala hii, niliokutaka kumuomba Mungu rehema
na kufanya mengineyo kama ukimya huo ni matokeo ya dhambi.
Hana mara
baada ya kugundua kuwa Mungu alikuwa kimiya aliamua kumtolea Mungu sadaka ya
Nadhiri kwa mtoto wake. Kumbuka ukimya huu haumaanishi kuwa Mungu akusikii,
hapana! Anasikia maana Yeye sio kiziwi wala mtu ama mwadamu ndo asinziye. Ila
kuna jambo anataka ujifunze, Ufanye ama anakufundisha Saburi kwa kukutaka kuwa
nayo.
Fungua nami kitabu kile cha 1
Samweli, 1Samweli 1:11 Akaweka nadhiri, akasema “Ee Bwana wa
majeshi, ikiwa wewe utaliangalia teso la mjakazi wako, nakunikumbuka, wala
usinisahau mimi mjakazi wako, na kunipa mimi mjakazi wako mtoto mume, ndipo
mimi nitakapo mpa Bwana huyo mtoto siku zote za maisha yake, wala wembe
hautapita kichwani mwake”
Mungu hakuweza kunyamaza hata
kidogo,kwani mstari wa 20, Hana
anapokea muujiza wake na kusema “Ikawa,
wakati ulipowadia, Hana
akachukuwa mimba na kuzaa mtoto mwanamume; akamwita jina lake Samweli, akisema
“Kwa kuwa nimemuomba kwa Bwana”
Maombi na Sadaka
ya Nadhiri yalimfanya Mungu kunena na hatimaye kumpatia majibu yake Hana. Na
wewe usipoteze muda kwa kufadhaika bali hakikisha una mtafuta Mungu kwa viwango
hivyo vya maombi kwa kushinda hekaluni na kisha kumuwekea Mungu Sadaka ya
Nadhiri ama kutoa Sadaka nyingineyo ili kumfanya Mungu kushindwa kuendelea
kukaa kimya na kukutokea katika kona iliyo sahihi.
Natamani
kuendelea kunena nawe kuhusu jambo hili ila Muda wangu umekuwa kama ukuta nami
naogopo kushindana nao kwani wahenga walishanena kuwa nikifanya hivyo nitaumia.
Nakusihi niombee ili nipate kibali cha kuendelea na somo hili katika sehemu ya
tatu.
Pia usikose
somo jingine lenye mukutadha kama huu liitwalo, EPUKA KUYAFANYA HAYA PUNDE
UMUONAPO MUNGU YUPO KIMYA. Ni miye Mwalimu wako Osar Samba
Na Huduma ya
UKOMBOZI GOSPLE, Arusha Tanzania, Kwa maombi, Ushauri, Maswali au Sadaka
wasiliana nasi, Barua pepe: ukombozigosple@gmail.com
Simu: +255 759 859 287 pia waweza itumia kwa M-PESA. Zaidi www.ukombozigosple.blogspot.com #UkomboziGosple#MwalimuOscarSamba
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni