Na Mwalimu Oscar Samba #Ug Ministry |
Ni kweli
Maziwa na Asali ni Ahadi ya Mungu maishani mwako, lakini kabla ya kuuvuka mto
Yoridani, nilazima ukutane na bahari ya Shamu, Kisha ugumu wa jangwa.
Yesu
aliwaambia wanafunzi wake na tuvupe mpaka ng’ambo, lakini kabla ay kuvuka
walikumbana na dhoruba kali baharini, Upepo ambao uliwapa hofu kuu. Petro
alitamani kutembea juu ya maji ili
amfike alipo Yesu. Ila kabla ya kumkaribia wimbi lilifanyika kikwazo
kwake.
Nawe ni
kweli Mungu amekuaidia kukupa Mume/Mke, Nyumba, Kiwanja, Biashara nzuri, Huduma
yenye ukubwa wa matendo ya miujiza na ishara, Kibali cha huduma, Maisha bora ya
kiuchumi na Upako kwa ajili ya kazi yake. Na dalili ya kwamba amekupa ni ndoto
unazoota ukiwa unachuma matunda, za mafanikio kihuduma na zile za mapesa mengi.
Lakini kwa kweli maisha unayoishi ni kama hayasadifu
hayo uliyoaidiwa, kwani kila sehemu kumejaa vikwazo, Uchumi mgumu, milango ya
Baraka ni kama imefungwa, Ndoa imepoteza tumaini, Furaha maishani imepotea,
kila ndugu wa kiroho na kimwili ni kama vile amekusahau. Watoto wanasoma na
kula kwa shida yamkini hata kodi ya nyumba kulipa ni matatizo.
Nisikilize
nikumegee siri ya hayo: Ahadi ya MUNGU maishani ni lazima itimiye, ila kabla
haijatimia hunabudi kuandaliwa kwa ajili ya kukuwezesha kuimudu hiyo ahadi, yaani Mungu hukupa maarifa katika
hilo jambo na akili ili mafanikio hayo yasije kukutoa kwa Mungu.
Kwa lugha
rahisi ni kwamba mapito unayoyapitia ni shule na majaribu hayo ni mtihani na
punde utakapo faulu ndiposa utakapopewa hiyo ahadi. Ndio maana kuna wakati
unaota ndoto upo darasani ikiwa ni ishara ya kwamba MUNGU anakufundisha. Kwa
hiyo usikimbiye hayo mapito kwani kama wanafunzi wa Yesu wangali kimbia kwenye
boti wasingeweza kufika ng’ambo. Na wana wa Iziraeli wale waliyoyachukiwa
maisha ya jangwani walifia hapo na kushindwa kuifikia Kanani yao.
Pia wakati
mwingine maisha hayo huwa ni matokeo ya vita kutoka kwa Shetani ambaye
huviachilia kwa shabaha ya kukukwamisha. Katika hali hii yakupasa sana kuwa
muombaji na sio mnung’unikaji. Unatakiwa kuhakikisha unafanya maombi ya vita, na
ya ulinzi pamoja na yale ya kuondoa vikwazo barabarani ili kumshinda adui
aliyepanga kukumeza.
Pia
unatakapo kutana na ugumu wo wote ule unatatikana kuwa mwepesi wa kumwendea
YESU na sio wanadamu ama kunung’unika kama baathi ya wana wa Iziraeli. Iga sana
tabia za Musa, Yoshua na Kelebu katika safari yako ya kuivuka Yoridani na
hatimaye kuingia ng’ambo ya pili. Kumbuka ng’ambo uliyopo ni ya Misiri ama
jangwani na kiu yako ni ukiingia ile ya Kanani.
Usikubali
kuacha hata ukwato Misiri ama jangwani, bali nenda na kila kilicho chako.
Wengine wanaacha vitu vyao. Kwa mfano, unakuta mtu ana mafanikio kiuchumi na
kiriho, maana yake katika hiyo yupo Kanani ya kiuchumi na kiroho ila ndoa yake
ina migogoro toka awali ile isiyoisha. Maana yake ameenda kanani na kufika
akiwa na uchumi na kiroho ila ameacha ndoa yake Misiri ama imekwama jangwani.
Nina maana
wakati unaombea maisha yako, usibaguwe baathi ya vitu na kuviona hivyo vina dhamani
zaidi ama kuona matatizo mengine ni kama vile hayana tiba, bali ombea yote na
beba vyote ili ufike ng’ambo ya Yoridani salama.
Tutafiti
maandiko haya ili kujionea tabia ile ya Musa ya kumlilia Mungu kwa haraka
anapokuwa na matatizo. Tuanze kwa kuchunguza mawazo au mtazamo ambao unapaswa
kuuepuka.
Kutoka 14:11 Wakamwambia Musa, “Je, kwa
sababu hapakuwa na makaburi katika
Misiri umetutoa huko ili tufe jangwani?
Mbona umetutenda haya, kututoa katika nchi ya Misiri? 12 Neno hili silo tulilokwambia huko Misiri, tukisema
‘Tuache tuwatumikiye wamisiri?’ Maana ni afadhali kuwatumikia Wamisiri kuliko
kufa jangwani”
Na yakupasa
uwe na mtazamo huu, ambao unaona njia pasipokuwa na njia.
Kutoka 14:13 Musa akawaambia watu, “Msiogope! Simameni
tu, mkauone wokovu wa Bwana atakao wafanyia leo; kwa maana hao Wamisiri
mliowaona leo hamtawaona tena milele.14 Bwana atawapigania ninyi, nanyi
mtanyamaza kimiya”
Ndivyo
unavyopaswa kutazama vikwazo vilivyopo mbele yako katika safari yako ya Maziwa na Asali. Kwani wasomaji
wa maandiko wanafahamu mara baada ya mtazamo huo wa Musa Mungu alimtumia
kuigawa Bahabari ya Shamu nayo ilitii na kuwagwanyika kisha wana wa Iziraeli wakavuka
na mbele wanaanza kuimba wimbo wa Musa uliojawa na Ushindi tele.
Unaonaje
kama Musa angalikuwa na matazamo kama huo wa wana wa Waebrania? .. Na wewe ukiendelea kutazama vikwazo kwa
namna hiyo ya kushindwa, je, wanao ama washirika wako au jamaa yako itaishi
maisha gani baadae? Ni kweli mtafika ng’ambo ya Yorida?
Mtazamo
mwingine, Ni pale Masa walipokosa maji. Kutoa
17:2 Kwa hiyo hao watu wakateta na Musa, wakasema “Tupe maji tunywe!” Musa
akawaambia kwanini kuteta na mimi ? Mbona
mnanijaribu ? 3 Watu wakawa na kiu huko; nao wakamnung’unikia Musa, wakisema, “Mbona
umetupandisha kutoka Misiri ili kutuua sisi na watoto wetu na wanyama wetu kwa
kiu?”
Musa kama kawaida yake alimlilia Mungu na
Mungu ukimlilia huwa hanyamazi kimia bali hufanya jambo.
Songa nami
hadi mstari wa 6, Tazama, nitasimama mbele yako huko, juu ya lile jabali katika
Horebu; nawe utalipiga jabali, na maji yatatoka, watu wapate kunywa.” Musa
akafanya hivyo mbele ya wazee wa Isiraeli.
Baada ya
hapo Mungu aliufanya mwamba kutoa maji, kumbuka sio udongo wala changarawe bali
ni mwaba ama jabali lilitoa maji, Mungu hakutaka kutoa maji chini ya mti ama
kando ya jiwe kubwa bali alitaka jiwe gumu liwatolee maji ili wajuwe ya kwamba
Mungu huyu ni Mungu wa mambo makubwa. Na wewe hayo mapito yaliyokuwa magumu ni
mahali ambapo Mungu anataka ajitwaliye Utukufu ili kila mwenye mwili ajuwe ya
kwamba Mungu wako ni Mungu wa mambo magumu, ila wewe uwe na mtazamo kama wa
Musa.
Wakati
wengine wanasema ya kwamba hapana njia wewe ona njia, wakati wengine wanaona ni
mwamba wewe ona maji ndani yake.
Nina kiu na
shauku yakuendelea nawe kama Ayala anavyoyaonea shahuku maji ya mtoa, ambaye
wanatheolojia wanasema ni aina ya mnyama aliyeishi zamani na alikuwa na tatizo
la kiu ama alikuwa ni mwenye kiu isiyoisha na akiyapata maji huyabugia kwa
kiwango kikubwa ila punde kiu ile humrejea akitoka majini.
Nami ndivyo
ninavyowiwa ndani mwangu kushinda nawe nikikujuza siri zilizopo ndani ya Biblia
ila sina budi kuishia hapa, tukutane tena kesho panapo majaliwa ya MOLA, nitakapo
kuwa nikiendelea na makala hii katika sehemu ya pili na hapo nitaanza na mfano
wa Dhoruba ziwani kwa wanafunzi wa Yesu na kukupa mbinu teule zitakazo
kuwezesha kuvuka jangwani ama kwenye mawimbi salama huku kesho kutwa nikikupa
KIGONGO ama MANA nyingine itwayo, YESU KAMA MTULIZA MAWIMBI AU DHORUBA. Ni
kweli mapito magumu yapo ila yupo Mwanamume aliyelala kwenye Sherti na wewe
muendee Yeye ukimwamsha kama wanafunzi wake ili atulize hayo mawimbi makali
kwenye ndoa yako ama kwenye uchumia au kwenye hiyo huduma. Pia hata upepo
anatuliza huyu MWANAMUME WA AJABU KWELI KWELI.Langu jina ni OSCAR PROSPA mwana
wa Flora na Mzee SAMBA. Mutu ya MUNGU kutoka Arusha Tanzania.
Kama
hujaokoka na unataka kuokoa tafadhali fwatisha nami maneno haya kwa Imani,
Sema: BWANA YESU, NINAKUPENDA, NINAKIRI NA KAUMINI KUWA WEWE NI MUNGU, ULIKUFA
NA KUFUFUKA KWA AJILI YANGU, INGIA NDANI YANGU KAMA BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA
YANGU LEO, AMENI.
Hongera kwa
kuokoka na tafuta kanisa la watu waliokoka ukasali hapa.
Na Huduma ya
UKOMBOZI GOSPLE, Arusha Tanzania, Kwa Maombi, Ushauri, Maswali au Sadaka
wasiliana nasi, Barua pepe: ukombozigosple@gmail.com
Simu: +255 759 859 287 pia waweza itumia kwa M-PESA. Zaidi www.ukombozigosple.blogspot.com #UkomboziGosple #MwalimuOscarSamba
Pia #Like
#Penda Page/Ukurasa wetu au kundila Fb, ili kuupta habari hizi kwa haraka,
zaidi. Ug Ukombozi Gosple,
PAGE: https://www.facebook.com/Ug-Ukombozi-Gosple
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni