Na Mwalimu Oscar Samba |
Ndugu yangu mpendwa katika Bwana ninakutaka kutokukata tamaa
na maisha ya wokovu, kwani haijalishi ni jambo gani unalolipitia, mbele upo
ushindi.
Wana wa Iziraeli walisafiri kutoka nchi ya utumwa ya mateso ya Misiri ili kuelekea nchi ya Maziwa na Asali kama Bwana alivyo waaidia, ila iliwalazimu kupita jangwani. Haikuwa safari nyepesi kutokana na ugumu na manthari ya Jangwa.
Ila wale walioshinda walifanikiwa kuingia Kanani na hatimaye kuyaishi maisha yale ambayo Mungu aliwaaidia. Na wewe yakupasa kushinda.

Kumbuka Yesu alishatutathararisha hapo awali kuhusu ugumu wa safari tuliyonayo.
Mathayo 24:9 Na wakati huo watawasaliti ninyi mpate dhiki, nao watawauwa; ninyi mtakuwa watu wakuchukiwa na mataifa yote kwa ajili ya jina langu.
13 Lakini mwenye kuvumilia hata mwisho, ndiye atakaye okoka. Shinda Ndugu yangu.
Ayubu naye alishinda, ingawaje alipita katika dhiki ngumu kama anavyosema hapa; Ayubu 7:2 Kama mtumishi atamaniye hicho kivuli, kama mwajiriwa anayetazamia mshahara wake, 3 ni vivyo nami nimepewa miezi ya ubatili iwe fungu langu, nami nimeandikiwa masiku yenye kuchokesha.
Baada ya dhiki ni faraja, Ayubu 42:10 Kisha Bwana akaugeuza uteka wa Ayubu hapo alipowa ombea rafiki zake; Bwana naye akampa Ayubu mara mbili kuliko hayo aliyokuwa nayo kwanza.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni