Na Mwalimu Oscar Samba Ug Ministry |
Yesu
akawambia wanafunzi wake, “Natuvuke mapaka ng’ambo ya ziwa”
Luka 8:22. Kisha mbele yake kukatoke dhoruba kali iliyolenga kuwazuia wateule
hawa wa Mungu kulifikia kusudi la Mungu lilopo ng’ambo ya Ziwa.
Mariko 4:37Ikatokea dhoruba
kuu ya upepo, mawimbi yakakipiga chombo hata kikaanza kujaa maji. 38 Naye
mwenyewe alikuwapo katika Shetri, amelala juu ya mto; wakamwamsha, wakamwambia,
Mwalimu sii kitu kwako kuwa tunaangamia?” 39 Akaamka, akaukeme upepo, akaiambia
bahari, “Nyamaza utuliye!” Upepo ukakoma, kukawa shwari kuu.
Wanafunzi wa
Yesu walitambua fika ya kwamba inawapasa kufika ng’ambo ya Ziwa ili kukutana na
kusudi la kimungu huko kama Yesu alivyowataka wavuke, ila jaribu ama kikwazo
kilitokea, na walifahau hawapaswi kupiga mbio kurudi nyuma bali ni lazima
wasonge mbele. Na katika kusonga mbele upinzani upo, nawe usikubali kukata tamaa
badala yake yakupasa uvuke ng’ambo nyingine ili kukutana na mujiza wako hapo.
Wana wa
Iziraeli walipokuwa katika nchi ya mateso, Mungu aliwapa ahadi ya kuwapa maisha
ya Mziwa na Asali lakini mambo hayo hayakutokea kirahisi hadi walipopambana na
ugumu wa jangwa ama nyika.
Jangwani
kulikwepo na vikwazo vingi sana ikiwemo njaa, kiu, nyoka wa moto, hali
iliyosabisha vifo kwa wengi wao waliopopungukiwa na Imani. Na wewe ahadi
uliyopewa na Mungu ni lazima ipitiye katika jangwa ndiposa ufike katika ng’ambo
yako.
Ninakuta
kuwa mwepesi wa kumkimbilia Mungu kama ilivyokuwa kwa Musa na kama
nilivyokujuza kwenye sehemu ya kwanza ya makala hii.
Mungu
akubariki na endelea na wokovu ila Kesho usikose kwani nimeakuandalia makala
nzuri inayomtaja YESU kama mtuliza mawimbi ama dhoruba baharini.
Langu jina
ni Mwalimu Oscar Samba, ninakupenda na endelea kuifwatilia mafundisho haya pamoja na kuchota Baraka kwa kuiwezesha
huduma hii kwa sadaka yako.
Kama
hujaokoka na unataka kuokoa tafadhali fwatisha nami maneno haya kwa Imani,
Sema: BWANA YESU, NINAKUPENDA, NINAKIRI NA KAUMINI KUWA WEWE NI MUNGU, ULIKUFA
NA KUFUFUKA KWA AJILI YANGU, INGIA NDANI YANGU KAMA BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA
YANGU LEO, AMENI.
Hongera kwa
kuokoka na tafuta kanisa la watu waliokoka ukasali hapo.
Na Huduma ya
UKOMBOZI GOSPLE, Arusha Tanzania, Kwa Maombi, Ushauri, Maswali au Sadaka
wasiliana nasi, Barua pepe: ukombozigosple@gmail.com
Simu: +255 759 859 287 pia waweza itumia kwa M-PESA. Zaidi www.ukombozigosple.blogspot.com #UkomboziGosple #MwalimuOscarSamba
Pia #Like
#Penda Page/Ukurasa wetu au kundila Fb, ili kuupta habari hizi kwa haraka,
zaidi. Ug Ukombozi Gosple,
PAGE:
https://www.facebook.com/Ug-Ukombozi-Gosple
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni