Ijumaa, 27 Machi 2020

Mwalimu Mwakasege Atoa Wito wa Kushiriki Maombi Dhidi ya Ugonjwa wa Korona

Anaandika katika mtandao wa kijamii ;
Bwana Yesu asifiwe.
Hili ni ombi kwa kila aliyewahi kuhudhuria kongamano letu,la maombi la kitaifa, tunalofanyia Dodoma kila mwaka. Lakini,hata kama hujawahi kuhudhuria kongamano hilo-ombi hili linakuhusu pia.Tunajua umekuwa ukiombea tatizo la ugonjwa wa 'Corona'. Pamoja

Alhamisi, 5 Machi 2020

MREJELEE YESU.


Na Mwalimu Oscar Samba
Waimbaji wakaimba; “Kale nilitembea Nikilemewa dhambi
Nilikosa msaada, kuniponya mateso.
Usifiwe Msalaba! Lisifiwe kaburi!
Linalozidi yote, Asifiwe Mwokozi!

Shalom Mwana wa Mungu, kwa moyo mkunjufu ninakukaribisha katika Makala hii murwa, yenye nia ya kukufanya umrejelee Yesu, ujumbe huu nimeupata usiku wa kuamkia leo nilipokuwa nimelala, ulinijia kama maomo nami nalisikia sauti hii, “mrejelee Yesu,” kisha na andiko hili kunijia; “Tangu wakati wa baba zenu mmegeukia mbali na amri zangu nanyi hamkuzishika. Nirudieni mimi, nami nitawarudia ninyi,” asema BWANA Mwenye Nguvu.   ‘‘Lakini mnauliza, ‘Tutarudi  kwa namna gani?” Mlaki 3:7.

Sijui ni jambo gani lililokutatiza kiasi cha kuiamcha Imani, kiasi cha kuamua kurudi nyuma kiroho, kiasi cha kukataa kabisa au kukata tamaa moja kwa moja na safari hii ya wokovu ?

Yamkini unasema mimi sijarudi nyuma kabisa mtumishi, Yesu bado na mpenda, ila nimeishiwa nguvu za kiroho, nimejikuta sina tena kiu wala hamu ya maombi, nimejikuta nimekuwa mzito kusoma neno, na kuudhuria ibada ! Na hali hii ilianza tu pale mama yangu, mume aa muke alipofariki, ama mtoto, na mwingine labla ni baada ya kuugua, au biashara yake kufa ama kufukuzwa kazi, kusema vibaya na wapendwa, kuacha au kukosa msadaa, mwingine yamkini anasema ni mwaka wa sita sasa Mungu hajanijibu, amekaa kimya, hanisiki: kwa hiyo mtumishi hizo ndizo au ndiyo sababu kuu.