Na Mwalimu Oscar Samba #UgMinistry |
Ipo nguvu ya
ajabu ipatikanayo katika msalaba wa Yesu Kristo iwezayo kukupa majibu ya masumbuko
unayoyahitaji. Na kama msaada upo basi haipaswi kukata tamaa ama kuendelea
kufadhaika bali wewe uhitaji huu msaada ili uwe salama.
Kuna kisa
kimoja kwenye Bibilia nacho ni cha Petro ambaye alitembea juu ya maji, ila
punde mara baada ya kuanza tendo hili la Imani alianza kuzama. Petro hakunyamza,
wala hakufikiria kuzijizamisha kama wengine hivi leo wanavyofikiria kujiua, kwa
kujinyonga ama kunywa sumu. Bali rafiki yangu huyu alimuita Yesu. Na Yesu
alimsaidia.
Kitu cha
ajabu ambacho nimejifunza hapa kwa Petro ni hiki, Alikuwa akizama na Yesu alimuona,
ila hakumsaidia hadi pale Petro alipohitaji msaada. Na wewe ni kweli unazama
ama umechoka kiroho ama kimaisha na umefikia hatua yakutamani hata kuacha
Wokovu ama kunywa sumu au kujinyonga na hata kujitupa gorofani kwa sababu ya
ugumu wa maisha ama jambo fulani.
Ukikaa na
hali hiyo ni hakika dhamira hiyo itatimia kama ilivyokuwa kwa Yuda aliyetembea
na Yesu na kuwa mwanafunzi wake kisha kujinyonga. Nataka ujifunze nami hapa kwa
Petro, alianza kuzama ila Yesu hakumsaidia hadi alipoita na kuomba msaada na
wewe yamkini unajiuliza mbona unateseka hivyo na Mungu unaye, ama na Yesu unampenda
au kumuamini?
Jibu ni
kwamba bado hujahitaji msaada na ukihitaji Yeye ni mwaminifu atakujibu punde kama
ilivyokuwa kwa Petro. Mathayo 14:25-33, 30 Lakini alipoona upepo, akaogopa, akaanza
kuzama, akapiga yowe, akisema, “Bwana niokoe.” 31 Mara Yesu akanyoosha mkono
wake, akamshika, akamwambia, “Ewe mwenye imani haba mbona uliona shaka?”
Ni baada ya
Perto kupiga YOWE kwa kuomba msaada
na wewe piga YOWE mbele za Yesu leo kwa kufanya maombi ya kumuita ili akuokowe
katika pito hilo ama teso hilo. Hata kama hujaokoka wewe piga YOWE Yesu hakuja
kwa ajili ya waliokoka tu bali ni kwa kila mtu aliye wa uzao wa Ibrahimu ama
uzao ule wa Ishmaeli na hata wa Esau na wale wengine wa mataifa. Wote ni wake
kwani aliwafia wenye dhambi wala sio wenye haki. Walio wazima hawakuwa na haja
na tabibu ndio maana wagonjwa ndio waendao hosipitalini na wazima ni
wasindikizaji. Kwa hyo wewe ni mlengwa mkuu wa ujumbe huu.
Ukisha piga
Yowe hakika upepo unaokuzamisha utakoma kama ilivyokuwa kwa Petro mara baada ya
kushikwa mkono, na atapanda na wewe chomboni wala hutatembea tena juu ya hayo
maji yaliyokuzamisha. Tuendelee na msatari unaofwata.
Mathayo 14:32 Na walipopanda chomboni upepo ulikoma.
Siku moja
niliota ndoto iliyonishangaza sana, siku hiyo sio mbali sana bali ni wiki kama
mbili zilizopita. Niliota nikiwa na malaika aliyekuwa na umbo kama la
kibinadamu. Alikuwa akinipitisha msituni na pembezoni kwenye majabli makubwa,
kuna mahali alikuwa akinifikisha. Ila aliniacha nyuma mita kadhaa huku akigeuka
kila mara ili kuniangalia nilipo fika.
Ilifika
wakati nikashindwa kuvumilia kuachwa nyuma na kumuita huku nikimfahamisha
kwamba nashindwa kutembea sambamba naye kutokana na mguu wangu wa kushoto kuwa
na jeraha kwenye unyayo. Alikuja kwa haraka na kunitoa kijiti kirefu
kilichokuwa kimenichoma na pia alitoa
kipande cha jani la aina ya “Isaale” (Ni mmea unaopatika na sana kanda ya
kasikarini hususani Maeneo ya Uchagani na Arusha).
Nilishangaa
sana, kilicho nishangaza ni; Ni kwamba nilitembea naye kwa muda mrefu na huku
nikichechemea ama nikishindwa kutembea sawa ila hakunisaidia hadi pale
nilipohitaji msaada. Jambo hili lilinipa kujiuliza na kuhitaji kupata ufumbuzi
wa kina kuhusu kanuni hii.
Ndiposa nilipokumbuka
lile andiko lisemalo ya kwamba, “Aliwaponya wale waliokuwa na haja ya
kuponywa” Andiko hilo lipo kwenye kitabu cha Luka. Ni kweli Yesu
alikutana na watu wengi wenye uhitaji ama wenye matatizo ila hakumponya kila
mtu bali ni yule aliyeonyesha kuhitaji msaada wake. Hakika kipofu Baltomayo
angeomba fedha angepewa fedha ila aliomba uponyaji na kupewa uponyaji.
Tazama kisa
hiki, Kulikwepo na mama mmoja aliyetokwa na damu kwa muda wa miaka 12, ila siku
moja aliamua kushika pindo la Yesu ndipo alipopokea mujiza wake. Ni kweli
kwamba Yesu toka juu mbinguni aliona teso la mama huyu tangu mwaka na siku ya
kwanza na hata kabla halijamkumba ila aliachilia uponyaji pundea mara baada ya
mtu huyu kuhitaji msaada kutoka kwake.
Alipoenda
kwa wagaga Yesu alikaa kimwia, alipowaendea matabibu alijifanya kama vile
amuoni ila alipoamua kushika upindo wa vazi lake mara Yesu alishindwa kujizuia
na cha ajabu hata Yesu hakujua kuwa
nguvu zimemtoka na Yesu anakuja kugundua kuwa kuna mtu amepona baada ya mtu
kuponywa na nguvu zake.
Ona kitu
hapo, Kumbe Nguvu za majibu zilizopo kwa Yesu huweza kufanya kazi bila hata
Yesu mwenyewe kuziamuru kujua kama
utafwata kanuni.
Katika uzuri
huu kweli ipo haja ya wewe kuendelea kufikiria kujinyonga? Kujiua? Ama kuwaza
kujitupa baharini ama juu ya Ghorofa ili ufe?
Hapa, Mshike
Yesu, mwite kwa YOE kama Petro, Naye atakujibu tena wala sio kesho bali ni leo.
Hata kama hujui kuomba wewe, Sema tu, “YESU, NIOKOWE, YESU NINAKUHITAJI”
Maneno hayo
kama yameambatana na imani kama kwa Petro aliyetamka maneno mawili na Yesu
kumsaidia, (Bwana, niokoe), itakuwa
hivyo kwako leo.
Kama hujaokoka,
na unamuhitaji huyu YESU ili akusaidiye, ama ulirudi nyuma kiroho kwa sababu kadhaa,
tamka sala hii ya toba kwa imani na utakuwa umeunganishwa na nguvu za Yesu
Kristo. Sema.
“Bwana Yesu,
NIMEKUJA KWAKO, MIMI NI MWENYE DHAMBI, NINAKUAMINI, NINAKUPENDA NA KUKUPOKEA
MOYONI MWANGU LEO. TAFADHALI FANYIKA BWANA NA MWOKOZI WANGU. AMENI”
Hongera kwa
kuokoka na tafuta kanisa lolote la kiroho ama la watu waliokoka ukasali hapo.
Na umtafute Mchungaji umuelezee kilichotokea ili awe karibu na wewe kiroho
zaidi. Ameni.
Na Huduma ya
UKOMBOZI GOSPLE, Arusha Tanzania, Kwa Maombi, Ushauri, Maswali au Sadaka
wasiliana nasi, Barua pepe: ukombozigosple@gmail.com
Simu: +255 759 859 287 pia waweza itumia kwa M-PESA. Zaidi www.ukombozigosple.blogspot.com #UkomboziGosple #MwalimuOscarSamba
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni