Na Mwalimu Oscar Samba Ug Ministry |
Wakati Dada
yake Lazaro anasema, Lazaro amekufa na
ni siku ya nne sasa, na kunuka ananuka, Jemedari YESU anasema, “Lazaro ajafa
bali amelala.” Na kumtaka dada huyu amini tu, ili mujiza utendeke.
Na kwako
wakati wanasema kuwa, ndoa yako, imekufa,Uchumi wako umedidimia, Eti ndoto zako
za kuwa mbunge, kiongozi, msomi ama dakitari na hata zile za kuwa na huduma
kubwa zimekufa, mimi ninakwambia kwa jina la Yesu aliye hai hazijafa bali
zimelala tu, na siku ya leo zitaamka kama Lazaro na kijana walivyo fufuliwa.
Ni kweli
katika macho ya nyama Lazaro na kijana walikuwa wamekufa, ila YESU aliye bingwa
wakufufua vitu vilivyokufa kwa kuvipa uhai alitazama kwa macho ya ndani na
aliona uhai wa watu hawa, kama alivyotazama mifupa ile mikavu kipindi kile cha
Nabii Ezekieli.
Yamkini bado
tatizo lako halijaonja mauti ila linaumwa, Nina kuhakikishia kuwa ugonjwa huo
sio wa mauti bali ni ili Mungu atukuzwe kwa mgogoro huo wa ndoa, ama uchumi
wako kuporomoka ama wewe kusimamishwa kazi, ili baadaye wamtukuze Mungu wako.
Yohana 11:Naye Yesu
aliposikia, alisema “Ugonjwa huu sio wa mauti, bali ni kwa ajili ya utukufu wa
Mungu, ili mwana wa Mungu atukuzwe kwa huo”
Na yamkini
unasema moyoni mwako ya kwamba Mwalimu Oscar ni mwezi wa tatu saa ama miaka
toka mume/mke wangu aondoke nyumbani, au toka nifukuzwe kazi ama biashara yangu
idode. Ninakwambia kama Yesu,
Yohana 11:11 Aliyasema
hayo; kisha, baada ya hayo, akawaaambia, “Rafiki yetu Lazaro amelala; lakini
ninakwenda nipate kumwamsha”
Usiwe kama
wanafunzi wa Yesu waliotazama mambo kimwili kwa kuzania ya kwamba amelala kweli
kimwili ila Yesu alinena kuhusu kufa kimwili na kwa macho ya rohoni aliona kulala.
Ikiwa ni kauli dhabiti ya Imani yake.
Tudodose
kwenye mstari unaofwatia jambo hili, 12 Basi wale wanafunzi wakamwambia, “Bwana ,
ikiwa amelala, atapona” 13 Lakini Yesu alikuwa amenena habari ya mauti yake;
nao walizani amenena habari ya kulala usingizi. Mstari wa 14 aliwaambia
wazi wazi kuwa Lazaro amekufa.
Pia usiwe na
mtazamo kama huu wakutaka kufa na Lazaro, nikiwa na maana kama ndoa ama uchumi
au hilo jambo lako limekufa na wewe unataka ufe kiro, yaani kukata tamaa kuacha
kabisa wokovu kwa sababu ya pito lako. Usikubali kuwa kama waliopoteza tumaini
maana unapaswa kuamini tu.
Msikilize
Tomaso wakati anawakilisha fikra za wenzake, “16 Basi, Tomaso aitwaye pacha,
akawaambia wanafunzi wenzake, ‘twendeni na sisi ili tufe pamoja naye.”
Baada ya
Yesu kwenda kwa Marehemu Lazaro dada yake aitwaye Martha alianza kumlaumu Yesu
ya kwamba kama angalikuwapo kaka yake asingali kufa. Dada huyu alitambua na
kuamini uweza wa Yesu wa kumponya Lazaro kwa haraka ila imani hiyo haikwenda hadi kwenye kuweza
kumfufua nduguye. Ndiposa Yesu analazimika kuanza kumjengea Imani ili mujiza
utendeke.
Ila dada
huyu hakuwapungukiwa kiasi cha kutokuamini kabisa, bali aliamini Yesu bado
anaweza yote, na kabla ya kuona jitiada za Yesu za kumjengea imani tuone kwanza
kiwango cha imani yake na uwelewa wake kuhusu uwezo wa ufufuo wa Yesu.
22 Lakini hata sasa najua
ya kwamba yoyote utakayomuomba Mungu, Mungu atakupa.
Yesu akasonga
mbele zaidi kwa kumwambia habri za kufufuka kwa nduguye na ona hapa fikra zake.
24
Matha akamwambia, “Najua ya kuwa atafufuka katika ufufuo siku ya mwisho.”
Mawazo kama
hayo nataka yakutoke kwenye fikra zako maana siku ya mujiza wako ni leo, na
hapa sineni habari za kutajirishwa mbinguni wala kupewa afya peponi ila ninanena
habari za kupokea ufufuo kwenye tatizo lako majira haya. Na kama ni mtoto
mwakani majira kama haya upakate mwana. Alikadhalika kama ni ndoa ama kuolewa
ama kuoa majira kama haya mwakani uitwe bibi ama bwana fulani.
Nimekwisha
kukujengea imani na wewe sasa amini tu, na tuone jinsi Yesu alivyoanza
kumjengea Martha imani mpya kuhusu ufufuo maana alimwamini Yesu kweli ila sio
katika jambo kama hii, Na wewe ni kweli yamkini unamwamini Yesu lakini sio
katika jambo kama hilo.
25 Yesu akamwambia, “Mimi
ndimi huo ufufuo na uzima. Yeye aniaminiye mimi, ajapokufa atakuwa anaishi”
Baada ya msingi huo unaonyesha pia asiyeamini
atakufa kwa mstari wa mbele yake, Yesu anataka kujua kama somo lake limeingia
kichwani kwa kumuliza hili swali.
26… Je, unayasadiki
hayo?
Na mimi ni
swali langu kwako leo, Je, unayaamini haya ninayo kwambia kuwa majira kama haya
mwakani utapakata mwana? Ya kwamba mume/mkeo atarejea nyumani tena mwenyewe
bila kuitwa? Au walio kufukuza kazi watakutafuta siku chache zijazo na kukuri
kuwa bila wewe ofisi haiendi?
Je,
Unasadiki pamoja nami kuwa waliokudharau na kukutenga kihuduma kanisani kwako
dakika chache zijazo watakutafuta nakukwambia tumpate wapi mtu kama wewe ambaye
roho ya miungu watakatifu wanakaa ndani yako, ama kwa kuwa Mungu amekupa akili
na maarifa na hekima namna hii basi utakuwa mkuu katika Misiri yote kama Farao
kwa Yusufu ama Nebukadreza kwa Belteshaza?
Tuendelee,
na Ujenzi wa Imani wa Yesu kwa Martha, Baada ya hapo Yesu aliwataka waliondowe
jiwe kaburini; (kwa lugha ya leo wafukuwe kaburi), ila dada huyu alisema ya kwamba
amekufa na ananuka ni siku ya nne sasa, ndiposa Yesu akamjibu,
40 Yesu akamwambia, “Mimi
sikukuambia ukiamini utauona utukufu wa Mungu?”
Usifeli
mtihani kwa kupungukiwa na imani, kumbuka mimi ni Mwalimu na hapa ninakujengea
imani na wakati wa “Pratical” yaani vitendo vya kudhibitisha imani yako
unakuja, na hapo amini tuu, ili nisije kukuhoji kama Yesu;
Mimi
ninakwambia kama Yesu, amini ili uone Utukufu wa Mungu, mara badaa ya Yesu
kujenga imani hiyo kwa Martha dadaye na Marehemu Lazaro, kilichotokea ni mujiza
kwa Lazaro aliyeitwa Marehemu kuwa mzima na jina marehemu kufutika.
Na wewe
itakuwa hivyo kwako leo, waliokuita aliyaechika, masikini, hohehaye, fukara wa
kwanza, na hata asiye na mbele wala nyuma. Watakuita mbarikwa, tajiri wa
matajiri, mama/baba wa mataifa mengi na hutaitwa tasa tena kwani vinywa vya
wakina Penina vinakwenda kukoma sasa. Ila wewe amini tu. Ili uone Utukufu wa
BWANA, Kwani wamisiri yaani watesi unaowaona leo hautawaona tena na BWANA
atakupigania na wewe utanyamaza kimia.
(Kutoka 14:13 Musa akawaambia watu, “Msiogope! Simameni tu, mkauone
wokovu wa Bwana
atakao wafanyia leo; kwa maana hao
Wamisiri mliowaona leo hamtawaona tena milele.14 Bwana atawapigania ninyi,
nanyi mtanyamaza kimiya”)
Kwa Neno hilo mashujaa walivuka bahari ya Shamu. Na kwa neno hilo nawe vuka.
Lazaro
hayupo tena kaburini, Yohana 11:43 Naye akiisha kusema hayo,
akalia kwa sauti kuu, “Lazaro njoo huku nje.” 44 Akatoka nje yule aliyekufa, ..
Na wewe utoke nje ule uchumi wako uliokufa, Ndoa ama Elimu yako, Huduma ama Afya
yako, ninaiita sasa nawe kwa imani itapamoja nami kwa sauti iliyo kuu. Njoo Ndoa
kwa Jina la Yesu, njoo Uchumi, Elimu, Afya, Huduma, Upendo, Kibali, Upako,
Karama kwa Jina la YESU KRISTO MNAZARETI NJOO NJE NAWE UFUFUKE KATIKA WAFU.
Ameni na hongera kwa Mujiza wako.
Kabla sija
kuaga kwa busu takatifu, nataka kukujuza jambo jingine muhimu hapo ikiwa ni
kanuni za kufufua kila kilichokwama maishani mwako na wewe kuwasaidai wengine,
1. Imani, 2. Ita kwa sauti iliyo kuu kamaYesu
alivyoita ama aliyo omba.
3. Kaa karibu a Yesu, na umalaki kama
Martha.
Na
4. Hakikasha unaomba kwa huzuni ya roho yenye dhima ama taswira ya kumaanisha
na yenye kumfadhaisha Yesu kama Mariamu dadaye mwingne wa Lazaro ili Yesu naye
aguswe na tatizo lako na hatimaye kukutendea mujiza.
Usikubali
kuomba kwa mazoea ama kibosi, hakuna ubosi mbele ya kufufua kilichokufa.
Ukiweza kugaragara , garagara na ukiweza kulia lia haswa bila woga.
Yohana 11:32 Basi
Mariamu alipofika pale alipokuwapo Yesu na kumuona, alianguka miguuni pake,
akamwambia, “Bwana, kama ungalikwepo hapa ndugu yangu asingali kufa” 33 Basi
Yesu alipomwona analia, na wale wayahudi waliofwatana naye, aliugua rohoni,
akafadhaika roho yake, 34 akasema, “Mmemweka wapi?” Wakamwambia, Bwana njoo
utazame.
Anauliza
alipowekwa Lazaro baada ya kuugua na
kufadhaika rohoni pamoja na Mariamu na wafariji wake, na wewe mfanye Yesu
afadhaike kwa kuugua pamoja naye kimaombi, sio kuugua mwilini na kulia sana! Hapana!!
Bali ni kuugua kwa kuomba ama kuanguka miguuni pa Yesu. Nao bila kupoteza muda
walimjibu, “Bwana njoo utazame”
Na wewe Yesu
akikuhoji, mwanagu nikutende nini, ama yupo wapi mwenzi wako, mwambiye kwa
haraka na weka mambo bayana. Achana na hadidhi za kukosa mtu wakukusaidia punde
maji yatibuliwapo , “Oho, mara wenzangu wananipita na kutangulia birikani punde
malaika atibuapo maji”, wewe mwambiye Yesu nataka ufufuwe ndoa yangu, mwenzangu
kaondoka, ama nataka kusoma sina ada mdhamini wangu kafarikia na kagoma, au
mwambiye nimefukuzwa kazi au biashara imedodo. Pia waweza weka bayana bila woga
ya kwamba, nina miaka kadhaa kwenye ndoa nami sina mwana, ama kiu yangu niolewe.
Nii Mwingi
wa tabasamu, lisilo pimika kwa uzani wala futi, ninakupongeza kwa ujasiri na
umahiri wako kama mtu apigaye mbiyo mashindanoni ya kufwatilia makala zangu
bila kuchoka, ni hakika ujumbe huu umefanyika msaada kwako, usisite kuwadokezea
ma kuwamegea wengine uzuri wa ujumbe
huu, na kama huja penda/kulike page/ukurasa wetu wa Facebook fanya hima kufanya
hivyo ili upate jumbe hizi kwa haraka na waalike na wengine pia. Ukurasa wetu
una jina la UG UKOMBOZI GOSPLE
Pamoja na kundi letu.
Tukutane
tena kesho panapo majali ya Mwenyezi MUNGU, na kama hujasoma makala za nyuma
zitafute hapa uzisome.
Na Huduma ya
UKOMBOZI GOSPLE, Arusha Tanzania, Kwa Maombi, Ushauri, Maswali au Sadaka
wasiliana nasi, Barua pepe: ukombozigosple@gmail.com
Simu: +255 759 859 287 pia waweza itumia kwa M-PESA. Zaidi www.ukombozigosple.blogspot.com #UkomboziGosple #MwalimuOscarSamba
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni