Na Mwalimu Oscar Samba
Usipoelewa jambo hili, huwezi elewa ni kwa nini Mungu aliamua kumfuata Yona baharini! Angeweza kuamuacha na kuinua mtu mwingine!
Anayefahamu swala hili kwa kina sio mwepesiwa kuimba ule wimbo wa “usifaye mchezo na Yesu na watu wengi! Wengine wanapanda na wengine anshuka!”
Japo ni kweli kabisa, ila kuna wakati mukutadha wake unagoma!
Hivi unajua ilimgharimu Mungu miaka mingapi kumuinu mbadala wa mfalme Sauli!
Ni rahisi sana kushangilia Mungu kumkataa Sauli! Ila fahamu iligharimu muda mrefu sana hadi kuja kutawala kwa mfalme Dudi!
Daudi hawezi kutawala kama muda hajaimarika, hajamaliza darasa la uongozi, hajafikia vigezo vya ufalme wa mbinguni.
Haya yote ni madahara ya mtu mmoja Sauli kugoma kukaa kwenye nafasi yake kwa kumuasi Mungu! Natumai kwenye mada ya madhara utajionea kwa mapana zaiadi, ila hapa nilitaka kukufikirisha tu kwa kiduchu kuhusu dhima hii!
Lakini sio hapo tu, tunaweza kujionea pia kwa Yona, Yona aliamua kuukimbia uso wa Mungu, Mungu hakumuacha, aliamua kumfuata huko huko baharini!
Najua kwenye mada ya hasara utajionea jinsi wengine walivyoingia hasara kwa kutupa vitu vyao baharini, ila nataka tu ufahamu kwa kina kwa kujiuliza ni kwa nini Mungu aliamua kumfuata Yona baharini!
Siri ni gharama ya maandalizi, kwa kifupi Mungu hakuwa na mtu mwingine ama “copy” au nakala ya Yona! Wewe nawe hatuna nakala yako!
Na hata mimi ninafahamu kuwa hakuna nakala yangu!
Unajua ilimgharimu Mungu miaka mingapi kumunda Musa?
Ilimgharimu miaka 80!
40 aliitumia akiwa Misri, ambapo mimi nawe twafahamu kuwa alikuwa chini ya ufalme wa Farao, akichukuliwa kama mtoto wa binti Farao yaani mjukuu wa mfalme, hapo alipata elimu ya kujua kusoma na kuandika, na aliweza kufahamu mambo mengi kuhusu ufalme na uongozi.
Baada ya hapo ilimgharimu tena miaka mingine 40, hii ilikuwa ni miaka ya kuvua “uraia” wa Kimisri, waliopitia jeshini watanielewa kiwepei maana kule kuna aina fulani ya mafunzo anayoyatapitia mtu ili kuvuliwa uraia, na kuvikwa ujeshi.
Miaka hii ya 40 ya pli ilikuwa na dhima kubwa sana kwake, hapo awali alikuwa na mzigo wa kuwakomboa ndugu zake, kama Waebraia isemavyo katika ile sura ya 11 kwamba kwa imani hakuona inafaa kuendelea kuitwa binti Farao, ila njia iliyotumika ilikuwa sio sahihi, utawala wa kimabavu wa kifarao ulimuadhiri, Mungu akaona huyu bado anahitaji shule nyingine!
Mwishoni mwa miaka ya arobani ya pili yaani akiwa na maika takriani 80 ndipo Mungu anamtokea na kumtwisha jukumu la ukombozi!
Sasa umeandaliwa miaka 80 alafu unajaribu kukwepa wito, unaweza sasa kufikiria ni kwa jinsi gani unavyouingiza ufame wa mbinguni hasara!
Ukibisha jaribu kuiuliza kampuni iliyomchukuwa mfanyakazi na kmpeleka shuleni kisha alipotoka huko na kuamua kuicha kampuni! Uwe na hakika watajianda kumfungulia mashitaka, na ndio maana walimsainisha mkataba kabla ya kwenda shule!
Sasa unadhania kuwa mbingu nazo hazikufungulii msahitaka unapojaribu kukaidi wito!
Kwenye mada ya tatu ya hasara natumai utanielewa zaidi.
Sasa utaelewa ni kwa nini wakati Musa anaitwa alipoaribu kukwepa, kwa kisingizio kuwa yeye hawezi kuongea vyema ama sio msemaji huku Mungu akimpatia atakayemsaidia na kuendelea kusisitiza athima hiyo Mungu alimkasirikia! Ndio ni kwa sababu ya gharama ambayo Mungu alishaiingia katika kumuandaa!
Hasira ya Bwana ikawaka juu ya Musa, akasema, Je! Hayuko Haruni, ndugu yako, Mlawi? Najua ya kuwa yeye aweza kusema vizuri. Pamoja na hayo, tazama, anakuja kukulaki; naye atakapokuona, atafurahi moyoni mwake. Kutoka 4:14.
Yesu ameandaliwa zaidi ya miaka 33, alafu anataka kugoma dakika za mwisho kupita msalabani unafikiria mbingu zingemuachia ama zingekuwa na hasara kiasi gani kama angekaza katika kugoma!
Huyu alitumwa katika kikao maalumu kilichokaa mbinguni kwenye Isaya 6, ni kweli pale tunaiona huduma ya nabii Isaya ikichukua sura mpya, lakini kiukweli atuachi kumuona Yesu pale akipokea wito. Mbingu ziliuliza zimtume nani, naye aliitika akitaka atumwe Yeye, Nabii Isaya katika sura ya 9 alishatabiri, na manabii wengine wengi tu, malaika Gabrieli alishamtaarifu mamaye na babaye mlezi kuwa ajae ni mkombozi, Simeoni alishalinena hilo pamoja na Anna bint Faueli.
Iligharimu takribani miaka 30 ndipo aje kuanza huduma, amefanya huduma miaka kama mitatu hivi, na siku zote ama mara kwa mara alikuwa akieleza kwamba inampasa kufa, ili kutimiza yote aliyoandikiwa, alafu dakika za mwisho mwili unataka kugoma kupita msalabani!
Sasa utanielewa ni kwa nini Yesu ilimbidi ashindane na mwili wake, vita ama mashindano yalikuwa makubwa kiasi cha jashola damu kutoka!
Kwa maana kwamba Yesu alitambua thamani ya ujio wake huku ulimwenguni!
Ni muhmu na wewe kuhakikisha unajua thamani yake!
Unaweza usijue sana muda ambao Mungu ameutumia kukuanda, ila upo! Nina hakika toka udogoni ulikuwa ukiandaliwa, ndio maana maisha yako ni tofauti kabsia na ndugu zako wa familia yako, ni tofauti na wanafunzi wengine uliosoma nao, pia u tofauti kabisa na wapendwa wenzako kansiani, mliokoka siku moja ila ukiwatazama kuna utofauti mbwa sana, kama sio kuna mahali umewaacha katika ukuajia basi uwenda hata wenzako walishaiacha neema, ikiwa na maana kwamba kuna namna Mungu alikupa cha ziada ili umtumikie, yaani wenzako wote walishafariki wale wa rika moja, mlikuwa wezi wenzako wakafa katika wizi wewe ukapona, uwe na hakika kuna kitu cha ziada kilikunusuru!
Wakati wenzake na Musa wakiuawa, Musa alinusurika na kuwa salama, alafu eti Musa huyu aliyenusurika kimuujiza leo anataka kugoma kumtumikia Mungu!
Hajui ni kwa kiasi gani Mungu alihakikisha Musa anakuwa hai!
Ninakumbuka kisa cha Mwalimu Mwakasege, ilipokuwa majira ya kutaka kuzaliwa kwake, anasema kuwa kijijini kwao kulikwepo na hosipitali ya kimisheni na pale paliwa na dakitari wakizungu ambaye kila mzazi anayejifungua pale kwa upasuaji iikuwa ni lazima afe yeye na mtoto!
Ilipofika zamu ya kukaribia kuzaliwa kwake kulikuwa na muuguzi ama dakitari ambaye alikuwa ni ngudu na mamaye akamueleza jambo hilo na kumwambia kuwa huyo dakitari ataenda nyumbani kipindi cha sherehe ya Krismasi, akishaenda tu njoo, kweli ikawa hivyo, na baada ya hapo mamaye akajifungua kwa upasuaji na yeye yaani mtoto na mama wakawa salama alipozaliwa, mmishenari mmoja mzungu alimshika na kusema kuwa utaitwa Christopher, ikiiwa na maana ya majina mawili, Christo, na Pher! Hapana shaka maana yake ni Mpenda Kristo!
Sasa jaribu kufikiri leo awe mtu mzima alafu ajaribu kumuacha Mungu au agome kumtumikia Mungu! Anaeleza tena kwa mamaye akiwa anasoma chuo cha ualimu cha Tosa-Maganga, “masisita” wa katoliki walimpenda na kumtaka siku moja aje asomee “usisita” ila moyoni ajenda hiyo iligoma, sasa alienda poroni na kumwambia Mungu kuwa akimsaida na kuolewa mtoto atakayezaliwa atampa Mungu kama sadaka amtumikie!
Sasa Christopher kazaliwa, alafu jaribu kufikiri anataka kugoma kumtumikai Mungu!
Hakika ni ngumu sana na ni hasara kubwa kwa mbingu zilizompigania mamaye, na kisha mtoto ili asife kama wengine walivyokuwa wakifa kwa kuuawa na yule dakitari! Tena huyu alikuwa akiua mama na mtoto! Na adui alilifanya hili makusudi akihakikisha kuwa Mwakasege hapatikani!
Jaribu kufikiri Tanzania bila Mwakasege! Maana hata mimi kwa kweli, na kiukweli ni zao muhimu la huyu baba wa Kinyakwisa.
Sijui kama nitapata kibali chakueleza ya kwangu huku, ila nataka tu ufikiri kuwa bila mimi! Hakika kuna pengo fulani lingesalia! Ni rahisi kusema kuwa Mungu ana watu wengini!
Lugha hiyo hapa haina nafasi!
Jaribu kufikiri gharama Mungu aliyoiingia kuhakikisha wazazi wa Yesu wanamnusuru mtoto! Licha ya kwamba kwamama yake ilifanyika jitihada kubwa za kuhakikisha ya kwamba anapokea mimba kwa mujiza lakini pia maandiko husema kuwa uvuli wa Roho Mtakatifu ulikuwa juu yake, ama alimjilia kama kivuli, ikiwa na maana kwamba kila alipokuwa akienda alikuwa pamoja naye, alikuwa akimlinda mtoto na mama!
Malaika akajibu akamwambia, Roho Mtakatifu atakujilia juu yako, na nguvu zake Aliye juu zitakufunika kama kivuli; kwa sababu hiyo hicho kitakachozaliwa kitaitwa kitakatifu, Mwana wa Mungu. Luka 1:35.
Alipozaliwa, Herode alitaka kumua, Mungu aliwajulisha mamajusi ili wasimrudie tena Herode, baada ya hapo alihakikisha baba na mama na mtoto wanakimbilia Misri, walirudi baada ya kifo cha Herode, walipangiwa mahali pa kuishi, na kadhalika, watoto wengine waliokuwa wamesalia weye umri chini ya miaka 2 waliuawa wote!
Alafu Yesu awe mtu mzima, aitwe na kuanza kupiga chenga wito!
Ni nani ajaue kuwa ule ugojwa uliokuja kijijni kwenu na kuvamia watoto wadogo nao kufa ilikuwa ni njama ya adui kama ilivyokuwa kwa Yesu, Musa na Mwakasege ila Mungu alikunusuru na wewe kuwa hai hadi leo!
Alafu unafika mahali pa kutaka kugoma kumtumikia Mungu, unajaribu kuhesabu gharama za kutumika na kuzifanya kuwa kikwazo, hujui nini kitatokea kama Mungu akikuhesabia za kwake alizozitumia ili kukunusuru hai hadi leo licha ya zilizozitumia kukufundisha ama kukuandaa kwa ajili ya utumihi huo unoukwepa, na ni hasara kiasi gani kama hutakaa kwenye nafasi yako!
Mungu ni kweli ana watu wengi, ila hana mtu ama Musa, hakuna “copy” ya Musa, na ndivyo ilivyo kwako kuwa hakuna nakala yako, wewe ni wewe, na ndivyo hata mimi ninavyoamini kuwa mimi ni mimi hakuna aliye kama mimi!
Fhamu kuwa vilivyoko ndani yako haviko kwa mtu yeyote yule, na kwa bahati nyingine ni kwamba viliwekwa kabla hujazaliwa; Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, na kabla hujatoka tumboni, nalikutakasa; nimekuweka kuwa nabii wa mataifa. Yeremia 1:5.
Ona hapa pia; alipoona vema kumdhihirisha Mwanawe ndani yangu, ili niwahubiri Mataifa habari zake; mara sikufanya shauri na watu wenye mwili na damu. Wagalatia 1:16.
(Ulizaliwa ukiwa mtumishi! “toka tumboni” Sasa leo unaanzaje kukataa wito!)
Sasa jaribu kufikiri kuwa kuna vitu vimewekwa ndani yako kabla ya kuzaliwa, ukiwa tumboni mwa mama yako vilikuzwa, umezaliwa Mungu amevikuza na kuvipalilia zaidi, na uwenda unapokea wito na kutakiwa kuanza kutumika ukiwa na miaka 30 kama Yesu, ama 80 kama Musa, alafu unagoma kuitika ama kutumika!
Maana yake unajaribu kumtaka Mungu aingie gharama ya kumuandaa mtu mwingine, na kuumbiwa ulivyopewa kabla ya kuzaliwa, alafu baada ya miaka 30 au 80 ndio aje kuanza kutumika!
Na kama hilo linawezekana fikiria pia je hiyo jamii inayotakiwa kuokoka leo itasubiria miaka hiyo yote! Na vifo vya watu vitasimama! Mungu aliyepanga muda wake wa kuwatoa wana wa Israeli utumwani je, yampasa kusubiri tena hadi miaka 80 ijayo! Na ni nani ajuaye huyo ajae kama itambidi kuandaliwa miaka 80 tu! Wengine huhitaji zaidi maana inategemea na aina ya moyo wa mtu ndipo darasa la Mungu liwe limekamilika!
Ni muhimu kuona thamani ya kuandaliwa kwako, thamani ya kuhitajika kukaa kwenye nafasi au utumishi ambao Mungu amekutia! Ndio maana ukijaribu kupanda melikebu ya kwenda tarishishi uwe na hakika Bwana atakufuta huko huko!
Maana amewekeza!
Naye sie Mungu wa hasara!
……
Sijui kama unaifahamu vilivyo Dhima ya Yohana Mbatizaji kwa Yesu! Licha wengine kumuita ama kumuona kama ndie baba yake wa kiroho, lakini kiuhalisia ni kwamba huyu ndie aliyekuwa na jukumu la kumfungulia njia, kuondoa visiki, kuodoa miiba na kila kizuizi katika ujio wa huduma yake.
Huyu ndiie aliyemtambulisha Yesu, alikuwa na jukumu la kumuandalia Yesu kikosi kazi cha kwanza kabsa, alimuandalia wanafunzi;
Kwa watumishi wanafahamu kuhakuna kitu muhimu kama unapoanza huduma mpya mahali ukakutana na wazawa au watu watakaoshikamana na wewe, watakaoikubali huduma yako na kukupa joto la kiroho, haijalishi wengine watakukataa kwa kiasi gani lakini ukipata mmoja au wawili watakaokwambia mtumshi tupo pamoja hilo ni jambo kubwa na muhimu sana hususani huduma ikiwa changa!
Siku ya pili yake amwona Yesu anakuja kwake, akasema, Tazama, Mwana-kondoo wa Mungu, aichukuaye dhambi ya ulimwengu! Huyu ndiye niliyenena habari zake ya kwamba, Yuaja mtu nyuma yangu, ambaye amekuwa mbele yangu; kwa maana alikuwa kabla yangu. Wala mimi sikumjua; lakini kusudi adhihirishwe kwa Israeli ndiyo maana mimi nalikuja nikibatiza kwa maji. Yohana 1:29-31
Ona hapa; Wale wanafunzi wawili wakamsikia akinena, (walimsikia Yohana) wakamfuata Yesu. Yesu aligeuka, akawaona wakimfuata, akawaambia, Mnatafuta nini? Wakamwambia, Rabi, (maana yake, Mwalimu), unakaa wapi? Akawaambia, Njoni, nanyi mtaona. Wakaenda, wakaona akaapo, wakakaa kwake siku ile. Nayo ilikuwa yapata saa kumi. Yoahana 1:37-39.
Jaribu kutenga muda na kufikiri kwa kina nini kingalitokea kama Yohana angegoma! Huyu alishaandaliwa kabla hata ya ujio wa Agano Jipya, alizaliwa mbele ya Yesu miezi kadhaa kwa kusudio kama hili!
Toka kitabu cha Isaya alishaandaliwa, tunajionea hapo akitajwa kama msafisha njia, aina ya roho itakayokuwa ndani yake ilishaandaliwa, ndiposa kitabu kile cha Malaki kikamtaja kama Elia wa pili, unadhania ilikuwa kwa Yahana tu!
Nani ameudanganya!
Kwako nawe ndivyo ilivyo! Ulishaandaliwa kabla hujazaliwa, Mungu alijua jukumu na kazi aliyokuwekea, alijua kitu alichokuitia humu ulimwenuni!
Ni muhimu kulijua hili ili ukae kwenye nafasi yako, kuna kazi uliyowekewa, kuna jukumu uliloitiwa ukikwama mambo mengi yatakwama pia.
Natumai kuna picha fulanai umeanza kuipata kuhusu umuhimu na thamani yako katika ufalme wa mbinguni! Na ndani yako kumeanza kuibuka kiu ya kuhakikisha ya kwamba unamtumikia Mungu tena ipasavyo!
Fahamu kuwa huu ujumbe nimekupa tu sehemu chache ya mada ya kwanza inayolenga kukupa thamani za kumtumikia Mungu na ipo ya pili ya Faida na ya Tatu ni ya hasara za kugoma kutumika, nakutia moyo kitabu kikitoka kitafute.
Hongera
kwa kusoma ujumbe huu, nakutia moyo kuzidi kumtazama Mungu, na pia uwenda hujaokoka, yaani Yesu sio Bwana na mwokozi wa maisha yako! Nakutia moyo tena kuokoka sasa! Yamkini ni uchumi, fedha, hazipatikani, unazingirwa na nuksi na mikosi, kila unalofanya haliendi, unakabwa na mapepo, ! Wewe njoo kwa Yesu na hayo yote yatapita kabisa ! Sasa natumi u tayari!Sema; MUNGU BABA, NINAKUPENDA, ASANTE KWA KUNIPENDA KWANZA, LEO NIMETAMBUA KUWA MIMI NI MWENYE DHAMBI, NA NIPO TAYARI KUOKOKA, TAFADHALI INGIA NDANI YANGU, SAMEHE DHAMBI ZANGU, NA FUTA JINA LANGU KATIKA KITABU CHA HUKU, NA ULIANDIKE SASA KATIKA KITABU CHA UZIMA WA MILELE, Ameni.
Kwa kufanya hiyo umekwisha kuokoka sasa, na tafadhali tafuta kanisa la watu waliokoka lililopo karibu nawe ukasali, hapo, waambie kuwa umeokoa hivi karibuni, ili wakulee vyema kiroho.
Mawasiliano yetu, kwa M-Pesa au Simu: +255 759 859 287, barua pepe: ukombozigospel@gmail.com
pia temnbelea: www.ukombozigospel.blogspot.com . AU www.mwalimuoscarvitabu.blogspot.com
#Habari-Njema ni kwamba, tumefanikiwa kutoa kitabu cha UKULIE WOKOVU, na cha USIFIE JANGWANI, vimetoka kwa njia ya PDF, tayari kwa ajili ya kusomwa kwenye simu na kompta, bei ni shilingi 5,000 za kitanzania; ukivihitaji au kukihitaji wasiliana nasi kwa simu +255759859287, barua pepe: ukombozigospel@gmail.com pia zidi kutembelea: www.ukombozigospel.blogspot.com #MwalimuOscarVitabu #MwalimuOscarSamba
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni