Jumapili, 7 Mei 2017

Wanafunzi wa Vyuo na Shule, Usimwache Yesu mfikapo vyuoni/Shuleni

Mwalimu Oscar Samba
+255 759 859 287  Kumekuwa na wimbi kubwa la wanafunzi kuyaacha maadili ya kikristo pindi wa fikapo shuleni ama vyuoni.

Jambo hili ni hatarishi kwao kwani mazingira ya masomo hufananishwa na eneo la kivita kwenye ulimwengu wa roho. Katika maeneo kama haya ndipo hujitokeza wanafunzi waliozoezwa kutumia ushirikina au wenye ujuzi katika mambo hayo. Na wewe ukiyumba kiroho maana yake ni kwamba utashindwa na mambo hayo na kujikuta ukididimia kiroho na kimwili huku maono au ndoto zako zikikwamia njiani.

Pia wachawi na waganga wa kienyeji ama washirikina hupenda kudhuru maeneo hayo kwenye ulimwengu wa roho ili kuiba nyota za wanafunzi, kuwachezea ama kuwatumikisha kichawi na hata kujipatia wajumbe wao hapo.

Ndio maana katika maeneo ya mashule ama yvuo hakuishi vituko vya kishirikina hususani kwenye vyoo na hata mabweni. Ukiwa na Yesu utayashinda haya kirahisi na wewe hawatakuweza.

Na sababu zifwatazo ndizo huwafanya wanafunzi wengi kumuacha Yesu punde wafikapo katika mazingira kama haya; 
1. Kufwata mkumbo, wanafunzi wengi hujikuta wakifwata mkumbo kwa kuiga mambo yasiyofaa, ikiwemo vitendo vya ulevi na hata ukahaba. Pamoja na mavazi.

2. Kukosa ujasiri wa kumtaja Yesu ama kuona wokovu kama ni aibu, Nisikilize kwa bidii ili upone, Yesu sio mzigo wala sio aibu kuwa naye bali ni sehemu ya Ushindi. Kumbuka msalaba kwao wapoteao ni upuzi bali kwetu siye ni ushindi, uzima, na nguvu tele maishani mwetu. Usikubali kuona haya kumtangaza Yesu maana anasema atakayemkana mbele ya watu naye atamkana mbele ya Baba.

3. Kuwa na marafiki waovu, siku zote rafiki wa mtu ni mtu, na unapojifanyia marafiki wasiofaa ni kwa uaribifu wa nafsi yako na maisha, na maono yako kwa ujumla. Mithali 18:24a Ajifanyiaye marafiki wengi ni kwa uaribifu wa nafsi yake.. 
Mithali 22: 24 Usifanye urafiki na mtu mwenye hasira nyingi, wala usiende na mtu wa gadhabu nyingi.

Bibilia inatupa muongoza sahihi wa namna ya kuwa na marafiki kwani ukiwa na rafiki mwizi na wewe utakuwa kama yeye, aliye kahaba ama mwenye tabia ya kuchuna wanaume "Mabuzi" ama mwenye macho ya kutamani mabinti, "Mademu" hakika na wewe utafanana naye. 
Katika hili ninakuta kuwa makini sana na marafiki, ingawaje dhumuni langu sio kukunyima kushirikia nao kimasoma, ila shabaha yangu ni kukuondolea ukaribu nao.

4. Kuwa na gelifrend au Boyfrendi, Kitendo hiki cha mwananfunzi kuamua kuwa na mpenzi kabla ya wakati wa kibibilia ama nje ya mpango wa kimungu ni dhambi na jambo hili hufungua mlango kwa Shetani unaomuwezesha kunyonya hali yako ya kiroho polepole na kujikuta ukianza kuwa na Wokovu wa mazoea ama wa kidini na hatimaye kuwa debe tupu litoalo upatu. 

Usidanganywe eti huo ni uchumba, hii ni hila ya Shetani kwani uchumba wakibibilia haufanyiki hivyo, na huwa na utaratibu ufwatao , Mchungaji wako ajue, Wazzzi wafahamishwe, kisha mchakato wa mahari ufanyike na utangazwe kanisani.
Kama hayo hayajafanyika ama hakuna rathi hiyo fahamu kuwa mpo mtegoni.
Na huku ni kumkosea Mungu Mpendwa, Wimbo uliobora 3:5 Nawasihi, enyi binti za Yerusalemu, kwa paa na kwa ayala wa porini: msiyachoche mapenzi, wala kuyaamsha, hata yatakapoona vyema yenyewe.

Ndugu yangu kiimani ninakutaka kumshika Yesu kwa bidii unapokuwa katika masomo yako na endelea na misingi ya kiroho ili kufanikiwa vyema. Usikubali kuwa mlokole ukienda likizo ila kibaka ama mwizi au mtukanaji ukiwa shueni. Achana na utamaduni wa kumwa mwema mbele ya wazazi ila muovu mbali ya upeo wa macho yako.

Swala la kiroho ni lako wewe na Mungu wako. Wakina Meshaki, Shedraki na Aberinego na Danieli walipofika uamishoni kule Babaeli na kuingizwa katika iamaya ya kifalume huku wakipelekwa darasani ili kuijua lugaha ya wazawa na maarifa ya kifalume kwa shabaha ya utumika kwa mfalume Nebukadreaza hawakumwacha Yesu; Badala yake waliongeza bidii na hatimaye Mungu wao kutukuzwa hapo.

Na wewe hapo ulipo inahitajika Mungu wako atukuzwe na kila mtu amptambuwe huyo uliye naye kama wakina Meshaki na Aberinego, Shedraki na Danieli kipindi kile. 

Pia kama hujaokoka fanya hima umpokee huyu Yesu kwani ndiye atakayekuwezesha kuishi maisha mazuri chuoni maana bila Yeye wachawi, walozi na wasoma nyota wanaweza kukuibia mafanikio yako na kujikuta unafukuzwa shule bila sababu za msingi ama kuishilia kwenye vitendo vya ulevi na ukahaba na hatimaye kuvurugikiwa maishani.

Kumbuka kuwa sio kila anayetenda mambo ya ajabu ama maovu vyuoni ama mashuleni amependa bali wengine wamelogwa au kuchezewa kwenye ulimwengu wa roho na watu wenye husuda, wivu na hata wenye nia mbaya. Wapo walioibiwa nyota, na waibao hutupa tabia za ulevi, ukahaba ama mwenendo mbaya pia magonjwa ili mshuhulike na hayo badala ya kugundua wizi huo wa nyota ama huwa kama bumbuzi kwa kutokuja kuwa ameibiwa.

Yesu pekee ndiye awezaye kumuweka huyu mtu salama,

Kama huja Okoka na unataka kuokoa ama ulikuwa umeokoka na ukalega kiroho ama wakati huu upotayari kurejea tafadhali fanya sala hii ya toba.

Sema, Mungu Baba, nipo mbele zako, Nimetambua yakuwa mimi ni mwenye dhambi, Na nipotayari kukufwata, Na ninakuamini na kukupokea kama Bwana na Mwokozi wa maisha yangu, ninakupenda Yesu, nilinde kiroho na kimwili. Ameni .

Hongera kwa kuokoka na tafuta kanisa la kihoho mahali ulipo ukaabudu, Ameni.

Na Huduma ya Ukombozi Gosple, kwa maombezi ama ushauri na sadaka Ya M-pesa tumia +255 759 859 287.  


Maoni 2 :

  1. Wimbo uliobora 3:5 Nawasihi, enyi binti za Yerusalemu, kwa paa na kwa ayala wa porini: msiyachoche mapenzi, wala kuyaamsha, hata yatakapoona vyema yenyewe.

    JibuFuta
  2. Wimbo uliobora 3:5 Nawasihi, enyi binti za Yerusalemu, kwa paa na kwa ayala wa porini: msiyachoche mapenzi, wala kuyaamsha, hata yatakapoona vyema yenyewe.

    JibuFuta