Na Mwalimu Oscar Samba #UgMinistry |
Kuna wakati
ukitazama mazingira uliyonayo na kulinganisha na ahadi ya Mungu maishani mwako,
unapata vitu tofauti ama visivyowezekana. Mungu alimuaidia Ibrahimu na Mkewe
Sara kuwafanya taifa kubwa, cha ajabu aliwapa mtoto mmoja. Kimazingira ilikuwa ngumu kwani
tungalitarajia kupewa watoto wengi.
Isaya 51:2 Mwangaliye Ibrahimu, baba yenu, na Sara aliyewazaa; kwa maana alipokuwa
mmoja tu nalimwita, nikambariki, nikamfanya kuwa wengi.
Mazingira
haya yalikuwa hayasadifu ahadi hii ya Mungu ila Ibrahimu na mkewe waliishika
kwa Imani iliyo kuu kwani licha ya kupewa mtoto mmoja pia walikuwa hawajapata
mtoto huyo hadi kufikia uzeeni ambapo Ibrahimu alimpata Isaka akiwa ni mtu wa
miaka mia na ushee, jambo hili halikuwa dogo kwake maana yeye na mkewe
walicheka wakati ahadi hii inatokea kwa kudhibitishwa.
Mwanzo 17:17 Ndipo Ibrahimu akaanguka kifudufudi akacheka, akasema moyoni, “Je, mtu
wa umri wa miaka mia, kwake atazaliwa mtoto? Naye Sara mwenye umri wa miaka
tisini atazaa?”
Mwanzo 18:12 Kwa hiyo Sara akacheka
moyoni mwake, akisema, “Niwapo mkongwe, nitapata furaha na, na bwana wangu
mzee?”
Ukitazama
mstari huu kwa Sara utadhania ya kwamba kicheko hicho ni cha furaha kwa kumpata
mtoto uzeeni na furaha kuzaliwa hapo, ila mistarii inayofwata malaika wa Bwana
anadhiriisha kuwa kicheko hicho kilikuwa ni cha kuonyesha shaka iliyotokana na
mazingira ya umri wao ama uzee kusema haliwezekani ingawaje Mungu hatazami hayo
mazingira kwani anasema inawezekana.
Mwanzo 18:13 Bwana
akamwambia Ibrahimu, “Mbona Sara amecheka akisema, ‘Mimi kweli nitazaa mwana,
nami ni mzee?’ 14 Kuna neno gani lilogumu la kumshinda Bwana? Kwa muhula wake
nitarudia, wakati uu huu mwakani, na Sara atapata mwana wa kiume.”
Ni kweli na
pasina shaka mazingira yalikuwa magumu kwa watu hawa wa Mungu, ila ahadi ya
Mungu ilitimia na wao walijilazimisha kumuamini Mungu katika ugumu wa hayo
mazingira na Imani ndicho kitu pekee kilichowawezesha kulitimiza hili Neno,
ingawaje hali hii iliwapa ugumu.
Waebrahia 11:8-12, 11
Kwa imani hata Sara mwenyewe alipokea uwezo wa kuwa na mimba, alipokuwa amepita
wakati wake; kwa kuwa alimhesabu yeye aliyeaidi kuwa mwaminifu.
Nataka
ujifunze kitu hapo, katika mazingira haya magumu Ibrahimu na Sara mkewe
walimwamini Mungu, na hapo tunamuona Sara akionyesha Imani ya utofauti
inayomuhesabu Mungu kama au kuwa ni mwaminifu. “kwa kuwa alimhesabu yeye
aliyeaidi kuwa mwaminifu” Licha mukutadha huo, pia linabainisha kuwa
hata umri wake ulikuwa umepita, “alipokuwa amepita wakati wake” Na
wewe haijalishi wakati wako wa kupata mtoto kibaolojia umepita, ama wakati wako
wakuolewa ama kuoa ukiutazama ni kama vile umesonga, yamkini ulitarajia kuwa
umesha jenga ama kusoma au kufikia ngazi fulani ya elimu na ukitazama mazingira
ya fedha ni magumu na umri wako umesogea kwani uzee ama utu uzima unakaribi au
majukumu kuongezeka.
Lisikiye
Neno la Bwana linalotoka kwenye kinywa changu na kudhibitishwa na vidole vyangu
vikuandikiavyo makala hii. “YASIOWEZEKANA KWA WANADAMU KWA MUNGU YANAWEZEKANA,
JE, NI JAMBO GANI LA KUMSHINDA MUNGU?”
Jibu Iake,
hakuna lolote lilo gumu kwa huyu Jemedari Yesu, bali wewe amini tu na uwe na
imani iliyo kamilifu kama wakina Ibrahimu na Sara kwani mara baada ya Imani yao
kilitokea hiki;
Waebrania 11:12 Na kwa
ajili ya hayo kazaliwa mtu moja, naye alikuwa ni kama mfu, watu wengi kama nyota
za mbinguni wingi wao ni kama mchanga ulio ufuoni, usioweza kuhesabika.
Mtu moja
anayetajwa hapo ni Isaka, ambaye alimzaa Yakobo na Yakobo kuzaa watoto kumi na
wawili, waliogeuka kuwa kabila kumi na mbili za Iziraeli ambazo ziliujaza
ulimwengu kwa wingi wake kama nyota za angania ama wingi wa idadi ya mavumbi ya
aridhi au mchanga wa baharini.
Mpendwa kwa
imani watu hawa waliyafilia mema yao maishani, na wewe kwa imani utayafikilia
yale ambayo Mungu amekuaidia, haijalishi leo unalala njaa, unashinda bila
chakula na kuamkia vyakula vilivyo lala ama dhaifu. Tazama ahadi ya Bwana
maishani mwako wala usitazame hapo ulipo hivi leo, macho yako ya ndani yaone
mafanikio makubwa.
Yamkini leo
wanakuita majina yaliyodharauliwa, “Kilaza, Kishoiya, Fukara, Ohehaye, Masikini
wa kutupwa.” Lakini wewe tazama majira
watakayokuita, “Mbarikiwa,” Watakapo imba Hosana na kutandika kanga zao ama
mashuka yao barabarani ili punda uliyempanda asikanyage mavumbi, hayo ndiyo
majira ya kuyatazama kiimani.
(Daudi
alidharauliwa kiasi cha kusaulika katika idadi ya watoto wa mzee Yese walioitajika
kupakwa mafuta, na wakati ule anataka kumwendea Goliati kaka yake alimdaharu na
kumwambia kuwa anajua kiburi chake, wakati kijana huyu alikuwa hana kosa. Ila
Daudi hakutishwa na mazingira ya kunukiwa kinyesi cha kondoo na harufu ya
mazizini wala kule kudharauliwa na nduguze ama kuonekana duni machoni pa familia
ya mzeee Yese, Bali aliyatazama majira haya hapa:
1 Samweli Nao wale wanawake wakaitikiana
wakicheza, wakasema
“Sauli amewaua elufu zake,
na Daudi makumi elufu yake ”
Hakutazama
majira ya nyimbo na miluzi ya kumkatisha tamaa bali ni majira ya wanawake
waliopita na kuimba sifa zake njema ikiwa ni ishara ya kuinuliwa na Bwana. Na
wewe tazama majira ya kuinuliwa na JEHOVA na achana na majira ya kupakwa
kinyesi na wanadamu wenye mwili wasioshiriki hata kwa harufu kikao cha kuitwa
kwako.)
Leo hii
wakifanya vikao vya maamuzi hawakuiti, wala hawakukumbuki, usitazame huko wewe
mtazame Yesu na yapo majira watakusanyika na kusema bila fulani yaani wewe hakuna
kitakacho amulika hapa. Yusufu huyu huyu aliyekaa gerezani ndiye aliyekuja
kufanyika msaada mkubwa kwa ndugu zake walio mdharau na kumchukia na taifa la
wamisiri liliomtia gerezani.
Mwanzo, 37:8…Wakazidi
kumchkia kwa sababu ya ndoto yake, na kwa maneno yake.
Ukiedelea utaoana jinsi walivyo muuza na hatimaye kutupwa gerezani.
Yamkini
umechukiwa na ndugu zako, kiasi cha kutokukudhamini na hukunenea maneno ya hadaha
na kejeli. Na kinachokumiza zaidi ni kwamba umejitaidi kuwatendea yaliyomema
ila malipo yake yamegeuka kuwa kejeli na dharau na kutegwa. Wewe sio wa kwanza bali
Yusufu na Yesu walipitia huko ila baadaye waliimba Hosana ni Mbarikiwa ajaye kwa
jina la Bwana. Ndugu wa Yesu waliwai kumwambia kuwa maerukwa na akili.
Kwa Yusufu hali ilikuwa ngumu
ila baadaye nduguze walisujudu kama andiko lilivyosema, na Farao kukiri ukuu wa
Mungu ndani yake hadi kusema haya:
Mwanzo 41:Frao akawaambia watumwa wake, “Tupate wapi
mtu kama huyu, mwenye roho ya Mungu ndani yake?” 39 Farao akamwambia Yusufu,
“Kwa kuwa Mungu amekufahamisha hayo yote, hapana mwenye akili na hekima kama wewe. 40 Basi wewe utakuwa
juu ya nyumba yangu, kwa neno lako
watu wangu watatawaliwa…”
Hayo ndiyo
majira ambayo imani isiyotishwa na mazingira inatazama, Yamkini ni kweli ndoa
yako imekufa, uchumi wako umekufa, afya yako imedhoofu, ukitazama ndoto zako
zakuwa dakitari ama mwanasiasa au kiongozi fulani ni kama zimefifia kabisa.
Usikubali kutishwa
na hayo mazingira, wewe mwamini Mungu kama Sara na mumewe. Ni kweli Lazaro
amekufa na ananuka. Ila Yesu anasema ugonjwa huo sio wa mauti angali ni mgonjwa.
Na sasa kafa, Yesu anasema kuwa Hajafa ila amelala.
Ni kiu yangu
kuendelea na makala hii murwa ila kwa kweli kengele ya muda inalia, ila usikose
kufwatilia makala mwenza hiyo kesho, itwayao, “LAZAZO HAJAFA, AMELAA NA WEWE AMINI TU” Kumbuka pia Yesu alisema
kijana hajafa ila amelala watu wale wakamcheka. Na wewe hiyo ndoa yako yaijafa
bali imelala na mkeo/mumeo atarejea wakati Yesu anatakaposema kijana “Tabitha”
Na Huduma ya
UKOMBOZI GOSPLE, Arusha Tanzania, Kwa Maombi, Ushauri, Maswali au Sadaka
wasiliana nasi, Barua pepe: ukombozigosple@gmail.com
Simu: +255 759 859 287 pia waweza itumia kwa M-PESA. Zaidi www.ukombozigosple.blogspot.com #UkomboziGosple #MwalimuOscarSamba
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni