Jumanne, 18 Julai 2017

NGUVU YA AGANO.Sehemu ya 11.

Na Mwalimu Oscar Samba wa Ug Ministry
Ni Siku nyingine yenye fanaka tele na uzima mwingi rohoni, ni yangu maombi kukutakia uzima huo kwa jina la Yesu kwa wewe ulioukosa, pia udumu ndani yako kwa wewe ulio nao. Ni sehemu ya kumi na moja ya makala yetu ya Nguvu ya Agano ikiwa ni sehemu ya kitabu changu cha NGUVU YA AGANO KIROHO. Ninacho kibali cha kukuletea kwa njia hii ya mtandao Agano hili moja na uwenda pia nikakudokezea lile la Yoshua lenye mizizi yake kwenye Kitabu cha Torati ya Musa ila maagano mengine kama lile la Sinai, La Chumvi,  Jipya, Daudi na hata lile la Nuhu; Huna budi kuwa na subira hadi kitabu kitoke kisha ukinunuwe.


Baada ya baraka tulizo ziona kwa wana wa Yusufu ambazo  zililenga kuwafanya kuwa mataifa makubwa na sehemu ya makabila mawili huku wakiwa na baraka zote za kiagano kwa nguvu kama walizokuwa nazo baba zao  katika mukutadha huo, leo natamani tufike mbali ya hapo kidogo.
Kitabu cha Yoshua sura ile ya kumi na sita, kinadhibitisha jambo hili la urithi kwa Efraimu huku ikitendeka kama Yakobo alivyokwisha mgaia Yusufu, pia sura ya 17, inanena habari za Manase naye anapewa sehemu ya aridhi ya Kanani kama Agano lilivyoelekeza.
Majira haya nataka kukuonyesha kitu cha ziada kwa wana hawa maana tumeona jinsi ambavyo hili Agano limewapa kitu cha ziada katika urithi wa aridhi.
Ni Yoshua 17: 14 Kisha wana wa Yusufu wakanena na Yoshua, wakasema, Kwa nini umenipa mimi kura moja tu na fungu moja kuwa ni urithi wangu, kwa kuwa mimi ni taifa kubwa la watu, kwa sababu Bwana amenibarikia hata hivi sasa?
15 Yoshua akawaambia, Kwamba wewe u taifa kubwa la watu, haya, kwea uende mwituni, ujikatie mahali hapo kwa ajili ya nafsi yako katika nchi ya Waperizi, na ya hao Warefai; ikiwa hiyo nchi ya vilima ya Efraimu ni nyembamba, haikutoshi.
16 Wana wa Yusufu wakasema, Hiyo nchi ya vilima haitutoshi sisi; lakini Wakanaani wote wakaao katika nchi ya bondeni wana magari ya chuma, hao walio katika Bethsheani na miji yake, na hao walio katika bonde la Yezreeli pia.
17 Kisha Yoshua alinena na nyumba ya Yusufu, maana, ni Efraimu na Manase, akawaambia, Wewe u taifa kubwa la watu, nawe una uwezo mwingi; hutapata kura moja tu;
18 lakini hiyo nchi ya vilima itakuwa ni yako; maana, ijapokuwa ni mwitu, wewe utaukata, na matokeo yake yatakuwa ni yako; kwa kuwa wewe utawafukuza hao Wakanaani, wajapokuwa wana magari ya chuma, wajapokuwa ni wenye uwezo.


Haleluya, na hii ndiyo Nguvu ya Agano, ambayo ninakujuza kwayo, hakika hakuna lisilotimia katika Agano kama wewe muhusika utajitambua, kumbuka miongoni mwa Nia yangu ya kukujuza jumbe hizi ni kukutaka wewe kujitambua ili uweze kudai. Hapo tunawaona wana wa Yusufu wakidai kuongezewa urithi maana huku waligawiwa kura moja ila hawakurithika maana alifahamu fika ya kwamba kuna kitu cha ziada walichopewa katika huu urithi kiagano. Maana yake wasinge fahamu na kudai wangesalia na kura moja. Na wewe nakutaka ufahamu kisha udai yale ambayo Mungu amekuaidia kwenye uimwengu wa Roho.

Katika pwenti hii ya kufahamu kisha kudai ninamuona Roho Mtakatifu akinikumbusha jambo alilonifuza siku kadhaa zilizopita katika moja ya darasa la kimaagano. Nami ngoja nikumegee.

Kalebu aliaidiwa na Musa kupewa urithi katika nchi ambayo aliipeleleza ila wakati wa Yoshu anagawa Urithi huo, alilazimika kumkumbusha kuhusu ahadi hiyo huku akidai hiyo haki yake. Nataka kabla sijakupa maandiko hayo ndani mwako kujengeke Fikra za kumkumbusha Mungu kuhusu yale aliyowai kukuaidia.

Ni Yoshua 14: 6 Wakati huo wana wa Yuda walimkaribia Yoshua hapo Gilgali; na Kalebu, mwana wa Yefune, huyo Mkenizi, akamwambia, Wewe wajua hilo neno Bwana alilomwambia Musa, huyo mtu wa Mungu, katika habari zangu, na katika habari zako wewe, tulipokuwa katika Kadesh-barnea.
7 Mimi nilikuwa mtu wa miaka arobaini umri wangu, hapo Musa mtumishi wa Bwana aliponituma niende kutoka Kadesh-barnea ili kuipeleleza hiyo nchi; nami nilimletea habari tena, kama ilivyokuwa ndani ya moyo wangu.
8 Lakini wale ndugu zangu waliokwea kwenda pamoja nami waliiyeyusha mioyo ya watu; ila mimi nilimfuata Bwana, Mungu wangu, kwa utimilifu.
9 Kisha Musa akaniapia siku hiyo, akasema, Hakika hiyo nchi ambayo miguu yako imekanyaga itakuwa ni urithi kwako wewe, na kwa watoto wako milele, kwa sababu wewe umemfuata Bwana, Mungu wako, kwa utimilifu.
10 Sasa basi, angalia, yeye Bwana ameniweka hai, kama alivyosema, miaka hii arobaini na mitano, tangu wakati huo Bwana alipomwambia Musa neno hilo, wakati Israeli waliokuwa wakienenda barani; na sasa tazama, hivi leo nimepata miaka themanini na mitano umri wangu.
11 Hata sasa mimi nina nguvu zangu hivi leo kama nilivyokuwa siku hiyo Musa aliyonituma; kama nguvu zangu zilivyokuwa wakati huo, na nguvu zangu ndivyo zilivyo sasa, kwa vita na kwa kutoka nje na kuingia ndani.
12 Basi sasa unipe mlima huu, ambao Bwana alinena habari zake siku hiyo; kwani wewe ulisikia siku hiyo jinsi Waanaki walivyokuwa huko, na miji ilivyokuwa mikubwa yenye boma; yumkini yeye Bwana atakuwa pamoja nami, nami nitawafukuza watoke nje, kama Bwana alivyonena.
13 Yoshua akambarikia, akampa Kalebu, huyo mwana wa Yefune, Hebroni kuwa urithi wake.
14 Kwa hiyo Hebroni ukawa urithi wa Kalebu, mwana wa Yefune, Mkenizi, hata leo; kwa sababu alimwandama Bwana, Mungu wa Israeli, kwa utimilifu.
15 Basi jina la Hebroni hapo kwanza uliitwa Kiriath-arba; huyo Arba alikuwa ni mtu mkubwa kupita wenziwe wote katika hao Waanaki. Hiyo nchi nayo ikatulia, vita vikakoma.


Nimetumia Nguvu kubwa kukuletea hayo maandiko ili jambo hili la kudai likae ndani ya Moyo wako kikamilifu, ni yangu kiu kukuona ukifanikiwa kwa njia hii ya kiagano maana mafanikio yake yakaa milele.

Majira haya nataka turudi kwenye kitabu kile cha Mwanzo maana kuna jambo nililiruka ama twapaswa kuendelea na mfululizo ule. Jambo hilo ni namna baraka za Yakobo kwa wanawe 12, zilivyokuja kuwa na Nguvu katika hatima yao yote ya kimaisha ndani ya Bibilia na hata leo.
Tutaanze kumtazama Yuda,...
Mpendwa wangu katika Bwana muda wangu umekuwa ni kikwazo kikuu cha kukuletea jambo hilo kiunaga ubaga, ila hakika kesho utalipata barahabara.
Kama hujaokoka na unataka kuokoka ama ulirudi nyuma kiroho na unataka kutengeneza na BWANA kwa upya leo, tafadhali fwatisha nami maneno haya kwa Imani, Sema: BWANA YESU, NINAKUPENDA, NINAKIRI NA KUAMINI MOYONI MWANGU KUWA WEWE NI MUNGU, ULIKUFA NA KUFUFUKA KWA AJILI YANGU, INGIA NDANI YANGU KAMA BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YANGU LEO, AMENI.
Hongera kwa kuokoka na tafuta kanisa la watu waliokoka ukasali hapo.

Na Huduma ya UKOMBOZI GOSPEL, Arusha Tanzania, Kwa Maombi, Ushauri, Maswali au Sadaka wasiliana nasi, Barua pepe: ukombozigospel@gmail.com  Simu: +255 759 859 287 pia waweza itumia kwa M-PESA. Zaidi www.ukombozigospel.blogspot.com   #UkomboziGospel  #MwalimuOscarSamba
Pia #Like #Penda Page/Ukurasa wetu au kundi la Fb, ili kupata habari hizi kwa haraka, zaidi. @ugukombozi Gospel 
 PAGE: https://www.facebook.com/ugukombozigospel/
Pia kwenye mtando Mpya wakitanzania wa
 Pia TAZAMA VIDEO ZETU HAPA  https://www.youtube.com/channel/UCv1tghnugOSpbmb5h6ebJtA  (Ukombozi Gospel)


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni