Na Mwalimu Oscar Samba Ug Ministry |
Nabii
Ezekieli alionyeshwa bonge lilojaa mifupa ya wafu na aliitabiria mara mifupa
ikageuka na kuwa maremu, kisha marehemu wakapata uhai kwa kufufuka. Na wewe leo
hicho kilichokufa maishani mwako na kusaulika, kitafufuka kwa JINA LA YESU na
kisha kuwa hai tena.
Kama ile
maiti ilivyogusana na mifupa ya Nabii Elisha ndivyo itakavyokuwa kwako leo, kwa
hicho kilicho kufa kugusana na YESU KRISTO MTENDA MIUJIZA. Aliyemfufua Lazaro,
Binti wa mama yule mjane wa mji wa Naini, Kijana aliyekuwa amekufa na Yesu
kusema amelala, kisha watu kumcheka. Ila punde si punde, maiti alifufuka.
Yamkini na wewe unapowambia nitaolewa, wanakucheka sana, kwani umri umesonga,
ama unapowaambia ya kwamba, utasoma, utajenga, utamiliki magari na hata
majumba, hucheka sana. Wewe endelea kumuamini Yesu aliyemfufua huyu mfu sanjari
na mifupa ile mikavu, ikawa mibichi, marehemu na kisha WALIO HAI.
Kumbuka kisa
cha waliokuwa wanaenda kuzika kile cha Mifupa ya Elisha, watu hawa hawakuwa na
tumaini la marehemu wao kufufuka ila kwa kuwa alikwepo Nabii wa Mungu
aliyeupendeza uso wa Mungu, Mungu aliliheshimisha jina lake. Na kwa kuwa nipo
Nabii, Mtume na Mwalimu wa Mungu mbele yako leo, Mungu lazima aliheshimishe jina
lake. Wewe Muone Elisha wako na maiti ama marehemu wako ambaye yamkini ni Ndoa,
Uchumi, ama mifupa hiyo ni Elimu au Afya, ITAPATA UHAI LEO. Sio UHAI tu, bali
itakuwa JESHI, Naam sio JESHI tu, Bali ni JESHI KUBWA, litakalo pigana na adui
zako wote.
Mimi nawe
tuangaziye macho yetu kwenye maandiko haya ili kujirithisha na niyasemayo kwa
kuanza na mujiza ule wa Bwana Mkubwa YESU,
Mathayo 9:24
akawaambia, “Ondokeni, kwa maana kijana hakufa, amelala tu.” Waka mcheka sana.
Ona hapo,
walimcheka Yesu, tena sio kumcheka tu, bali sana. Sasa wewe una ona nini aibu
kuchekwa unapo waambia nitaolewa, na wakiatama umri umeenda, nitasoma,
wakiatzama, fedha hakuna, nitajenga, ndoa yangu itapata amani, na wakitazama
hivi leo ni kama maisha yap aka na
panya?
Kama Yesu
aliye Mungu alichekwa, itakuwaje kwako wewe? Tuendelee na ona kilichotendeka
hku andiko hilo likianza na neno, “Lakini,” Amablo kisarufi linaamana ya ama
dhima ya kuonyesha ukinyume ama utofauti na fkra fulani. Na hapa utofauti huo
ni wa wale waliomcheka Yesu, ambapo kwako ni kwa hao wanaokusagia meno na
kujaribu kukukwamisha kwa kukucheka.
25 Lakini makutano
walipoondoshwa, akamshika mkono; yule kijana akasimama. (Ndugu yangu hapa ni kwamba,
Marehemu kawa hai. Tazama kilichoendelea) 26 Zika enea habari hizi katika nchi ile
yote. Nawe ziamini habari
hizi ili mujiza wako uenee katika nchi yote wakisema, huyu si yule aliyekuwa
omba, omba pale mtaani, mbna leo anamiliki HAMA. “Eti, Yule aliyepakata mapacha
ni yule aliyekuwa maepitiliza umri wa kuolewa?” Huku na wewe ukiwafinya watoto
kidogo kwa makusudi ili wasikie wakilia, alafu unawabembeleza kwa kuwainu inua
na kuwaambia kwa sauti ya upole ila watakayoisikia, “Pole, pole wanagu, pole ,
nawapenda.” Wakijifanya hawakuoni unawapungia na kuwaambia, “Watoto jamani
wanadeka hawa.” Ni ili Mungu wao atukuzwe na vinywa vyo vimgeukie Bwana kama
laa aibu ya kushindwa iwafunike usoni huku wewe ukipeta katika YESU WANGU.
Kama Nabii
wa Bwana ninakwmabia tena leo kwa mara nyingine ya Kwama, Yaliyoshdikana kwa
madakitari Bingwa, wanajimu, wachawi na walozi kwa Yesu yote yanawezekana, Iwe
ni UKIMWI,UKOMA, MALERIA SUGU, TAIFODI, KASWENDE, UPOFU, UKIZIWI, UBUBU, UPOFU,
na hata EBOLA, KANSA ama Kukataiw ana ndugu YESU anaweza yote hayo.
Kama
alivyofufua mifupa mikavu na hayo yaliyoshindik kwako na kwa kila hosipitali
kwake yanawezekana. Tuangaziye kwa pamoja kisa hiki chenye kuinua IMANI sana.
Kwa mwendo wa poe fungua nami kitabu kile cha Nabii Ezekieli.
Ezekieli 37:4
Akaniambia tena, “Toa unabii juu ya mifupa hii, uiambiae, Enyi mifupa mikavu,
sikieni neno la Bwana. 5 Bwana Mungu aiambia mifupa hii amneno haya, Tazama,
nitatia pumi ndani yenu, anyi mataishi. 6 Nami nitatia mishipa juu yenu, nami
nitaleta nyama iwe juu yenu, na kuwafunika ngozi, na kutia pumzi ndani yenu,
nanyi mtaishi; nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi Bwana”
Hayo ni
maneno ya Mungu kwa Nabii Ezekieli, na mimi leo ninataka yawe maneno yako ili
kitokee kama kilichotokea, tukione hapo mbeleni.
7Basi nikatoa unabii
kama nilivyo amriwa; hata nilipokuwa nikitoa unabii, palikuwa na mshindo mkuu;
na tazama, tetemeko la nchi, na ilemifupa ikasogeleana, mfupa kwa mfupa
mwenziwe. 8 Nikatazama, kumbe! Kulikuwa
na mshiapa juu yake, nyama ikatokea juu yake, ngozi ikaifunika juu yake, lakini
haikuwamo pumzi ndani yake.
Huyu tarari
ameshatoka kwenye hatua ya kuwa mifupa mikavu na kuitwa marehemu, sasa
kinachohitajika ni pumzi ili awe hai yani afufuke. Na wewe hilo teso lako
limesha fikia hatua hii, kwa mifupa kusogeleana, mishipa juu yake, nyama na
hatimaye ngozi kuifunika. Na wale walikuwa awaambni waanza kuwa na imani
ingawaje ni haba kwa kuona dalili za kutokewa na Mungu wako.
Kwa hiyo
vuta pumzi, kidogo kwa kuhewa alafu chukua hatua ya kuongeza IMANI yako ili
marehemu awe hai. Tuendelee;
9 Ndipo
akaniambia, “Tabiri, utabiriye upepo, mwanadamau, ukauambiye upepo, Bwana Mungu
asema hivi, Njoo kutoka pande za pepo nne, ee pumzi, ukawapuliziye hawa
waliouawa, wapate kuishi” Nami ninayatabiria masha yako sasa, “KWA JINA LA YESU KILA KILICHOKUFA MAISHANI
MWA HUYU MTU, KIPOKEE UHAI SASA, IWE NI NDOA, UCHUMI, ELIMU, AFYA, KIBALI KWA
NDUGU AMA HUDUMA, UPAKO AU AMANI, KWA JILA LA YESU NATMA PUMZI YA UHAI,AMENI”
10 Basi nikatabiri kama alivyoniamuru; pumzi
ikawaingia, wakaishi, wakasimama kwa miguu yao, jeshi kubwa mno.
Sio kikosi, bali ni jeshi kubwa, sio
kubwa tu, bali ni kubwa mno. Na walisimama kwa miguu yao wala sio ya jirani zao
ama kwa msaada wa magongo bali ni yao. Naiwe kwa hivyo leo, kama mifupa
mikavu/wafu walikwa marehemu na ksha kuwa hai, hakika kila kilichokufa kwako kinawezekana.
Usiniambiye ama kuniuliza na hili Mtumishi linawezekanaje,? Mimi niachojua
hakuna lisilowezekana kwa Mngu, kama Sara wa maika tisini na Ibrahimu wa maika
mia waliapata mwana. Je, kwako itakuwaje? Waliokuwa viikongwe kupakata mwana.
Huku mzee wa wa miaka tisini akienda Leba, Je kwako?
Tukutane
kisho mpebdwa wangu katika safu hii ya makala, nan i hakika MANA niliyoiandaa
kesho, iatakuacha ukiwa kinywa wazi kwa kutirika mate kama mtu alaye asali,
kwani ni tamu nan i yenye Afya, ithili ya Alwaa ileya Zenji. Langu jina
nililopewa na wazazi ni Oscar, na Mungu kunipa wito wa huduma ya Ualimu kwa
hiyo wa weza niita Mwalimu Oscar aliyezaliwa kwene ukoo wa Samba mwana wa Flora
katika familia teule ya Mzee Prospa, waliokoka.
Nawe kama
hujaokoka fanya hima leo uokoke ili uwe na uwalali wakupokea huo mujiza huku
ukiuutunza kama mwana wa Mungu, Kama upo tayari kuokoka sema nami maneno haya
hapa.
BWANA YESU,
NINAKUPENDA, NINAKIRI NA KAUMINI KUWA WEWE NI MUNGU, ULIKUFA NA KUFUFUKA KWA
AJILI YANGU, INGIA NDANI YANGU KAMA BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YANGU LEO,
AMENI.
Hongera kwa
kuokoka na tafuta kanisa la watu waliokoka ukasali hapa.
Na Huduma ya
UKOMBOZI GOSPLE, Arusha Tanzania, Kwa Maombi, Ushauri, Maswali au Sadaka
wasiliana nasi, Barua pepe: ukombozigosple@gmail.com
Simu: +255 759 859 287 pia waweza itumia kwa M-PESA. Zaidi www.ukombozigosple.blogspot.com #UkomboziGosple #MwalimuOscarSamba
ninaomba tafsiri ya neno la kwa msaada wa Mungu nafuatia jeshi
JibuFuta