Kijana mmoja
akasema, “Sitowi tena sadaka maana kila nikitoa ndo kama matatizo yanaongezeka”
Wengine
wameanguka kwenye uzizi na uasherati huku sababu ikiwa ni kumuona Mungu kama
awasikii ama amechelewa kuwaletea majibu yao, aidha ya kuolewa ama mtoto.
Sarai akamwambia Abrahamu/Ibrahimu, “Basi sasa, Bwana amenifunga tumbo nisizae,
umwingiliye mjakazi wangu, labla nitapata uzao kwa yeye.” Abrahamu akaisikiliza
Sauti ya Sarai. Mwanzo 16:2.
Baada ya
hapo kilichofwata ni Ibrahimu kuzaa na kijakazi huyo wa bibi Sarai na hatimaye
kumpata Ishmaeli ambaye
kimaandiko hakuwa mrithi maana mrithi alipaswa kuwa
Isaka. Kumuona Mungu amechelewa ama yupo kimya kulimfanya Sarai kuchukuwa
maamuzi yasio sahihi na kumshawishi mumewe kutenda jambo ambalo halikuwa mapezi
makamilifu ya Mungu.
Nawe nakutaka
kuwa mwenye subira wala usikubli kutenda kama hayo maana utendaji huo
utakufanya kuziepuka Baraka za Mungu wako ama kukupa mathara makubwa sana
kiroho. Kumbuka ukimya wa Mungu sio wa milele ama wa kudumu, ama unapomuona
Mungu amekawia haimaanishi kuwa hatakujibu, Bali fahamu kuwa atakujibu na
majira yake yamkini yamekaribia na ulipotoka ni mbali kuliko unakotazamia
kwenda. Wakati Ibrahimu anampata Ishmaeli alikuwa na mika 86, ikiwa bado miaka
14 ili ampate Isaka. Jaribu kufikiria ya kwamba amevumilia miaka mingapi ? na
imesalia miaka mingapi mbeleni?
Nani ajuaye
ya kwamba kwako zimebaki siku chache, ama masaa machache ilikuifikia mema yako.
Yesu pale msalabani wakati analalama ya kwamba Mungu wake mbona amemwacha, alikuwa
amebakisha dakika ama sekunde chache akaketi na baba yake katika mkono waka wa kuume.
Na kwako yamkini ni sekunde zimesalia ama hata sekunde hazifiki.
Kitu
kingine, Epuka kunena maneno ya kufurua ama ya kwazayo au yasiyofaa mbele za
Bwana au Wivu. Tuone kisa hiki kimaandiko. Mwanzo
30:1 Naye Raheli alipoona ya kuwa
hamzalii Yakobo mwana, Raheli alimwonea ndugu yake wivu. Akamwambia Yakobo,
“Nipe wana; kama sivyo, nitakufa mimi.”
Jambo hili halikuwa jema machono pa Yakobo, 2 Yakobo akamgadhabikia Raeli.
Akasema, “Je, mimi ni badala ya Mungu, aliyekuzuilia uzao wa mimba?”
Hii yote
ilikuwa ni matokeo ya yeye kukosa majibu yake kutoka kwa Mungu kwa muda mrefu.
Unaweza kuniuliza, Mwalimu angalifanyaje? Rejea makala zangu mwenza za “MUNGU ANAPOKUWA
KIMYA FANYA YA FWATAYO”.
Lakini pia
tuangaziye alichokifanya baba mkwe wake na mama mkwe wake walipokosa nao mtoto,
ambapo njia hii ndiyo iliyomfanya Mungu kumpatia Yakobo mumewe anayemnenea
yasiofaa kutokana na uvumilivu kupungua ama waswahili husema kuwa “ziro (0)”.
Walifanya
hivi, Isaka akamwomba Bwana kwa ajili ya mke wake, maana alikuwa tasa. Naye
Bwana akamwitikia, na Rebeka mkewe akachukuwa mimba. Mwanzo 25:21.
Kumbuka
walikosa watoto kwa muda wa miaka takiribani 20, Maana walioana na Isaka akiwa
na mika 40, Na Kujibiwa, Isaka akiwa na miaka 60. Nawe fanya hivyo na usichoke
kumlilia Bwana.
Jambo
jingine la kuepuka ni Manung’uniko, hali hii ni hatari sana katika maisha ya
kiroho maana humfanya Mungu kugadhabika na kukuathibu. Katika kitabu kile cha
Hesabu 11, Wana wa Iziraeli walifanya kosa hili na Mungu aliwaadhibu kwa kuwapa
nyama za kware zilizowatokea puani. Katika Hesabu pia 13, na 14 Mungu
aliwakasirikia baada ya kuzikubali taarifa za kukatisha tamaa na kuingiwa na
roho hii ya manung’uniko hali iliyowafanya kushindwa kuifikia Kanani yao.
Ni kweli waliiona safari ni ndefu
ya kufika kanani ila hawakupaswa kunung’unika. Pia katika kitabu hicho cha
Hesabu 21, utaona jinsi Mungu alivyowaangamiza kwa nyoka ya moto kwa sababu ya
jambo hili.
Hesabu 21:4 Wakasafiri
kutoka mlima wa Hori kwa njia ya Bahari ya Shamu, ili kuizunguka nchi ya Edomu;
watu wakafa Moyo kwa sababu ya ile Njia.
5 Watu wakamnung’unkia Mungu
na Musa “mbona mmetupandisha kutoka nchi ya Misiri, ili tufe jangwani? Maana
hapa hakuna chakula, wala maji na roho zetu zinakinai chakula hiki dhaifu”
6 Bwana akatuma nyoka za moto kati ya watu, wakawauma
watu wengi wakafa.
Epuka
jambo hili la manung’uniko ili kuwa salama. Wakati Mungu ananipitisha katika
maandiko haya nilimuliza jambo la ajabu sana na kumshangaa maana nilitazamia
kuwahurumia kwa kuto kuwaadhibu kwa makali haya kwani walikuwa katika hali ya
kuchoka kiroho.
Ila Mungu huwa na desturi ya kutoa adhabu kwa
dhambi kama hii na haijalishi unapitia ugumu mkubwa kiasi gani bali hawezi
kukuacha salama kama utafanya kosa hili. Soma kuanzia mwanzo hadi Ufunuo
ukitafuta madhara ya kosa hili na mtaji wako mkubwa uwe ni safari ya wana wa
Iziraeli.
Usiache
kutenda mema, Wagalatia 6: 9 Tena tusichoke
katika kutena mema; maana tutavuna kwa
wakati wake, tusipozimia roho..
Kuna
watu wameacha kabisa kutoa sadaka kwa madai ya kwamba Mungu amechelewa
kuwabariki ama amekaa kimya, na wanapotoa wanaona ni kama hali ndo inazidi kuwa
ngumu zaidi kimaisha. Mtazamo huu huwafanya kuacha kutenda mema na badala yake
huleta kuzimia roho na mathara yake ni kutokuvuna kwa wakati na mara nyingine
kuto kuvuna kabisa.
Unapofanya
maombi ama kusoma Neno au kujisogeza mbele za Mungu kwa kuutafuta uso wake na
kisha kuona kama Mungu hakujibu, fahamu fika ya kwamba hupaswi kuacha kutenda
hilo jambo jema kwa kuwa na matazamo ya kwamba Mungu yupo kimya au kumuona kama
hana dhamira ya kukupa majibu yako.
Mungu
wetu husikia yale tumuombayo kwani ni Mungu aliyekaribu sana nasi. Yeremia
23:23 “Mimi ni Mungu niliyekaribu, asema
Bwana, mimi si Mungu aliye mbali.
Na
kukumbusha tena ya kwamba ukimya wa Mungu sio kwamba hakusikii bali anasubiri
majira yake ya kunena kama ilivyokuwa kwa Ayubu, ama anakuhitaji ufanye jambo
fulani kama kwa Hana aliyeomba na kutoa na Sadaka ya Nadhiri. Ama ni Ishara ya
kukuandalia mapokezi mema kama ilivyokuwa kwa Yesu.
Mungu
akitujalia tutaendelea na makala hii siku yoyote ile panapo majaliwa yake, Miye
ni mwalimu wa Neno la Mungu; Mwalimu Oscar Samba.
Na Huduma ya
UKOMBOZI GOSPLE, Arusha Tanzania, Kwa maombi, Ushauri, Maswali au Sadaka
wasiliana nasi, Barua pepe: ukombozigosple@gmail.com
Simu: +255 759 859 287 pia waweza itumia kwa M-PESA. Zaidi www.ukombozigosple.blogspot.com #UkomboziGosple#MwalimuOscarSamba
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni