Jumatano, 3 Julai 2019

JINASUWE KWENYE ROHO AU VIFUNGO VYA KURITHI, FAMILIA, KABILA NA UKOO.

Ujumbe huu ni matokeo ya kiu ya kijana fulani anayesoma kidato cha Sita kunitaka nimfundishe maana amekuwa akisumbuliwa na mkuu wao wa ukoo ambaye humtokea na kumtangazia kumkwamisha kimasomo, japo yeye hamjui maana ni wa miaka mingi, ila hujitambulisha hivyo, na amekuwa akipitia wakati mgumu kitaaluma, hata kugubikwa na usingizi mzito mwalimu aingiapo darasani na kadhalika !
Pia ni nimeelezea jambo hili kiupana sio kitaaluma tu, natumai litakusaidia namna ya kujinasua kindoa, kiuchumi, na hata kimaisha, unapojiona umeokoka ila maisha yako yamekwama kama ndugu zako, una ugonjwa ambao husumbua jamii zako, unatatizo la kindoa kama nduguzo, unakataliwa na ndugu, huna kibali kwao, uwe na hakika hizi roho zipo kazini.


Nimekuwa pia nikiombea wanafunzi na mara kwa mara nimegundua kuna roho za kurithi ambazo hazitaki wao wasome, ndio maana huachilia uzito kwenye akili zao, fahamu zao, na kadhalika, mmoja leo nimepigiwa simu na mama yake naye kuniambia kuwa ameota mwanaye anafukuzwa na ng'ombe kisha ngombe huyo kumchoma na pembe, na aliniuliza ng'ombe anawakilisha nini na mimi kumjibu kuwa huwakilisha mizimu au miungu, hii ni ishara tosha kuwa hali aliyo nayo manae ya kusahau, uzito kiakili hadi kufikia hatua ya walimu kujiuliza mbona awali alikuwa vyema ni ishara ya upinzani kutoka kwenye hizi roho !

Kinachoshanga zaidi ni kwamba kabla ya kuokoka hakuwa na huo uzito, ila alipookoka ulijitokeza ! Hii ina maana kwamba miungu ile ilipewa jukumu la kumfanikisha kimaisha kupitia elimu, sasa ametangaza kuikataa nayo imemgeuzia kibao na kuanza kupigana naye !

Visa kama hivi vipo,na hata yupo mwingine wa sekondari ambaye kabla ya wokovu hakuwa na shida kama hiyo,sasa huyu anahitaji maombi ya kina ya kujinasua hapo, na ajifunze sana kuachilia sadaka maalumu ya ukombozi kwa mchungaji au kanisani ama mtumishi atakayesukumwa kumpatia ili ajiunganishe na madhabahu sahihi, ila umakini hapa ni kuunganisha maombi hayo na sadaka,sio sadaka bila maombi, bali maombi na sadaka, na sio sadaka na maombi, la ni maombi kwanza kisha utoaji, na usitowe kwa mtu ni mtu,maana utaoji usio sahihi ni nira, toa kwa mtumishi aliyeokoka, na sio kila mtumishi na uongozwe na Bwana ! ( Mzazi wa weza msaidia mwanao !)

Kuna mmoja nilimuombea na ninaendelea naye huyu ni binti, na nilisukumwa kumuongoza sala ya toba, maana nilimuona anafukuzwa na nyoka, nilipomuliza ndoto anazoota mara kwa mara alibainisha hiyo ya kufukuzwa na chatu, nilitambua kuwa huyo ni mungu wa kwao, au wa asili ya kwao, na uwokovu ndio njia pekee ya kumtenga !

Maana nje ya wokovu hata ukimuombea haya maombi kwa mwenye vita vya miungu ni rahisi baadae kurudiwa tena, japo sikuzuilii kumuombea ambaye hataki au hajaamua bado kukoka !

Ukiokoka, ni rahisi kukabiliana na hizi roho, na yule anaye okoka na kukutana na hizi adha ni sawa na mtu aliyetoka kwenye shimo na kurushiwa mawe na mtu aliyeko shimoni, sasa huyu kushinda ni rahisi, maana anaweza kumkimbia, au akakasirika na kumfukia adui yake, ila ambaye hajaokoka ni sawa na aliyefungwa shimoni na kurushiwa huko mawe, huyu kujinasua au kuzuia kurushiwa mawe na adui aliyenaye shimoni ni vigumu sana japo uwezakano upo, ila hata ukimzuia kukurushia mawe au kukupiga nayo bado utasalia shimoni ! Nimeongea mengi, ngoja sasa nikuletee huo ujumbe ! Karibu:

Roho za ukoo au familia, kabila ama za kurithi huwa na tabia za kupambana na urithi wa kibaraka au wenye mafanikio kwa mtu, mfano elimu, uchumi, kukua ama kuongezeka kiroho, ' kuna mtu mmoja aliniambia mtumishi kuna namna naona nataka kuongezeka ujazo wa Roho Mtakatifu ila kuna kama kitu kina nizuia,' kuna msemo mmoja wa walimu wa haya maswala usemao kuwa urithi mbaya huwa unazuia au unapambana na urithi mzuri, na hii ni kibiblia kabisa !
Kabla ya baraka za Ibrahimu, ambazo ni urithi mzuri kutufikilia, maandiko hutoa imizo kwa laana kushuhulikiwa kwanza !

Wagalatia 3:13 Kristo alitukomboa katika laana ya torati, kwa kuwa alifanywa laana kwa ajili yetu; maana imeandikwa, Amelaaniwa kila mtu aangikwaye juu ya mti;
  14 ili kwamba baraka ya Ibrahimu iwafikilie Mataifa katika Yesu Kristo, tupate kupokea ahadi ya Roho kwa njia ya imani.

Tunajionea andiko hilo la baraka likitanguliwa na kushuhulikiwa kwa laana kwanza ! Kama Mungu amekupangia kusoma hadi shahada ama shahada ya juu ya uzanivu, uwe na hakika kuwa adui akitaka kukukwamisha hataacha kuokota laana ya kutokufanikiwa mahali fulani ili akukwamishe, hutumia pia roho za nyumbani !

Daudi alikuwa anajipanga kupigana na Goliathi, katika ile 1 Sam 17, ila kaka yake Eliabu alisimama kama kikwazo, Daudi Mungu alimuandaa ili kuwa mfalme, na alituma huo ujumbe wa kutengwa kwa utumishi wa Samweli,ila roho za kifamilia ziliwahi na kuachilia hali ya kudharauliwa au kukataliwa kwake !
Yesu alikuwa mbeba maono, ila ndugu zake walimkataa hata kufika mahali pa kusema kuwa amerukwa na akili wakitaka kumkamata !
Marko 3:21 Jamaa zake walipopata habari wakatoka kwenda kumkamata; maana walisema, Amerukwa na akili.

Unapoona upinzani wa mafanikio yako ukiwa unatokea nyumbani kwako, kimwili na kiroho, ama unapojikuta ukiota ndoto za kukupinga na unaowaona rohoni ni watu wa nyumbni uwe na hakika kuna roho zimekaa hapo kama Eliabu kwa Daudi, uwe na hakika ni nduguze na Yusufu wanaosema na tumuuwe kisha tutaona zitakuaje ndoto zake !

 Upinzani wa hizi roho ni mkubwa na hatari zaidi maana kwanza zinakufahamu kiundani, pili zina uhalali mkubwa, wa kinasaba, kidamu, kimaagano, kimadhabahu, kiaridhi na kadhalika, ndiposa kujua namna ya kujinasua ni muhimu, kuna njia kuu mbili, ya kwanza ni ile ya kujitenga, na ya pili ni ile ya kuvunja, ushauri wangu kwako anza na ya kujitenga.

Hapa ni unakikata kitovu chako ikiwa na maana ya kutoka kwenye asili au muunganiko wao kwa njia ya maombi ya vita, tumia upanga wa Roho na Damu ya Yesu, fahamu imeandikwa ktk Ezekieli 16:1-5, kuhusu asili ya watu ambayo iliwasukumia katika urithi mbaya wa kuabudu miungu ya kigeni, nawe yaweza kukusukumia katika asilli ya tabia hatarishi, au kukwama kama ndugu au jamaa zako walivyo kwama katika elimu, ndoa, ama sehemu fulani ya kimaisha !

Ila awali ya yote anza na rehema, tumia sana Damu ya Yesu, tubu kama Danieli katika ile Danieli 9, usijihesabie haki, kumbuka Maombolezo 5:7 husema kuwa baba zetu walitenda dhambi wala hawapo na sisi kuchukuwa maovu yao, hata katika Hesabu 14 watoto walichukuwa mizigo ya uovu wa wazazi wao, kwa hiyo tubia dhambi zilizotangulia kufanywa nao hata kama leo hawapo, sawasawa na Warum 3:25, ukitumia Damu ya Yesu Yenye uwezo wa kwenda kizazi na kizazi !

 Pia Mathayo 26:28 na Luka 22:20, ni maandiko yanayokupa uwezo wa kutumia Damu ya Yesu ya kiagano, na hapo inauwezo mkubwa wa kupambana na kila nira au vifungo vya kimaagano, na Waebrania 9:22, itumie kujisafisha, au kukisafisha kitovu chako, tangaza pia kulitoa jina lako na nafsi yako katika madhabahu au maagano yao !

Baada ya hapo, tangaza kuachilia urithi mzuri yaani baraka za kimaagano, kama Waefeso moja isemavyo kuwa tumebarikiwa kwa baraka zote za rohoni na za mwilini, kama Ujumbe wa Yohana kwa Gao na maombi yake kwake kuwa tufanikiwe kama roho yetu zifanikiwavyo, achilia sasa hizo baraka maana urithi mbaya umeshatengwa nawe, ziachilie kindoa,' hata kama uri wa kuoa na kuolewa bado, wewe iachilie kindoa maana maombi ni akiba' kiuchumi, kiroho na kielimu, kwako na kwa uzao wako pia !


Mpendwa , kama hujaokoka na unataka kufanya hivyo sasa tafadhli kwa imani kubwa nakuu kabisa fuatisha pamoja nami maneno haya, au sala hii ya toba ili uweze kuokoka, Sema;

BWANA YESU, NIMETAMBUA KUWA MIMI NI MWENYE DHAMBI, NATUBU MBELE ZAKO LEO, NISAMEHE NA NINAKUOMBA UFUTE JINA LANGU KWENYE KITABU CHA HUKUMU, TAFADHALI LIANDDIKE KWENYE KITABU CHA UZIMA, NINAKUKIRII NA KUKUPOKEA MOYONI MWANGU KAMA BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YANGU, HAKIKA WEWE NI MUNGU NA ULIFUFUKA KATIKA WAFU, Amen.

Hongera kwa kuokoka na tafuta kanisa la watu waliokoka ukasali hapo, kwa maombi, sadaka kwa njia ya M-Pesa, kupiga simu au Wasats App, ni +25559859287. Tupo Arusha Tanzania.

Kwa undani wa Mafundisho au Habari zetu tembelea; www.ukombozigospel.blogspot.com .
#MwalimuOscarSamba #UgMinistry #UkomboziGospel #MwalimuOscarVitabu #Neno #Biblia #Zaburi #Pic #Picha #Tanzania #Afrika

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni