Jumanne, 30 Mei 2017

NAMNA YA KUJINASUA KWENYE VIFUNGO VYA PEPO MAHABA. Sehemu ya 1.

 Na Mwalimu Oscar Samba #Ug Ministry 
 #SHARE  #SAMBAZA Ili kueneza injili hii Zaidi.
Kuna watu wanasumbuliwa kwa kuota ndoto wakiwa na Wanazini na mapepo Mahaba aidha kwa muonekano wa watu wanaowajua ama wasio wajua. Pia wapo wanaofanya ukahaba, Uzizi na hata vitendo vya kinyume na maumbile huku wakiwa hawapendezwi na hali hiyo na wamejaribu kutafuta msaada bila mafanikio.

Baya zaidi wapo wanandoa wenye kusumbuliwa na hali kama hiyo na tatizo hili linaiweka ndoa yao njia panda kwani hufanya ama huleta ugumu hata kwenye tendo la ndoa kwa mwenzi wake. Usiogope ama usiendele kulia tena kwani Mungu amesikia kilio chako na leo amenituma kukunasua hapao.

Nimekuandalia mbinu kadha wakadha ili kukuwezesha kutoka hapo na zote zipo kwenye kitabu changu cha NGUVU YA NDOTO KWENYE ULIMWENGU WA ROHO. Pia tukizimaliza hizo nitakuongezea nyingine kwa kibali cha Mungu. Na bila kukuficha ni bora kuwa wazi kwako ili kukusaidia bayani, Kama unataka ukombozi kamili njia iliyo kuu ni wewe kuokoka kama huja fanya hivyo na kama ni tayari basi hakikisha unasimama kiroho. Tafadhali pia kama unamjua mtu anayesumbuliwa na matizo haya ikiwemo ya Ukahaba, ama Umalaya hakikisha ujumbe huu unamfikia na ukiweza kumtag fanya hivyo sanjari na wewe kushare kwenye timeline yako ama kwenye makundi mbalimbali ya mitandao ya kijamii  ikiwemo yale yaliyotekwa na MAPEPO MABAHA ili nao wafikiwe na Ukombozi huu.
Kaa sasa mkao wakupata mafundisho hayo na nitakupa dalili hadi njia za kujinasua za kitabuni na baadaye nitapanuka zaidi ya hapo, “Mapepo mahaba, mtu huota anafanya tendo la ndoa na mapepo au mtu fulani na wakati mwingine hata wanyama hususani ng’ombe ambaye huwakilisha mzimu.
Wakati mwingine huweza kuota akitizama picha za utupu ama kuwaona watu wakiwa watupu ndotoni. Baya zaidi wengine huota wakifanya tendo hilo na watu wajinsi kama yao.
Niliwai kusikia habari ya uwepo wa jini moja liitwalo “Popo Bawa,” ambalo ni kinara cha uchafu huu. Mambo haya yapo na ni ya kweli kwani katika utumishi wangu nimepokea kesi kama hizi na kuzishuhulikia.
Ndoto hii zina mathara makubwa kama nilivyo kwisha kuelezea kwenye kipengele husika.
Unapoota hivyo na kujikuta hali hiyo ikijirudia jua kwamba kwenye ulimwengu wa roho una ndoa na Mapepo Mahaba. Na ndio maana hukutumia.
Unapoota ukifanya tendo hilo na mtu unayemjua kuna mambo mawili.
1. Ni mtu wa kimwili halisi kiroho. Mtu huyu ni kweli anafanya na wewe tendo hilo na hufanya hivyo kwa kujua na kuamua kwa njia ya kichawi/kishirikina.
Kuna simulizi moja ya mtu moja ambaye alikuwa ni mchawi na alikuwa akiwaingilia wake za watu ndotoni. Wakati huo huweza humtoa mumewe na kumlaza chini kisha kuzini na mkewe.
Pia kuna binti mmoja ambaye alikuwa ameokoka na alisumbuliwa sana na tukio kama hilo. Ilikuwa ni siku moja alipokutana na mwanaume mmoja ambaye ni jirani yake na kumtaka amkubaliye kulala naye na binti huyu alikataa. Mara baada ya hapo kila akilala usiku mwanaume yule huja na kulala naye na akiamka hujikuta amechafuka. Cha ajabu kila akifanyiwa hivyo siku inayofwata au kumkia usiku huo ni lazima akutane na huyo mwaume njiani mwilini, na huwa mwanaume huyo amwangali husoni, hutizama chini. Binti huyu alisumbuka sana kwani alikuwa ameokoka na alijiuliza kwanini anaomba lakini afanikiwi kushinda hali hiyo. Alimwendea mtumishi mmoja naye akamwelekeza namna ya kuomba na hatimaye toka siku ile hakuiona ile hali tena.
Na ndivyo wengi wanavyosumbuka hivi leo, ila jua ya kwamba kitabu hiki kitakutoa kwenye ufedhuli na uchafu huo usioupenda wala kutamani kuiskia.
Sio hao tuu bali yupo kijana mmoja ambaye alikuwa ni mlokole na mwadilifu mbele za Mungu. Siku mmoja akakutana na kijana mwenzake ambaye hajaokoka na kumtaka kuiga njia zake za uasherati ila alimkatalia. Kijana huyu alimwambia maneno yaliyomsumbua na kufungua mlango huo kwa pepo hili kwa muda wa miaka zaidi ya 14. Alimwambia “Utaloanisha shuka paka uone”, Ni wie radhi kama maneno hayo yamekukwaza kwa ukali wake, ila tupo darasani.
Kijana huyu alipinga swala hilo kwa kukemea na kujaribu kuyafuta hayo maneno ila hali ile ilipenya. Katika hayo yote nimekuletea mbinu teule ambazo ukizifwata kwa Imani Pepo Mahaba hatakutesa tena. Tumaliziye maana ya pili ya mtu umuonaye ukizini naye ndotoni.
2. Ukimuota mtu, Fahamu Shetani ametumia sura yake lakini mtu huyu amefanyika kama mlango kwenye ulimwengu wa roho. Kuna kesi moja ninaishuhulikia hivi sasa ya mtu mmoja ambaye anasumbuliwa na pepo hili na huona sura ya kijana ambaye alimuaidia kumuoa. Kwa hiyo pepo hili linatumia ule mlango wa ahadi ile. Huweza hata kutumia mlango wa Mke au Mume kama ungali wazi.
Dalili za mtu anayesumbuliwa na Pepo Mahaba.
Kuzini ndotoni. Hii ni dalili kubwa na inayowasumbuwa wengi. Dalili hii ndio iliyotufanya kujifunza jambo hili kwa mapana. Ila ukiota unafanya tendo hili ndotoni na unafuraia au unaye muhitaji ni wewe, jua kwamba tatizo halipo kwenye mlango wa ndoto tu! Bali nafsi yako imefungamanishwa au kuambatanishwa na muhusika au Mapepo Mahaba. Na ukiona unakataa kufanya tendo hilo ila unalazimishwa fahamu ya kuwa tatizo lake lipo kwenye mlango na ukishuhulikia hilo ni rahisi kushinda hali hiyo. Kwa hiyo kwa huyu anayefurahia au kuhitaji ndotoni ama kuonyesha kutokupinga inampasa ahakikishe anajifanyia au anafanyiwa maombi ya kuikomboa nafsi yake huku akishuhulikia swala la Mlango. Maombi hayo yaombe kama nilivyokuelekeza kwenye kipengele cha kumshinda Pepo Mahaba hapo mbeleni.
Mwili kuwaka tamaa bila sababu za msingi. Bila sababu za msingi mtu huyu huwa na hisia za haraka na kali za kufanya tendo la ndoa. Anaweza kuona kitu ambacho kikawaida kisingali mfanya kufikia hatua hiyo ila kwake humfikisha hapo. Utakapo waona vijana au watu wakimtizama sana msichana na kisha kuonesha ishara za kumtaka au mvulana huku miili yao ukiwatizama ni kama inasisimka jua kuwa tayari Pepo Mahaba kashaweka kambi kwao.
Natamani kuendelea kukujuza zaidi ila muda wanu unnishika shati, ila kesho pia ni siku mpendwa wangu, nami bila iyana nitaendelea hapo tulipoishia na ninatumai utabarkiwa zaidi.

Kama hujaokoka na unataka kuokoka ama ulirudi nyuma kiroho na unataka kutengeneza na BWANA kwa upya leo, tafadhali fwatisha nami maneno haya kwa Imani, Sema: BWANA YESU, NINAKUPENDA, NINAKIRI NA KUAMINI MOYONI MWANGU KUWA WEWE NI MUNGU, ULIKUFA NA KUFUFUKA KWA AJILI YANGU, INGIA NDANI YANGU KAMA BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YANGU LEO, AMENI.
Hongera kwa kuokoka na tafuta kanisa la watu waliokoka ukasali hapo.

Na Huduma ya UKOMBOZI GOSPLE, Arusha Tanzania, Kwa Maombi, Ushauri, Maswali au Sadaka wasiliana nasi, Barua pepe: ukombozigosple@gmail.com  Simu: +255 759 859 287 pia waweza itumia kwa M-PESA. Zaidi www.ukombozigosple.blogspot.com   #UkomboziGosple  #MwalimuOscarSamba
Pia #Like #Penda Page/Ukurasa wetu au kundi la Fb, ili kupata habari hizi kwa haraka, zaidi. Ug Ukombozi Gosple,                                                                                       PAGE: https://www.facebook.com/Ug-Ukombozi-Gosple                                              

Pia kwenye mtando Mpya wakitanzania wa                                                                          2 DAY SKY: https://www.2daysky.com/home

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni