Alhamisi, 27 Februari 2020

JIFUNZE KUMTUMAINI BWANA.

Na Mwal Oscar Samba

“Mtumaini Bwana kwa moyo wako wote, Wala usizitegemee akili zako mwenyewe” Mithali 3: 5.
Akili zako zinza mipaka, ufahamu wako kuna mahali unafikia ukingoni, utashi wako na upeo wako “ni-limited” nikiwa na maana kuwa kuna mahali unaishia, ila ukuu wa Mungu huvuka na ushinda ufahamu wote, ni yote katika yote.
“Je! Wewe hukujua? Hukusikia? Yeye Mungu wa milele, Bwana, Muumba miisho ya dunia, hazimii, wala hachoki; akili zake hazichunguziki.” Isaya 40:28.
Embu nenda name sanjari katika andiko hili; “Msijisumbue kwa jambo lo lote, bali katika kila jambo kwa kuomba na kusihi pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu. Nayo amani ya Mungu, inayopita fahamu/akili zote, itawalinda/hifadhi mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu.” Wafilipi 4.6-7.

Ina maana kwamba, unapokuwa taabuni, au katika adha, kitu kimoja wapo Mungu anachokifanya ni kuachilia Amani yake, ambayo huzidi akili zako, na ufahamu wako, ikiwa na mantiki kwamba ukiiruhusu ndani yako, akili yako au ufahamu wako utapata utulivu, na njia moja wapo ya kuiruhusu ni moja tu ambayo ni kuweka Imani na tumaini lako kwa Mungu, ni kweli tumeumbwa ili kutumia akili ila sio kuitegemea, wa kutegemewa au kutumainiwa ni Mungu pekee !

Kwa nini ? kwa sababu akili na uelewa wetu huwa na mipaka ! madakitari hutegemea akili zao, ufahamu na maarifa yao, wakishindwa watakwambai hapa hatuwezi, wanasheria au mawakili watakueleza kuwa hapa haiwezekani, mazingira ya uchumi au kiuchumi, ama mapito kwenye ndoa, au ugumu fulani unaweza kufikia mahali na kukueleza au kukwambia kuwa hili haliwezekani tena ! ni kweli na ni jibu zuri kabisa maana akili zetu zina mipaka!