Jumatatu, 13 Desemba 2021

SULUHU KWA JAMIII AU ENEO LENYE KUKABILIWÀ NA TATIZO LA WATU KUJIUA

Na Mwalimu Oscar Samba

Mithali 28:17 Aliyelemewa na damu ya mtu Atalikimbilia shimo; wala mtu asimzuie.

Andiko hilo hapo la Mithali linatupa kufahamu kuwa watu wanaojiua au kukimbilia mauti (ambao hapo imetumika au yametumika maneno kukimbilia shimo) ni matokeo ya kulemewa au kuwa na deni au mzigo wa damu iliyowahi kumwagika.

Sasa inawezekani aliimwaga yeye, au imemwaga kwenye eneo anaoloishi ama i juu ya uzao au jamii yake. Kwa ujumla ni kwamba kuna deni juu yake.

Damu huweza kukaa kwenye uzao nasi twajua hivyo, maana hata wale waliomsulibisha Yesu walikiri kuwa iwe juu yao na uzao wao. Pia eneo laweza kubeba damu maana hata aridhi iliyonunuliwa na fedha za usaliti wa Yuda ilitwa konde la damu.

Lakini pia damu ya Habili ililia kutoka aridhini. Kuna somo au kipengele cha kwenye kitabu fulani nichowahi kukiandika kinaitwa, ARIDHI KAMA KIUMBE HAI. Hapo nafunza vyema namna ya kushughulika na mambo kama haya.

Jumatano, 24 Novemba 2021

NI JUKUMU LAKO KUITUMIA MAMLAKA Mathayo 28:18










Mathayo 28:18 Yesu akaja kwao, akasema nao, akawaambia, Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani.

Ni wajibu na jukumu lako, na jitihada zako kuhakikisha ya kwamba unaweka imani na unaipa matendo tena kwa kujiamini ili mamlaka hiyo iweze kuwa halisi kwako.

Wewe ni sawa na askari mwenye bunduki, aspojua kuitumia bado hataweza kumdhuru adui. Na adui akijua muhuska hajui kuitumia basi naye hatamuogopa.

Tumia mamlaka uliyonayo vilivyo.

*Kumbuka* : Sio Jukumu la Yesu kuitumia. Ni lako. Yesu yupo kuiwezesha ifanaye kazi.

Ni muhimu kulielewa hili maana kuna wakati tunamlaumu Yesu na kumuona hajatusaidia kanakwamba Yeye ndie aliyepaswa kuitumia..hapana..alipokabithiwa yote ama vyote, alitukabithi sisi.

Nikikupa bunduki, usipofwetua risasi ni makosa kuilaumu bunduki ama aliyekukabithi... www.ukombozigospel.blogspot.com

 

Alhamisi, 18 Novemba 2021

Maelekezo Muhimu kwa Watumishi na Wapendwa

 Kuna wakati tunampa adui nafasi sisi wenyewe, wanapata nafasi ya kutushitaki kutokana na makosa ya ulimi na mwenendo.


Ila tukijifunza kutenda vyema, kwa akili kama Daudi alivyokuwa akitegewa mitego na mfalme Sauli kisha naye kutenda kwa maarifa, hakika adui hatapata uhalali wa kututia hatiani.


Hata akipambana itakuwa ni kwa hila tu, na hila zinamwisho wake.


1 Samweli 18:21 Naye Sauli akasema moyoni, Mimi nitamwoza huyu, awe mtego kwake, tena kwamba mkono wa Wafilisti uwe juu yake. Basi Sauli akamwambia Daudi mara ya pili, Leo utakuwa mkwe wangu.


:29 Naye Sauli akazidi kumwogopa Daudi; Sauli akawa adui yake Daudi sikuzote.


Mbinu pekee ya kumshinda adui wa namna hii ni kutenda kwa akili, hususani adui anapokuwa ni mwenye nafasi fulani ikiwemo kubwa kukuzidi kama ya mchungaji wako, mwangalizi, askofu na kadhalika, na hata mkuu wako wa idara au kiongozi fulani.


Ama akiwa ni mwanandoa mwenzako. Busara inahitajika siku zote, maana kwa nafasi yake anaweza kukushitaki na kukuhesabia hatia japo nia yake sio kosa alilokushitakia bali ni ile chuki iliyopo moyoni, na wewe ili kumdhibiti ni kuhakikisha unamnyima nafasi.



:30 Wakati huo wakuu wa Wafilisti wakatoka; kisha ikawa, kila mara walipotoka, Daudi akatenda kwa busara zaidi ya watumishi wote wa Sauli hivyo jina lake likawa na sifa kuu.


Zaidi tembelea:

www.ukombozigospel.blogspot.com


Zaburi 119:110 Watendao uovu wamenitegea mtego, Lakini sikuikosa njia ya mausia yako.


Jumanne, 5 Oktoba 2021

KUPENDA MAFUNDISHO au NENO

 Na Mwalimu Oscar Samba

Ujumbe huu ni sehemu ya kitabu chetu cha NGUVU YA NENO LA MUNGU KWENYE MAISHA YA MWANADAMU, pwenti ya; . PENDA MAFUNDISHO. Kiu ya Mafundisho imepotea kwenye kanisa leo; kuna kiu ya mambo mengine! Hata kwa wale wenye kiu ya Kiungu, wamejikuta wakitekwa na misisimko wa wahubiri wenye mbwembwe na kujisifia mali, na vitu vya dunia hii sanjari na ujanja wa maneno kuliko neno la kweli na yale yenye maarifa ya kiungu ndani yake. Itisha semina ya VIKOBA au ujasiriamali kanisani, utashangaa hata mwenye wiki tatu ambaye hajaja kanisani atakavyowahi, siku hiyo hakuna mchelewaji! Tuendelee;

Mahubiri, mawaitha ya Yesu,

Jumatano, 29 Septemba 2021

KWETU NI MBINGUNI



Waebrania 13:14 Maana hapa hatuna mji udumuo, bali twautafuta ule ujao.

Sijui wewe! Ila nijualo ni kwamba Sisi Tuliokoka, ama Tuliomuamini Bwana Yesu kwetu ni Mbinguni hapa Duniani sio kwetu!

Ni sawa na kituo cha Mabasi cha Ubungo ama kile cha Mbezi, ni sawa na stendi ya Daladala au Matatu! 

Hapa Duniani ni sawa na Njiani..mimi sijafika wala wewe hujafika, bali tunapaswa kukaza mwendo, huku tukiwa na taraja ama shabaha yetu ikiwa ni kuvikwa taji ama kupata Thawabu ile isiyoharibuka..

Kwa hiyo huna haja ya kujitaabisha na mateso na shida ama manyanyaso ya dunia hii..

Jumanne, 28 Septemba 2021

Mtazame Yesu Sio Wimbi

 

MTAZAME YESU NA SIO WIMBI

Mathayo 14:29 Akasema, Njoo. Petro akashuka chomboni, akaenda kwa miguu juu ya maji, ili kumwendea Yesu.

30 Lakini alipouona upepo, akaogopa; akaanza kuzama, akapiga yowe, akisema, Bwana, niokoe.

Sijui umekwamia wapi..? Nina chojua ni kwamba ulianza au ulipokea wazo hilo la biashara katika imani kubwa, na moyoni mwako ulisema huyu ni Mungu ndie aliyenipatia wazo hili, kazi hii, mke au mume huyu..ila mara baada ya kuanza kumeanza kuinuka vikwazo naq ghafula ukajikuta unaanza kukata tamaa kiasi cha kuyumbisha imani yako sio katika hilo jambo tu bali hata kwa Mungu kama kweli ulimsikia sawasawa ama kama kweli bado yu pamoja nawe..


Alhamisi, 16 Septemba 2021

KARAMA YA KUONYA

Bwana Yesu asifiwe ndugu yangu katika Bwana. Hapana shaka u mzima tena buheri wa afya? Kama sivyo basi Bwana Yesu akupe amani na furaha tele, huku ukimtwika Yeye yale yaliyokulemea na iruhusu furaha yake itawale maisha yako.

Leo Bwana amenipaka mafuta kukuletea ujumbe huu muhimu sana. Sio mara kwa mara utasikia ukifundishwa japo ni kitu ambacho hutakiwa kukifanya kila sehemu. Mashuleni kuna maonyo, kazini, njiani, kwenye vyombo vyetu vya usafiri utasikia nako wakionyana, kwenye makusanyiko mbalimbali hili nalo lipo. Nyumbani na hata makanisani twapaswa kuonyana.

Nawiwa kukueleza kwa upana wake namna ambavyo tunapaswa kuonyana, na jinsi ambavyo karama hii hutakiwa kuwa na vitu muhimu ambatanishi aidha iwe tabia au roho fulani au karama saidizi kwayo. Haijalishi ni karama zinazojitegemea ila hapa zinapaswa kuambatana na hii, alikadhalika tabia ama tunda la Roho.

MSINGI WA KARAMA KIUJUMLA

1 Wakorintho kinaeleza kiupana kuhusu aina 9 za karama, na mbele yake kuna huduma tano zinatajwa. Lengo la karama na huduma ni kujenga mwili wa Kristo kama Waefeso inavyotanabaisha;

Ijumaa, 30 Julai 2021

UPENDO WA MUNGU KWAKO NI WA MILELE, HAUFUNGWI NA MSIMU WALA MUDA

Na Mwalimu Oscar Samba

Ujumbe hu ni Sehemu ya Kitabu chetu cha MUNGU ANAKUPENDA. Kitabu kinachonuia kukusaidia kuliona pendo lake hata kama upo wakati mgumu, ukifahamu kuwa haupitii kwa sababu Mungu amekuacha, hakupendi ama amekukatataa.

Yeremia 31:3-7

Bwana alinitokea zamani, akisema, Naam nimekupenda kwa upendo wa milele, ndiyo maana nimekuvuta kwa fadhili zangu.
 Mara ya pili nitakujenga, nawe utajengwa, Ee bikira wa Israeli mara ya pili utapambwa kwa matari yako, nawe utatokea katika michezo yao wanaofurahi. Mara ya pili utapanda mizabibu juu ya milima ya Samaria; wapanzi watapanda, nao watayafurahia matunda yake.
Maana kutakuwa siku moja, ambayo walinzi watalia juu ya vilima vya Efraimu, Inukeni, tukaende Sayuni, kwa Bwana, Mungu wetu.
Maana Bwana asema hivi, Mwimbieni Yakobo kwa furaha, mkampigie kelele mkuu wa mataifa, tangazeni, sifuni, mkaseme, Ee Bwana, uwaokoe watu wako, mabaki ya Israeli.

 

Jumatano, 21 Julai 2021

KAWIA UFIKE

 Na Mwalimu Oscar Samba

Ni kweli ngoja ngoja huumiza matumbo, au fahamu pia simba mwendapole ndie mla nyama! Maana mtaka yote kwapupa hukosa yote! Hawakuwahi kukosea waliosema kuwa subra yavuta heri!

 Ni hakika haraka haraka haina baraka! Maana hata waingereza ama wenye kingereza chao husema kuwa, njia ya kato siku zote ni njia isiyo sahihi.

 Kuna watu wengi wamjejikuta wakiingia hasara maishani mara baada ya kutaka mafanikio kwa haraka! Wamejikuta wakipoteza ama wakiharibikiwa kimaisha, ni kweli ni tajiri ila kapoteza mke na woto kwa sababu ya mashariti ya mganga! Ni kweli ana fedha sawa na elimu sawa ila ni muadhirika wa UKIMWI! Kapenda chipsi hatimae ni mjamzito na ndoto za kusoma zimakomea hapo!

 Ni heri ukawie lakini ufike uendako, kuliko kukimbia ukajikuta unakimbia hadi unasahau nyumbani ama unashindwa kuangalia taadhari ya alama za barabarani na hatimae ukaingia katika kusababisha ama kujisababishia ajali!

Narudia tena na tena kuwa kawia ufike, pole pole ndio mwendo! Unaonaje mkulima akapanda mbegu leo na kutaka kuvuna siku hiyo hiyo! Kama kwa mkulima haiwezekani uwe na uwakika kuwa na katika safari ya mafanikio ndivyo ilivyo.   

Embu tujionee jinsi maandiko mtakatifu ya Biblia yanavyotufunza katika kitabu kile cha Yakobo: 5:5 Kwa hiyo ndugu, vumilieni, hata kuja kwake Bwana. Tazama, mkulima hungoja mazao ya nchi yaliyo ya thamani, huvumilia kwa ajili yake hata yatakapopata mvua ya kwanza na ya mwisho.

8 Nanyi vumilieni, mthibitishe mioyo yenu, kwa maana kuja kwake Bwana kunakaribia.9 Ndugu, msinung'unikiane, msije mkahukumiwa. Angalieni, mwamuzi amesimama mbele ya milango.

 

Jumamosi, 3 Julai 2021

Mwalimu Oscar Samba KUMFANANIA KRISTO Mkimbizi Iringa Ibada ya 1

Mwalimu Oscar Samba THAMANI YA KUMKABITHI MUNGU MAISHA YAKO YA BAADAE na...

Nilipata nafasi ya Kuwafundisha wanafunzi wahitimu wa Chuo Kikuu cha Mipango Dodoma CASFETA
Ujumbe huu utakusaidia uliye mwanafunzi na usie mwanafunzi kujua umuhimu wa kumshirikisha Mungu katika kila hatua muhimu ya maisha yako ikiwemo ile ya mawazo ama upangaji wa mipango

Jumatano, 24 Machi 2021

Ujumbe huu ni sehemu ya #kitabu chetu cha MTUMIKIE MUNGU, UKubali #Wito, #Kuna Faida katika Kumtumikia Mungu, na Kuna Hasara za Kukaidi Wito.

Na Mwalimu Oscar Samba

Usipoelewa jambo hili, huwezi elewa ni kwa nini Mungu aliamua kumfuata Yona baharini! Angeweza kuamuacha na kuinua mtu mwingine!

Anayefahamu swala hili kwa kina sio mwepesiwa kuimba ule wimbo wa “usifaye mchezo na Yesu na watu wengi! Wengine wanapanda na wengine anshuka!”
Japo ni kweli kabisa, ila kuna wakati mukutadha wake unagoma!
Hivi unajua ilimgharimu Mungu miaka mingapi kumuinu mbadala wa mfalme Sauli!
Ni rahisi sana kushangilia Mungu kumkataa Sauli! Ila fahamu iligharimu muda mrefu sana hadi kuja kutawala kwa mfalme Dudi!
Daudi hawezi kutawala kama muda hajaimarika, hajamaliza darasa la uongozi, hajafikia vigezo vya ufalme wa mbinguni.
Ndio maana hata baada ya Sauli mfalme kukataliwa na Mungu aliendelea kutawala hadi wakati ulipofika, na hata alipofariki bado Dauli hakuruhusiwa kutawala Israeli yote! Kwa hiyo bado kuna maeneo tena eneo kuba sana lilikuwa halina utawa ambao Mungu anautaka.

Jumamosi, 6 Machi 2021

Muombee Elia ama Yusufu wako, Ni Msaada wa kutoka kwenye Majanga kama ya Corona. #Corona #Covd19

 nA mWALIMU oSCAR sAMBA

Ujumbe huu ni sehemu ya #kitabu chetu cha MAMBO MUHIMU YA KUFANYA AU KUZINGATIA KUNAPOKUWA NA ADHABU YA KIUNGU INYOIJUMUISHA ENEO ULILOPO AU JAMII

18. Muombee Elia ama Yusufu wako; Kuna mtu MUNGU amemuweka ili kukuvusha ama kulivusha taifa na hata dunia kwa ujumla! shida kubwa ya wapendwa ni kwamba katika mambo kama haya kuomba kwa maarifa kumekuwa ni tatizo kubwa sana kwao! Wamisri walivushwa kutokana na akili, na hekima, pamoja na Roho wa Bwana ndani ya Yusufu kama Farao anavyokiri kwenye ile Mwanzo 41, kuwa hapana mtu mwenye akili, hekima na Roho wa Bwana ndani yake kama Yusufu! Ina maana gani! Kama Misri na dunia ya kipindi kile ilivushwa katika janga la njaa kutokana na sifa hizo zilizopelekea uwekaji wa akiba, basi na wewe muombee mtu ambaye mbingu zimemuandaa au kumtazamia kama sehemu ya majibu ya janga husika, kama ni la njaa, sawa, kama la kijografia pia sawa. Mfano kama ni la ugonjwa, ambao tena hauna dawa au kinga, waweza muombea Mungu ampe maarifa zaidi, na uwezo zaidi ama kuwaombea wanasayansi wapate maarifa zaidi ya kuwawezesha kugundua chanjo sahihi, na yenye uwezo stahiki, na isiyo na madhara katika mwili wa mwanadamu. Pili wagunduwe dawa, au tiba, huku ukiombea na viwanda vunavyotengeneza au vitakavyotengeneza dawa hizo, na vifa ambazo pia hutumika kipindi kama hiki, pamoja na kuwaombea madakitari na wauguzi ulinzi maalumu, maana nini kitatokea kama ukienda hosipitalini na kukuta madakitari na wauguzi wote hawapo ama wamaelemewa na wagonjwa kuiasi cha kushindwa kukusaidi na sababu ni baadhi yao kufariki!
Waombee pia wafadhili wataojitoa kwa fedha zao ili kuwezesha upatikana wa dawa hizo na vifaa pamoja na kuchangia gharama ili watu wengine wazipate, na huku sio kupungukiwa na imani bali ni kiroho kabisa. Kuweka akiba kwa Yusufu ni jambo la mwilini, na dawa pia ndivyo ilivyo, sayansi ni kiroho kabisa. Sasa tumekuwa na injili ambayo huiita injili makorokocho, kuwa hata chanjo ni pepo, hususani za ambao unaendeleao sasa, kuwani njama za watu wa mataifa fulani wanaotaka kutuua! Unafikiria mwenye fikra kama hizi ataombea sayansi isaidie kupembana na tatizo kweli! Maelekezo ya Paulo mtume kwa Timotheo kutumia mvinyo ilikuwa ni sayansi, maana kuna tiba hapo! (Sasa sina maana na kwako ufanye hivyo la!) Ila ninataka uione nafasi ya sayansi katika mambo kama haya! Tunajua kwa Yesu kumpaka mtu tope na kumtaka akanawe na Isaya kutumia makate wa tini ilikuwa ni ufuno sawa, ila sayansi nayo ni kiroho, waombee wafunuliwe dawa!

Jumamosi, 27 Februari 2021

Kitabu chetu cha: MAMBO MUHIMU YA KUFANYA AU KUZINGATIA KUNAPOKUWA NA ADHABU YA KIUNGU INYOIJUMUISHA ENEO ULILOPO AU JAMII.

Na Mwalimu Oscar Samba 

Neno Kiungu huwakilisha kutoka kwa Mungu au Shetani, ujumbe huu ni sehemu ya hiki kitabu chenye mada na pwenti kadhaa, ila hapa nimezicha,bua mbili tu; #Corona #Covd19 #Tsunam #Majanga  #Kimbunga #magonjwayamlipuko  #tanzania

1. Lifanye Eneo Unloishi kuwa Ghosheni yako. 2. Ijue na Uitumie Damu ya Yesu ya Pasaka; 3. Mulize Mungu kama Daudi; 4. Litengenezee Kusudi la Mungu Kisafina kama Musa, ama Nuhu; 5. Jifunze Jambo kwa Mke wa Lutu;

6. Sadaka kama Ulinzi; 7. Sadaka kama Sehemu ya Rehema, Mfano ile ya Daudi kipindi cha adhabu ya Tauni, 8. Taka Kujua pigo Hilo au Adhabu hiyo Inataka nini ili Ujisalimishe kwa Bwana, Mfano Rahabu, na Epuka kosa la Farao.

 9. Yajue na Uyaombe Maombi ya Musa ya Kulitengeneza Boma, 10. Mtafute na Umuondoe Akani, 11. Jitenge na Kusanyiko, au Kiunganishi cha Kusanyiko ama Waadhibiwa, ondoa jina lako kwenye watu wanaotakiwa kupewa hiyo Adhabu kwa Damu ya Yesu.

 

12. Tafuta Maelekezo Maalumu ya Mungu juu yako, kama Isaka dhidi ya Janga la Njaa na Wazazi wa Yesu. 13. Unapoisikia Hofu Usiipuzie, Taaka Kujua ni Aina gani ya Hofu ala Uikabili..

 

14. Tafuta Kukumbuka kama Mungu Aliwahi Kukujuza hapo Awali na Hukumsikia Vyema au Hukumbuki. (Amosi 3:7 Hakika Bwana MUNGU hatafanya neno lolote, bila kuwafunulia watumishi wake manabii siri yake.) Sijui sana ni kwa nini kanisa la leo lina uzito kwenye hili,  nijualo ni kwamba uwezo wa kusoma alama za nyakati, au majira umekuwa ni adimu sana kwa kizazi cha leo! Nafahamu kuwa hali ya kupuzia ndoto, kutokutambua jinsi Mungu anavyoongea, na mafundisho manyonge kuhusu uhusiano wetu na Roho Mtakatifu ni miongoni mwa sababu ambatanishi.

 

Kama kuna mahali Shetani amefanikiwa leo ni kuondoa, ama kuzimisha kama sio kufifisha karama ya unabii, na huduma ya nabii, pamoja na neno la maarifa!

 

Na anatumia njia kuu kama mbili hivi, moja ni kuhakikisha kanisa linapoteza imani na manabii au wanaotumiwa na karama hizi, kwa kujiwekekea manabii wa uongo, ili kuwakatisha watu tamaa na kuwafanya wa waone hata wale wa Mungu nao ni kama hao wengine!

Pili analitumia kanisa lenyewe, kwa kufikia hatua ya kupinga, na kukataa, na kuzimisha huduma na karama hizi, na sababu zao ni nyingi ila hazina hoja timilifu kibiblia, maana kama kuna wimbi la mafundisho na huduma potofu, suluhu bado sio kuzima na kukataa ile ya kweli, bali wafunze watu namna ya kutambua kweli na uongo. Mchele ukiwa na chuya, dawa sio kukataza nyumbani wasipike tena mchele bali ni kuwafunza kuzitoa, na kama ni mcahanga basi watake kuwa makini kuchambua maana mawe mengine ni yale meupe, kwa hiyo yanafanana kwa karibu na mchele, lakini pia kama ni vigumu, wafunze kupembua au kuuchambua wakati wanauosha na maji, njia ambayo ni salama zaidi.

 

Maharage yakiwa na mchanga au mawe, hayamwagwi, bali huchambuliwa! Na wewe ukiona dosari katika hudumka na karama hizi, hakikisha unazikabili!

 

Maandiki yako wazi kabisa katika biblia kuwa tunatakiwa kujifunza na kuhakikisha kuwa tunasoma alama za nyakati, au tunajua mabadiliko kwa kuzitambua dalili zake, mkulima asipojua kusoma uso wa nchi, hakika atakuwa akipitwa na maamuzi dhabiti katika majira husika, wakati wengine wanandaa mashamba yeye atashindwa kufanya hivyo, ama atajikuta akiwacheka wengine, maana kwa wengine ili walime ni hadi waone mvua imenyesha bila kujua kwa kufanya hivyo ni gharama zaidi maana aridhi husumbua kwani kulima kwenye tope ni kugumu zaidi! Pia ipo hatari ya kushindwa kufanya vyema maana kuna uwezekano wa kunyeshewa! Kuna kuchelewa pia kupanda, maana wakati wa kuotesha wewe ndo kwanza unakwatua udongo.

 Hosea hufananisha jambo la kuukwatua udongo sawa na kuomba, maana husema tumtafute Mungu, akitangulia na kututaka kuukwatua udongo wa mashamba yetu! Kiroho kuna vipindi kama hivi! Kuna kipindi cha kumtafuta Mungu kabla ya adahabu haijaja! Ukichelewa gharama yake ni kubwa sana! Unaweza kujikuta umeshapoteza ndugu wengi, ama hasara kubwa imeshatokea!

 Mama yangu wakati ugonjwa huu unaingia au umeanza kushamiri, ndipo aliponitaarifu kuhusu ndoto aliyowahi kuiota! Japo hakuwa ameielewa kipindi hicho! Ila nataka ufahamu kuwa Mungu alikuwa ameshaongea naye!

 Elimu na ufahamu wa kuzijua nyakati ni muhimu sana, na ni kiroho kabisa, jihakikishie kwa watu hawa, ambapo hata leo makanisani wapo, na kama hawajafungwa

Jumapili, 17 Januari 2021

kitabu cha UKULIE WOKOVU

#Habari-Njem ni kwamba, tumefanikiwa kutoa kitabu cha UKULIE WOKOVU, Kimetoka kwa njia ya PDF, tayari kwa ajili ya kusomwa kwenye simu na kompta, bei ni shilingi 5,000 za kitanzania; ukikihitaji wasilaina nasi kwa simu +255759859287, barua pepe: ukombozigospel@gmail.com pia zidi kutembelea: www.ukombozigospel.blogspot.com