Jumanne, 18 Julai 2017

NGUVU YA AGANO. Sehemu ya 10.

Na Mwalimu Oscar Samba wa Ug Ministry.
Laiti kungalikuwa na miwani inayoweza kukuonyesha tabasamu nililonalo dhidi yako leo kupitia haya maandishi, ningali kuazima ama kukununulia; Ni fika kila uchwao huwa na furaha kukupakulia chakula hiki cha kiroho ila ya leo ina mapana yake.
Jana nilikupa ahadi ya kukuletea huu ujumbe nami sinabudi kuitimiza hususani katika uzao wa Yusufu. Yusufu ni miongoni mwa wana wa Mzee Yakobo aliyepitia misukosuko mingi na alishinda huku mingi ikiwa na sura ya kiagano, tuliona alivyomiliki malango ya adui zao huko Misiri. Pia kabla ya nduguze  kuhamia ama kushuka Misiri alikuwa amepata watoto wa wili. Manase na Efraimu.

Manase ndiye aliyekuwa wa kwanza na kisha kufwatiwa na Efraimu; Mwanzo 41: 50 Kabla ya kuja miaka ya njaa, Yusufu akazaliwa wana wawili, ambao Asenathi, binti Potifera, kuhani wa Oni, alimzalia.
51 Yusufu akamwita jina lake yule aliyezaliwa kwanza, Manase, maana alisema, Mungu amenisahaulisha taabu zangu zote, na nyumba yote ya baba yangu.
52 Na wa pili akamwita jina lake Efraimu, maana alisema, Mungu amenipa uzazi katika nchi ya mateso yangu.


Ingawaje baadaye walikuja kuzaliwa wengine ila mie nataka twende na hawa wawili kwani kuna kitu kikubwa cha kiagano kilichukuwa juu yao.
Kabla ya kifo cha Mzee yakobo yaani babu yao na Manase na Efraimu alihitaji kuwabariki watoto hawa, na alizinena baraka za kiagano kwao, kilichonishangaza ni yeye kuwaongeza katika uzao wake wa kabila kumi na mbili, kisha jambo hilo kutimia katika kuirithi Kanani ikiwa ni matokeo ya mema ya Yufusu baba yao.

Kikubwa hapa kwangu kabla sijakuonyesha maandiko haya ni hiki hapa: Hakikisha na wewe unaupendezesha uso wa Mungu kwa gharama yoyote ile hata kama itakuwa ni yakupitia katika mapito magumu ili Mungu afanye kitu cha ziada kwako na kwa uzao wako, Tukiona kilichotokea baadaye utafahamu kuwa Manase na Efraimu wanaitwa mataifa kubwa ama makabila yenye nguvu ikiwa ni matokeo ya wema na uhodari wa baba yao.

Swali kwako, ni hili; Unaacha urithi gani kwa wanao? Je, Ukifa leo Mungu atasema ninalikumbuka Agano nililofunga na baba yako ama mama yako nami nitafanya haya na yale?
Ni jambo la msingi sana kwa wale wenye kuyaelewa haya mambo kiroho. Kitu cha pili hapa ni kile cha Mzee Yakobo kumuwekea Efraimu mkono wa kuume jambo ambalo kikawaida angaliwekewa mtoto wa kwanza ambaye ni Manase.
Nataka kukusaidia hapo, kwa Yakabo na Esau tulisema kuwa Esau aliuza uzaliwa wake wa kwanza, ila hapa hatuoni chakula cha dengu bali tunaona nguvu ya kiagano kwa mfumo wa aina yake.
Jambo hili linauwalisia hadi leo, wapo watu wanaokuwa pamoja kiutumishi gafula wanashangaa mtu waliomdharau ama kumuona wa kawaida Mungu anampandisha na kumuinua juu kuliko wao na swala hilo linakuwa kama kaa la moto kooni mwao; Nisikilize nikukwamuwe hapo, Baraka zakiagano zina macho yake na wakati mwingine zina sababu yake katika kutembea na watu.

Esau alipewa urithi wake katika milima, Yakobo katika Kanani na uzao wake, Ishmaeli alipewa katika jangwa la Parani na kuwa mpiga upinde huko, Ila Isaka alirithi mali zote za babaye huku watoto wa masuria wa Mzee Ibrahimu wakipewa zawadi tu. Fahamu maana ya zawadi, ina maana kuwa wangeweza kupewa ama wasipewe, na hutokana kiwango cha mtoaji bila kuhojiwa, badala yake wapaswa kuipokea kwa sangwe na nderemo hata kama ni pipi. Lakini kibaolojiwa wote ni watoto wa Yakobo, Isaka ama hapo kwa Ibrahimu, na huku kwa Yusufu; ila kimungu kila mtu anasehemu yake inapofika swala la uriti wa kiagano, ikiwa ni wamjakazi ama wa muungwana, ni Esau ama Yakobo, alikadhalika ni Manase au ni Efraimu.
Tuanze na baraka hizi za Kuwa makabila kisha tutaangazia zile za Kanani.
Lakini awali ya yote tuanze na utangulizi huu wa mzee Yakobo kwa mwanaye unaolenga kumjuza kuwa ninachoenda kukifanya sio cha kwangu miye bali ni kitu cha kiagano ndiposa anahusisha maswala yote muhimu yaliyopo kwenye hili Agano la Ibrahimu na Mungu.
Mwanzo 48: 3 Yakobo akamwambia Yusufu, Mungu Mwenyezi alinitokea huko Luzu, katika nchi ya Kanaani, akanibariki,
4 akaniambia, Mimi hapa, nitakuongezea uzao wako, na kukuzidisha, nami nitakufanya uwe kundi la mataifa; kisha nitawapa wazao wako nchi hii baada yako, iwe milki ya milele.
5 Basi sasa wanao wawili uliozaliwa katika nchi ya Misri kabla sijaja kwako Misri ni watoto wangu, yaani, Efraimu na Manase watakuwa wangu, kama Reubeni na Simeoni.
6 Na wazao wako utakaozaa baada ya hawa watakuwa wako; kwa jina la ndugu zao wataitwa katika urithi wao.
Umeona hilo jambo? Wajukuu wanaingizwa katika nafasi ya watoto, cha ajabu tena na watakao zaliwa waliingizwa ama walipewa ofa yakuitwa majina ya baba zao wakubwa ama mdogo kabla ya kuzaliwa, ikiwa na maana kwamba walipewa kitu cha kiagano cha ziada kabla hata hawajajulikana. Fahamu kuwa Agano lina Nguvu kwako kabla hata haujazaliwa, na uzaliwapo “otomatikali” unakuwa sehemu ya hilo Agano.
Tusonge mbele; 13 Yusufu akawaweka wote wawili, Efraimu katika mkono wake wa kuume, kuelekea mkono wa kushoto wa Israeli; na Manase katika mkono wake wa kushoto, kuelekea mkono wa kuume wa Israeli, akawasogeza karibu naye.
14 Israeli akanyosha mkono wake wa kuume akauweka juu ya kichwa cha Efraimu, aliyekuwa mdogo, na mkono wake wa kushoto akauweka juu ya kichwa cha Manase, huku akijua atiavyo mikono; maana Manase ndiye aliyezaliwa kwanza.
Hilo jambo hapo alilifanya Yusufu ili kutimiza lililopo moyoni mwake, ila Agano halipo hivyo, haijalishi Mchungaji wako ama wazee wakanisa wanakupenda au laa, wazazi au jamaa yako, ila inapofika wakati wa baraka za kiagano hakuna anayeweza kuingiza mawazo yake hapo. Kwani mbeleni nitakuonyesha kilichotokea lakini kama upo makini hapo umeshaona mkono wa kuume wa Mzee Yakobo ulipoelekea kinyume na mbinu ya Yusufu. Yamkini unaniambia Mwalimu unanifundisha nini hapa?
Ni hiki hapa: Usijipiganiye ilikupata baraka hizi, wewe cha msingi kaa kwenye mapenzi makamilifu ya Mungu wako, kwani mwisho wa siku kitajulikana tu, kwamba wewe ni Manase au ni Efraimu, Ni mwana wa mungwana ama mjakazi.
Tuone, nani ni nani majira haya; Mwanzo 48: 17 Yusufu alipoona kwamba babaye anaweka mkono wake wa kuume juu ya kichwa cha Efraimu, ikawa vibaya machoni pake. Akauinua mkono wa babaye auondoe katika kichwa cha Efraimu, ili auweke juu ya kichwa cha Manase.
18 Yusufu akamwambia babaye, Sivyo, babangu, maana huyu ni mzaliwa wa kwanza; weka mkono wako wa kuume kichwani pake.
19 Babaye akakataa, akasema, Najua, mwanangu najua, yeye naye atakuwa taifa, yeye naye atakuwa mkuu; lakini ndugu yake mdogo atakuwa mkubwa kuliko yeye, na uzao wake watakuwa wingi wa mataifa.
20 Akawabariki siku ile akasema, Katika ninyi Waisraeli watabariki, wakisema, Mungu na akufanye kama Efraimu na Manase. Akamweka Efraimu mbele ya Manase.

Umeipata hiyo taswira nyofu hapo? Sentesi hii imenifuraisha na kunithiirishia, hususani anaporudia mara mbili neno najua, ikithibitisha kuwa halikuwa tukio la bahati mbaya. “19 Babaye akakataa, akasema, Najua, mwanangu najua, yeye naye atakuwa taifa,...

Kuna kitu mubashara nilikiruka hapo awali, nami nataka kukujuza, Ni hiki, Yakobo anaachilia baraka hizi, lakini anathibitisha kuwa sio za kwake bali ni zakiagano, ndiposa anamtaja Mungu kama Mungu wa baba zake, Isaka na Ibrahimu, kisha anathibitisha jambo muhimu ama mambo muhimu yaliyopo kwenye hili Agano ikiwemo la Uzao.
(Mwanzo 48: 15 Akambariki Yusufu, akasema, Mungu ambaye baba zangu, Ibrahimu na Isaka, walienenda mbele zake, yeye Mungu aliyenilisha, maisha yangu yote, hata siku hii ya leo,
16 naye Malaika aliyeniokoa na maovu yote, na awabariki vijana hawa; jina langu na litajwe juu yao, na jina la baba zangu, Ibrahimu na Isaka; na wawe wingi wa watu kati ya nchi.)

Waoo!! Inasahangaza sana kuifahamu bibilia kwa sura ya namna hii yenye kutia ladha Akilini na Nafsini, Tafadhali kubali ombi langu la kukutaka tuishiye hapa leo ili kesho asubui na mapema nikuletee sehemu ya 11 ya somo hili huku nikianza na kipengele kile cha Kanani ama uthibitisho wa wao kuwa kabila kubwa ama taifa kubwa.
Nakutaka sana kutengeneza na Bwana leo kwani ni jambo lenye umuhimu mkubwa mno ili uweze kuwa sehemu ya hili Agano kiukamili na kiudhairi, sina la ziada bali kiukweli kama hujaokoka hakikisha unafanya hivyo leo.
Kama hujaokoka na unataka kuokoka ama ulirudi nyuma kiroho na unataka kutengeneza na BWANA kwa upya leo, tafadhali fwatisha nami maneno haya kwa Imani, Sema: BWANA YESU, NINAKUPENDA, NINAKIRI NA KUAMINI MOYONI MWANGU KUWA WEWE NI MUNGU, ULIKUFA NA KUFUFUKA KWA AJILI YANGU, INGIA NDANI YANGU KAMA BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YANGU LEO, AMENI.
Hongera kwa kuokoka na tafuta kanisa la watu waliokoka ukasali hapo.

Na Huduma ya UKOMBOZI GOSPEL, Arusha Tanzania, Kwa Maombi, Ushauri, Maswali au Sadaka wasiliana nasi, Barua pepe: ukombozigospel@gmail.com  Simu: +255 759 859 287 pia waweza itumia kwa M-PESA. Zaidi www.ukombozigospel.blogspot.com   #UkomboziGospel  #MwalimuOscarSamba
Pia #Like #Penda Page/Ukurasa wetu au kundi la Fb, ili kupata habari hizi kwa haraka, zaidi. @ugukombozi Gospel 
 PAGE: https://www.facebook.com/ugukombozigospel/
Pia kwenye mtando Mpya wakitanzania wa

 Pia TAZAMA VIDEO ZETU HAPA  https://www.youtube.com/channel/UCv1tghnugOSpbmb5h6ebJtA  (Ukombozi Gospel)

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni