Jumanne, 18 Julai 2017

NGUVU YA AGANO. Sehemu ya 9.

Na Mwalimu Oscar Samba wa Ug Ministry.
Asante Yesu kwa juma pili hii njema yenye kuvutia na ya fanaka, na pili ninakuta kimaombi kukaa na msomaji wangu huyu kwa kumsaidia kuelewa somo hili na kulifanyia kazi. Kumbuka ndugu yangu katika Bwana wetu YESU KRISTO leo ni siku ama ni sehemu ya tisa ya makala yetu hii na hapo jana nilianza kukudokezea sehemu muhimu sana ya hili Agao la Ibrahimu na Mungu lililochanua matunda kwa wana wa Iziraeli tukiwemo mimi na wewe.


Tunawatazama wana wa Iziraeli na ikumbukwe kuwa hata kuishi kwao hapa yaani Misiri  ni sehemu ya agano hili ambalo Mungu amefunga nao. Kama vile Mungu alivyo wasaidia kuwazidisha kiuzao hapa ndivyo ilivyokuwa.
Jambo la Kwanza nilitakalo ulioone kabla la Uzao ni hili la Mali. Kazi kuu ya wana wa Iziraeli ilikuwa ni Ufugaji.Na kwa Wamisiri swala la Ufugaji wa mifugo lilikuwa ni chukizo, ila Mungu kwa kuwa ni Mungu na huliheshimu Agano lake aliwapa kibali cha watu hawa kufuga mifuko huko na kisha kufanikiwa. Kumbuka hata katika kuondoka kwao waliondoka na hiyo mfugo kwani hawakuacha hata Ukwato.
Ona jinsi Farao alivyoridhia jambo hilo. Mwanzo 47: 5 Farao akamwambia Yusufu, akisema, Baba yako na ndugu zako wamekujia;
6 nchi ya Misri iko mbele yako, palipo pema pa nchi uwakalishe baba yako na ndugu zako; na wakae katika nchi ya Gosheni. Tena ukijua ya kuwa wako watu hodari miongoni mwao, uwaweke wawe wakuu wa wanyama wangu.
Nguvu ya Agano, itakupa kufanya biashara katika mazingira ambayo wenzako wanasema hapa ruhusiwi. Hukusheria zote za mji na majiji zikipinga, taratibu na tamaduni ila Nguvu ya kiagano hushuka na kukufanikisha hapo maana nilazima utajirike.
Fahamu kuwa katika hii nchi Uzao wao ndipo ulipoongezeka kwani walishuka wakiwa watu wasiofika mia moja, ni takiribani watu sabini. Ila walitoka wakiwa wengi. Kutoka 1: 5 Na nafsi zile zote zilizotoka viunoni mwa Yakobo zilikuwa ni nafsi sabini; na huyo Yusufu alikuwa huko ndani ya Misri tangu hapo.
7 Na wana wa Israeli walikuwa na uzazi sana, na kuongezeka mno, na kuzidi kuwa wengi, nao wakaendelea na kuongezeka nguvu; na ile nchi ilikuwa imejawa na wao.
Kesho Mungu akijalia nitakuonyesha jambo la Ajabu sana ambalo Mungu amenijuza Muda huu, Nalo ni kuhusu wana wa Yusufu jinsi Nguvu ya Agano hili lilivyoamua ni yupi wakuwekewa mkono wa baraka wa kuume na kushoto huku likitokea jambo la utofauti sana kwa Manase na Efraimu kuingizwa katika  wanaa  12 wa Yakobo yaani Iziraeli na tutaenda hadi kule Kanani kwenye kitabu kile cha Yoshu kutazama Urithi wao na nitakujuza ama kwa mtaji huo utakuwa umefahamu kwanini kwenye kitabu cha Yoshua wanatajwa kama makabila mawili tena yenye Nguvu.

Ni jambo lenye utofauti mkubwa na katika yote hayo usiache kuungana nami kesho ili kujipatia MANA hiyo iliyo adimu na Adhimu. Kiu yangu ni kukutaka wewe ambaye umeokoka kumshika sana Yesu ili mambo haya matamu yawe alisi kwako. Pia kwako wewe ambaye  bado hujaokoka kufanya hivyo ili kukusaidia kuzifikilia hizo baraka.
Na Huduma ya UKOMBOZI GOSPEL, Arusha Tanzania, Kwa Maombi, Ushauri, Maswali au Sadaka wasiliana nasi, Barua pepe: ukombozigospel@gmail.com  Simu: +255 759 859 287 pia waweza itumia kwa M-PESA. Zaidi www.ukombozigospel.blogspot.com   #UkomboziGospel  #MwalimuOscarSamba
Pia #Like #Penda Page/Ukurasa wetu au kundi la Fb, ili kupata habari hizi kwa haraka, zaidi. @ugukombozi Gospel 
 PAGE: https://www.facebook.com/ugukombozigospel/
Pia kwenye mtando Mpya wakitanzania wa
 Pia TAZAMA VIDEO ZETU HAPA  https://www.youtube.com/channel/UCv1tghnugOSpbmb5h6ebJtA  (Ukombozi Gospel)


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni