Ila kumbuka
hali hii ilimkuta hata Yesu, “Mungu wangu, Mungu wangu mbona umeniacha?”,
Mathayo 27:46. Kiukweli Mungu
alikuwa Kimya. Hatumuoni akiongea naye wala kumjibu lolote baada ya kukamatwa
kwa Yesu.
Kuna taswra
kuu mbili za Mungu kunyamaza kimya, ya kwanza ni ile ya mtu kutenda dhambi na
Mungu kumuacha, na ya pili ni ile ya mtu kuwa katika hali ya pito huku Mungu
akipima subira yake iliyondani ya Saburi ya Kimungu ama Mungu akimsubiria
achukuwe hatua fulani ndipo amjibu.
Tuanze
kuidodosa ile ya kwanza ya mtu kutenda dhambi, Mfalume Sauli alikuwa kipenzi
cha Mungu, ila alipotenda dhambi ya kukataa kufwata maelekezo ya Mungu; Mungu
alimwacha na hakumjibu ama hakuzungumza naye kwa njia yoyote ile hata ile ya
kinabii mara baada ya kifo cha Kuhani na Nabii Samweli.
Alikadhalika
Yuda Iskariote, mara baada ya kumtenda Yesu, Matokeo yake yalikuwa ni mabaya na
hii ilikuja baada ya kuachwa na Mungu.
Yuda alihitaji msaada ili kumzuilia kujinyonga, Kumbuka Mungu husema
kuwa hapendi kuinona nafsi ya mwenye dhambi ikipotea.
Silengi tuu
kuwasaidia wakina Yuda na Sauli bali hata wakina Petro, Petro alipata msaada wa
karibu sana kutoka kwa Yesu na Roho Mtakatifu alimsaidia kwa haraka sana kwa
ishara ya Kengele ya Jogoo kuwika. Na mimi ninaguswa na wakina Yuda ambao hawaijui
ama huipuzia ishara ya jogoo kuwika.
Sauli mara
baada ya kumuasi Mungu na mbele yake kulikuwa na mtihani mgumu sana wakupigana
na wafilisti, kabla ya mtihani huo hakuona umuhimu sana wakutafuta msaada na
kwa bahati mbaya sana alikuwa akitegemea nguvu za Nabii Samweli na hakujua
dhamani na umuhimu wa kwenda mbele za Mungu.
Bali
alijikuta akitafuta msaada kwa waganga wakienyeji, 1 Samweli 28:3-25,7Ndipo Sauli
akawaambia watumishi wake, “Nitafutieni mwanamke mwenye pepo wa utambuzi nipate
kwenda kuuliza kwake.” Watumishi wake wakamwambia “Tazama, yuko mwanamke mwenye
pepo wa utambuizi huko Endori.”
Matokeo yake
yalikuwa ni Sauli kupata adhabu ya kimungu hali iliyopelekea mauti yake na kwa
watu wa nyumbani kwake huku Wafilisti wakijipiga kifua mbele ya taifa la Mungu
wetu Iziraeli.
1Mambo ya
Nyakati 10: 13 Basi Sauli alikufa kwa
sababu ya kosa lake alilomkosa Bwana, kwa sababu ya neno la Bwana,
asilolishika; na tena kwa kutaka shauri kwa mwenye pepo wa utambuzi, aulize
kwake, 14 asiulize kwa Bwana; kwa hiyo akamua na ufalume akamgeuzia Daudi,
mwana wa Yese.
Sio yeye tu
bali na watu wa nyumbani mwake, 1Mambo ya Nyakati 10:6 Hivyo sauli akafa na wanaye watatu, na nyumba yake yote wakafa pamoja.
Kiu yangu
hapo ilikuwa ni kuona madhara ya kutokutenda vyema punde Mungu anapokuacha
kutokana na dhambi uliyoitenda, Kumbuka Sauli aliangukia Upanga, na Yuda
alijinyonga. Hayo ni matokeo yakutokuamua vyema. Na nimekuandalia chakufanya
ili usikumbwe na hayo.
Unapotenda
dhambi hakikisha unaomba rehema kwa Mungu na wala usiruhusu kiburi kuinuka ndani yako kwa kukataa maonyo kwani hali hii ni hatari sana na kitabu cha Mithali
kimeonya kiundani jambo hili la kukataa maonyo.
Pili hakikisha hurudii kosa lilokufanya
kukorofishana na Mungu.
Kama dhambi
yako ama kosa lako limfikia lile la Sauli la kuachwa na Mungu kiasi ambacho
hata maombi ya Rehema ya Samweli juu yako hayajibiwi, Hakkisha utafuta nalohiji
Mungu juu yako nawe ulifanye na sio kumwinda Daudi kwani kufanya hivyo ni
kuchochea hasira na gadhabu ya Mungu juu yako.
Sauli
alipogundua kuwa Mungu amemwacha hakutafuta kuupendezesha uso wa Mungu badala
yake aliaza kupanga mipango na kuitekeleza ile ya kumua Daudi. Cha kufanya kama
Mungu ameshaurarua ufalume wako na kumpa jirani yako hakikisha unaukabithi kwa
aliyepewa lli wewe uwe salama usijiuwe wala wakina Yonathani wasife na
Mefiboshethi kuwa kilema.
Matokeo ya
kuvaa miwani nyeusi kwa kujifanya haujali eti una kiburi ama kumuona Mungu kama
ni mdogo wako na anapaswa kujinyenyekeza mbele yako ni mabaya sana. Kumbuka
huwezi kujifanya wakiroho kuliko Sauli ama Yuda aliyeonana na Yesu ana kwa ana.
Cha msingi ni wewe kujishusha na kupondeka kifudifudi mbele zake kama Petro. Luka 22:60-62, 62 Akatoka nje akalia kwa majonzi.
Nimewaona
watu wengi walioanguka kwenye uzinzi na kujikuta wameacha wokovu kabisa na
mwisho wao kuwa mbaya kabisa kiimani na hatimaye kufa kifo cha aibu.
Kulikuwa na
Mtumishi mmoja wa Mungu natumai ni kule mkoani Morogoro, Mtumishi huyu
aliifanya kazi ya Mungu katika viwango vikubwa sana, Alitumiwa katika ishara na
miujiza ya hali ya juu. Ikafika kipindi akaanguka kiroho na hatimaye kuoa wanawake
wa wili kisha mwanaye alijitaidi sana kumuombea.
Siku moja
Mungu akamuotesha ndoto ya kuwa anaitafuta silingi iliyodumbukia kwenye tundu
la shimo la choo. Ndoto iliyokuwa na tafsiri ya kwamba ache kumuombe baba yake
kwani tayari amekwisha fikia kiwango cha kuachwa na Mungu, na hali hii ndiyo
iliyokuwa kwa Samweli dhidi ya Sauli.
1Samweli 16:1 Bwana akamwambia Samweli, “Hata lini utamlilia Sauli, ikiwa mimi
nimemkataa asimiliki Iziraeli?..”
Mara bada ya
ujumbe huo siku chache mbeleni mtu huyu aliyekuwa mtumishi alivamiwa na
majambazi na kuuwawa. Tazama kifo chake! na kosa lake.
Tugeukiye
taswira ya pili ambayo ni ya Mungu kukaa kimnya angali ujatenda dhambi bali upo
kwenye pito fulani. Kumbuka kuwa hata kwa Ayubu Mungu alinyamaza na kuja
kumjibu mwishoni kabisa.
Tafadhali
ungana nami tena kesho ili kusoma sehemu ya pili ya makala hii…
Na Huduma ya
UKOMBOZI GOSPLE, Arusha Tanzania, Kwa maombi, Ushauri, Maswali au Sadaka
wasiliana nasi, Barua pepe: ukombozigosple@gmail.com
Simu: +255 759 859 287 pia waweza itumia kwa M-PESA. Zaidi www.ukombozigosple.blogspot.com
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni