Na Mwalimu Oscar Samba #UgMinistry |
Ila yapo
majira ya mambo hayo kukoma, na ndiposa Yesu pale msalabani akasema IMEKWISHA,
na Mungu akawaambia wana wa Iziraeli wakati wanazunguka ile milima ya Seiri
yakwamba YATOSHA. “Mlivyouzunguka
mlima huu yatosha; geukeni
upande wa kasikazini.” Ni Torati
1:2.
Na wewe
imetosha sasa kuteseka kulala njaa, Nasema imetosha kulialia kwani majira ya
furaha yako yamekwisha kutimia. Kwa waliyokosa watoto kwa muda mrefu ninaachilia
Neno la kinabii kwao ya kwamba majira kama haya mwakani watapakata wana na kama
ilivyokuwa mwisho wa machozi ya Hana kwa kumpata Samweli na kwao itoshe hivyo.
Hana
aliteseka ila mateso yake yalikoma kwa Bwana kumpatia kitulizo cha moyo wake.
Umechumbiwa na kuachwa kila uchwao ila wakati huu pokea neno hili litokalo
katika kinywa na kudhibitishwa na mikono ya Mtumishi wa Mungu aliye hai ya
kwamba majira ya kuowa ama kuolewa kwako yamekaribia na punde BWANA atakutokea
wewe anza kuanda rangi ya nguo ya “Send-off” na arusi bila kusahau pozi la siku
ya pete.
Wewe ni
mwana wa Mfalume tena atawalaye kwa haki na kwa mamlaka, kwa hiyo huna tena
haja ya kuishi kama jogoo wa mjini aliyenyeshewa na mvua kwa kujikunyata ama
kujiona huu mnyonge kifikra bali anza kuruka ruka kama ndama wa mazizini kwani
IMETOSHA KWA KUSOTA KWAKO BILA KAZI.
Mungu wetu
anasema ya kwamba imetosha. Mwanaume Yesu walimkamata kwa dharau na kuvunjiwa
heshima kama mwivi ama mnyanganyi katika majira ya kuteseka kwake, wakamtesa
kwa kumpiga mijeleji, mate akatemewa, mavazi ya aibu na kejeli akavikwa,
Alidhiakiwa Yesu, alipigwa bila hatia.
Alibaguliwa,
walimuona Banaba mwizi na jambazi kuwa na haki kuliko huyu Mwebrania aliyekuwa
mpole uso na mnyenyekevu wa moyo, mweye fikra za utulivu kama mwanakondoo apelekwaye machinjoni ama
atuliavyo wakati wa kukatwa manyoya.
Maneno ya
kebei ndiyo yaliyokuwa chakula chake, hata mwizi aliyesulubiwa naye alimnenea
mabaya.
Ila atukuzwe
Mungu BABA Duniani na juu mbinguni ajuaye kuyapitisha majira ya uaribifu na
mateso kwa kasi ya ajabu. Kwani kufumba na kufumbua KIDUME Huyu anayeukosha
moyo wangu alishida na hatimaye kuketi mahali pa juu palipo inuka sana horofa
za wanadamu.
Kubwa yake
ni KITIMU TIMU siku ile ya tatu pale mjini Galilaya alipowatangulia, Sio hapo
tuu bali katika Iziraeli yote na Ulimwengu, zilivuma habari na sio zile za
mateso na aibu bali ni zile za USHINDI.
Aliteseka
kweli ila majira yalipofika, alisema; “IMEKWISHA,” Na kuanzia hapo kila mwenye mwili
alitambua kuwa mtu huyu alikuwa ni mwenye haki, na mimi na wewe tuseme wote kwa
IMNAI iliyo KUU ya kwamba; “IMEKWISHA.”
Maana yake YATOSHA sasa, Neno hilo linakaribisha ukurasa mpya wa Mafanikio na
Ushindi uliyopo kwenye kitabu cha FANIKIWA KIMUNGU huku mwandishi wake akiwa ni
YESU mwenyewe na amekuandikia yaliyo mema sasa kazi ni kwako kuamini pamoja nami
ya kwamba. Kuzunguka mlima ama milima ya Seiri kumefika mwisho ama kulizunguka
jangwa kwa Muda wa miaka arobaini kumekoma kwani mwaka huu ndio wa kuivuka
Yoridani na kuingia Kanani.
Ninakutakia
kila la heri katika maisha hayo mapya ya Kanani mpendwa mwenzangu katika Bwna
Yesu ila taadhari yangu ni kukutaka usisahau yale uliyofundishwa na kuonywa na
Bwana katika jangwa kwenye kitabu kile cha Torati wala usilialifu Agano lake
ili yasije kukupata mabaya na wala usiseme ya kwamba ni akili zako ndizo
zimekupatia utajiri huo.
Kumbukumbu la Torati 8:17
Hapo usiseme moyoni mwako, ‘Nguvu zangu na uwezo wa mikono yangu ndivyo
vilivyonipatia utajiri huo.’ 18 Bali utamkumbuka Bwana Mungu wako, maana ndiye
akupaye nguvu za kupata utajiri, ili alifanye imara agano lake alilowapa
baba zako, kama hivi leo.
Ona lakini
hii, Tujongee hadi mstari ule wa kumi na
tisa. 19 Lakini itakuwa, kama ukimsahau Bwana, Mungu wako, na kuiandama miungu
mingine, na kuitumikia na kuiabudu, nawashuhudia leo yakuwa mtaangamia bila
shaka.
Kila la heri
na Mola wangu akuepushie kila la Shari na Fanikiwa kama Mtende uliopandwa kando
ya Mto. Miye ni Mwalimu wa Neno la Mungu Mwl. Oscar Samba wa Huduma ya Ug.
Kama
hujaokoka na unataka kuokoa ama ulirudi nyuma kiroho na unataka kutengeneza na
BWANA kwa upya leo, tafadhali fwatisha nami maneno haya kwa Imani, Sema: BWANA
YESU, NINAKUPENDA, NINAKIRI NA KAUMINI KUWA WEWE NI MUNGU, ULIKUFA NA KUFUFUKA
KWA AJILI YANGU, INGIA NDANI YANGU KAMA BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YANGU LEO,
AMENI.
Hongera kwa
kuokoka na tafuta kanisa la watu waliokoka ukasali hapo.
Na Huduma ya
UKOMBOZI GOSPLE, Arusha Tanzania, Kwa Maombi, Ushauri, Maswali au Sadaka
wasiliana nasi, Barua pepe: ukombozigosple@gmail.com
Simu: +255 759 859 287 pia waweza itumia kwa M-PESA. Zaidi www.ukombozigosple.blogspot.com #UkomboziGosple #MwalimuOscarSamba
Pia #Like
#Penda Page/Ukurasa wetu au kundila Fb, ili kuupta habari hizi kwa haraka,
zaidi. Ug Ukombozi Gosple,
PAGE: https://www.facebook.com/Ug-Ukombozi-Gosple
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni