Na Mwalimu Oscar Samba #Ug Ministry |
Kwa furaha
isiyo na kifani wala uzani ninakukaribisha ndugu yangu katika Bwana wetu Kristo
kwenye safu hii ya makala za kiroho zenye dhima ya kukuinua kiroho, langu jina
ni Mwalimu Oscar mwana wa Flora Samba kipenzi cha Mzee Prospa.
Katika
makala hii sehemu ya kwanza nitakujuza athari ya maneno huku sehemu ya pili
nikikupa mbinu za kupambambana na silaha hii ya maneno yenye nguvu kuliko
bunduki ama mabomu yatengenezwayo na wanadamu.
Awali ya
kukuletea uhodo huo natamani nikujuze maana ya bonde la kukata maneno. Huu ni
ufunuo nilioupata na unamaanisha ya kwamba mtu yupo kwenye mazingira magumu ya
kiroho kivita huku hali hiyo ikiwa ni matokeo ya maneno mabaya anayosemwanayo
kutoka kwa watesi wake na nguvu ya vita hivyo ni ukaribu wa watu hao aidha
kimwili au kiroho.
Katika
kitabu changu cha NAMNA YA KUSIHI WAKATI WA MAJARIBU AU MAPITO nimelielezea kwa
kina jambo hili na mathara pamoja na Suluhu lake husani kwenye kipengele chenye
mukutadha wa kuchoka kiroho na maneno yakiwa ni kisababishi moja wapo.
Ninataka
ujione pamoja nami kipengele hicho;
Tutazame
maneno kama slaha ya uongo, Zaburi 144:8 Vinywa vyao vya sema
visivyofaa, na mkono wao wakuume ni mkono wa uongo.
Kwa hiyo mtu asemapo au anenapo
kusingizia jambo la uongo kwenye ulimwengu wa roho anapigana na wewe kutumia
mkono na kama ujuavyo mkono hukunja na kurusha ngumi, kofi hata kwenzi pamoja
na kushika silaha yoyote ile kwa hiyo usikubali kuchoshwa na jambo kama hili
bali wewe tumia Upanga wa Roho Mtakatifu ambao ni Neno la Mungu kuukata huo
mkono wa uongo na kukifunga hicho kinywa huku ukiomba kwa kutumia pia andiko
lile la Isaya 54:17. Ambalo hubatilisha kila silaha iliyokuinukia na
kuvihukumu hivyo vinywa vya uovu kuwa mkosa.
Kabla ya kutazama mifano ya
watu kwenye bibilia waliochoka kutokana na maneno, nataka ufahamu rasimi ya
kwamba maneno yanauwezo wa kupiga au kufanya kazi kama silaha, ndio maana
likanenwa hili;
Ayubu 5:21a Utafichwa na
mapigo ya ulimi..,Kwa hiyo Ulimu
hupiga na ukikupiga usipopambana au kuuzuia unakuchosha, ndiposa utamsikia mtu
akisema, “sifanyi tena huduma au
siendi tena kanisani maana wamenisema eti najipendea kwa Mchungaji, wamesema
mimi sijui kuimba?, siimbi tena, wamenijerui sana” Kama Nafsi yako
imejeruhiwa kwa njia hiyo, omba uponyaji kama Daudi, Zaburi 22:20a Uniponye
nafsi yangu na upanga…
Tutazame adhari zake kwa mifano
ndani ya Bibilia,Tumuone Daudi ambaye Nafsi yake inachoka kwa kuinama ikiwa ni
matokeo ya kusemwa na adui au watesi wake,
Zaburi 42:3 Machozi yangu yamekuwa chakula changu
mchana na usiku, pindi wanaponiambia mchanakutwa,
“Yuko wapi Mungu wako?”. Umeyaona
hayo maneno? (“Yuko wapi Mungu wako?”)
Tutazame kinachofwata,
4 Nayakumbuka hayo nikiweka wazi nafsi yangu ndani
yangu, jinsi nilivyokuwa nikienda na mkutano, na kuwaongoza nyumbani kwa Mungu,
kwa sauti ya furaha na kusifu, mkutano wa sikukuu.
Kwa hiyo hayo maneno yalikuja
kama silaha na kuipiga nafsi kama nilivyo kujuza hapo juu kwamba hupenda sana
kushambulia nafsi na Daudi mwanzoni mwamsitari huu analidhibitisha hili
anaposema,
“Nayakumbuka hayo nikiweka
wazi nafsi yangu ndani yangu” Sasa tutizame kilichotokea mara baada ya
nafsi yake kushambuliwa au kupigwa na maneno hayo yaliyonenwa “Yuko wapi
Mungu wako?” Mstari wa 5a Nafsi yangu kwa nini kuinama, na
kufadhaika ndani yangu? Kwa hiyo Nafsi inainama sababu kubwa ikiwa ni
Maneno ya watu ila Daudi anatafuta dawa yake na kujitaidi kujiponya kwa maneno
ya tumaini na faraja ambayo pia ni dawa sahihi na sala,
5b.Umtumaini Mungu kwa maana
nitakuja kumsifu, aliye afya ya uso wangu, na Mungu wangu.
Fahamu
kuwa anaposema uso anawakilisha moyo wake. Ka hiyo ukiondoa neno hilo na kuweka
hapo moyo mstari huo utasomeka hivi; “Umtumaini
Mungu kwa maana nitakuja kumsifu, aliye
afya ya moyo wangu, na Mungu wangu.”
Pia maneno yakikujia katika
mfumo wa Laumu, Laumu huja pale unapotenda kosa na watu kuishia
kukulalamikia au kukusema vibaya kutokana na kosa ulilolitenda huku dhamira yao
ikishindwa kukusaidia, na hujeruhi zaidi pale kosa linapokuwa dogo na kisha
mashutumu yakawa makubwa zaidi.Ama unapowaomba msamaha na kuitaji matengenezo,
kisha baada ya hapo wewe unasamehe kama nao walikutenda na unasahamu kosa ulilotendewa
maana pia umeshatengeneza na Mungu, kisha baada ya muda unawasikia wakitumia
jambo lile lile na kulifanya kama fimbo ya kukuchapia au kama silaha ya
kukudhoofisha ili uonekane una hatia au wao wapate ushindi kwa hatia ambayo
ulishaitubia ingawaje na wao ni wakosa katika hilo.
Ama pia mashutumu au laumu hiyo
yaweza kuelekezwa kwako pasipo kuwa na hatia, jambo hili huuvunja moyo na nafsi
pia na tiba yake ina muhitaji Yesu, hali hii huwa na maumivu zaidi kama
wakulaumuo ndio uliowategemea wangekuwa msaada kwako. Tumtazame tena Daudi
yalivyo msibu;
Zaburi 69:20 Laumu
imenivunja moyo, nami ninaugua sana, Nikangoja aje wa kunihurumia, wala
hakuna; na wakunifariji, wala sikumuona mtu.
Ni vyema kuifuta kumbukumbu ya
dhambi uliyoitenda kwenye ulimwengu wa roho, na kama ni masingizio, futa pia
kwa Damu ya Yesu.
Tumtazame Yeremia alivyodhurika
na silaha hii ya maneno, Yeremia
18:18 Hapo ndipo waliposema , “Njooni na tufanye mashauri juu ya
Yeremia,…..Njoni, natumpige kwa
ndimi zetu, wala tusiyaangaliye maneno yake yoyote.”
Kwa hiyo adui zake kwa makusudi
waliamua kuitumia silaha hii ili kujaribu kumdhofisha maana wanasema na tumpige
kwa ndimi yaani kwa maneno.
Tutazame kilichotokea mara badaa
ya mishale kurushwa: pinde hizo kupindwa na panga kutumika yaani maneno kama
silaha ya adui; Mstari wa 19.
Niangaliye, Ee Bwana, ukasikilize sauti ya wanao shidana nami. 20 Je, mabaya
yalipwe badala ya mema? Mana wameichimbia nafsi yangu shimo. Kumbuka
jinsi nilivyosimama mbele yako ili niseme mema kwa ajili yao, nikaigeuza
gadhabu yako isiwapate.
Pigo hilo linamfanya kulia, ila
uzuri wake alimlilia Mungu hakulia kama Daudi ambaye machozi yaligeuka kuwa
chakula chake mchana kwa usiku, hapo tunaona uwepo wa silaha nyingine ambayo ni
maneno kama shimo, kwa hiyo maneno pia huweza kukuchimbia shimo kwenye ulimwengu
wa roho hususani watakaposema “natuone
sasa kama atafanikiwa” au “hapa
atoboi” wakiwa na maana haufanikiwa ukifika hatua fulani.
Ndio maana ipo haja kubwa ya
kubatilisha au kufuta maneno ya adui zako kwa Damu ya Yesu, na maandiko mfano Isaya 54:17Kila silaha itakayofanyika
juu yako haitafanikiwa, na kila ulimi utakaokuinukia juu yako katika hukumu
utauhukumu kuwa mkosa…;
Na kama yana uhalali kwa dhambi
uliyoitenda au yoyote ile omba kwanza rehema kwa damu ya Yesu kisha yafute na
utayarike hizo silaha na kuhukumu vinywa vyao kuwa mkosa pamoja na kuondo
madhara yake rohoni.
Tunamuona Yeremia akiwa wazi ya
kwamba maneno hayo yameiadhiri nafsi yake kama nilivyokujuza hapo awali,
anaposema “Maana wameichimbia nafsi yangu shimo”. Pia
anaumizwa na yeye kutenda mema ikiwemo kuwaombea rehema adui zake na badala
yake kulipwa mabaya jambo ambalo hata Daudi kwenye hiyo Zaburi ya 42:4 analiliamikia.
Yamkini hata mimi na wewe
tunaposemwa na mtu ambaye tulimsaidia au kumuonyesha fadhili huwa tunaumia sana
ila mtazame Mungu na muone kama aliyetumumika na adui na pambanae rohoni maana
ukiziruhusu fikra kama hizo huta pambana na hatimaye nafsi yako italemewa kwa
majeraha na kuchoka hatimaye kuchukua maamuzi yasiyo sahihi.
Kumsema Mtumishi wa Mungu au
Mchungaji wako vibaya ni jambo la hatari sana maana wakati wowote hata bila
kujua anaweza kuomba ya kwamba Bwana apigane na wanaopiga naye na huenda hajui
uliwai kumsema, ukashangaa unakumbwa na mabaya bila kufahamu yalipotoka, na
wapendwa wengi wa leo hatujui kumuliza Mungu kwa nini hili limetokea; bali
likija baya sisi ni kukemea tukidhani limetoka kwa Shetani maana ndiko kutokako
kila lililo baya na likija jema hushangilia kwa mtazamo kwamba kila jema hutoka
kwa Mungu bila kufahamu ya kwamba ipo njia ionekanayo kuwa njema machoni petu
bali kwa Mungu ni laa!.
Pia kwa kufahamu anaweza
akaamua kuomba Maombi kama ya Yeremia hususa au kama jeraha lake ni kubwa na
uchungu ungali mifupani mwake au moyoni mwake na maombi hayo yakakupata bila
kujali Mungu alisema ombea mema adui zako na wale wanaokuudhi, tuone maombi
hayo ya Yeremia dhidi ya adui zake mara baada ya kuumizwa na maneno yao.
Tuendelee na kitabu hiki sura
hiyo ya 18: 21 Kwa sababu hiyo, watoe
watoto wao waone njaa, uwatoe nguvu za upanga ziwapige; wake zao wafiwe na
watoto wao, na kufiwa na waume zao, wanaume zao wauwawe, na vijana wao wapigwe
kwa upanga vitani.
22 Kilio na kisiwe kitokacho katika nyumba zao, hapo
utakapo leta kikosi juu yao kwa ghafula; kwa maana wamenichimbia shimo
waninase, nao wameifichia miguu yangu mitego.
23 Lakini wewe Bwana, unajua mashauri yao yote juu
yangu, yakuniua; usiwasamehe uovu wao, wala usifute dhambi yao mbele ya macho
yao .Bali wakwaze mbele zako; uwatende mambo wakati wa hasira yako.
Kwa muombezi
hayo sio maombi sahihi sana ila wewe epuka kusengenya ili usipatwe na hayo,
maana hata Musa aliposemwa hakuomba ila Mungu alishuka na kumuadhibu Haruni na
Miriamu, pia jiuluze kama Musa asinge waombea rehema au angeamua naye kuomba
kama Yeremia, nini kingalitokea? Ukitaka kupata picha ya kile ambacho
kingetokea nenda kasome kisa cha Korana, Dathani na Abiramu, Hesabu sura 16
hadi sura ya 17 (Hes 16-17), (Kwa kifupi walilambwa na moto baathi, na
wengine Mungu alipasua aridhi ikawameza na ikajifunga). Tusonge mbele na
sababu nyingine.
Hiyo sababu nyingine sitakuletea maana hiyo ilikuwa ni nukuu kutoka
hapo kitabuni na nililenga tu kipengele cha Maneno, kwa zaidi kitabu kikitoka
kitafute sokoni. Na ni yangu imani kuwa ujumbe huu umekupa nguvu na fahamu
zaidi katika safari hii ya kiroho. Ninakuaga katika jina la Bwana huku
nikikutaka kuendelea kufwatilia makala zangu.
Usikose
makala murwa na Mubashara kutoka hapa UG MINISTRY kesho itwayo, MAJIRA YA FARAO ASIYEMJUA YUSUFU.
Kama
hujaokoka na unataka kuokoka ama ulirudi nyuma kiroho na unataka kutengeneza na
BWANA kwa upya leo, tafadhali fwatisha nami maneno haya kwa Imani, Sema: BWANA
YESU, NINAKUPENDA, NINAKIRI NA KUAMINI MOYONI MWANGU KUWA WEWE NI MUNGU,
ULIKUFA NA KUFUFUKA KWA AJILI YANGU, INGIA NDANI YANGU KAMA BWANA NA MWOKOZI WA
MAISHA YANGU LEO, AMENI.
Hongera kwa
kuokoka na tafuta kanisa la watu waliokoka ukasali hapo.
Na Huduma ya
UKOMBOZI GOSPLE, Arusha Tanzania, Kwa Maombi, Ushauri, Maswali au Sadaka
wasiliana nasi, Barua pepe: ukombozigosple@gmail.com
Simu: +255 759 859 287 pia waweza itumia kwa M-PESA. Zaidi www.ukombozigosple.blogspot.com #UkomboziGosple #MwalimuOscarSamba
Pia #Like
#Penda Page/Ukurasa wetu au kundila Fb, ili kuupta habari hizi kwa haraka,
zaidi. Ug Ukombozi Gosple,
PAGE: https://www.facebook.com/Ug-Ukombozi-Gosple
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni