Jumamosi, 6 Machi 2021

Muombee Elia ama Yusufu wako, Ni Msaada wa kutoka kwenye Majanga kama ya Corona. #Corona #Covd19

 nA mWALIMU oSCAR sAMBA

Ujumbe huu ni sehemu ya #kitabu chetu cha MAMBO MUHIMU YA KUFANYA AU KUZINGATIA KUNAPOKUWA NA ADHABU YA KIUNGU INYOIJUMUISHA ENEO ULILOPO AU JAMII

18. Muombee Elia ama Yusufu wako; Kuna mtu MUNGU amemuweka ili kukuvusha ama kulivusha taifa na hata dunia kwa ujumla! shida kubwa ya wapendwa ni kwamba katika mambo kama haya kuomba kwa maarifa kumekuwa ni tatizo kubwa sana kwao! Wamisri walivushwa kutokana na akili, na hekima, pamoja na Roho wa Bwana ndani ya Yusufu kama Farao anavyokiri kwenye ile Mwanzo 41, kuwa hapana mtu mwenye akili, hekima na Roho wa Bwana ndani yake kama Yusufu! Ina maana gani! Kama Misri na dunia ya kipindi kile ilivushwa katika janga la njaa kutokana na sifa hizo zilizopelekea uwekaji wa akiba, basi na wewe muombee mtu ambaye mbingu zimemuandaa au kumtazamia kama sehemu ya majibu ya janga husika, kama ni la njaa, sawa, kama la kijografia pia sawa. Mfano kama ni la ugonjwa, ambao tena hauna dawa au kinga, waweza muombea Mungu ampe maarifa zaidi, na uwezo zaidi ama kuwaombea wanasayansi wapate maarifa zaidi ya kuwawezesha kugundua chanjo sahihi, na yenye uwezo stahiki, na isiyo na madhara katika mwili wa mwanadamu. Pili wagunduwe dawa, au tiba, huku ukiombea na viwanda vunavyotengeneza au vitakavyotengeneza dawa hizo, na vifa ambazo pia hutumika kipindi kama hiki, pamoja na kuwaombea madakitari na wauguzi ulinzi maalumu, maana nini kitatokea kama ukienda hosipitalini na kukuta madakitari na wauguzi wote hawapo ama wamaelemewa na wagonjwa kuiasi cha kushindwa kukusaidi na sababu ni baadhi yao kufariki!
Waombee pia wafadhili wataojitoa kwa fedha zao ili kuwezesha upatikana wa dawa hizo na vifaa pamoja na kuchangia gharama ili watu wengine wazipate, na huku sio kupungukiwa na imani bali ni kiroho kabisa. Kuweka akiba kwa Yusufu ni jambo la mwilini, na dawa pia ndivyo ilivyo, sayansi ni kiroho kabisa. Sasa tumekuwa na injili ambayo huiita injili makorokocho, kuwa hata chanjo ni pepo, hususani za ambao unaendeleao sasa, kuwani njama za watu wa mataifa fulani wanaotaka kutuua! Unafikiria mwenye fikra kama hizi ataombea sayansi isaidie kupembana na tatizo kweli! Maelekezo ya Paulo mtume kwa Timotheo kutumia mvinyo ilikuwa ni sayansi, maana kuna tiba hapo! (Sasa sina maana na kwako ufanye hivyo la!) Ila ninataka uione nafasi ya sayansi katika mambo kama haya! Tunajua kwa Yesu kumpaka mtu tope na kumtaka akanawe na Isaya kutumia makate wa tini ilikuwa ni ufuno sawa, ila sayansi nayo ni kiroho, waombee wafunuliwe dawa! Nathani kuna mambo makuu mawili hapa ambayo watu wanachanganya, moja ugonjwa kama pepo, au kama wa kiroho tu, na pili ugonjwa wa kiroho ila upo kibaolojia, (au wa kibaolojia unaotumiwa kiroho). Ni kweli hata katika ugonjwa wa kiroho uliopo kibaolojia Shetani ama Mungu huweza kuwa nyuma yake! Hiyo ipo kabisa, maana ile tauni (Hesabu 16) hata kama ilikuwa ikija kiroho, ila kuna namna ilikuwa ikifanya kazi kibaolojia ndio maana wakina Musa na Haruni wakatakiwa kujitenga na kusanyiko, na ugonjwa huu tulionao kipindi hiki, (cha uwandishi wa kitabu) unatutaka kujitenga na kusanyiko, kujitenga nako ni kiroho jamani! Ila kiroho Haruni alipaswa kuingia kwenye maombi, akitumia chetezo na hapo ulikoma kabisa, maana hata kwa Daudi pia alitumia njia ya kiroho, aliomba na kutoa sadaka, Mungu akaikomesha tauni. Lakini sio kila mahali njia hiyo tu, kuna muda maombi, na njia za mwilini pia hutumika. Maana ni hatari kuwa na fikra ambazo sio za kiroho katika mambo kama haya, usije kuwa kama ile dini ambayo hawaamini kuhusu kwenda hosipitalini, kwao hata mama mjamzito hutaka ajifungue kwa maombi, nasikia kuna mahali walifanya hivyo wakampoteza mama na mtoto, wakaishilia kuwa mikononi mwa polisi! Cha ajabu wapentekoste wenzangu mtu akiugua huu ugonjwa hupelekwa hosipitalini, ila katika kuchukua taadhari na kutakiwa kuudhibiti hawataki kufuata maelekezo ya dakitari! Hili nalo ni ajabu na kushangaza! Ningali kuwa Sulemani wa leo ningesema nimeona baa jipya chini ya jua! Kuugua ni hospitalini, ila kujilinda na kutokuugua ni maombi tu yatosha! Kuomba tuombe, ila na akili pia tutumie! Labla kama unamaelekezo tofauti ya Mungu sawa, nje ya hapo ni makorokocho ama imani uchwara kama nisemavyo humu kitabuni. Jambo la pili ni ule ugonjwa ambao asili yake na ndivyo ulivyo kuwa ni wakiroho tu! Huku huitwa kupagawa kwa mapepo, ama magonjwa ya kipepo, haya kwa kweli kemea, na pambana na maombi tu, maana pepo haliwezi kupelekwa hosipitalini! Hakuna kipimo cha kupima pepo! Ila sio kila ugonjwa ni hali hii, ndiposa kama umemuombea mgonjwa na unasikia msukumo wa hosipitali tii! Lakini fahamu hata kama ni ugonjwa wa kibaolojia kwa asilimia mia moja, Munbu wetu ni “Omisciendce” an “Omnipotent” akiwa na maaana ya kuweza yote, kujua na kadhalika, Yeye ni yote juu ya yote, kwa hiyo magonwja yote ni muhumu kudhibitiwa kiroho, ila pia na sayansi ni muhimu maana nayo ipo rohoni kabisa, ukikwama hapa una matataizo katika kumjua Mungu!
Ukigundua kuwa “Corona” ni ugonjwa wa kibaolojia, hata kama nyuma yake kuna nguvu nyingine, basi utaikabili kiroho na kibaolojia pia, kama vile ukiugua ni lazima utafute dawa, basi na kujilinda pia tafuta kufanya kadri iwezekanavyo, japo wengine husema ni vigumu, ila jitahidi kadri uwezavyo, nimekuwa nikiwashauri watumiaji wa vipaza sauti kanisani kujaribu walau kuvipaka dawa za kuulia vijidudu ila wamekuwa wakinitazama kama aliyepungukiwa na imani! Hili nalo ni baa jipya chini ya jua! Sijui ni nani aliyeziloga hizi fikra ila najua ni kukosa mafundisho sahihi! Maana hata zamani watu walifundishwa kuwa ukiumwa sema siumwi utapona!
Lakini pia muombee Elia wako, Yusufu yupo katika nyanja ya kwimwili zaidi, yaani kisayansi au kimaarifa, japo anategemea msaada wa Roho Mtakatifu (hata kama hajaokoka), ni nikwambie kuwa kumuombea ni muhimu maana Shetani alimuweka jela, sasa kama Yusufu wako yupo jela uwe na hakika njaa itakuja tu! Ni kumuombea atoke huko, na awe na utulivu wa kuweza kumsikia Mungu ili awe na majibu ya Mungu, pia umuombee Farao wako aweze kukubali kumtumia au kumpokea au kumuamini, maana kama una rais au waziri wa afya, ama mtu yeyote mwenye dhamana husika, ambae hataki chanjo, hataki dawa, hataki hata vifaa vya kupima vitumike,anasema nchi nyingine zinataka kuwaua kwa hiyo zimeandaa chanjo bandia, uwe na hakika kwamba Yusufu ameshaanza kukaa kwenye nafasi yake, ila Farao hataki kuweka akiba, na njaa itawaangamiza tu! Na wasio na upeo wa kufkiri humuunga mkono Farao kama huyu! Tafadhali usiwe wewe, ila wewe muombee!
Elia wako ni muhimu sana ukajua kumuombea, na wewe ujiombee ili akija na neno la Bwana uweze kulipokea, na kama wewe ni Elia wa familia yako, jamii au kanisa, ujuwe kujiombea ili uwe na mbinu za kuwasaidia watu wako kama Elia wa mama mjane wa Sarepta, mama huyu alipungukiwa na imani, ila Elia alimwabia usiogope, ukinipa mimi kwanza hiki na hiki kitatokea! Na wewe watu wako wakipungukiwa na imani, usife moyo, usiwaache, endelea kunena nao iliwashike maelekzo hayo!
Huyu ni mtumishi ambaye hutumwa ili kukuletea neno la Mungu, ambalo hunuia kukuvusha mahali fulani Ni kwambie tu ukweli ni kwamba, hakuna kipindi muhimu ambacho unahitaji neno la Mungu kama hiki kipindi! Hongera kwa kusoma ujumbe huu, nakutia moyo kuzidi kumtazama Mungu, na pia uwenda hujaokoka, yaani Yesu sio Bwana na mwokozi wa maisha yako! Nakutia moyo tena kuokoka sasa! Yamkini ni uchumi, fedha, hazipatikani, unazingirwa na nuksi na mikosi, kila unalofanya haliendi, unakabwa na mapepo, ! Wewe njoo kwa Yesu na hayo yote yatapita kabisa ! Sasa natumi u tayari! Sema; MUNGU BABA, NINAKUPENDA, ASANTE KWA KUNIPENDA KWANZA, LEO NIMETAMBUA KUWA MIMI NI MWENYE DHAMBI, NA NIPO TAYARI KUOKOKA, TAFADHALI INGIA NDANI YANGU, SAMEHE DHAMBI ZANGU, NA FUTA JINA LANGU KATIKA KITABU CHA HUKU, NA ULIANDIKE SASA KATIKA KITABU CHA UZIMA WA MILELE, Ameni. Kwa kufanya hiyo umekwisha kuokoka sasa, na tafadhali tafuta kanisa la watu waliokoka lililopo karibu nawe ukasali, hapo, waambie kuwa umeokoa hivi karibuni, ili wakulee vyema kiroho. Mawasiliano yetu, kwa M-Pesa au Simu: +255 759 859 287, barua pepe: ukombozigospel@gmail.com pia temnbelea: www.ukombozigospel.blogspot.com . AU www.mwalimuoscarvitabu.blogspot.com #Habari-Njem ni kwamba, tumefanikiwa kutoa kitabu cha UKULIE WOKOVU, na cha USIFIE JANGWANI, vimetoka kwa njia ya PDF, tayari kwa ajili ya kusomwa kwenye simu na kompta, bei ni shilingi 5,000 za kitanzania; ukivihitaji au kukihitaji wasiliana nasi kwa simu +255759859287, barua pepe: ukombozigospel@gmail.com pia zidi kutembelea: www.ukombozigospel.blogspot.com #MwalimuOscarVitabu #MwalimuOscarSamba

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni