Na Mwalimu Oscar Samba
Waimbaji wakaimba; “Kale nilitembea Nikilemewa dhambi
Nilikosa msaada, kuniponya mateso.
Usifiwe Msalaba! Lisifiwe kaburi!
Linalozidi yote, Asifiwe Mwokozi!”
Shalom Mwana wa Mungu, kwa moyo mkunjufu ninakukaribisha
katika Makala hii murwa, yenye nia ya kukufanya umrejelee Yesu, ujumbe huu
nimeupata usiku wa kuamkia leo nilipokuwa nimelala, ulinijia kama maomo nami
nalisikia sauti hii, “mrejelee Yesu,” kisha na andiko hili kunijia; “Tangu
wakati wa baba zenu mmegeukia mbali na amri zangu nanyi hamkuzishika. Nirudieni
mimi, nami nitawarudia ninyi,” asema BWANA Mwenye Nguvu. ‘‘Lakini mnauliza, ‘Tutarudi kwa namna gani?” Mlaki 3:7.
Sijui ni jambo gani lililokutatiza kiasi cha kuiamcha Imani,
kiasi cha kuamua kurudi nyuma kiroho, kiasi cha kukataa kabisa au kukata tamaa
moja kwa moja na safari hii ya wokovu ?
Yamkini unasema mimi sijarudi nyuma kabisa mtumishi, Yesu
bado na mpenda, ila nimeishiwa nguvu za kiroho, nimejikuta sina tena kiu wala
hamu ya maombi, nimejikuta nimekuwa mzito kusoma neno, na kuudhuria ibada ! Na
hali hii ilianza tu pale mama yangu, mume aa muke alipofariki, ama mtoto, na
mwingine labla ni baada ya kuugua, au biashara yake kufa ama kufukuzwa kazi,
kusema vibaya na wapendwa, kuacha au kukosa msadaa, mwingine yamkini anasema ni
mwaka wa sita sasa Mungu hajanijibu, amekaa kimya, hanisiki: kwa hiyo mtumishi
hizo ndizo au ndiyo sababu kuu.
Nami nakwambia kuwa wewe uliyeamua kabisa kuacha Imani, na
wewe uliyelega kiroho kutokana na ugumu fulani, umrejelee sasa, japo wengine ni toka wamebarikiwa na Mungu
ndipo ilipokuwa mwisho wa ushirika wao, wamesahau maagizo ya Kumbukumbu la
Torati, saba na nane, kuwa ukiingia katika hiyo nchi usimuache Mungu, wala
usiseme ni akili, au uwezo wako ndio uliokutajirisha.
Wote ninyi, ujumbe huu ni wako, Bwana anasema mrejee Yeye,
mrudie leo, naye atakurudia, sijui upo katika hali gani leo, au majira haya,
ila hata wewe mwenyewe moyoni mwako u wajua kuwa ujumbe hu ni wako.
Fanya hima leo kumrejelea Mungu, kumbuka alikokutoa, wengine
walikuwa wagonjwa Bwana akawajibu, wengine walikuwa hawana kazi au ndoa, ama
walikuwa na adha fulani na Mungu kuwatokea, kisha leo mambo yamekuwa mazuri
wamemsahau, ni kama vile Mungu alikosea kuwabariki au uwapa majibu yao,
sikiliza, siku inakuja, na hicho unachokitumainia hautakiona tena, hakitakwepo
tena, utakuta siku moja kimetoweka. Mujiza huo uliokufanya kumwamini Yesu
utageuka kuwa “shubiri.”
Inasikitiksha sana mtu alikuwa hana kazi, alikuwa masikini,
kabla ya ndoa alikuwa muimbaji na shemasi mzuri kanisani, kipindi cha taabu
yake alikuwa haachi kuudhuria kanisani, kila wakati na hata majira ya maombi ya
mkesha huwezi kumkosa kwenye kusanyiko, ila sasa toka amejibiwa, anatoa
visingizio vingi, “ubize” sasa sijui Mungu amnyanganye kazi ili awe na nidhamu?
Mtu mmoja alikuwa hana mtoto, na alikuwa muudhuriaji mzuri
sana wa ibada, ila alipompata, kisingizio ni mtoto! Sasa mujiza wa mtoto
umekuwa kikwazo, mchungaji wake akamwambia vipi tuombe Mungu amchukuwe huyo
mtoto ili upate muda sasa wa kuja kanissani ?
Uhusiano wako na Mungu usijengwe na vitu, au kitu, maana
kama umerudi nyuma kwa sababu Mungu hajakujibu ombi lako la kuolewa au kuoa,
ama la uponyaji wa ndoa yako, au kwa kuwa hajakuponya au kumponya ndugu yako,
mkeo ama wewe mwenyewe, ama kwa kuwa tu huduma haikui, ama uliomba ndugu ama
mtu wako wa karibu asife na akafa, alafu kwa jambo hilo umerudi nyuma,
umekaukiwa kabisa nguvu za maombi, huwezi hata kuomba dakika moja, huwezi tena
kusoma neno, kwa sababu tu ya ugumu wa maisha, hakika umejenga msingi wako juu
ya udongo, tope au mchanga.
Leo nakusii umrejelee Mungu, naye anasema kuwa atakurejelea,
wewe, ni muhimu na lazima kujua na kufahamu kuwa Mungu atabaki kuwa Mungu hata
kama hajajibu maombi yako, hata kama hajafaya kama ulivyohitaji, hata kama
hajakupatia haja ya moyo wako, kukujibu au kutokujibu, hakumbadilishi, Yeye
husalia kuwa Mungu.
Hili ni jambo muhimu sana, Daudi alifunga na kuomba, ila
bado mtoto alifariki, na jambo ile halikubadlisha Uungu wa Mungu, Ayubu
alipitia mahali pa gumu na alikuwa mwenye haki, na jambo hilo halikuondoa Uungu
wa Mungu !
Uliomba apone, na amefariki, bado Mungu ni Mungu, uliomba
uolewe nabo milango ni migumu, Mungu ni Mungu, habadiliki, atasalia kuwa Mungu,
na uhusiano wako na Mungu usijengwe kwemye vitu, maana hata Ayubu anatufundisha
hili jambo, kwani ungejengwa kwenye vitu ni lazima angekwama, ndio maana akatuambia
haya maneno;
“Kwani msiba utokao kwa Mungu ulikuwa na kitisho kwangu, na
kwa sababu ya ukuu wake sikuweza kufanya neno.
‘Kama nimeweka tumaini langu kwenye
dhahabu, au kuiambia dhahabu
safi, ‘Wewe ndiwe salama yangu,’ kama
nimefurahia wingi wa utajiri wangu,
ustawi ambao mikono yangu ilikuwa
imepata, …” Ayubu 31:23-25.
Ukuu wa Mungu sio wa kuhojiwa, Mungu ni Mungu, amekujibu,
hajakujibu, asaliye kuwa Mungu kwako, wala usiinuwe kinywa chako kwa maneno ya
ukaidi kama ya yu wapi Mungu mbona hajanijibu, mbona hataki kunijibu, mbona
hajibu maombi, huyu Mungu sio sahihi, na kadhalika, kama una mwaswali iwe ni
katika kuhojiana naye katika heshima kuu, katika unyenyekevu, katika sala na
sio katika manung’uniko, maana kitu kikubwa kilichowaponza wana wa Israeli
ilikuwa ni manung’uniko, sasa wewe epuka hili ili uwe salama.
Mkuu wangu wa chuo, Mwalimu Mkuboba aliwahi kusema hivi,
kuwa kipindi akiwa anasoma kuliwahi kutokea msiba wa mwanafunzi mwenzao
waliompenda sana, na alikufa akiwa katika kutumwa na chuo, “na kama unavyojua
ni mwanafunzi wa chuo cha Biblia” sasa hili liliwaumiza naye aliumia, sasa
alijipanga kwenda kwenye ukumbi wa maombi au ibada ili kumuhoji Mungu, akiwa
njiani anasema, alikutana na maswali magumu sana ya Mungu, “Wewe ni nani hata
uhoji ukuu wangu, ulikwepo wapi wakati na muumba, mkataba wangu na wewe
unakuhusu nini?”
Anasema baada ya hapo alijikuta akimtukuza Mungu, na
kumshukuru, na kumsifu, ama kumuadhimisha, katika hili jaribu kujiuliza kama
Ayubu angalitazama aliyoyapitia katika jicho la namna hii ? hakika ni kwamba
angekwama tu !
Jifunze sana kumfanya Mungu kuwa ni Mungu hata kama
hajakujibu kama ulivyotaka au kuhita, jicho lako lizidi kumtazama Yeye daima,
naye sio dhalimu atakutokea na kukujibu tu, ila fahamu kuwa ni kwa muda wake,
ni katika majira yake, sio yako, hufanya kama apendavyo Yeye, usimlazimishe
kama upedavyo wewe, maaana sasa hapo unataka kumfanya Yeye awe wewe na wewe uwe
Yeye, haya hayawezekani.
Natumai sasa upo tayari kumrejelea ! maana nje ya hapo jehanam
ya moto inakusubiri, usifikirie utaenda mbinguni kwa kuzingatia historia la ! Mtu
mmoja akaniambia kuwa mimi nilimjengea Mungu ubavu mmoja wa jengo la kanisa
nikausimamisha unafikiria Mungu ataniacha ?
Huu nao ni ujinga ule wa kwanza, maana bora wa mwisho maana
yake ni mwenye kiwango kidgo cha ujinga, ila wa kwanza kazidi wengi kwa huo
ulumbukeni!
Mwingine anadhani kuwa ataenda mbinguni au kuhesabiwa haki
kwa kuwa tu anatoa sana sadaka kanisani, au anawategemeza sana watumishi, ni
kweli mbele ya mchungaji wako unaweza kuwa na kibali, ila sio mbele za Mungu !
MUGU wetu ni mwenye haki, utakatifu ndio sifa pekee
ikuwezeshayo kufika mbinguni au kuhesabiwa haki, na sio vinginevyo, kuwa mtoto
wa mchungaji, mama mchungaji au mchungaji ama mwinjilisti au nabii mstaafu sio
tiketi ya wokovu, au kuhesabiwa haki !
Geuka leo, ni kwli tunakuona u mtumishi mzuri ila kwa kweli
umeoza, unazini kwa siri, unalewa kwa kificho, umejaa masengenyo na uchonganishi,
Mungu anakutaka kurejea kwake leo, umemuacha na kumuasi vya kutosha, leo rudi,
leo rejea kwake, na fanya hima maana mlango bado haujafungwa, kumbuka enzi za
Nuhu,w atu waliendelea kunywa, na kulewa na kuzini, ila muda wa mwisho
ulipofika, walijikuta wakitafuta msaada na kuukosa, rejea leo, ile watu wanakuona
u mtumishi, sio kigezo cha kuhesabiwa haki, kumbuka hili daima.
Sasa kama u, tayari kurudi, imizo langu kwako ni hili, tubu
sasa, omba msamaha sasa, nyeyenyekea sasa, na ukaache ule uovu wako wote, 2
Nyakati 7:14, hapo kuna na uponyaji na kuondolewa misiba, kama tu utamaanisha,
na urejesho wa mali, ndoa, uchumi, na maisha kama tu utamaanisha kiukweli.
Sasa yamkini unataka kuokoka, mara baada ya kuguswa na Mungu
katika ujumbe huu, au ulikuwa umeokoka na kurudi nyuma, au ulilega katika
uhusiano, tafadhali fanya sala hii ya toba pamoja nami kwa Imani;
Sema, MUNGU BABA, NINAKUJA MBELE ZAKO, NINATAMBUA YA KUWA
MIMI NI MWENYE DAHAMBI, NINAKUOMBA UNISAMEHE, NA ULIONDOWE JINA LANGU KWENYE
KITABU CHA HUKUMU, NA TAFADHALI ULIANDIKE KWENYE KITABU CHA UZIMA WA MILELE, NA
NIPE KUMAANISHA KWENYE WOKOVU, NISHINDIE VISHAWISHI NA KILA DHAMBI INIZANGAYO
KWA HARAKA, NINAKUAMINI NA KUKUPOKEA MOYONI MWANGU KAMA BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YANGU, Amen.
Hongera kwa kukoka, na sasa tafuta kanisa la watu walioka,
ukasali hapo sasa, wambie umeokoka hivi karibuni, ili wakulee vyema, na kama
ulishaokoka ukarudi nyuma, tafadhali eleza udhaifu wako wa awali kwa mchungaji
ili aombe pamoja nawe, na usitende dhambi tena, pi usikubali kujihukumu nafsini
mwako kwa makosa yoyote yale ya awali maaana Damu ya Yesu imeshakuondolea hatia
zote.
Kwa mawasiliano tafadahli wasiliana nasi, Simu 0759859287,
baruapepe: ukombozigospel@gmail.com.
Asante, ujumbe huu nimeuombea na hakika utasalia moyoni
mwako daima, na kukupa nguvu wewe uliyeko katika hali ya kuzimia, au kuchoka
kiroho, Isaya 40:28-31.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni