Jumanne, 18 Julai 2017

NGUVU YA AGANO. Sehemu ya 14.

Na Mwalimu Oscar Samba wa Ug Ministry.
Ninakukaribisha ndugu msomaji wangu katika safu  hii ya mafundisho ya Neno la Mungu kupitia makala zetu, leo tunamalizia kulitazama kabila la Yuda.
Mstari unaofwata una mantiki ya aina yake katika hii Nguvu ya Kiagano,
12 Macho yake yatakuwa mekundu kwa mvinyo, Na meno yake yatakuwa meupe kwa maziwa.
Wekundu wa macho unawakilisha Ghadhabu na Mvinyo kulevia, weupe wa meno ni umaridadi wa maneno yake ama hotuba zake. Tukimtazama Yesu alikuwa ni mwenye hekima kinywani mwake na aliyekubalika kwa maneno yake.
Kwa uapnde wa Mvinyo ama kulevia na Ghadhabu wasomaji wa maandiko wanafahamu fika ya kwamba ipo silaha ya ajabu sana ya kupigania vita kwenye ulimwengu wa roho itwayo kikombe cha ghadhabu, kikombe hiki hulevia kisha huaribu na kuangamiza. Mimi binafsi hukitumia sana kikombe hiki ninapokuwa nikipigana vita vya kimaagano na mizimu. Maana hutambua silaha hii ina nguvu ya ziada katika hivyo vita.

NGUVU YA AGANO. Sehemu ya 13.

Na Mwalimu Oscar Sama wa Ug Ministry.
Asante Yesu Kristo kwa majira haya mazuri uliyonikutanisha na msomaji wangu huyu, Leo mpendwa ni sehemu ya kumi na tatu ya makala hii na tunaendelea kuitanzama Nguvu ya Agano kwa kabila la Yuda.
Tutaanze na ule Mstari wa kumi,
10 Fimbo ya enzi haitaondoka katika Yuda, Wala mfanya sheria kati ya miguu yake, Hata atakapokuja Yeye, mwenye milki, Ambaye mataifa watamtii.
Nisikilize, Baraka hizi zilinenwa miaka mingi ila zilibeba hatima nzima ya kiutawala na kifalume katika Iziraeli na Ulimwengu mzima.

Fimbo maana yake ni Mamlaka, tuna fahamu kuhusu habari za fimbo ya Haruni na Musa, kwa hiyo swala la Utawala katika Izireli lilikuwa chini ya kabila hili, ndio maana tunamuona Mfalume Daudi, Sulemani, na wengineo ambao walitoka katika hili kabila na kuwa watawala wenye historia kubwa.
Kisha anatajwa  Mwenye Miliki ambaye mataifa watamtii huyu sio mwingine bali ni YESU. Hii ni Nguvu ya Agano ya ajabu sana, ya kwamba usipo ifahamu unaweza ukaona mambo yanatokea kwenye maisha ukadhani yanakuja bahati mbaya ama kwa kubahatisha kumbe tayari mpangilio upo.
Jambo hili halikuishia hapo bali hata Nabii Isaya alilinena katika kulithibitisha kisha likaja jithiirisha katika Agano Jipya.
Ni Isaya 9: 6 Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, Tumepewa mtoto mwanamume; Na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake; Naye ataitwa jina lake, Mshauri wa ajabu, Mungu mwenye nguvu,

NGUVU YA AGANO. Sehemu ya 12.

Na Mwalimu Oscar Samba wa Ug Ministry.
Furaha ya leo iliyopo Moyoni Mwangu ni zaidi ya ile ya Jana, yamkini nimatokeo ya kuvushwa kwako kiroho kwa maudhui ya ujumbe wa jana. Leo ninakuletea matokeo ya baraka kwa makabila kumi na wawili ya Mzee Yakobo na uwenda nikapata kibali cha kudodosa machache ila ninaanza na kabila la Yuda. Tutaona siri ya Yesu kuitwa Simba wa kabila la Yuda ikiwa ni Jina la Kiagano huku wengine wakisalia bila kulijua hilo.

Katika kuwabariki wanaye ambao ndiyo makabila ya Iziraeli Mzee Yakobo aliwatamkia maneno ya baraka yaliyoambatana nao hadi kwenye hatima ya Maisha yao yote.
Tuone, Mwanzo 49: 1 Yakobo akawaita wanawe, akasema, Kusanyikeni, ili niwaambie yatakayowapata siku za mwisho.
2 Kusanyikeni, msikie, enyi wana wa Yakobo, Msikilizeni Israeli, baba yenu.
 

YUDA: Mwanzo 49: 8 Yuda, ndugu zako watakusifu, Mkono wako utakuwa shingoni mwa adui zako. Wana wa baba yako watakuinamia.
Jambo hili limekuwa halisi, kwani Mfalume Daudi, Yesu, Mfalume Sulemani, Ni miongoni Mwa watu waliosifiwa sana katika historia ya Bibilia kwani wao wote ni watu wa Yuda.

NGUVU YA AGANO.Sehemu ya 11.

Na Mwalimu Oscar Samba wa Ug Ministry
Ni Siku nyingine yenye fanaka tele na uzima mwingi rohoni, ni yangu maombi kukutakia uzima huo kwa jina la Yesu kwa wewe ulioukosa, pia udumu ndani yako kwa wewe ulio nao. Ni sehemu ya kumi na moja ya makala yetu ya Nguvu ya Agano ikiwa ni sehemu ya kitabu changu cha NGUVU YA AGANO KIROHO. Ninacho kibali cha kukuletea kwa njia hii ya mtandao Agano hili moja na uwenda pia nikakudokezea lile la Yoshua lenye mizizi yake kwenye Kitabu cha Torati ya Musa ila maagano mengine kama lile la Sinai, La Chumvi,  Jipya, Daudi na hata lile la Nuhu; Huna budi kuwa na subira hadi kitabu kitoke kisha ukinunuwe.

NGUVU YA AGANO. Sehemu ya 10.

Na Mwalimu Oscar Samba wa Ug Ministry.
Laiti kungalikuwa na miwani inayoweza kukuonyesha tabasamu nililonalo dhidi yako leo kupitia haya maandishi, ningali kuazima ama kukununulia; Ni fika kila uchwao huwa na furaha kukupakulia chakula hiki cha kiroho ila ya leo ina mapana yake.
Jana nilikupa ahadi ya kukuletea huu ujumbe nami sinabudi kuitimiza hususani katika uzao wa Yusufu. Yusufu ni miongoni mwa wana wa Mzee Yakobo aliyepitia misukosuko mingi na alishinda huku mingi ikiwa na sura ya kiagano, tuliona alivyomiliki malango ya adui zao huko Misiri. Pia kabla ya nduguze  kuhamia ama kushuka Misiri alikuwa amepata watoto wa wili. Manase na Efraimu.

Manase ndiye aliyekuwa wa kwanza na kisha kufwatiwa na Efraimu; Mwanzo 41: 50 Kabla ya kuja miaka ya njaa, Yusufu akazaliwa wana wawili, ambao Asenathi, binti Potifera, kuhani wa Oni, alimzalia.
51 Yusufu akamwita jina lake yule aliyezaliwa kwanza, Manase, maana alisema, Mungu amenisahaulisha taabu zangu zote, na nyumba yote ya baba yangu.
52 Na wa pili akamwita jina lake Efraimu, maana alisema, Mungu amenipa uzazi katika nchi ya mateso yangu.

NGUVU YA AGANO. Sehemu ya 9.

Na Mwalimu Oscar Samba wa Ug Ministry.
Asante Yesu kwa juma pili hii njema yenye kuvutia na ya fanaka, na pili ninakuta kimaombi kukaa na msomaji wangu huyu kwa kumsaidia kuelewa somo hili na kulifanyia kazi. Kumbuka ndugu yangu katika Bwana wetu YESU KRISTO leo ni siku ama ni sehemu ya tisa ya makala yetu hii na hapo jana nilianza kukudokezea sehemu muhimu sana ya hili Agao la Ibrahimu na Mungu lililochanua matunda kwa wana wa Iziraeli tukiwemo mimi na wewe.

UG Tv, ASANTE YESU, TUMEFANIKIWA KUFUNGUA OnLine Tv Yetu.