Na Mwalimu Oscar Samba #Ug Ministry |
Baraka zako
ama majibu ya maombi yapo nyuma ya mlima
mpendwa kwa hiyo usichoke kuupanda huo mlima kwani ukiumaliza utakutana na majibu yako.
Ninakuhakikishia
ya kwamba PITO hilo ulilonalo ni kama mlima maishani mwako na uhakikisho ni
huu; Ukilimaliza salama utakumbana na majibu ya maombi yako.
Wana wa
Izirali waliizunguka milima ya Seiri siku za kutosha ila mara baada ya kumaliza
kuizunguka nyuma yake walikutana na majibu yao yaliyolenga kuwapitisha salama
na Mungu kufungua ukurasa wa kanuni za kuishi nchi ya ahadi sanjari na
kuwawezesha kuifikia Kanani yao kwa wepesi zaidi.
kumbukumbu la Torati
2:1 “Ndiposa tukageuka, tukashika safari yetu kwenda jangwani kwa njia
ya Bahari ya Shamu, kama alivyoniambia Bwana; tukawa tukiizunguka milima ya Seiri siku nyingi. 2Bwana
akanena akaniambia 3 Mlivyouzunguka mlima huu yatosha;
geukeni upande wa kasikazini.
Usichoke
kuupanda huo mlima bali endelea kukaza mwendo ndugu yangu kipenzi, Kuna
mwimbaji mmoja wa nyimbo za Yesu aitwaye Jenifa Mgendi katika wimbo wake
ameimba na kusema ya kwamba mbele yake kwa macho ya nyama anaona mlima ila kwa
macho ya ndani anayaona majibu yake yakiwa nyuma ya mlima. Kwa hiyo anaupanda
huo mlima ili ayapate hayo majibu.
Na wewe
nakutaka kufanya hivyo kwa Imani na bidii iliyokuu, Usikubali mtu wa ndani ama
wewe wandani kuona mlima ila wewe ona majibu nyuma ya mlima na mtu wa nje mtiye
moyo kwa kumuonyesha dhamani ya majibu hayo ili asikate tamaa.
Wana wa Iziraeli wengi walikata tamaa kwa sababu
hawakuwa na taswira kama hii kwani mtu wa nje hakuona dhamani ya majibu yale
bali alikuwa mwepesi wa kutazama ugumu wa mlima ule ikiwemo, kukosa maji,
chakula, na wakati mwingne kukinai chakula na kujikuta wakikiita kidhaifu
sanjari na umbali wa safari. Ila wachache kama wakina Yoshua na Kalebu walitazama
sana nyuma ya mlima.
Rafiki yangu
katika BWANA na Mpendwa mwenzangu, Usichoke kuuzunguka ama kuupanda mlima kwani
Mungu yu karibu kukujibu kama ilivyokuwa kwa hao wana wa Waebrania
alipojitokeza kwenye mstari ule wa tatu na kuwaambia, “Mlivyouzunguka mlima huu
yatosha; geukeni upande wa kasikazini.”
Na kwako
Itakuwa hivyo karibuni. Wewe mtazame YESU aliyekuaidia Baraka tele. Usikubali
kukwama hadi umsikiye BWANA akikwambia yakuwa “YATOSHA.” Na hakika akinena hivyo sikiliza maelekezo atakayokupa na
yamkini yakawa ya kuchuma matunda yako ama kuelekea njia nyepesi na isiyo na
mlima ya upande wa Kasikazini kama ilivyokuwa enzi zile za Musa pale Seiri.
Wakati huu ninapokuandikia
makala hii Roho Mtakatifu ndani yangu anaimba wimbo huu.
Usichokee kuubeba Masalabaa,
Katika huoo Mujiza wako upoooo, X Rudia zaidi kuimba.
Ninakutakia
majira yenye Fanaka na Mubashara katika safari hii ya kwenda mbinguni, Usikose
makala ya Kesho itwayo, YATOSHA. Ni
fika na bayana ya kwamba mapito yapo, mateso, dhiki na taabu, kulala njaa na
kutengwa ama kukataliwa na ndugu au wapendwa.
Ila yapo majira
ya mambo hayo kukoma, na ndiposa Yesu pale msalabani akasema IMEKWISHA, na
Mungu akawaambia wana wa Iziraeli wakati wanazunguka ile milima ya Seiri;
YATOSHA. “Mlivyouzunguka mlima huu yatosha; geukeni upande wa
kasikazini.” Na wewe imetosha sasa kuteseka…. Tafadhali ni kesho maana
upako nilionao naweza maliza mboga jikoni kwa kukuonjesha.
Kama
hujaokoka na unataka kuokoka ama ulirudi nyuma kiroho na unataka kutengeneza na
BWANA kwa upya leo, tafadhali fwatisha nami maneno haya kwa Imani, Sema: BWANA
YESU, NINAKUPENDA, NINAKIRI NA KUAMINI KUWA WEWE NI MUNGU, ULIKUFA NA KUFUFUKA
KWA AJILI YANGU, INGIA NDANI YANGU KAMA BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YANGU LEO,
AMENI.
Hongera kwa
kuokoka na tafuta kanisa la watu waliokoka ukasali hapo.
Na Huduma ya
UKOMBOZI GOSPLE, Arusha Tanzania, Kwa Maombi, Ushauri, Maswali au Sadaka
wasiliana nasi, Barua pepe: ukombozigosple@gmail.com
Simu: +255 759 859 287 pia waweza itumia kwa M-PESA. Zaidi www.ukombozigosple.blogspot.com #UkomboziGosple #MwalimuOscarSamba
Pia #Like
#Penda Page/Ukurasa wetu au kundila Fb, ili kuupta habari hizi kwa haraka,
zaidi. Ug Ukombozi Gosple,
PAGE: https://www.facebook.com/Ug-Ukombozi-Gosple
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni